Friday, September 2, 2016

TOA SADAKA YAKO KWAAJILI YA SEMINA YA NENO LA MUNGU NGUDU - KWIMBA, MWANZA (Tarehe 30/09/2016 hadi 02/10/2016)

Shalom!!!

Semina ya Neno la MUNGU, kwa muda wa siku tatu, kuanzia tarehe 30/09/2016 hadi 02/10/2016

Huduma ya Uzima wa Milele International Ministries (UMIM) kwa kushirikiana na huduma ya MANA mkoa wa Mwanza imeandaa semina ya Neno la MUNGU, kwa muda wa siku tatu, kuanzia tarehe 30/09/2016 hadi 02/10/2016 katika mji wa NGUDU wilaya ya Kwimba. Semina itakuwa ni semina ya tatu kufanyika katika mji huu wa Ngudu, semina zingine zilifanyika Februari na Mei mwaka huu (2016). Semina hizi zimekuwa za mafanikio makubwa sana kiroho na hata kimwili.

Tunamshukuru Mungu kwaajili ya watu wa MANA Mwanza kwa jinsi wanavyojitoa kwa muda wao na mali zao katika kuhakikisha semina hizi zinafanikiwa kila zinapopangwa, Mungu wa mbinguni azidi sana kuwabariki na kuwainua katika huduma aliyoiweka ndani yenu

Makadirio ya bajeti kwaajili ya semina hii ni shilingi milioni 3.Tunaomba sadaka yako ili tufanikishe semina hii. Pia ungana nasi kufunga na kuomba siku za Jumanne na Ijumaa ili kuombea semina hii ili kusudi la Mungu litimie.

Unaweza kutuma sadaka yako kwa njia ya:-

M-pesa namba 0752 606 041 Lucy Lusoloja (Mratibu UMIM - Kwimba, Mwanza) au 

0759 565 600 - Levina Deogratius, 

Tigo pesa 0713 664 338 Samson Mollel


Mungu akubariki kwa sadaka yako.

Tuesday, August 30, 2016

HISTORIA YA MAISHA YAKO INABADILIKA LEO Isaac Ridhiwan Omary


Imefundishwa na Mtumishi Isaac Ridhiwan Omary (Semina ya MVUMO – Morogoro, 28th August 2016)
Imeandikwa na Samson Mollel – 0767 664 338 (www.uzimawamileleministries.blogspot.com)

*Yohana 9:1-9* _“1 Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. 2 Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? 3 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. 4 Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. 5 Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu. 6 Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho, 7 akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona. 8 Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba? 9 Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye.”_

Unapokutana na Yesu Kristo, kubadilisha historia ya maisha yako sio jambo linalohitaji miaka mingi, ni dakika moja tu na historia ya maisha yako inabadilika kabisa.

Ilimchukua dakika moja tu mwizi pale msalabani kubadilisha historia nzima ya maisha yake. Yesu hakumuuliza umebatizwa wapi au umezaliwa na nani, ukikutana na Yesu dakika ileile maisha yako yanabadilika.

*Luka 23: 39-42* _“39 Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. 40 Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? 41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa. 42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. 43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.”_

Fahamu yakwamba dunia hii inatafsiri mambo isivyofaa. Yaani ukipita katika changamoto/matatizo yoyote basi unaonekana wewe umetenda dhambi; inawezekana haujaolewa, haujapata mtoto, watoto wako wanaumwa, haujapata kazi, n.k. Basi hapo watu husema kuwa wewe au wazazi wako wametenda dhambi.

*Yohana 9:1-2* _“1 Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. 2 Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?_

Kuna mahali unapitia sasa katika maisha yako na watu wansema maneno mengi na hayo wanyoyasema yankufikia na kukuumiza. Umejitahidi kufanya toba za kila namna kwa habari ya maovu na makosa na dhambi za kwako na za familia yako lakini bado uko kwenye hali ile ile.

Nakuambia leo kama umeshatubu usiitafute hiyo dhambi kwako na hizo hatia ulizojibebesha uzifute kwa damu ya Yesu kwakuwa mambo hayo yameachiliwa na Mungu ili kazi za Mungu zidhihirishwe.

*Yohana 9:3* _“3 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.”_

Yesu unayekutana naye leo anaenda kubadilisha kabisa maisha yako, jambo la msingi ni kuheshimu anakuambia ufanye nini. Heshimu mambo ya Mungu hata kama unayaona ni ya kipumbavu *1Wakorintho 1:25* _“Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.”_

Yesu alitema mate chini na kumpaka matope yule kipofu kama tunavyosoma katika *Yohana 9:6-7* _“6 Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho, 7 akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona._

Alipofika katika birika la Siloamu na kunawa, hakuona mara moja ila wakati akirudi kutoka Siloam kwenda kwa Yesu ndipo alipopata kuona

Inawezekana katika hali uliyopo sasa ndio unanawa, yaani upo Siloam unanawa na bado macho yako hayajafunguka, usikate tama endelea kunawa. Ondoa magonjwa, umasikini, kila aina ya udhaifu wewe endelea kunawa kwani umekutana na Yesu leo na nilazima maisha yako yatabadilika kabisa.


SIRI ZA UFALME April 5, 2016 by tunzomnzava


1.      UTANGULIZI
Math. 13:10-17
10Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano? 11Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa. 12Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa. 13Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.14Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. 15Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. 16Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. 17Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.
Sura ya 13 ya Mathayo ni mwanzo mpya wa mafundisho ya Bwana Yesu  – hasa akielezea yatakayotokea baada ya Yeye kurudi mbinguni kama “Mfalme atakayetawala”.
Wasomaji wa Biblia wanajua kuwa Mathayo anaanza Injili yake kwa kuonyesha
1.      Kuwa Yesu NDIYE Mtoto wa kiume aliyetabiriwa atakayemiliki katika Kiti cha Enzi cha Daudi – Sura 1
2.      Kuwa ushahidi wa ufalme wake ni Mamajusi toka Mashariki waliokuja kumwona pamoja na tunu; na ubatizo aliobatizwa na Yohana pale Yordani – Sura 2 &3
3.      Kuwa baada ya Ubatizo na Majaribu, Bwana Yesu alitoa Kanuni sa Ufalme wake ujao – katika Hotuba ya Mlimani – Sura 5-7
·         Misingi ya kanuni hizi ni misingi ya kiroho na Kimaadili – kanuni zinazosimamia Ufalme wa Mungu
·         Kanuni hizi ndizo zile zilizotabiriwa juu ya ufalme wake hapa duniani ambazo Masihi-Mfalme angelizileta akitokea
·         Kanuni hizi zina kweli ambazo hata leo zinatumika na zitatumika katika Utawala wake wa Miaka 1000
4.      Miujiza inayomdhihirisha kuwa ndiye Mfalme – Sura 8-10
Hadi hapo ilikuwa dhahiri kuwa Wayahudi walikuwa wamekataa kabisa ushahidi wowote kuwa Yesu ndiye Masihi na Mfalme aliyetabiriwa
5.      Kukataliwa na kuahirishwa kwa Ufalme wake vikitabiriwa.Bwana anaonyesha hili kwa kuikemea miji ile ambayo miujiza yake mingi ilifanyika, na miji ile haikutubu – yaani Korazini, Bethsaida nan Kapernaumu – Sura 11 (Hasa 21-25).
6.      Kuwa Mafarisayo wanafikia kiwango cha juu sana kukana katakata Umasihi na Ufalme wa Yesu na kuanza kudai kuwa Bwana Yesu anatoa pepo kwa Belzebul – mkuu wa pepo – Sura 12 (Hasa mistari ya 14, 22-29)
Sura ya 13 inakabili swali la nini kitakachotokea wakati Mfalme aliyekataliwa atakaporudi mbinguni, yaani wakati ufalme aliouahidi utakapoahirishwa hadi ajapo mara ya pili.
Wazo la kuahirishwa kunaeleweka tu kibinaadamu – kama ilivyotokea kule Kadeshi-Banea – lakini sio kaka mpango wa milele wa Mungu, kwani mpango wa Mungu haubadiliki.
Labda sasa tuone kwa kifupi sana kilichotokea pale  Kadeshi-Banea:
1.      Hesabu 12 (Huko Hazeroth – Mst 16)
–          Haruni na Miriam wanampinga Musa kwa sababu ya kuoa mwanamke Mkushi
–          Mungu anampiga Miriam kwa ukoma
2.      Hesabu 13 (Nyika ya Parani – Mst 3,26)
–          Musa anatuma wapelelezi kuipeleleza Kanaani
–          Wapelelezi wanarudi wka Musa  (Mst 26)
–          Wapelelezi wanatoa taarifa mbaya ya kukatisha tamaa (Mst 28-33)
3.      Hesabu 14 (Kadeshi-Banea)
–          Uasi mkuu (Mst 1-10).
–          Mungu anaamua kuwaangamiza wote (Mst 11-12)
–          Musa anawaombea neema kwa Mungu (Mst 13-19)
–          Mungu anawasamehe (Mst 20-21)
–          Mungu anaahirisha kwa wana wa Israeli kuingia Kaanani kwa kizazi kile hadi kifie jangwani. Mungu anaamua kuwa kila siku waliyopeleleza Kanaani italipiwa kwa mwaka (Mst 26-35). Yaani Miaka 40 baadae ndio wataingia Kaanani
–          Wale walioleta taarifa mbaya wanapigwa kwa tauni na kufa palepale (Mst 36-37)
–          Watu wanatubu na kuasi hapohapo (Msh 39-45)

2.      MPANGO WA MUNGU HAUBADILIKI
Jambo lililo la dharura kwa mwanadamu kwa Mungu liko katika mpango wake kabisa. Kuna mambo ambayo katika mipaka ya muda tunaona ni dharura, lakini kwa Mungu kila kitu kiko katika muda unaoitwa sasa. Mambo yaliyopita, na mambo yajayo yako sasa kwa Mungu.
Mpango wa Mungu kwenye mtazamo wetu unapaswa wakati wote uonekane KUHUSISHA YALE YOTE AMBAYO YAMESHATOKEA (The plan of God always includes what actually happened). Ndani ya mpango huo, bado mwanadamu mhusika anawajibika sana.
Hebu tuone mistari mingine kuelezea ukweli huu:
Math. 18: 7Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!
Math. 26:24Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.
Luka 24: 25Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!26Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? 27Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
Isaya 53: 10 Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake; 11Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.
Tukijua kanuni hii haitakuwa shida kuelewa maneno ya Petro katika Matendo ya Mitume 3:13-21:
13Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe. 14Bali ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe mwuaji; 15mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua katika wafu; na sisi tu mashahidi wake. 16Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote. 17Basi sasa, ndugu, najua ya kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda. 18Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo.19Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; 20apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani; 21ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.
Yaani, kukataliwa kwa Yesu, kuuawa kwa Yesu, Kifo chake, Ufufuo wake, nk – vyote vilikuwa bado muhimu sana katika mpango wa milele wa Mungu kwa ajili ya wokovu wetu!
Kwa mantiki haya, Ufalme wa Mungu ambao ulikuwa utokee mara ULIAHIRISHWA hadi wakati mwingine. Mwanadamu alipokataa, Ufalme ULIAHIRISHWA – yaani Ufalme aliouleta Yesu duniani uliahirishwa!
3.      UFALME WA MBINGUNI NA UFALME WA MUNGU
Kwanza kabisa nadhani ni muhimu sana tuone kwa kifupi sana tofauti Iliyoko kati ya Ufalme wa MBINGUNI na Ufalme wa MUNGU.
Ukisoma Biblia utaona yakini kuwa kuna Ufalme wa MBINGUNI na Ufalme wa MUNGU, na sehemu nying imeelezwa kuwa ni kitu kilekile. Ukiwa makini zaidi kidogo kulinganisha maandiko utaona tofauti kubwa ya Ufalme wa MBINGUNI na Ufalme wa MUNGU.
Ufalme wa MBINGUNI unazungumzia na unahusu tabia ya ukiri (professing character) ya Ufalme – nawo unawahusu wasioamini kwa ndani, jinsi wanavyoonekana kwa nje kuwa ni waumini na wanaoamini halisi – ndani na nje. Ufalme huu unazo “ngano” na “magugu”.
Ufalme wa MUNGU unawahusu tuwaumini wa kweli (kwa ndani na kwa nje). Ndio Bwana alitufundisha kuwa tuombe: “Ufalme wako uje”.
Kuona tifauti za kimafundisho ya ufalme wa MBINGUNI na Ufalme wa MUNGUvitatusaidia sana kuelewa histria ya mpango wa Mungu katika Biblia. Ni uelewa tu haba unaosababisha tusione hasa nafasi na kipindi cha Kanisa na Israeli, kwa mfano, kwa sababu hatuoni tofauti hizi za Ufalme.
Inaweza kukushangaza kugundua kuwa Biblia ni ujumbe kuhusu mashindano juu ya UFALME – yaani Ufalme wa Mbinguni wenye Ufalme pale Yerusalemu (duniani). Waweza mara kujiuliza: kwa nini Wayahudi walimkataa Bwana Yesu kama Masihi na Mfalme? Ni kwa sababu (kwa sehemu kubwa) walitegemea Yeye atakayekuja amiliki Israeli ili Israeli sasa waitawale dunia. Tunasoma hivi katika Maandiko:
5Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. 6Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu. 7Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema Bwana, ambapo hawatasema tena, Aishivyo Bwana, aliyewatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri;8lakini, Aishivyo Bwana, aliyewapandisha na kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi zote nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe. – Yeremia 23
Na tena:
1Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu. 2Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu. 3Mungu katika majumba yake Amejijulisha kuwa ngome. 4Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walipita wote pamoja. 5Waliona, mara wakashangaa; Wakafadhaika na kukimbia. 6Papo hapo tetemeko liliwashika, Utungu kama wa mwanamke azaaye. 7Kwa upepo wa mashariki Wavunja jahazi za Tarshishi. 8Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa Bwana wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu ataufanya imara hata milele. Zaburi 48
Ndio maana Bwana alipowapa mikate, walimfuata wote. Tunasoma hivi katika Injili ya Yohana 6:
24Basi mkutano, walipoona ya kuwa Yesu hayuko huko wala wanafunzi wake, waliingia mashuani wenyewe, wakaenda Kapernaumu wakimtafuta Yesu. 25Hata walipomwona ng’ambo ya bahari, walimwambia, Rabi, wewe umekuja lini hapa? 26Yesu akawajibu, akasema, Amin, amin, nawaambieni, Ninyi mnanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.27Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.
30Wakamwambia, Unafanya ishara gani basi, ili tuione tukakuamini? Unatenda kazi gani? 31Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale. 32Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni. 33Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. 34Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki.35Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe. 36Lakini naliwaambia ya kwamba mmeniona wala hamwamini. 37Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. 38Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. 39Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho. 40Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
41Basi Wayahudi wakamnung’unikia, kwa sababu alisema, Mimi ni chakula kilichoshuka kutoka mbinguni.42Wakasema, Je! Huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu, ambaye twamjua babaye na mamaye? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?
Alipoingia Yerusalemu, wote walimfuata wakiimba “Hosana…” yaani “Okoa sasa…” (Yohana 12:13 na Marko 11:9-10). Walijua kuwa sasa Mfalme wao wa kuwaokoa dhidi ya dola gandamizi la Kirumi amekuja, na pia kwa mara ya kwanza wataanza kuitawala dunia!
Mafarisayo walimuulizauliza: Ufalme wa Mungu utakuja lini? Na Yesu aliwajibu juu ya Ufalme wa Mungu kuwa UPO NDANI YAO – wala hauji kwa kuuchunguza chunguza! Tunasoma hivi:
20Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; 21wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu. Luka 17
Ukweli huu wa kiroho kuhusu Ufalme haukueleweka kwa Israeli kama vile leo usivyoeleweka sana wka Kanisa.
Bwana Yesu alipoulizwa na Pilato kuhusu UFALME WAKE Yesu, Bwana alimjibu wazi kuwa kwa sasa Ufalme wake sio wa hapa duniani:
33Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi? 34Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? 35Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?
36Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. 37Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.
38Pilato akamwambia, Kweli ni nini? Naye akiisha kusema neno hilo akawatokea Wayahudi tena, akawaambia, Mimi sioni hatia yo yote kwake.
Bwana Yesu alimwambia nini Pilato? Alimwambia kuwa Yeye ni Mfalme ambaye bado Ufalme wake halisi haujaja. Sasa ni Ufalme wa Mbinguni unaoonekana, na Ufalme wa Mungu upo ndani ya watu!
Hebu, kwa mfano, tazama alivyomjibu mtu mmoja siku moja (Luka 12):
13Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu.14Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?
(Yohana 8): 15Ninyi mwahukumu kwa kufuata mambo ya mwili; mimi simhukumu mtu. 16Nami nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli; kwa kuwa mimi si peke yangu, bali ni mimi na yeye aliyenipeleka.
Hata wakati mwingine walitaka kumfanya awe Mfalme, akakataa. Tunasoma hivi (Yohana 6):
14Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.15Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.
Iko siku Ufalme wake utakuja – yaani Ufalme wa mbinguni na falme zote za duniani vitakuwa ni Ufalme mmoja, Ufalme wa Mungu – Ufalme wako uje!:
15Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele. Ufunuo 11
10Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Ufunuo 12
Siku moja inakuja – asubuhi ya milele, wakati Haki itakapomiliki duniani kwa sababu Ufalme wa Mungu utakuwa unatawala maisha wa duniani huku. Biblia inatufundisha hivi:
44Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. Danieli 2
13Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. 14Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. Danieli 7
Na tena:
13Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, 14kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; 15ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; 16ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina. 1Timotheo 6
Wanafunzi wa Yesu walijua yakini kuwa:
1.      Ufalme wa Mungu uko ndani yao.
2.      Ufalme wa Mbinguni haujaja kwa nguvu kati yao. Wakamuuliza Bwana kuwa huo Ufalme wa Mbinguni utakuja lini? (Mdo 1:6-10). Labda walikuwa na maana juu ya Ufalme wa Mbinguni ambao umekuwa ni wa Mungu kwa maungamo na kwa madhihirisho.
Bwana akawaambia wazi kuwa hiyo sio kazi yao kuyajua hayo majira wala nyakati ambazo Baba ameweka katika mamlaka yake mwenyewe! Bwana akawaambia kuwa wakati wanasubiri majira ya Baba, wahubiri juu ya Ufalme wa Mungu ndani ya mioyo ya wanadamu – yaani Haki ipatikanayo kwa Imani katika Yesu Kristo, ambaye hapo baadae atakuja kuuleta Ufalme wa Mungu duniani – yaani Mbingu zitatawala duniani.
Wakati fulani Paulo alifundisha kuwa: “17Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 18Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu.” Warumi 14
Baadhi ya viongozi wa dini ya Kiyahudu hawakupenda kabisa Bwana Yesu atawale juu yao. Tangu mwanzo Shetani na mawakala na wafuasi wake hawakutaka (na hawataki) dunia itawaliwe na Mbingu za Mungu! Ndio maana walimkataa Yesu kuwa Mfalme wao – wakampenda Kaisari zaidi ya Yesu. Na kwa kweli walimpenda mnyang’anyi na muuaji – Baraba, badala ya Yesu (Yohana 19:12-15 na Luka 23:2 Mathayo 27:15-23).
Bwana Yesu alitoa unabii kuhusu Israeli kumkataa kabisa kama Mfalme wao na Masihi. Katika Luka 19:11-27 Bwana anatoa mfano huu kwa sababu walikuw anakaribia Yerusalema, na kuwa Wayahud walidhani kuwa Ufalmewa Mungu ungelwa Mungu ungelitoitokea mara (Mst 11). Mfano huu unasema:
12Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi. 13Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja. 14Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale15Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. 16Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. 17Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi18Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida. 19Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano20Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.21Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.22Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda; 23basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake? 24Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi. 25Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi. 26Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho. 27Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu. (msisitizo ni wangu)
Bwana Yesu ndiye aliyekwenda / amekwenda hadi sasa – Mbinguni “nchi ya mbali” kuupokea (Ufalme wa Mungu) na kurudi – ATARUDI.
Wenyeji wa mji wake walimchukia. Hawa hayumkiniki ni Wayahudi waliomkataa! (Yohana 1:12)
Aliporudi aliugawa Ufalme kwa miji kwa wale waaminifu (Bwana atakaporkwa miji kwa wale waaminifu (Bwana atakaporudi ataugawa Ufalme wake kwa wale waliokuwa waaminiflme wake kwa wale waliokuwa waaminifu)
Adui zake – yaani wale ambao walimkataa aliwaadhibu: “Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.” Bwana atakaporudi pia atafanya hukumu kwa wale wote waliomkataa!
Bwana Yeu atakaporudi mara ya pili (kumbuka sikusema “atakapokuja mara ya pili” kwa makusudi) kama Mfalme, Mkuu wa Vita na Simba wa Yuda, tutagundua tofauti kuu sana na ile ya kwanza alipokuja kama Mwana Kondoo wa Mungu, mpole na mnyenyekevu sana!
Alipokuja mara ya kwanza ALICHINJWA, akamnunulia Mungu, kwa Damu yake, “watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,” akawafanya “kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi” – Ufunuo 5:9-10
Mpendwa, Kumiliki juu ya nchi kunakuja kwa hakika sana, tukiendelea kuwa waaminifu kwa Bwana aliyesafiri.
Bwana ali[okuja mara ya kwanza alituacha tujenge UFALME WA MUNGU ndani ya mioyo ya watu na kujenga mazingira hayo kwa kujenga Ufalme wa Mbinguni duniani – yaani Kanisa! Kila anayeupokea Ufalme huu anaokoka na uharibifu ulioko duniani kwa sababu ya tamaa (2Petro 2:4), na kuwa sehemu ya huo Ufalme ambao Biblia inauita UFALME WA KIKUHANI (1Petro 2:9).
Iko siku Bwana Yesu atakuja duniani kama Mfalme wa Ufalme wa Mungu duniani.
Tukisoma Injili zote tunagundua kuwa Bwana alipokuwa duniani alihubiri jumbe mbili kubwa tofauti
1.      Kwa Wayahudi walioahidiwa Ufalme wa kisiasa, alihubiri Ufalme wa Mbinguni (Math 4:17). Ni Ufalme ambao hata Yohana aliuhubiri (Math 3:2)Mitume nao waliambiwa wahubiri vivyo hivyo (Math10:7): Tubuni kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia
2.      Kwa wanadamu wote kwa ujumla – Wayahudi na Mataifa – Bwana alihubiri Ufalme wa Mungu kuwa unakuja. Tazama kwa mfano Marko 1:14-15: Tubuni na kuiamini Injili!
Kama mara tano tu Mathayo anasema kuhusu Ufalme wa Mungu (Math 6:33, 12:28, 19:24, 21:31&43. Marko yeye anasema mara 15. Tunajua kuwa kuna sehemu ambazo Ufalme wa Mungu umetajwa kama Ufalme wa Mbinguni na kinyume chake – kama Mathayo 18:3 na Marko 10:14, Mathayo 13:24 na Marko 4:28, Mathayo 11:12 na Luka 16:16
4.      TOFAUTI ZA MITAZAMO YA WAINJILISTI KATIKA INJILI
Injiili zote nne (4) katika Biblia, zinamtazama Bwana Yesu kwa sura mbalimbali, labda pia kwa sababu Mungu aliwaandaa waandishi wake kwa jinsi mbalimbali pia.
Marko na Luka hawakuwa wanafunzi (Thenashara) wa Yesu. Wao walisikia habari za Bwana Yesu kutoka kwa wale waliotembea naye, nao wakaandaa kumbukumbu kadhaa simulizi kumhusu Yesu. Luka, kwa mfano, anasema (Luka 1):
1Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu, 2kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, 3nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu, 4upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa.
Yohana na Mathayo ndio waandishi pekee wa Injili ambao walikuwa wanafunzi wa Yesu.
Yohana anamtafakari Yesu katika ukiroho zaidi. Namhudhurisha kwa wasomaji wake kama Mchungaji Mwema, Njia, Kweli, Uzima, Mkate wa Uzima, Maji yaliyo hai, Neno la Mungu, Nuru, na kadhalika. Injili yake imejaa ukweli kuwa Yesu Ni Mwana wa Mungu, Mwokozi wa ulimwengu (Yohana 20:30-31).
Mathayo (au Lawi) aliitwa kuwa mwanafunzi wa Bwana Yesu akiwa mtoza kodi. Walikutana na Bwana Yesu forodhani (Mathayo 9:9, Luka 5:29). Bwana alipomwita, aliacha kazi yaek ya kutoza kodi akamfuata.Mathayo anamtazama Yesu kama Mpango wa Mungu kwa Israeli uliotimizwa, na mpango wa Mungu kwa mataifa pia.
Akiandika Injili anajenga hoja ya siri ya Mungu kwa dunia. Hoja hii inaanza na kumfunua Yesu kuwa Yeye Ndiye Mfalme aliyeahidiwa kwa Israeli. Hebu sasa kwa kifupi tuone anavyojenga hoja hii:
Mathayo Sura1
Mathayo anaelezea ukoo wa Yesu ili kuonyesha kuwa huyu mtoto Yesu NDIYE Mtoto wa Kiume aliyetabiriwa, atakayemiliki katika Kiti cha Enzi cha Daudi (Isaya 7:17)
Mathayo Sura2&3
Anaonyesha Ushahidi wa Ufalme wake unaokuja – yaani:
a.      Mamajusi wa Mashari(Mst 11) – Linganisha na Ushuhuda wa Wakuu wa Makuhani na Waandishi (Mathayo 2:4,5, na Mika 5:2)
b.      Ubatizo wake pale Yordani na amdhihirisho mbalimbali (Mathayo 3:16-17): “Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye”
Matokeo yake?
Herode (M-edomu, kizazi cha Esau) akatamani kumuua – na Mungu akamuokoa.
Mathayo Sura 5-7
Baada ya ubatizo na Majaribu, Bwana Yesu anatoa sasa kanuni za Ufalme wake ujao – katika “Hotuba ya Mlimani”
Hizi ni kanuni ambazo zimejaa maadili na uadilifu katika Ufalme wa Mungu ujao.
Mathayo Sura 8-10
Baada pia ya Ubatizo, Bwana anafanya miujiza mingi inayomdhihirisha kuwa Yeye ndiye Mfalme ajaye.
Kwa mara ya kwanza watu wanafunguliwa dhidi ya mateso ya pepo na magonjwa. Katika historia ya mwanadamu, kwa mara ya kwanza, pepo wanawatoka watu!
“Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.” – Mathayo 4:24
1.      Wenye ukoma wakatakaswa
2.      Mtoto wa akida akaponywa
3.      Mama mkwe wa Petro akaponywa homa
4.      Bwsana akatuliza mawimbi ya bahari
5.      Mgerasi mwenye pepo akaponywa
6.      Wenye kupooza wakaponywa
7.      Binti wa miaka 12 akaponywa
8.      Mama aliyetokwa damu kwa miaka 12 apaponywa
9.      Vipofu wakapata kuona tena
10.  Viziwi na bubu wanafunguliwa
“Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.” Mathayo 8:16-17 (Mathayo 9:31ff)
1Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. 7Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. 8Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.” – Mathayo 10
Matokeo yake?
Tangu wafadhaike alipozaliwa hadi ajifunue kwa Israeli, wakuu wa Israeli walichochea watu kukataa ushahidi wowote kuwa Bwana Yesu NDIYO Masihi na Mfalme aliyetabiriwa!
Ni muhimu sana kujua kuwa katika sura ya 10 Bwa aliwatuma Mitume wake 12 wakahubiri kwa Israeli tu. Aliwaamuru:
*        Wasiingie kwa mataifa
*        Wasiingie kwa walio machotara wa mataifa na Waisraeli – yaani Wasamaria
*        Watafute tu Waisraeli waliopotea
*        Wakatangaze kuwa Ufalme wa Mbinguni umekaribia (Mstari 5-7)
Mathayo Sura11
Bwana Yesu anakataliwa rasmi kuwa Mfalme na Masihi kwa Israeli. Ni katika sura hii tunasikia kwa mara ya kwanza makemeo ya miji ale ambayo Bwana alifanya miujiza mingi – miji ya Korazini, Bethsaida na Kapernaumu (Mathayo 11:21-25)
Mathayo Sura12
Sura hii ni kama Mafarisayo wanafikia kiwango cha juu cha kukataa umasihi na ufalme wa Bwana Yesu. Wanadai kuwa anatoa pepo kwa Belzebuli, mkuu wa pepo (Math 12:24).
Mpango wa Mungu ulikuwa wazi tu – yaani kuinua Israeli kama Taifa la Mfalme, ili dunia ibarikiwe KUPITIA WAO.
*        Israeli wakakataa mpango huu
*        Israeli wakakataa Ufalme wa Mungu katikati yao.
Mathayo Sura13
Sura 13 ya Mathayo inaanza na
*        Somo jipya kabisa
*        Mbinu mpya kabisa za kuelezea mambo ya mbinguni, na za kufundishia.
Kabla ya hapo, Bwana Yesu alitumia vielelezo (illustrations). Kuanzia sura ya 13 Bwana anaanza kutumia mifano (parables). Wakati yaonyesha kuwa vielelezo vilikuwa na nia ya kumdhihirisha Bwana katika Israeli, mifano inakuwa na nia ya kuufunua ukweli kwa wake wanaoamini tu, na hata kwa hao ilimpasa Bwana kuwaeleza maana zake. Mifano ilikuwa ni kama vitendawili vyenye viashiria vya maana zake.
Toka sura ya 13 na kuendelea, kila alipozungumza na wasioamini,Bwana alitumia mifano.

5.      MPANGO WA KUMILIKI DUNIA KUPITIA ISRAELI UNAAHIRISHWA
Mpango wa Mungu hauwzi kutotimia kamwe. Kuna ushahidi kwenye Biblia kuwa mpango wa Mungu waweza kuahirishwa hadi baadae.
Katika Agano la Kale Mungu aliwahi kuahirisha kusudi na mpango wake kwa Israeli pale Kadeshi-Banea. Tunasoma haya katika Kumbukumbu 1 na Hesabu 12-14.
Hesabu Sura 12 (Hazerothi)
*        Miriamu na Haruni wanampinga Musa kwa sababu ameoa mwanamke Mkushi. Mungu anampiga Miriamu kwa ukoma, na kuelesa jinsi anavyojifunua kwa wanadamu
Hesabu Sura 13 (Mst 3,36 – Parani)
*        Musa anatuma wapelelezi kuipeleleza Kanaani
*        Wapelezi wanarudi kwa Musa (Mst 26) kutoa taarifa
*        Wapelelezi wanaleta taarifa mbaya kwa wana wa Israeli na luwakatisha tamaa sana (Mst 28-33)
Hesabu Sura 14
*        Sura hii inafunua uasi mkuu kwa Israeli (Mst 1-10)
*        Mungu anaamua kuwaangamiza wote (Mst 11-12)
*        Musa anawaombea neema kwa Mungu (Mst 13-19)
*        Mungu, kwa neema yake anawasamehe (Mst 20-21)
*        Mungu anaahirisha mpango wa kuingia Kanaani kwa Israeli kwa kizazi kile (Mst 22-23)
*        Mungu anaamuru miaka 40 ya kutangatanga jangwani – yaani mwaka 1 kwa kila siku 1 ya upelelezi (Mst 26-35)
*        Watu wanatubu na kuasi hapohapo (Mst 39-45 cf Kumb.1:40-45)
Mpango wa Mungu lazima utekelezeke!
Ni muhimu sana kujua kuwa jambo lolote lililo dharura kwa wanadamu liko katika mpango kamili wa Mungu. Ni muhimu sana kujua, kwa mfano, kuwa Kutataliwa kwa Yesu, Kuuawa kwa Yesu, Kifo cha Yesu, Ufufuo wa Yesu, na Utawala wake – vyote vilikuwa na ni muhimu sana katika mpango mzima wa wokovu wetu (Mdo 3:13-26).
6.      SURA YA 13 INAYO MIFANO SABA – 7 –  KUHUSU SIRI ZA UFALME
Sura ya 13 inayo mifano saba ya muhimu sana kujifunza kuhusu Ufalme wa Mbinguni.
Mfano 1: Mfano wa “Mpanzi”:
3Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda.  4Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; 5nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; 6na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka. 7Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga; 8nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini. 9Mwenye masikio na asikie.
Mfano 2: Mfano wa “Ngano na Magugu”
24Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; 25lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. 26Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. 27Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema atika konde lako? Limepata wapi basi magugu? 28Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? 29Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.30Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
Mfano 3: Mfano wa “Punje ya Haradali”
31Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; 32nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.
Mfano 4: Mfano wa “Chachu Ndani ya pishi Tatu”
33Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia.
Mfano 5: Mfano wa “Hazina iliyositirika”
44Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.
Mfano 6: Mfano wa “Lulu Nzuri, Moja ya Thamani Kubwa”
45Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; 46naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.
Mfano 7: Mfano wa “Juya Lililotupwa Baharini”
47Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna;48hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.
Ni Mathayo peke yake anayeelezea mifano yote saba. Mifano ya “Mpanzi” na “Haradali” pia hupatikana katika Injili za Marko 4:1-9,13-20, 30-32 na Luka  8:5-15.
Mfano wa “Chachu” pia hupatikana katika Injili ya Luka 13:20-21
Wanafunzi wa Yesu walipomuuliza juu ya mifano – kwa nini ameamua sasa kutumia mifano badala ya vielelezo, ndipo aliposema maneno yale makuu: NINYI MMEJALIWA KUZIJUA SIRI ZA UFALME (Mathayo 13:11).

7.      LAKINI SIRI  NI NINI?
Kabla hatujapita kuzipeleleza Siri za mifano ya Bwana katika Mathayo 13 na pengine, hebu tujaribu kujibu swali hili:SIRI NI NINI?
Siri (mystery) katika Agano Jipya (AJ) ni Ukweli ambao haukuwa dhahiri katika Agano la Kale (AK), bali umefunuliwa katika AJ kwa Watakatifu.
Tunasoma hivi katika Wakolosai 1:26: “siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake”.
NA katika Waefeso 3 tunasoma: “5Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho”
Kulingana na maelezo hayo hapo juu, Siri inazo sifa kuu mbili:
1.      Ukweli ambao ulifichwa na haukuwa dhahiri katika Agano la Kale
2.      Ukweli uliofunuliwa katika Agano Jipya kwa Watakatifu.
Sio lazima Siri iwe jambo gumu kulielewa – hasha! Ni ukweli unaoeleweka vyema kwa kufafafnuliwa.
Kwa mfano, Agano la Kale linasema wazi juu ya Ujio wa Kristo na kutawala katika Kiti cha Enzi cha Daudi – huu ukweli sio wa kificho.
Katika Mathayo 13 na kwingineko tunasoma juu ya Ufalme wa Kiroho anaotawala Yesu wakati Yeye yuko Mbinguni, yaani kabla ya Yeye kurudi mara ya pili kutawala.
Hivyo Siri za Ufalme Ufalme zinahusiana na kipindi katikati ya ujio wake wa kwanza na ule wa pili – na sio utawala wake wa miaka 1000 akirudi mara ya pili. Bwana katika hekima yake ameamua kutufunulia sisi kwa Roho.
6Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;  8ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu; 9lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. 10Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 11Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. 12Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. 13Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. – 1Wakorintho 2
SIRI ZA UFALME WA MUNGU
Bwana Yesu anawaambia wanafunzi wake kuwa wamejaliwa kuzijua SIRI ZA UFALME WA MUNGU – yaani akili na ufahamu wao vimefahamu wao vimefunguliwa ili wajue. Unajua inamgharimu Mungu kwa Roho wake kutufungua tujue hata maandiko ndani ya Biblia. Tunawajua akina Kleopa waliokutana na Bwana Yesu wasimjue hadi akili zao zilipozibuliwa!
25Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!26Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? 27Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe. 28Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele. 29Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao.30Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.31Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. 32Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko?  – Luka 24
Ziko siri nyingi za Ufalme wa Mungu, bali zile zilizofunuliwa kwetu zinatokana na huyu Yesu. Tunasoma hivi katika Neno:
2ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo; 3ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.- Wakolosai 2
Katika Mathayo 16:17 Bwana Yesu akizungumza kumhusu Simon mwana wa Yona anasema: “…Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.” Au kwa lugha nyingine anamwambia kuwa yeye amefunuliwa Siri – Kristo – yaani sio Kristo Mwana wa Daudi tu, bali Mwana wa Mungu!: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai”.
Katika Mathayo 16 Bwana Yesu anataja Siri ya ajabu sana  – yaani:
1.      Uahirishwaji wa Ufalme kwa Israeli – na anampa Simoni (Labda Mnaftali toka Bethsaida, sio M-Yuda toka Bethlehemu) majukumu makuu ya ukuu: “18Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.”
2.      Usimikwaji wa Masihi kwa ungamo la Petro: Kristo (yaani Mpakwa Mafuta, yaani Masihi) Mwana wa Mungu aliye hai
3.      Uanzishaji wa “Taifa jingine” (Mathayo 21:43), taasisi mpya iitwayo Kanisa: “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda”.
·         Hii ni taasisi yenye ushindi
·         Hii ni taasisi inayojenga Ufalme wa Mbinguni na kuuleta Ufalme wa Mungu – kwanza kwa Israeli na kwa mataifa yote.

8.      NDANI YA YESU UMESITIRIKA MPANGO WOTE WA MUNGU
Hebu sasa turudi nyuma kidogo kwenye maandiko tuuone unabii kuhusu mpango mzima wa Mungu na jinsi ulivyo kupitia Yesu.
KUIBARIKI DUNIA KUPITIA ISRAELI
Kupitia Israeli, Mungu alitamani sana kuibariki dunia kwa ahadi au maagano mawili makubwa Mungu aliyoweka na Ibrahimu.
AHADI / AGANO 1: Ahadi / Agano la kubariki dunia kupitia Abramu (Kumbuka sikusema Ibrahimu, kwa sababu alikuwa hajabadilishwa jina na alikuwa hajatahiriwa. Alikuwa badi sio baba wa mataifa yote!) – Mwanzo 12:3
Ahadi au agano hili ni kwa sababu ya uteule wa Abramu
AHADI / AGANO 2: Ahadi / Agano la kujibariki (kulingana na Union Version Bible) – Mwanzo 22:18 (kumbuka Mwanzo 26:4 – Isaka – ahadi kwa Israeli ya kumiliki nchi, na dunia kubarikiwa!)
Ahadi au agano hili ni kwa sababu ya UZAO (sikusema Wazao bali Uzao) wake – yaani uzao wa Ibrahimu.  Katika Wagalatia 3 tunasoma: “Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo.”
Ndani ya Ibrahimu Mungu tayari alikuwa na Masihi, Mwokozi wa dunia. Mungu katika hekima yake akamchagua Isaka – na sio wale watoto wengine wa Ibrahimu. Ibrahimu alipata neema kuwa na watoto nane. Ismaeli – mtoto wa Hajiri (aliyemzaa akiwa na umri wa miaka 86), Isaka – mtoto wa Sara (aliyemzaa akiwa na miaka 99). Baada ya Sara kufa, Ibrahimu alimuoa mwanamke aitwaye Ketura (Mwanzo 25:1-6) akamzalia watoto 6, yaani Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Sua.
Inawezekana pia kuwa Ibrahimu, kwa kuwa ni baba wa mataifa mengi, alikuwa hivyo kupitia kwa watoto hawa – yaani Waisraeli, Waishmailia, Waedomu kupitia kwa Esau (Mwanzo 25:12-18), Waamaleki kupitia kwa mjukuu wa Usau (Mwanzo 36:1-40), Wakenazi kwa Esau huyuhuyu(Mwanzo 36:12-16). Wamidiani kupitia kwa Midiani, mtoto wa Ibrahimu, na Waashuru kupitia kwa Yokshani (Mwanzo 25:1-5).
Ndani  ya Isaka Mungu akawa na Mwokozi wa dunia. Mungu akamchagua Yakobo (baadae Israeli) na sio Esau.
Ndani ya Israeli Mungu alikuwa na mwokozi wa Dunia – yaani Yesu. Mungu akamchagua Yuda. Katika Mwanzo 49:10 Biblia inaitaja “Fimbo ya Enzi” ambayo “haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.” Mungu hakuwachagua wengine 11!
Ndani ya Yuda, Mungu alimwona Daudi aliyefanywa kuwa mfalme wa pili wa Israeli. Mungu akafanya naye Agano la milele la ufalme wake – Biblia inaliita “Agano la Chumvi”
Hesabu 18:19 – “Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa Bwana, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za Bwana kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe.”
Walawi 2:13 – “Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.”
2Nyakati 13:5 – “je! Haikuwapasa kujua ya kwamba Bwana, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa agano la chumvi?”

YESU NI MWANA WA DAUDI
Yesu alipodhihirishwa duniani, alijulikana kama ‘Mwana wa Daudi’. Hatujui kuwa wazo hili la ‘Mwana wa Daudi’ lilijengwaje ndani ya watu kwa sababu kila alipopita – Yudea, Samaria hata nje ya mipaka ya Uyahudi, watu walishuhudia kuwa Yeye ndiye ‘Mwana wa Daudi’ waliyemtarajia. Naamini ni Roho wa Mungu aliliweka ndani yao!
Haikuhitaji watu kufundishwa kuwa Yesu ni nani! Wote walimjua kuwa Yeye ni Mwana wa Daudi! Hadi mbali sana, mipakani mwa Tiro na Sidoni, kwa Wakananayo, Yesu alijulikana hivyo hivyo – Mwana Daudi!Math.15:21-22: “Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.”.
Kumbe ndiyo maana unabii kuhusu Agano Jipya kwa Israeli unasema kuwa Israeli “hawatafundishana kila mtu na jirani yake, na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana, kwa maana wote watanijua, tangu mdogo wao hata mkubwa wao…” (Waeb.8:11).
Huyu ndivyo alivyofunuliwa. Ndivyo alivyo hadi milele. Katika Ufunuo wa Yohana alionekana hivyo, Mwana wa Daudi, Mfalme! Malaika alishuhudia kuwa yeye Yesu anao “Ufunguo wa Daudi” Uf.3:6-8.  Yeye ni “Simba aliye wa Kabila la Yuda, Shina la Daudi”.
Katika Uf.5:4-6 tunasoma:
Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba. Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.
Huu ni ushuhuda wa wale Wazee wa mbinguni. Yesu mwenyewe anashuhudia kuwa yeye ndiye “Shina la Mzao wa Daudi”  Uf.22:15-17.
Nia ya Msingi ya wokovu wa Mungu ilikuwa ni kuiokoa dunia kupitia Israeli!
Yesu alipofunuliwa aliendelea kukiri kuwa huduma yake ni Israeli – “Kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” Math. 10:5-7. Hata alipotakiwa na wanafunzi wake afanye muujiza wa kumponya mtoto wa mama kule katika mipaka ya Tiro na Sidoni, Yesu alisema wazi kuwa wito wake wa msingi sio mataifa – la! Ni Israeli!
23Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. 24Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 25Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie. 26Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. 27Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao. 28Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile. Math.15

LAKINI ISRAELI WALIKATAA
Mara nyingi Yesu alitahadharisha hatari ya Israeli kutojali nafasi ya uteule wao waliyopewa. Tena aliweka bayana kuwa Mungu anaweza kabisa kuahirisha  hata kubadilisha uteule wao.
Kwa tahadhari hiyo, Bwana Yesu alitoa mfano katika Luka 14:16-24, mfano wa bwana mmoja aliyefanya karamu lakini walioalikwa walitoa udhuru kwa nia moja.
16Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,  17akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.8Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. 19Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. 20Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.21Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo..
Walioalikwa walipoamua kwa sababu zao kutofika, nafasi ilitolewa kwa wale waliokuwa hawakualikwa mwanzo.
Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. 22Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi. 23Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. 24Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.””.
Katika Math.22:2-14 tunasoma zaidi habari ya wale waliokuwa wamealikwa mwanzo:
2Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi. 3Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja arusini; nao wakakataa kuja. 4Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng’ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini.
5Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake; 6nao waliosalia wakawakamata watumwa wake, wakawatenda jeuri, na kuwaua. 7Basi yule mfalme akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.
8Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili. 9Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini. 10Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni.
11Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi.12Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa. 13Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 14Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.
Unaona? Neno linasema kuwa wale walioila ile karamu ni wale waliotoka “katika njia kuu na vichochoro vya mji”. Ni wale walioshurutishwa kuingia ndani ili nyumba ya Bwana ipate kujaa. Ndipo Yesu akasema: “Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana mmoja atakayeionja karamu yangu” Luka 14:24. Maneno makuu sana, maneno ambayo wahubiri wengi hata leo hawataki kuyasikiliza kabisa. Bwana akisema “katika wale walioalikwa, hapana mmoja atakayeionja karamu yangu”, ana maana ileile!
Walioalikwa, hatuna shaka, ni Israeli. Ndio waliofanyiwa sherehe, wakatoa udhuru kila mmoja. Aina ya upinzani Yesu aliokutana nayo katika huduma ulikuwa mkubwa. Wakati fulani alitamka `ole’ nyingi sana kati ya viongozi wa Israeli (Math.23) kisha akatoa unabii juu ya Yerusalemu (Yaani Israeli!): “Kwa maana nawaambia, hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa Jina la Bwana” Math. 23:39.
Nyumba ya Israeli, Yesu alitamka, itaachwa ukiwa, na kweli imeachwa ukiwa! Math. 23:38
Wakati Yesu akiingia Yerusalemu mara ya mwisho kabla ya kuuawa alisema maneno haya magumu kwa machozi:
Laiti ungalijua hata wewe, katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.  Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakujengea boma, likuzunguke, watakuzingira na kukuhusuru pande zote, watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako. Wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako – Luka 19:41-44.

Labda ni hekima tukagusa kidogo juu ya Israeli kumkataa Bwana.
Katika Injili ya Yohana (Yoh. 1:11) tunasoma wazi kuwa Yesu alipokuja kwake, walio wake hawakumpokea. Katika Yoh.5:43 Yesu anasema wazi kuwa yeye amekuja kwa Jina la Bwana, na hawampokei! Ndiyo maana Yesu alipokuwa  anaingia Yerusalemu kama Mfalme  aliulilia mji ule mtakatifu (Luka 19:41-44) – kuwa laiti  wangalijua juu ya siku ile aliyoingia Yerusalemu, juu ya yapasayo amani. Ole wa Yerusalemu kwa sababu hawakujua majira ya kujiliwa kwake!
Yeremia  ni nabii wa ajabu aliyeona Mungu akikumbuka hukumu ya Israeli kwa sababu ya kumkataa Masihi wao. Katika (Yer.30:4-11) tunaona juu ya mateso kwa Israeli.
Na haya ndio maneno alivyosema BWANA, katika habari za Israeli na habari za Yuda. Maana BWANA asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko na hofu, wala si ya Amani. Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanaume aona utungu wa uzazi; mbona basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye na utungu, na nyuso zote zimegeuka rangi? Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hakuna inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.
Yesu hakuacha kutahadharisha Israeli juu ya jambo hili. Katika Math. 21:33-43 Yesu ananukuliwa akitoa unabii wa ufalme kutolewa kwa Israeli na kupewa  mataifa mengine (`taifa lingine’ – Swahili Union Version).
33Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. 34Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake.
35Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe. 36Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile. 37Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. 38Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. 39Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua.
40Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima?
41Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.
42Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu? 43Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. kuzaa matunda yake.
Yesu alipotoa tuhuma nyingi za waandishi wa sheria ya Musa na waamini wa dhehebu la Wafarisayo katikaMath.23, anasema juu ya mji uliopendwa. “Ee Yerusalemu Yerusalem…. angalieni nyumba yenu mmeachwa hali ya ukiwa. Kwa maana nawaambia hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema ‘amebarikiwa ajaye kwa Jila la Bwana’”. Math 23:37-39
Kalvari  ikawa ndio mwisho wa nyumba ya Israeli mpaka kipindi cha baadaye. Mpango wa Israeli ukaahirishwa!
MAJUMA 70 YA DANIELI 9:20-27
Ni muhimu sana kukumbuka kuwa unabii kuhusu Israeli kumkana Mwokozi ulitolewa na manabii wengi. Mmoja aliyetaja sana jambo hili ni Danieli. Danieli 9 ni unabii unaohusu mpango wa Mungu kubariki mataifa kupitia Israeli pamoja na matokeo yake.
Katika sehemu hii malaika anamwambia Danieli: “Muda wa majuma sabini umeamuriwa juu ya watu wako na juu ya mji wako mtakatifu” – yaani watu wa Danieli – Israeli, na mji mtakatifu – yaani Yerusalemu. Hii ni amri kwa watu wa Israeli. Muda huu ni majuma 70  kiunabii au miaka mia nne na tisini (490). Kanuni hii ya “sabato ya miaka” inatajwa katika Walawi 25:3-4.
24Majuma sabini yameamriwa kwa ajili ya watu wako na kwa ajili ya mji wako mtakatifu ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, kuleta haki ya milele, kutia muhuri maono na unabii pia kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu sana. 25Ujue na kuelewa hili: Tangu kutolewa kwa amri ya kuutengeneza na kujenga upya Yerusalemu mpaka kuja kwa Mpakwa mafuta, aliye mtawala, kutakuweko majuma saba na majuma sitini na mawili. Barabara zitajengwa tena pamoja na mahandaki, lakini katika wakati wa taabu. 26Baada ya majuma sitini na mawili Mpakwa mafuta atakatiliwa mbali wala hatabakia na kitu – Danieli 9
Katika muda huu, malaika anasema kuwa mambo yafuatayo yatatokea:
1.      Kukomesha makosa
2.      Kuishiliza dhambi
3.      Kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu
4.      Kuleta haki ya milele
5.      Kutia muhuri maono na unabii
6.      Kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu
Mtiririko wake ni mrahisi tu. Mwanzo wa miaka 490 tunasoma wazi kuwa ni tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kujenga upya Yerusalemu – yaani kipindi cha mfalme Artashasta kule Babeli. Twajua kuwa amri hii iliwekwa tarehe 1 mwezi wa Nisan mwaka 445KK, mfalme alipomruhusu Nehemia aende Yerusalemu aujenge (Nehemia 2).
Miaka 483 (majuma saba na majuma sitini na mawili = majuma 69) baadaye unabii ulitimia. Ni kweli, Masihi alikatiliwa mbali – kwa sababu unabii ulisema kuwa “Masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu”. Kikalenda, hili ni lile juma walilomwimbia Yesu “Hosana Mwana wa Daudi” – akiingia Yerusalemu, na siku chache wakamuua (Luka 19:37 na kuendelea).
Majuma 69 ya Daniel yakakoma hapa, likabaki juma la 70, kwa sababu “Muda wa Majuma sabini umeamuriwa juu ya (Israeli) na juu ya mji wa Yersalemu” – Dan. 9:20-27.
Utaona wazi kuwa kati ya majuma 69 na 70 bado juma moja, na kipindi kile cha juma moja kikaahirishwa. Hapo ndipo kipindi cha Kanisa kikaingia katikati.
Baada ya “Kukomesha makosa” na “Kuishiliza dhambi” na “Kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu”, bado “Kuleta haki ya milele”, “Kutia muhuri maono na unabii”, na “Kumtia mafuta yeye aliye Mtakatifu”.
Tunashangaa sana sasa na kuelewa kwa nini unabii wa Isaya katika Isaya 61 unatimia Mstari 1-2a tu. Tunayaona haya kwa Yesu mwenyewe akisoma gombo la chuo pale hekaluni siku ya kwanza ya huduma yake hekaluni hivi:
16Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 17Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, 18Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
20Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21Akaanza kuwaambia, ‘Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.’ – Luk 4:16-21 (linganisha na Isaya 61:1-2).
Pia tunaona kuwa unabii wa Yoeli (Yoeli 2) ukatimia mstari 28-29 tu. Tunajua kuwa bado 30-32.
Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu, wanaume kwa wanawake, watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.  Naam, hata watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, nitawamiminia Roho wangu, siku zile, nao watautangaza ujumbe wangu. Nitatenda miujiza juu angani, na ishara chini duniani; kutakuwa na damu, moto na moshi mzito; jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya kutokea ile siku kuu na tukufu ya Bwana. Hapo, yeyote atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.  Mdo 2:17-21
TAASISI NYINGINE INAANZA – “TAIFA” JINGINE
Yesu aliagiza: “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili” (Math. 28:19, 20 na Marko 16:15-16). Hii ni baada ya kuwaagiza kuwa katika njia ya mataifa wasiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria wasiingie; na kuwa afadhali wafuatilie kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Math. 10:5, 6). Je, utume wa Bwana umebadilika?
Mitume wakidhani kuwa Israeli wangelishituka wageuke, walianza kuhubiri kwa nguvu Yerusalemu kwa Waisraeli.
Lakini  Yesu aliwaambia kuwa sasa waanzie Yerusalemu – Uyahudi wote, Samaria  na hatimaye, mwisho wa nchi. Tunasoma:
6Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme? 7Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. 8Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi (miisho ya dunia).  Mdo 1:6-8.
Mitume walidhani, kwa ushahidi wa mahubiri yao, kuwa maeneo yote hayo – Yerusalemu, Uyahudi kote na Samaria na hata mwisho wa dunia – ni kuwaleta Wayahudi katika Imani ili Yesu arejee haraka! Mara Petro akahubiri siku ya kwanza Yerusalemu kwa Wayahudi (Waisraeli). Matunda yakawa ya kutisha, wakaongoka watu zaidi ya 3,000 siku ile moja. Baada ya hapo tunasoma katika kitabu cha Mdo 3:17-26 kuwa mkazo wa mahubiri ukawa kuwa watu watubu na kurejea, ili Yesu Mfalme arejee haraka kama Mfalme wao!
Matokeo ya mwendelezo wa Injili ukawa mbaya sana! Wakafungwa gerezani (Mdo 4:1-3) na mateso yakaanza rasmi. Stefano akauawa (Mdo 7-8:3) na mitume wakatawanyika huko na huko.
Lakini jambo lingine la ajabu likatokea: mataifa na wachawi wakaanza kuokoka (Mdo 8:4-40). Mara Sauli – Mbenjamini akaokoka  (Mdo 9), na akapewa naye ufunuo wa kuhubiri injili kuanzia kwa mataifa.
SAULI MJUMBE WA MATAIFA
Wongofu wa Sauli ni muhimu sana kwa Kanisa. Yeye aliwekwa kuwa “chombo kiteule (kwa Mungu) alichukue Jina (la Mungu) mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli” – Mdo.9:15. Mjuzi wa torati huyu hakuamini kuwa aanzie kwa mataifa, bali alianzia Dameski katika Masinagogi.
Matokeo yake yakawa mabaya sana. Wakataka kumuua hadi ndugu wakamtorosha usiku baada ya kupata habari ya njama ile (Mdo 9:23-25). Biblia inasema kuwa Sauli akakimbilia Yerusalemu kwa ndugu. Kule Yerusalemu, akahojiana na Wayahudi wa Kiyunani na kuwafadhaisha sana kwa elimu yake kubwa. Matokeo yake yakawa vilevile – mabaya. Wakajaribu kumuua. Ndugu wakaona vyema wamrudishe Tarso – kwao – na Uyahudi kukatulia! Mdo 9:29-31
Hatimaye, Mungu alimwita rasmi, yeye na Barnaba (Mdo 13:1-3), kwa wito mpya kabisa. Kwa neema ya Mungu wakawaacha Israeli rasmi na kugeukia mpango mpya wa Mungu uitwao Kanisa.
“Hata hivyo, Paulo na Barnaba waliongea kwa uhodari zaidi, wakasema, ‘Ilikuwa ni lazima Neno la Mungu liwafikieni ninyi kwanza; lakini kwa kuwa mmelikataa na kujiona hamstahili uzima wa milele, basi, tunawaacheni na kuwaendea watu wa mataifa mengine. Maana Bwana alituagiza hivi: `Nimekuteua wewe uwe mwanga kwa mataifa, uwe njia ya wokovu kwa ulimwengu wote.’` Watu wa mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi, wakausifu ujumbe wa Mungu; na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uzima wa milele, wakawa waumini”. Mdo 13:46-48
Tunasoma hivi pia katika Mdo 18:1-11:
“ … Walipompinga na kuanza kumtukana, aliyakung`uta mavazi yake mbele yao akisema, ‘Mkipotea ni shauri lenu wenyewe; mimi sina lawama yoyote juu ya jambo hilo. Na tangu sasa nitawaendea watu na mataifa mengine’.  Basi, akatoka hapo akaenda kukaa nyumbani kwa mtu mmoja mcha Mungu aitwaye Tito Yusto. Nyumba yake Tito ilikuwa karibu na lile sunagogi… Wakorintho wengi waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na kubatizwa.  …Basi, Paulo alikaa huko akifundisha neno la Mungu kati yao kwa muda wa mwaka mmoja na nusu”.
Kwa kweli waliwageukia mataifa ili mataifa na wana wa Israeli sasa waingie katika mstakabali mpya wenye taasisi mpya iitwayo KANISA.
Biblia inasema wazi juu ya kundi la Israeli pamoja na mataifa – yaani taasisi iitwayo Kanisa, ikaingia kati ya Majuma 69 na lile la 70 la Israeli. Hii ni siri, Kanisa.
Siri hii walifunuliwa mitume na hasa Paulo. Hebu soma Neno lisemavyo:
3ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache.4Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. 5Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; 6ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili; 7Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake. 8Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; 9na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; 10ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho; 11kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.12Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini. Waef.3.1-12
Tunasoma katika Warumi kuwa ni kweli ugumu umewapata Israeli “mpaka utimilifu wa mataifa uwasili” (Swahili Union version)– na mpango wa Israeli utaendelea, yaani “juma lao la 70” litaendelea.
Ninyi watu wa mataifa mengine, kwa asili ni kama tawi la mzeituni mwitu, lakini mmeondolewa huko, mkapandikizwa katika mzeituni bustanini mahali ambapo kwa asili si penu. Lakini, Wayahudi kwa asili ni kama mzeituni bustanini, na itakuwa jambo rahisi zaidi kwao kupandikizwa tena katika mti huohuo wao…Maana Mungu akisha wapa watu zawadi zake na kuwateua, hajuti kwamba amefanya hivyo. Hapo awali ninyi mlikuwa mmemwasi Mungu, lakini sasa mmepata huruma yake kutokana na kuasi kwao. Hali kadhalika, kutokana na huruma mliyojaliwa ninyi, Wayahudi wanamwasi Mungu sasa ili nao pia wapokee sasa huruma ya Mungu. Maana Mungu amewafunga watu wote katika uasi wao ili apate kuwahurumia wote.  Warumi11:24-32.
Katika  War 9:25-33 tunasoma hivi:
“Maana ndivyo asemavyo katika kitabu cha Hosea: “Wale waliokuwa `Si watu wangu` nitawaita: `Watu wangu!` Naye `Sikupendi` ataitwa: `Mpenzi wangu’! Na pale walipoambiwa: `Ninyi si wangu` hapo wataitwa: `Watoto wa Mungu hai`”. Naye nabii Isaya, kuhusu Israeli anapaaza sauti: “Hata kama watoto wa Israeli ni wengi kama mchanga wa pwani, ni wachache tu watakaookolewa;  maana, Bwana ataitekeleza upesi hukumu yake kamili juu ya ulimwengu wote….”
Tena Paulo anaandika:
18Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. 19Lakini nasema, Je! Waisraeli hawakufahamu? Kwanza Musa anena, Nitawatia wivu kwa watu ambao si taifa, Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhibisha. 20Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema, Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia. 21Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na wakaidi. War 10:18-21
Katika War 11:8-12 anaongeza:
…Basi, nauliza: je, Wayahudi wamejikwaa hata wakaangamia kabisa? Hata kidogo! Kutokana na kosa lao ukombozi umewajia watu wa mataifa mengine, ili Wayahudi wapate kuwaonea wivu.  Kosa la Wayahudi limesababisha baraka nyingi kwa ulimwengu, na utovu wao kwa kiroho umeleta baraka nyingi kwa watu wa mataifa mengine. Basi, ni dhahiri zaidi kwamba utimilifu wao utasababisha baraka nyingi zaidi.
Tangu kipindi hiki cha Kanisa kianze hadi kitakapofikia ukomo, watu wote huingia kwenye kundi liitwalo Kanisa – Israeli kwa mataifa – kwa kumwamini Yesu! Nasema tena,wote – Wayahudi kwa Mataifa! Haya tunasoma katika Waef.3:1-12, kama tulivyoona hapo juu. Watu wote, bila upendeleo huingizwa kwa kumpokea Yesu moyoni!
Katika Wakolosai 1:13-29 tunasoma tena ukweli huu ukijirudia:
“Yeye alituokoa katika nguvu ya giza, akatuleta salama katika ufalme wa Mwanae mpenzi, ambaye kwa njia yake tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa…Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani, nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani Kanisa.  Nami nimefanywa kuwa mtumishi wa Kanisa kufuatana na mpango wake Mungu ambao alinikabidhi kwa faida yenu. Mpango wenyewe ni kuutangaza kwa ukamilifu ujumbe wake, ambao ni siri aliyowaficha binadamu wote tangu milele, lakini sasa amewajulisha watu wake. Mpango wa Mungu ni kuwajulisha watu wake siri hii kuu na tukufu ambayo ni kwa ajili ya watu wote. Na, siri yenyewe ndiyo hii: Kristo yuko ndani yenu, na jambo hilo lamaanisha kwamba ninyi mtaushiriki utukufu wa Mungu… Maneno mazito sana!
Unajua, katika kitabu cha Ufunuo Neno linasema kuwa Yesu anasimama mlangoni anabisha, na ni wajibu wa mtu kufungua mlango na kumkaribisha Yeye. Tena katika Yohana tunapata ukweli kuwa wote waliomkaribisha – yaani waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu – yaani wale waliaminio Jina lake. (Soma Uf 3:20 naYoh.1:12).
Kanisa ni Mwili wa Kristo Mwenyewe. Katika Waef 1:22-23, 5:23 tunasoma:
Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake, akamkabidhi kwa Kanisa akiwa mkuu wa vitu vyote.  Kanisa ni mwili wa Kristo, na ukamilifu wake yeye anayekamilisha vitu vyote kila mahali…  Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya Kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa Kanisa, mwili wake.
Kanisa nalo linajengwa na Yesu mwenyewe.“Nami nakwambia: wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu; wala kifo chenyewe hakitaweza kulishinda” – Math.16:18
Mungu alimsimamisha Paulo kama mjenzi mkuu wa Kanisa. Huu ndio ushuhuda wake katika kuungana na Yesu:
10Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.11Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. 12Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. 13Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. 14Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.”. 1Wakor 3:10 – 14.
Watu wengine wote katika utumishi huliendeleza Kanisa kwa Karama mbalimbali walizokirimiwa na Roho Mtakatifu!  Tazama pia Waef 4:15-16, 1Wakor 12:23-27.
Tumeona kuwa kumekuwa na kuahirishwa kwa mstakabali wa Israeli baada ya kumkataa Masihi, bali kwa kitambo kidogo. Hapo juu tumeona kuwa baada ya “majuma 69”, Mungu alisitisha “juma 1” la sabini kwa kipindi kisichojulikana – na kipindi hiki kinaitwa cha Kanisa. Na katika kipindi hiki ambacho tumekiona kuwa kinaitwa kipindi cha Kanisa, tunajifunza kuwa kitaendelea hadi “utimilifu wa mataifa uwasili”.
Mpendwa, sasa tunavyozungumza, Waisraeli na mataifa ni sawa mbele za Mungu. Siku zinakuja Mungu atakapoanza kushughulikia Israeli kama Israeli – yaani juma la sabini lililoahirishwa!
Kuna watu wanasumbua watu wa Mungu juu ya uteule wa Israeli ya sasa. Hata wanapotaka kwenda kuhiji, sio kuona tu historia ya imani yao bali wanadai kuwa ni ili kuvuna baraka kwa kulibariki ‘taifa la Mungu’. Huu ni uzushu mkubwa! Baraka zetu hazitoki hapo. Tena Taifa la Mungu sasa ni Kanisa, ambalo ndani yake lina Israeli na ‘mataifa’.
Kuna mambo makubwa mawili ambayo lazima kuyajua:
Baraka za mtu aliyempokea Yesu hazipo katika ‘kuwabariki Israeli’. Hiki sio kipindi hicho! Kwa mtu aliyeokoka, AMEBARIKIWA KWA BARAKA ZOTE, ndani ya Yesu. Hivi ndivyo Biblia inavyoshuhudia: “Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo” – Waef.1:3
Katika Yesu Kristo, hakuna tofauti kati ya Myahudi au Myunani, wote ni sawa kabisa mbele za Mungu. Biblia inasema hivi: “Kama yasemavyo Maandiko, ‘Ye yote amwaminiye hatatahayarika’. Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani, Yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao. Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokoka’’ – Warumi 10:11-13.
Katika 1Wakor 1:22-24 tunasoma: “Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu”.
Tena Paulo anakaza katika Wagal 3: 26-29 kuwa
26Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. 27Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.29Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.



9.      MAWAKILI WA SIRI ZA MUNGU
Katika 1Wakorintho 4:1-2 Paulo anasema kuwa watu watuhesabu kuwa tu watumishi wa Kristo na mawakala wa siri za Mungu. Paulo pamoja na Mitume wengine walifunuliwa siri kadhaa zinazohusiana na Ufalme wa Mungu.
Hebu sasa tuone siri kadhaa hasa zinazohusiana na Ufalme.
Katika Wakolosai 2:1-2 Biblia inasema wazi kuwa Yesu ndiye Siri ya Mungu! Siri zote za Munguzimefichwa ndani ya Yesu Kristo.
Paulo akiwaandikia Waefeso, anakwenda kwa undani kuhusu SIRI, na kuwa Yesu NDIYE Siri ya Mungu kwa dunia.
Katika Waefeso 1:3-14 Neno linatuonyesha bila tashwishi kuwa NDANI YA YESU tuna vitu vyote. Siri iko ndani ya Yesu Kristo. Tunasoma kuwa:
1.      Mungu AMEtubariki kwa baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa roho, NDANI YAKE KRISTO (Mst 3)
2.      Mungu AMEtuchagua – KATIKA YESU – kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo (Mst 4) – na sio katika Sheria na Torati.
3.      Mungu ALITANGULIA kutuchagua ili tufanywe wanawe kwa NJIA YA YESU KRISTO sawasawa na uradhi wa mapenzi yake (Mst 5)
4.      KATIKA YESU tumepata neema (Mst 6)
5.      KATIKA YESU – kwa Damu yake – tunao ukombozi – yaani masamaha ya dhambi sawasawa na wingi wa neema yake (Mst 7).
6.      KATIKA YESU Mungu amekusudia kutuzidishia hekima na ujuzi wa kumjua Yeye (Mst 8) – kwa kuamua kutufunulia Siri ya Mapenzi yake – sawasawa na uradhi wake alioukusudia katika Yesu (Mst 9)
Siri ya mapenzi yake ni kuleta madaraka ya wakati mtimilifu (Wagal.4:4) ili kuvijumulisha vitu. vyot katika Yesu – vitu vyote duniani na mbinguni (Tazama Wakol1:20) (Waef.1:10). Rejea pia 1Wakor.3:21-23 na Wafil.2:9-10.
1.      Mungu ametufanya sisi kuwa urithi wa Kristo na warithi pamoja na Kristo (Rejea Waef.1:11, War.8:17, Waeb.1:1-4 ukilinganisha na Israeli katika Kumb.4:20, 32:9 na Hosea 2:23)
2.      Mungu alituchagua hivyo tangu awali sawasawa na kusudi lake Yeye, kwa shauri lake Yeye – ili tuwe sifa na utukufu wake (Mst 12)
3.      Mungu, kwa sababu hii, ametupa muhuri wa Roho wa Ahadi, Mtakatifu, na Roho kama arabuni ya urithi wetu. Nia yake ni kuleta ukombozi wa milki yake (yaani sisi – Kanisa) kuwa sifa ya utukufu wake (Mst 13).
10.  KANISA NI SIRI YA MUNGU
Ndani ya Yesu kuna KANISA. Huu NDIO ufunuo mkuu sana wa Siri ya Mungu.
Kama kuna sehemu Paulo ameandika kwa undani juu ya Ufunuo wa Mungu ndani ya Yesu ni Waefeso 2,3 alipoandika kuhusu Ufunuo wa KANISA. Hebu kwa neema ya Mungu tupitie kwa kifupi kuhusu funuo hizi.
Waefeso 2:1-3
Biblia inasema ukweli wa ajabu sana kuwa sisi sote tulikuwa WAFU.  Kuna kweli 7 kuhusu UFU katika Agano Jipya
1.      Kuna watu wanaoishi lakini ni wafu (dead living people). Math 8:22, 2Wakor 5:14, Uf.3:1: “Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao”
“Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote”
“Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa”
2.      Watu waliokufa bali ni hai (Living dead people). War.6:2,7-14, 2Tim2:11:
2Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?… 7 kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. 8Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye; 9tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena. 10Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu.
11Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. 12Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; 13wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. 14Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.”
“Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia”
3.      Miili iliyokufa kwa sababu ya dhambi, yenye roho zilizo hai kwa sababu ya haki. War.8:10: “Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.”
4.      Miili iliyokufa. Yohana 5:28-29, Yakobo 2:26: “28Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”
“Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa”
5.      Kazi mfu. Waeb.6:1,9:14: “1Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai,…”, “14…basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?”
6.      Imani mfu. Yakobo 2:17,20,26: “17Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. 20Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? 26Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.”
7.      Dhambi iliyokufa. War.7:8: “Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.”
Waefeso 2:4-7
Mungu alituhuisha PAMOJA na Kristo – yaani tumeokolewa kwa neema:
·         Alitufufua pamoja na Kristo
·         Alituketisha pamoja na Kristo katika ulimwengu wa roho KATIKA Kristo (Mst 6)
·         Kuna jinsi atakavyoudhihirisha wingi wa neema yake upitao kiasi – katika siku zijazo (Mst.7)
“Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu” – Waefeso 1:12
Waefeso 2:11-12
Zamani tulikuwa (sisi wa Mataifa):
·         Wasiotahiriwa
·         Watu wasio na Kristo
·         Watu waliofarakana na jamii ya Israeli
·         Wasio na maagano na ahadi ya urithi
·         Wasio na tumaini
·         Watu wasiokuwa na Mungu
Lakini katika Kristo hali yetu IMEbadilika sasa
Waefeso 2:13-22
Biblia inafungua ukurasa mpya kabisa – KATIKA YESU:
Tumeletwa karibu na Mungu kwa damu ya Yesu (Mst 13)
Uadui na tofauti za Israeli na Mataifa ZIMEKUFA – wawili (yaani Israeli na Mataifa) waMEkuwa mmoja – yaani kuna amani sasa (Mst 14)
Matika MWILI wa YESU – Waisraeli na Mataifa ni MMOJA! Uadui umefishwsa kwa Msalaba wa Yesu (Mst 16-17)
Yesu sasa NDIYE NJIA ya pekee ya kumkaribia Baba kwa Roho mmoja (Mst 19)
Sasa Mataifa, kama walivyo Israeli, ni wenyeji pamoja na Watakatifu – watu wa nyumbani kwake Mungu (Mst 19-22)
HII NDIYO SIRI  Mungu aliyoifunua katika Kristo – Siri ya Munbgu juu ya wanadamu wote! Katika Waefeso 3:1-13 Biblia inafafanua juu ya Siri hii. Hebu tuone kidogo:
1.      Neno linasema kuwa kwa kweli Mungu ndiye aliyeamua kutujulisha Siri yake Kristo (Mst 1-5)
2.      Siri hii ni: MATAIFA NA ISRAELI NI:
·         Warithi pamoja, wenye urithi mmoja (Mst 6)
·         Washiriki wa Mwili mmoja (Mst 6)
·         Washiriki pamoja wa Ahadi za Mungu (“Ahadi yake” iliyo) katika Kristo (Mst 6)
·         Tamko la Ushiriki huu ni INJILI!
3.      Injili – ambayo Paulo alifanywa mhudumu wake (Mst 7) – ni hii:
·         Kuwahubiria Mataifa kuwa sasa mlango umefunguliwa (Mst 8)
·         Kuwaangazia watu wote – Mataifa na Israeli – wajua madaraka (au mamlaka) ya Siri hii
·         Kuwafunulia wanadamu ukweli kuwa sasa Mungu amejifunua kwa “taasisi” iitwayo KANISA (Mst 10-11)
·         Kuwaamsha watu wote wajue kuwa kwa Yesu
·         Tuna Ujasiri na uwezo wa kukaribia kwa Mungu katika tumaini
·         Tuna Njia ya kumkaribia Mungu katika tumaini, Njia hiyo ni KUMWAMINI YESU (Mst 12)
Ndio maana paulo anasema wazi kuwa sasa WATU WOTE (Mataifa na Israeli) wanaweza kuwa washiriki wa Ufalme wa Mungu kwa NJIA MOJA TU, nayo ni KUMWAMINI YESU.
Katika Wakolosai sura ya kwanza tunasoma wazi:
24Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake; 25ambalo nimefanywa mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu;26siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake; 27ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu 28ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. 29Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.
11.  LAKINI MUNGU HAKUWAACHA ISRAELI
Kwamba Mungu hakuwatupa kabisa Israeli ni Siri nyingine ambayo Munbu ameifunua kwetu. Labda bado tunakumbuka ile picha:
Biblia inasema wazi kuwa karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake (Warumi 11:29).
Kipindi cha kanisa kilianza baada ya majuma 69 ya Danieli – kama tulivyosema hapo juu. Hii ni baada ya Israeli kumkataa Mfalme asiwe Mfalme wao. Mpango wa Mungu ukasitishwa kwa muda, na kuliahirisha JUMA LA 70 la Israeli.
Mungu katika hekima yake akatangaza “Taifa jingine” lenye kuzaa matunda, yaani KANISA (Mathayo 21:33-43).
Lakini JUMA LA 70 litaanza SIKU ZA KANISA ZIKIKOMA – yaani Kanisa litakaponyakuliwa.
Katika Warumi 11:25-32 Paulo anaweka ukweli huu bayana sana:
25Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 27Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao. 28Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu. 29Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake. 30Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao; 31kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema. 32Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.
Tmesoma nini?
1.      Mataifa wasiwe wajinga – bali waijue Siri ya Mungu pia kuhusu Israeli
2.      Kuwa ugumu umewapata Israeli kwa muda tu – na sio milele
3.      Kipindi cha ugumu wa Israeli Mungu amewaruhusu Mataifa waingie – na idadi yao Mungu ameiweka (“mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili”), Kumbuka Luka 11:24 na War.11:7-12:
24Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.”
7Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata; lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa uzito. 8Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo. 9Na Daudi asema, Meza yao na iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao;
10Macho yao yatiwe giza ili wasione, Ukawainamishe mgongo wao siku zote. 11Basi nasema, Je!Wamejikwaa hata waanguke kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa lao wokovu umewafikilia Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu. 12Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao?”
4.      Israeli wote hatimaye wataokoka – yaani Mabaki! “27Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.28Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.” War.9
Kipindi hii cha Israeli nj kipindi kipya kabisa chenye kanuni tofauti na zile za Kanisa. Ni Juma la 70 la Danieli 9.
Katika Juma hili – yaani miaka kama 7 hivi,
1.      Kanisa litakuwa halipo – limeondoka. Waaminifu wamenyakuliwa, na taasisi iitwayo Kanisa imefungwa!
Unyakuo utakuwa umetokea. Hebu kwa kifupi sana niseme juu ya Unyakuo:
1.      Utakuwa SIO KWA WATU WOTE, yaani sio kwa Wakristo wote! Utakuwa kwa wanawali wenye busara (Math.25:1-13). Wale wasiokuwa na busara Bwana atawaambi “siwajui” ni sio “sikuwajua”. Aliwajua kwa kuwa waliokoka, bali kwa habari ya unyakuo, hawakujiweka tayari, hivyo HAWAJUI. Linganisha na Math 7:21-23 na Luka 13:23-30 Bwana anaposema “Sikuwajua”
2.      Tunajua kwa hakika kuwa Bwana AMECHELEWA kuja (Math 25:1-13)
3.      Katika Unyakuo huu kutakuwa na matengano makuu! Watu wawili watakuwa kitanda kimoja, au wakisaga nafaka, au wakiwa shambani, mmoja atwaliwa mmoja aachwa.(Math.24:39-42 na Luka 17:34-37). Wakati wa unyakuo wa Elia, kulikuwa na matengano makuu kati ya Elia na Elisha (2Wafalme 2:1-18)
4.      Watu wengi watabaki, na watajaribu kuwa na maelezo mengi juu ya jambo lililotukia. Baada ya Unyakuo, miujiza mingi pia yawezekana itafanya duniani, kwa sababu Roho wa Neema na Kuomba atakayemwagwa kwa Israeli atafanya miujiza mara dufu kwa Kanisa – yaani upako mara mbili. Kumbuka kuwa Elisha alikuwa na upako mara mbili ya Elia (Elia alifanya miujiza 8 iliyonukuliwa katika Biblia wakati Elisha alifanya 16). Kumbuka pia Ufunuo 7 juu ya wahubiri 144,000 walio na upako – labda ni uke upako wa Zekaria 12:10
5.      Roho Mtakatifu atakuwa ameondoka na Kanisa
6.      Roho atakayeletwa duniani ni Roho wa Neema na Kuomba – kama asemavyo Zekaria 12:10: “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.”
7.      Roho wa Muhuri atakaa juu ya waisraeli 144,000 – kila kabila watu 12,000. Nao wataitwa “Watumwa” wa Mungu (Ufunuo 7
8.      Kutakuwa na amani kwa Israeli kwa miaka 3kulingana na Danieli 9:27: “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu”
9.      Hekalu la Yerusalemu litajengwa ili kuanza ibada za daima na kafara
10.  Kipindi cha miaka 3ya kwanza kitakuwa mateso kwa Wakristo waliochwa, kwa kuwa hawana taasisi ya kuwasaidia, wala Roho Msaidizi. Lakini inawezekana kutakuwa na Mvua za Mwisho – yaani uamsho mkuu sana dumiani (Hosea 6:3, Yoeli 2:23, na Zekaria 10:1)
11.  Baada ya miaka 3Israeli itaanza kipindi cha mateso. Kumbuka unabii huu: “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu”. Watateswa kwa maana watampinga mtawala ajiinuaye juu ya Mungu – yaani Mpinga Kristo na Nabii wa Uongo. Kumbuka Nabii hizi: 2Wathe.2:1-4,Yer.30:1-15, Dan 9:12, 12:1, Amosi 5:18 na Zephania 1:14.
12.  Vita vitainuka kuimaliza Israeli. Tunasoma juu ya uvamizi toka Kaskazini (Ezekieli 38:1-16)
Mungu atawapigania sana – Zekaria 14:1-5, 12
Labda hii ndio vita ya Harmagedoni ya Ufunuo 16:12-21, 19:11-21.
12.  SISI TUKIJUA SIRI HIZI TUNAPASWA TUWEJE?
Katika 2Petro 3:1-15 tunasoma haya:
… 9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. 10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, 12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? 13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. 14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake. 15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu…
Tena Petro anasema: “Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele zake”. Kuna mambo matatu yanatajwa hapa katika eneo hili. Jambo la kwanza ni wito wa kuishi maisha matakatifu, na la pili ni sisi kuitazamia siku ile ije, na jambo la mwisho ni sisi kuihimiza siku ile.
TABIA YA UTAKATIFU NA UTAUWA
Jambo la kwanza litakalokuhakikishia unyakuo si asili ya utakatifu tu bali tabia ya utakatifu iliyo matokeo ya asili ya utakatifu. Asili ya utakatifu ni YESU aliyeko moyoni mwako.  Mungu alimfanya Yesu kwetu kuwa haki, utakatifu na ukombozi – 1Wakor.1:30.
Ukimpokea Yesu moyoni unazaliwa kuwa na asili nyingine iitwayo mwana wa Mungu au tabia ya uungu (Yoh. 1:12, 2Petro 3, 4). Asili yako inabadiliki. Unazaliwa katika “boma” jingine – boma la Mungu mwenyewe; na unarithi asili hii ya utakatifu kwa sababu aina ya roho unayepewa ni Roho wa Utakatifu – au Roho Mtakatifu.
Mungu anataka nini baada ya hayo?  Wewe na mimi tubadilike tabia ili idhihirishe utakatifu tulioupata!  Huu ni wito – utakatifu  kwa tabia. Biblia inasema wazi kuwa lazima tutafute kwa bidii utakatifu (Waeb. 12:14, War. 6:21-23, 2Wakor.7:1-2, Waef. 4:23-25).
Wapendwa, Njia ya Mbinguni bado haijawa pana, wala mlango wa kuingilia juu haujaongezeka hata kidogo (Math. 7:13,14). Matakwa ya Mungu ya utakatifu ni yale yale aliyoyaweka kwa Danieli (dhidi ya dola lile ovu la Babeli), ni yaleyale aliyowawekea mitume kipindi kile cha Warumi wabaya wale hadi kipindi cha leo chenye elimu iliyozidi sana – 1Pet. 1:16-25! Bado viwango vya utakatifu (1Pet. 1:16-25) ambavyo Mungu anavyotaka tuviamini na kuvifikia ni vile vile vyake mwenyewe: “Kama yeye aliyewaita alivyo Mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote” mst.15.
Mungu tunayemtumikia hata leo ni Mungu yule yule MTAKATIFU. Roho anayeliongoza Kanisa la Mungu leo ni Roho yule yule wa Mwanawe ambaye Biblia inamwita Roho Mtakatifu. Bado vigezo vya kuingia  kule Mbinguni na mtindo wa hukumu havijabadilika! Kila mtu atahukumiwa sawasawa na matendo yake! Uf.20:12,13 (Linganisha na Dan. 12:2).
Utakatifu wa Yehova aliouona Isaya ni ule ule utakaotuangusha mbele zake kama mtu mfu (Isa.6:1ff) – kwa sababu pamoja na unabii wake mkuu, mbele za Yehova alisema: “Ole wangu” kwa sababu aligundua AMEPOTEA.
Mungu tunayemngojea ni Mungu Mtakatifu. Huyu ndiye aliyekutana na Simoni mwana wa Yona kando ya Ziwa la Genesareti akampa muujiza wa samaki wengi hata vyombo vikataka  kuzama, akaanguka miguuni/magotini kwa Yesu akasema:  “ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana” – Luka 5:1-11.
Huyu ndiye Mungu aliyekutana na Sauli pale njiani Dameski akasema na Sauli. Ndiye aliyemwambia Sauli:  “Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo” – Mdo 26:14. Huyu ndiye Mungu aliyepambana na kiburi cha Herode: “Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu, akaliwa na chango, akataka na roho” Mdo 12:20:23. Kwa nini? Kwa sababu hatampa mwingine utakatifu wake (Isa 48:10,11)!
Kila watu katika kizazi chao, Mungu alidai utakatifu kwao. Haijalishi kuwa hali iko je, Mungu alidai Utakatifu kwa sababu aliandaa mawezesho. Mungu hadai kitu kwetu asichotuwezesha kukifanya. Katika utumishi wetu, katika shida zetu, katika mafanikio yetu, Mungu anadai Utakatifu. Hebu tuone mifano kidogo kuelezea ukweli huu:
MUSA
Tunamjua mtumishi huyu wa Bwana kwa jinsi anavyonenwa katika Biblia, kuwa alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya nchi (Hes.12:3). Katika Waebrania 3:5  tunasoma kuwa Musa alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi. Ndiye ambaye alikataa kabisa kwenda hudumani kwa sababu aliona hawezi na Mungu akamtia nguvu.  (Kut. 3:9-4:1-16).
Pamoja na Mungu “Kum’bembeleza”, bado alidai utakatifu kwake! Katika Kut.4:22-26 tunamwona Mungu akipambana naye kwa sababu alidharau agano la tohara. Tunamshukuru Mungu kuwa katikati ya hali hiyo, Sipora alikuwepo! Akamtahiri mwanae (labda alikuwa Gerson) kwa dhiki nyingi ili kuutimiza utakatifu!  Ndiye Musa huyu huyu aliyechoshwa na uasi wa Israeli hata akajikwaa kwa MANENO NA MAZOEA yake.
Utakumbuka Kut 17:1-7 kwenye bara la Sini kule Refidimu? Mungu alimwamuru Musa alipige jabali ambalo Mungu AMESIMAMA JUU YAKE – maji yakatoka, watu wakanywea lile jabali. Lakini  katika Hes 20:1-13, miaka mingi baadae, tunaona tena kule Kadeshi.  Mungu alimwamuru Musa auambie Mwamba utoe maji YAKE – Mwamba wenye maji ndani yake! Musa hakufanya hivyo kwa sababu ya uzoefu wa kwanza pamoja na maudhi ya wana wa Israeli aliokuwa anawaongoza; na likawa kosa kubwa sana mbele za Bwana. Bwana akamwambia yeye na Haruni kuwa hawataingia Kanani “Bwana akajionyesha kuwa Mtakatifu kati yao” Hes. 20:13.
SAULI.
Mungu wetu aliyemchagua Sauli na kumkataa baadaye! – Sauli mfalme wa kwanza wa Israeli.
Vita ya kwanza iliyomjaribu ni ile ya Wafilisti (1Sam.13:5-14). Sauli hakuwa mvumilivu, kwa sababu alipaswa amsubiri Samweli kwa ajili ya kutoa sadaka ya kuteketeza. Badala yake akawa na pupa na kuitoa sadaka ya kuteketezwa – naye sio kuhani. Samweli akauita UPUMBAVU (Hebu soma Mst. 13-14)! Unabii ukatoka juu ya Sauli hivi: “Bwana amejitafutia mtu ampendaye moyo wake….”.
Vita ya pili ni ile ya Waamaleki (1Sam.15). Sauli alipewa amri kuwa aende akawaangamize Waamaleki kabisa: “Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda ” (mst. 3). Biblia inasema kuwa Sauli hakufanya hivyo: “… Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng’ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa ” (mst. 9). Sauli akawaogopa watu, akazirukia nyara (mst. 19) na kufanya uovu mbele za Mungu. Unajua alilolifanya Mungu? Samweli akamwambia Sauli, “… je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme ” (mst. 22,23) Mungu akauraruwa ufalme wake milele!
DAUDI
Daudi, kipenzi cha Mungu, hakukosa kupitia kwenye moto wa vipimo vya utakatifu wa Mungu! Katika 2Sam.11 tunasoma dhambi ya Daudi na Bathseba mkewe Uria. Toba yake haikuondoa ukweli kuwa aliwapa “adui za Bwana nafasi kubwa ya kukufuru” 2Sam.12:14 – na mtoto aliyezaliwa Mungu alimuua!
Tunapochezea maisha ya utaua na utakatifu, tunawapa ‘adui za Bwana nafasi kubwa ya kukufuru’, na Mungu anawaka hasira juu yetu. Mungu hawezi kukaa nasi iwapo hatujali kuishi maisha ya utakatifu.
ANANIA NA SAFIRA
Anania na Safira – leo hii tunawaona sio watu wa kiroho.  Walikuwa ndugu, tena wapendwa walioongolewa na Bwana – lakini waliuchezea utakatifu wa Mungu (Mdo 5:1-11). Hawakuweza kuhimili vishindo vya kumwambia uongo Roho Mtakatifu. Tunapofanya dhambi, tunauchezea utakatifu wa Mungu.
Mungu huyu mtakatifu hivi ndiye tumwabuduye. Mungu aliyewafanya watoto wa Anania na Safira kuwa yatima, na Kanisa likamwogopa Mungu.
Mpendwa kama tulivyotangulia kusema, katika Waeb. 12:14 Neno liko wazi: tafuteni kwa bidii. Narudia tena; utakatifu wetu chanzo chake ni Yesu aliyeko moyoni (1Wakor.1:30). Katika Waeb.10:14 tunasoma pia kuwa “kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa”. Tunapoingia katika kuokoka tunampokea Yesu Moyoni.  Roho zetu zinaokoka lakini wokovu wetu hauishii hapa.
Wapendwa, Mungu anatamani tuwe watakatifu. Neno liko wazi kuwa utakatifu kama ilivyo amani na watu wote hutafutwa kwa BIDII -Waeb. 12:14. Paulo amefundisha katika 1Wathe. 4:3-8 kuwa mapenzi ya Mungu ni kutakaswa kwetu – kwa sababu Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso! Katika 2Wakor. 7:1 Biblia inafundisha juu ya kujitakasa nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.
Mtume Petro katika Roho amefundisha kuwa HATUNA UDHURU katika kuishi maisha ya utakatifu (2Pet. 1:3,4). Mungu ametupa sisi mawezesho yote ya kuishi maisha ya UZIMA, yaani kuokoka, na utauwa – yaani usafi na utakatifu. Tena Mtume anatufundisha kuwa tabia hii ya UTAKATIFU ni tabia ya uungu ambayo TUNAWEZA KABISA KUWA WASHIRIKA WAKE – na mpango kamili wa Mungu ni kutuokoa sisi na uharibifu ulioko duniani kwa sababu ya tamaa. Neno linasema: “Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa ” (2Petro 2:3,4).
NJIA YA UTAKATIFU
Hebu tuone Neno lasemaje katika Isaya 35:8-10: “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo. Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo. Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia”.   Katika kifungu hiki tunasoma juu ya Njia kuu na Njia iitwayo “Njia ya utakatifu”.  Utakatifu sio kituo au hali tunayofikia wakati tunapookoka, bali ni HATUA, NI NJIA. Tena si hivyo tu, tunasoma kuwa ni jambo moja kukwea juu ya njia hii, ni jambo jingine kupita juu ya njia hii.  Njia hii ni kwa wale walioamua kusafiri – na Bwana ameahidi kuwashika mkono, WAJAPOKUWA WAJINGA, hawatapotea.
TUNAANZAJE KUTEMBEA KATIKA NJIA YA UTAKATIFU?
Katika kitabu cha Ezekieli 36:25-27 tunasoma: “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda”. Hapa tunapata utaratibu Mungu alionao kwa wale wanaotamani kwenda Mbinguni. Katika mistari hii, Neno la Mungu liko wazi kabisa juu ya hatua za kuokoka na kuishi maisha ya Utakatifu. Tunaelezwa wazi kuwa maisha yetu ya kiroho yanayo hatua mbalimbali zenye mambo mawili tu – KUFANYIWA (mambo 5) na KUFANYA (jambo 1) – hii ndiyo neema!
HATUA 1.  Kuwa safi kwa kunyunyiziwa maji – KUFANYIWA
HATUA 2.  Kutakaswa na uchafu na vinyago vyetu – KUFANYIWA
HATUA 3.  Kupata moyo mpya: kutoa moyo wa Jiwe ndani yetu na kupewa ule wa nyama – KUFANYIWA
HATUA 4.  Kupata roho mpya :  kutia roho ya Mungu ndani yetu – KUFANYIWA
HATUA 5.  Kutuendesha katika sheria za Mungu  – KUFANYIWA
HATUA 6.  Kuzishika na kuzitenda Sheria za Mungu- KUFANYA
Yawezekana na ni hakika kuwa sisi sote tuliookoka tumeletwa hadi  HATUA 5. hapo juu – tunaye Roho wa Mungu, na Mungu anatuendesha katika sheria zake. Swali ni hili, moyo wako na roho yako vimeongoza mwili wako hadi  UKAMTII BWANA? Je umeanza KUZISHIKA na  KUZITENDA sheria za Bwana?
UMEPONDEKA VYA KUTOSHA?
Namna nyingine ya kutazama Ezek. 36:25-27 ni kupondeka, kama inavyoelezwa na Bwana mwenyewe katika Math.21:43-44: “Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki”. Yawezekana umeliangukia jiwe (Yesu) maishani – yaani uliamua kuokoka. Je, umepiga hatua kukubali jiwe likuangukie – Yesu sasa atawale maamuzi yako? Paulo katika Wagal. 5:25 anasema:  “Tukiishi kwa roho (tukiamua kuokoka), tuenende kwa roho (tuvunjike na kumtii Mungu).”
Hii inawezekana unapopiga hatua kuomba sasa ili  mwili wako na nia/nafsi yako pia viokoke. Hapo ndipo unapogundua kuwa udhaifu wako uko hapa na pale, na unapaachia Msalabani (Waeb.12:1-4).
Paulo katika War. 6:11-14 anawafundisha Warumi kuwa “Short Cut” ya utakatifu ni:
1.      Kujihesabu mfu kwa dhambi
2.      Kujihesabu hai kwa Mungu katika Kristo
3.      Kukataa kutii tamaa ya mwili – kusema “No” kwa dhambi
4.      Kutompa Shetani viungo vyako avitumie kutendea dhambi
5.      Kumpa Yesu viungo vyako avitumie kama “Silaha za haki”
Ukifanya mambo haya kuna matokeo ya ajabu sana: “… dhambi haitawatawala ninyi”.
JE UTAPIMWAJE UTAKATIFU WAKO?
Utakatifu wetu unapimwa kwa matunda matatu ambayo tunapaswa kuyadhihirisha:
1.      Tunda la Roho: 5:22
2.      Tunda la Nuru: 3:4
3.      Tunda la haki: Yakobo 3:18
Hatua hii ndiyo Biblia inaiita KUWA NDANI YA YESU – 2Wakor. 5:17 (1Yoh.4:17). Yesu alisema kuwa mtu wa jinsi hiyo HUZAA SANA (Yoh. 15:1-5). Ahadi ya Yoh.15:7 ni kwa watu walio ndani ya Yesu na sio kinyume chake! Mtu aliye na Yesu ndani, bali yeye hakuyaendea masafa ya Utakatifu, Biblia inamwita mtu wa “tabia ya mwilini” naye ni mtoto mchanga katika Kristo – 1Wakor.3:1-3. Tabia ya mwilini ni  tofauti na wa “tabia ya asili” (1Wakor. 2:15). Mtu wa tabia ya asili ni mtu ambaye kabisa hajawahi kuokoka. Mtu wa tabia ya mwilini ni mtu ambaye ameokoka, bali bado anaishi maisha ambayo sio ya utakatifu.
Nikupe shauri – Tafuta kwa bidii utakatifu! Anza leo kuishi maisha ya utakatifu. Hii ni hatua ya kuanzia, na wewe na mimi tuna safari ndefu ya kuyaishi maisha ya utakatifu ambayo lazima tuyaanze. Kweli tutaomba neema ya Mungu imwezeshe kila anayesoma maneno haya ili aweze kuanza.  Mungu anasubiri ukomavu wako – siku zimekwenda, anza.
Sijui kama unajua kuwa ingawa Mungu atashughulikia magugu yaliyoota na ngano siku ya hukumu (Math.13:24-30), lakini pia atashughulikia makapi yaliyotia joto ngano (Math.3:12) na ni ngano tu iliyostahimili vishindo vya pepeto itaingia ghalani! Watu wengi sana wanadhani ni rahisi sana kwenda mbinguni – sio! Ni ngano tupu zitakazoingia ghalani.
Dunia hii na elimu zake tutaishinda tu kwa kuweka changamoto kwake – MAISHA YA UTAKATIFU!

 HALELUYA GIZA LAISHA  
Haleluya siku i karibu, kumwona Mwokazi wetu
Kuachana na dunia hii, ya machozi kwenda Mbinguni.
Tutaipa dunia kwaheri, Mwokozi akitunyakua
Tukipaa juu Mawinguni, kumlaki Mwokozi wetu.
Sasa wangojani msafiri, kushuhudia ya Mwokozi
Kesha, funga, omba, shuhudia, leta Roho kwa Bwana Yesu.
Hivyo ndugu yangu jipe moyo, tumalize huduma yako,
Wajiandaaje kusimama mbele ya Kiti cha hukumu
٪   Aleluya giza kwisha, Yesu anarudi mawinguni
Natamani toka nchi hii, ya machozi kwenda Mbinguni.

 SIRI YA UTAKATIFU 
Ungejua siri ya Utakatifu, ya kukaa  ndani ya Yesu.
Ungejua jinsi ya kumtumikia, na kupata baraka zake.
Ungejua giza lililo njiani, unaposafiri kwenda juu
Ungejua vita vya waendao juu, ungeomba nguvu kwa Yesu.
Ungejua Pendo na nguvu za Yesu, kwao wamtegemeao
Ungempa Yesu Moyo wako wote, na kuleta watu kwa Yesu
Sasa wangojani, wewe msafiri, tulia-tu ndani ya Yesu
Siku zinakwisha, Yesu anarudi, maliza safari vizuri
٪  Ungemwita Yesu akusaidie katika udhaifu wako!
Wahitaji nguvu za Roho wa Kweli kumaliza safari yako

KUTAZAMIA SIKU YA BWANA NA KUIHIMIZA
Jambo la pili ni kuishi kama wasafiri.  Siku kwa siku lazima tutazamie kuondoka.
Siri ya Sikukuu ya Vibanda kati ya Israeli ni hii: wao ni wasafiri! Ibrahimu na wanawe waliishi katika mahema daima kwa sababu walijihesabu kuwa wao siku zote ni wasafiri. “Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile… Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji ”Waeb.11:9, 13-16.
·         Asubuhi tazamia Unyakuo, mchana tazamia Unyakuo
·         Jioni tazamia Unyakuo.
·         Ukiwa kazini tazamia Unyakuo, ukilala tazamia Unyakuo.
·         Ukisafiri tazamia Unyakuo!
·         Ukiumwa tazamia Unyakuo,
TAZAMIA UNYAKUO!
Lakini watazamiao huhimiza pia siku hiyo. Je, tunawezaje kuihimiza?  Yesu alifundisha kuwa Habari Njema ya Ufalme itahubiriwa kila mahali, ndipo mwisho utakapokuja – Math. 24:14. Tunavyowavuta wengine ufalmeni ndiyo siri ya kuhimiza siku ije!
Ukijua siku iko karibu, unakuwa na haraka na wepesi wa kumaliza kazi ya Bwana. Unajua, siku ya kutoa hesabu iko karibu sana. Unaihimiza.  Math. 25:24-30. na Danieli 12:1-3.
Bwana ametuita kuwa tuwaelezee wengine kuwa Yesu ni Bwana. Lazima wengine waelezwe habari za Yesu Kristo.
Lazima tulie sana mbele za Mungu ili wengine wazaliwe. Watu wengi ni mateka kwa shetani – hata watu wengi waliookoka ni mateka, hadi neema iwazukie waweze kufunguliwa. Kanisa lazima lilie machozi.