Madhabahu
ni nini?
Ni daraja la kuunganisha katika
ya ulimwengu wa roho wa Mungu au shetani.
Kuna aina 2 za madhabahu, Madhabahu
ya MUNGU (Nuru)na madhabahu ya shetani (giza)
***MADHABAHU
YA MUNGU
Watu/watumishi wa Mungu katika
Biblia walianza kwa kujenga madhabahu kabla ya kufanya chochote
NUHU – Mwanzo 8:20“Nuhu akamjengea
Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege
aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.”
MUSA – Kutoka 17:15“Musa akajenga
madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;”
YOSHUA – Yoshua 8:30“Ndipo Yoshua
alijenga madhabahu kwa Bwana, Mungu wa Israeli katika mlima Ebali.”
GIDEONI – Waamuzi 6:24“Ndipo Gideoni
akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi
leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.”
SAMWELI – 1 Samweli 7:17“Na kurudi
kwake kulikuwa mpaka Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko
alikowaamua Israeli; na huko akamjengea Bwana madhabahu.”
***MADHABAHU
YA SHETANI
shetani na watumishi wake wana
madhabahu ambayo hutumia kupitisha mambo mabaya/maovu kutoka katika ulimwengu
wa roho (giza) kuingia katika ulimwengu wa mwili.
Kutoka 34:11-13 “11 Liangalie
neno hili ninalokuamuru leo; tazama, mbele yako namtoa Mwamori, na Mkanaani, na
Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. 12 Ujihadhari nafsi yako, usije
ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako.
13 Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata
maashera yao.”
Mungu anawaagiza wana wa
Israeli wasifanye maagano na wenyeji bali wabomea madhabahu zao kwani matatizo
ili yakupate lazima yatokee katika madhabahu ya shetani.
Kumb 12:2-3 “2 Vunjeni kabisa
mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya
milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi; 3
nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao
yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina
lao lifutilieni mbali na mahali hapo.”
MAMBO
MUHIMU YANAYOUNDA MADHABAHU
1. Mungu
wa madhabahu
2. Kuhani
wa madhabahu
3. Washirika
wa madhabahu
4. Kafara
ya madhabahu
5. Nguvu
ya madhabahu
1.
MUNGU
WA MADHABAHU
Neno “mungu” ni nafasi au cheo
kama ilivyo kwa Rais. Kwa maana hiyo unapotaja jina la mungu inakubidi uainishe
ni mungu yupi unayemtaja.
Kutoka
6:1-3“1 Bwana akamwambia
Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa
kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake. 2 Kisha Mungu
akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; 3 nami nilimtokea Ibrahimu, na
Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana
kwao.”
**MUNGU
WA MADHABAHU ZA KISHETANI
shetani ndiye mungu wa
madhabahu za wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota na mawakala wote wa
mauti.
2Kor
4:4“ambao ndani yao mungu
wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya
utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”
1Wafalme
16:32“31 Ikawa, kama
ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa
Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali,
akamsujudia. 32 Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga
huko Samaria.”
*****FANYA MAOMBI
YA KUWAANGAMIZA MIUNGU WA MADHABAHU ZA KISHETANI*****
2.
KUHANI
WA MADHABAHU
Kuhani wa madhabahu ni mtu
mwenye uwezo wa kuleta mambo kutoka ulimwengu wa roho kuingiza katika ulimwengu
wa mwili.
Mwanzo 14:18 “Na Melkizedeki
mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu
sana.”
**KUHANI
WA MADHABAHU ZA KISHETANI
1 Samweli 5:5 “Kwa hiyo
makuhani wa Dagoni, na mtu awaye yote aingiaye nyumbani mwa Dagoni, hawakanyagi
kizingiti cha nyumba ya Dagoni huko Ashdodi, hata leo.”
1Wafalme 18:25-26 “25 Eliya
akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana
ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini. 26
Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu
asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti,
wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya.”
**** FANYA MAOMBI
YA KUWAANGAMIZA MAKUHANI WA MADHABAHU ZA KISHETANI
3.
KAFARA
YA MADHABAHU
Madhabahu haiwezi kukamilika
kama hakuna kafara kwasababu kila mungu wa madhabahu huhitaji kafara.
Walawi
2:2“kisha atauleta kwa wana
wa Haruni, hao makuhani; naye atatwaa konzi moja katika huo unga mwembamba, na
katika mafuta yake, na huo ubani wote; kisha kuhani atauteketeza kuwa ndio
ukumbusho wake juu ya madhabahu, ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya
harufu ya kupendeza kwa Bwana;”
Zaburi
40:6“6 Dhabihu na matoleo
hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi
hukuzitaka.”
Zaburi
50:8“Sitakukemea kwa ajili
ya dhabihu zako, Na kafara zako ziko mbele zangu daima.”
**KAFARA
KWENYE MADHABAHU YA KISHETANI
Zaburi
106:36-38“36
Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao. 37 Naam, walitoa wana wao na
binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani. 38 Wakamwaga damu isiyo na hatia, Damu ya
wana wao na binti zao, Waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani; Nchi ikatiwa
unajisi kwa damu.”
Yeremia
32:35“Tena walijenga mahali
palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha
wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza;
wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha
Yuda.”
****MAOMBI
YA KUANGAMIZA KAFARA ZA MADHABAHU ZA KISHETANI
4.
WASHIRIKA
WA MADHABAHU
Washirika wa madhabahu ni watu
muhimu sana kwenye madhabahu. Kama vile wewe ulivyo ni mshirika wa kanisa
Fulani vivyo hivyo kila madhabahu ya kishetani inayo washirika wake.
Eliya alifahamu umuhimu
wa kuwa na washirika. 1Wafalme 19:9-10“9 Akafika kunako pango, akalala ndani yake.
Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya?
10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa
wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua
manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho
yangu, waiondoe.”
Mungu anamtoa Eliya hofu
1Wafalme 19:18“Pamoja na hayo nitajisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti
lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu.”
**WASHIRIKA WA MADHABAHU ZA KISHETANI
Hawa ni watu hatari sana,
kwakuwa matatizo yote huanzia kwenye madhabahu za kishetani, wanao peleka jina
lako/kazi yako/ndoa yako/elimu yako…… ni washirika wa madhabahu ili lijadiliwe
kwa lengo la kuharibu maisha yako.
Washirika wa madhabahu
ya kishetani mara zote ni watu wako wa karibu
Waamuzi 16:5 “Nao wakuu
wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu
zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi
tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.”
Mathayo 10:36“na adui za mtu ni wale
wa nyumbani mwake.”
Na Mika 7:5-6“5 Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya
midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari. 6 Kwa
maana mwana humwaibisha babaye, na binti huondoka ashindane na mamaye; na
mwanamke aliyeolewa hushindana na mavyaaye; adui za mtu ni watu wa nyumbani
mwake mwenyewe.”
****MAOMBI
YA KUWAANGAMIZA WASHIRIKA WA MADHABAHU ZA KISHETANI
5.
NGUVU
YA MADHABAHU
Nguvu ya madhabahu inategemea
mambo yote yanayounda madhabahu yaani
Mungu wa madhabahu, kuhani wa madhabahu, kafara ya madhabahu na washirika wa
madhabahu.
Mashetani walio katika
madhabahu wanao mfumo wa uongozi wa kifalme. Imeandikwa Waefeso 6:12 “Kwa maana
kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka,
juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa
roho.”
****FANYA MAOMBI
YA KUHARIBU NGUVU YA MADHABAHU ZA KISHETANI
Isaya
47:9-12 “9
lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na
watoto, na ujane; yatakupata kiasi kitimilifu, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na
uganga wako mwingi mno. 10 Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana
anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni
mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi. 11 Kwa sababu hiyo
ubaya utakupata; wala hutajua kutopoa kwake; na msiba utakuangukia; hutaweza
kuuondoa; na ukiwa utakupata kwa ghafula, usioujua. 12 Simama sasa na uganga
wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda
utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda.”
Ezekiel
13:17-22“17 Na
wewe, mwanadamu, kaza uso wako juu ya binti za watu wako, watabirio kwa akili
zao wenyewe; ukatabiri juu yao, 18 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao
wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu
ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu
wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe? 19 Nanyi mmeninajisi kati ya watu
wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za
watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa
kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo. 20 Basi Bwana MUNGU
asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda
roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami
nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege. 21 Na leso zenu nazo nitazirarua,
na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu
tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. 22 Kwa kuwa ninyi
mmemhuzunisha moyo mwenye haki kwa uongo, ambaye mimi sikumhuzunisha; na kuitia
nguvu mikono ya mtu mbaya, hata asigeuke, na kuiacha njia yake mbaya, na
kuhifadhika; 23 basi, kwa sababu hiyo ninyi hamtaona tena ubatili, wala
kutabiri mambo; nami nitawaokoa watu wangu katika mikono yenu; nanyi mtajua ya
kuwa mimi ndimi Bwana.”