Monday, March 21, 2016

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE (Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam) SOMO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO NA WALIO NA HAJA YA KUPONA.

SIKU YA NANE

Mistari ya kusimamia: Isaya 61:1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.” Yeremia 6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.”

SOMO LA LEO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO KWASABABU YA KUCHOKA MOYONI KULE KUNAKOLETA KUKATA TAMAA.

1.     Nini maana ya kuchoka moyoni kunakoleta kukata tamaa?
Ø  Kukata tamaa ni maneno mawili. Kukata. Tamaa.
Ø  Tamaa maana yake ni hamu, kiu, msukumo, kiu  kutoka moyoni wa kutaka kupata unachotaka kukipata.
Ø  Kukata ni kuachanisha au kutenganisha kitu kunakoumiza kwa nia ya kuondoa muunganiko au mtiririko wa kitu.
Sasa kukata tamaa ni kitendo kinafanywa na mhusika wakati kukatishwa kinafanywa na mwingine.
Hivyo, Kukata tamaa maana yake Kuchoka moyoni kunakuja na maumivu kunakukuvunja nguvu kuendelea kufuatilia unachotaka kukifuatilia. Kunaondoa tarajio au tumaini. Matokeo ya kukata tamaa unakuona tu. Unaacha kufuatilia. Hapo ujue moyo umeumia. Utafutie msaada haraka.

2.     Moyo haukuumbwa ili uchoke. Kule kuchoka kunakokatisha tamaa
Isaya 40:28-31 “28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. 29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. 30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; 31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”
Mwanzo 1:26-27 “26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.”
Moyo haukuumbwa peke yake. Uliumbwa na uungu ndani yake. Kama Mungu hachoki kule kukata tamaa sio zao la moyo wa Mungu.  Kuokoka ni kuchukua sura ya Kristo. Ukiona umechoka moyo kuna shida. Usijifiche. Usijihesabie haki. Msalaba wa Yesu pekee unakupa dawa.

3.     Mifano ya kuchoka kwa moyo wa mtu kunakoleta kukata tamaa. Mifano kutoka kwenye Biblia.
Hatusomi somo hili kwakuwa tunazo notes! Ni kwasababu Mungu amelitoa kwa kusudi maalum kwa wakati huu, kama wewe haujavunjika moyo chukua somo hili kama chakula cha njiani kwani itakusaidia.

A.     Vita vya muda mrefu bila kupata ushindi uliotarajia.
1Samweli 31:3-4 “3 Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde. 4 Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.”

Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata, hata akafadhaika sana kwasababu ya wapiga upinde. Ndipo Sauli akamwambia yule mchukia silaha zake, futa upanga wako unichome nao, wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli ukautoa upanga wake akauangukia.
Moyo wake Sauli ndio uliomuua kutokana na mazingira. Mazingira yalimuua kabla ya upanga wake. Alifadhaika sana. Alipomwambia mbeba upinde wake amchome inaonyeshwa hakutaka kufa. Mazingira yalimuua.

1Wafalme 19:1-4
Mfalme Ahabu alimsimulia mkewe Yezebeli mambo yote aliyofanya Elia na jinsi alivyowaua manabii wa Baali kwa upanga. 2Yezebeli akatuma mjumbe kwa Elia amwambie: “Miungu waniulie mbali, nakuapia, ikiwa saa hizi kesho sitakuwa nimekufanya kama mmoja wa hao manabii.” 3Elia akakimbilia mjini Beer-sheba mkoani Yuda, alikomwacha mtumishi wake, 4naye akatembea mwendo wa siku nzima kuingia jangwani. Basi, akafika, akaketi chini ya mti mmoja, mretemu. Hapo, akaomba afe, akisema, “Imetosha! Siwezi tena. Ee Mwenyezi-Mungu, sasa utoe uhai wangu. Mimi si bora kuliko wazee wangu.”
Eliya anaomba kwa maneno magumu sana kwenye sala yake. Eliya yule yule tunayemuona kwenye sura iliyopita(18) akiwa na upako mwingi sana lkn anaumia moyo wake tena badala ya kusherekea ushindi. Vita kubwa kwa muhubiri sio jumamosi au jumapili bali jumatatu. Unapomuombea mtumishi mbele wakati wote

Zaburi 69:1-4 “1 Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. 2 Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha. 3 Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu. 4 Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.”
Unapokuwa kwenye maombi magumu na moyo wako unakata tamaa angalia ndoto zake sasa.
Mithali 24:10 “Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.”
Eliya alichoka kwakuwa hakuwa anakula chakula. Ndio yule malaika anamletea chakula. Wengi wanaishiwa nguvu sana kwakuwa wanajitahidi kutafuta mistari kwenye Biblia badala ya chakula. Kila kitu kinapaswa kuwa na uwiano. Malaika alimwambia kwanini anampa chakula. Kama wakristo wengi leo ambavyo wakila maneno ya Mungu jumapili wanalala mpaka jumapili tena. Wanalala kwenye mretemu

Ayubu 7:1-6 “1 Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa? 2 Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake; 3 Ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha. 4 Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke. 5 Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena. 6 Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.”
Wengi huwa tunawafikiria wanaotupiga vita. Lakini wewe lala ukimtumaini Bwana ingawa si rahisi kumtumaini wakati umevunjika moyo, jitahidi. Inapofika hapo ndipo tunapaswa kujilisha mapema Neno la Bwana wakati ukiwa salama halafu ukifika wakati wa shida unatumia tanki la akiba!

B.     Kuuchosha moyo kwa hasira na uchungu na kujikuta unalipa kisasi
Yeremia 6:11 “Lakini nimejaa ghadhabu ya Bwana; nimechoka kwa kujizuia; imwageni juu ya watoto walio njiani, na juu ya kusanyiko la vijana pia; maana hata mume atatwaliwa pamoja na mkewe, mzee pamoja na yeye aliyetimiza siku zake.”

Yeremia 15:6-7 “6 Umenikataa mimi, asema Bwana, umerudi nyuma; ndiyo maana nimenyosha mkono wangu juu yako, na kukuangamiza; nimechoka kwa kughairi. 7 Nami nimewapepea kwa kipepeo katika malango ya nchi nimewaondolea watoto wao, nimewaharibu watu wangu; hata hivyo hawakurudi na kuziacha njia zao.”

Yeremia amejawa na hasira ya Bwana. Anaogopa asiseme maana yatawapata mambo magumu sana. Ukiwa na cha Mungu unapaswa kuwa mwangalifu sana unachokiongea. Unaweza ukajikuta umekivaa kibwebwe umemvaa mtesi wako na kuokoka unaweka pembeni. Unahitaji hekima.
Hasira ni pepo. Usisubiri ishuke. Kemea litoke. Au ingia kwenye maombi hata kama ni kazini nenda chooni kaombe huko au kalie huko mbele za Bwana naye anachukua machozi yako na kukufariji.


C.      Kuuchosha moyo kwa kutafuta msaada kwa miungu mingine

Isaya 16:12 “Tena itakuwa, Moabu akionekana, na kujichosha kwa kulia juu ya mahali pa juu, na kuingia katika patakatifu pake aombe, hatapata kushinda.”

Isaya 47:12-15 “12 Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda. 13 Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata. 14 Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao. 15 Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatanga-tanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.”

Kuna watu wanatafuta msaada tangu ujana wao lakini wanatafuta kwa miungu mingine. Unauchosha moyo wako. Unakata tamaa ya maisha. Dawa ipo kwa Yesu tu. Hata ukienda kwa Yesu kama ni wa dini yoyote mfuate Yesu kama daktari basi. Ukishapona ndio utauliza dini!

D.     Kuchoka moyo kwa kuutafuta mlango
Mwanzo 19:11 “Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango.”
Kuna watu wamechoka mioyo kwakuwa wamechoka kuutafuta mlango. Nenda kwa Yesu maana ndiye mlango. (Yohana 10:1-9 “1 Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang'anyi……….. 9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.”)
Isaya 43:22 “Lakini hukuniita, Ee Yakobo, bali umechoka nami, Ee Israeli.”
Moyo uliovunjika unaondoa msukumo kabisa. Usione kama Mungu amekuangusha. Achana na marafiki wataabishaji. Wasikuondolee msukumo wa kumtafuta Mungu wako. Kama marafiki wa Ayubu.

Yesu kakupitisha kwenye mangapi miaka yote hii mpaka umkatie tamaa leo kwenye hilo tuu??!  Biblia inasema siku za mwisho kutakuwa kuna njaa ya neno la Mungu. Biblia zitakuwepo lkn maneno ya Mungu yakupayo tumaini ndio hayatakuwepo. Utazunguka kutafuta neno la Mungu hata ibada 4 asubuhi moja hutapata. Jilishe neno la Mungu sasa kuupa usalama moyo wako.

Ukichoka kushindana na dhambi unakuwa mtumwa wa dhambi. Una jisalimisha. Unahitaji kujisalimisha kwa Yesu. Vita ya jana sio ya leo. Mungu anakulisha chakula kipya kila siku. Wokovu sio dini mpya bali upya ndani yako. 

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE (Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam) SOMO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO NA WALIO NA HAJA YA KUPONA.

SIKU YA SABA

Maneno ya msingi: Isaya 61:1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.” Yeremia 6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.”

SOMO LA LEO: UPONYAJI WA JERAHA LA MOYO WA MTU BINAFSI UNAVYOTENGENEZA MAZINGIRA YA UPONYAJI WA JERAHA LA MOYO WA TAIFA.

Tuliangalie hili kwa mtiririko ufuatao.

1.     Kilichojeruhi moyo wa mtu mmoja kinaweza kusababisha jeraha kwenye mioyo ya watu wengi.

Tutaangalie kwa mifano ktk maeneo mawili

        i.            Uchungu
Efeso 4:26 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;”
Waebrania 12:14-15 “14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; 15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.”
Fahamu kuwa shina la uchungu linapochipuka linanajisi wengine wanaohusiana na huyo mtu. Maana linaambukiza kwa wengine.

     ii.            Dhambi
1 Yoh 3:4 “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.”
Rum 5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;”
Dhambi ni uasi.
·         Na penye dhambi/uasi pana mauti
·         Uasi unaweza kuanza kwa mtu kisha kuendelea kusambaa hadi kwenye taifa.

1.     Kiini cha uhai wa kitaifa kinapojeruhiwa ina maana moyo wa kitaifa umejeruhiwa.
Yeremia 30:4,12-14 “4 Na haya ndiyo maneno aliyosema Bwana, katika habari za Israeli, na katika habari za Yuda. 12 Maana Bwana asema hivi, Maumivu yako hayaponyekani, na jeraha yako ni kubwa. 13 Hapana mtu wa kukutetea; kwa jeraha yako huna dawa ziponyazo. 14 Wote wakupendao wamekusahau; hawakutafuti; maana nimekujeruhi kwa jeraha ya adui, kwa adhabu ya mtu mkatili; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zilikuwa zimeongezeka.”
Taifa la Israel lilijeruhiwa na kugawanyika, hii inaonesha kuwa taifa linaweza kujeruhiwa.
2.     Kufuatana na Biblia kiini cha taifa lolote ni cha kiroho
Mungu ndiye aliyefanya taifa. Kuna mambo kadhaa yanayofanya taifa kuwepo/ kuunda taifa; nayo ni:
a.      Lango/ Mwanzilishi ambaye ni mtu mmoja.
Matendo 17:26 “Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;”

b.     Majira/Nyakati
Matendo 17:26 “Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;”

c.      Mipaka
Matendo 17:26 “Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;”

d.     kabila
Kufuatana na biblia kila kabila lina baraka zake.
Mwanzo 49:1, 2, 28 “1 Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. 2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu. 28 Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa mbaraka wake aliwabariki.”
Kumb 4:34 “Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile Bwana, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu?”

e.      Hali ya kiroho ya kitaifa
Zaburi 33:12 “Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, Watu aliowachagua kuwa urithi wake.”

f.        Familia
Ufunuo 5:9-10 “9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, 10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.”
Kabla halijawa taifa kwanza, inaanza familia

g.      Lugha
Ufunuo 5:9-10 “9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, 10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.”

3.     Mifumo ya majeraha inaweza kuumiza moyo wa mtu na moyo wa taifa kwa pamoja
Mfano:
·         Moyo unapojeruhiwa na kushindwa kuelewa lugha ya walio karibu nawe
Mwanzo 11:1, 6-9 “1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. 6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.”

Ufunuo 13:2 “Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.”
Fahamu:
·         Lugha moja inaleta usemi mmoja.
·         Lugha inaleta kusikilizana.
·         Lugha inaleta umoja.
·         Lugha inaleta kushirikiana na kufanya kazi kwa kufanikiwa.
·         Kwa hiyo lugha ikiharibika ni hatari sana katika taifa.

Ø  Mioyo ya watu ikijeruhiwa, watu wanakuwa na lugha tofauti katika taifa.
Ø  Haki inapoondolewa katika taifa, hupelekea watu kujeruhiwa kunakopelekea watu kutofautiana katika lugha

Mithali 14:34 “Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.”
Ø  Kiu ya udini kwenye uongozi pia inaweza kujeruhi mioyo ya watu katika taifa
Ø  Kutokuelewana juu ya mfumo wa kupata viongozi
Ø  Hii pia inaweza kujeruhiwa mioyo ya watu kisha kuharibu moyo wa taifa



SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE (Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam) SOMO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO NA WALIO NA HAJA YA KUPONA.

SIKU YA SITA

Mistari ya kusimamia: Isaya 61:1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.” Yeremia 6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.”

UTANGULIZI
Mambo mawili ya msingi ya kukumbuka
·         Maana ya neno moyo (rejea somo la siku ya kwanza)
·         Moyo uliovunjika ni moyo wa namna gani (pia rejea somo la siku ya kwanza)
Kumbuka MUNGU husema na watu kwa njia ya ndoto pia tena si mara moja Ayb 33:14-18
Ukiona uoti kabisa si zile za kuota siku moja moja ujue kuna shida sehemu msihi MUNGU afungue mlango huu pia kwako

VIPENGELE MUHIMU VYA KUOMBEA IKIWA MOYO WAKO UMEJERUHIWA NA NDOTO

1.     Omba maelekezo kutoka kwa BWANA juu ya kufuatilia ndoto uliyoota

Daniel 4:19, 27-29 “19 Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako. 27 Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha. 28 Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza. 29 Baada ya miezi kumi na miwili, kuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. 30 Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?”
·         Si kila kilichopo kwenye ndoto lazima kitimie
·         Daniel alimwambia mfalme ndoto hii isikupate wewe wala tafsiri yake..alimpa ushauri na maelekezo ya kufanya lakini mfalme akufanya hivyo ndipo ndoto ile ikatikilizika kwake
·         Wewe unaweza kubadilisha/kuhahirisha matokeo ya ndoto maana mfalme alipewa nafasi ya kutengeneza miezi 12 lakini hakufanya hivyo

2.     Omba MUNGU akupe tafsiri ya ndoto
Daniel 1:17 “Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.”
·         Omba MUNGU akupe ufahamu wa ndoto
·         Omba tafsiri yake
·         Omba MUNGU akusaidie kusoma NENO la kutosha likusaidie kutafsiri ndoto hizo

3.     Omba Toba kwa kutokufuata maelekezo na maonyo yaliyokuja na ndoto na hukuyafuata
Ayubu 33:14-18 “14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; 16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, 17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; 18 Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.”

·         MUNGU husema nawe pia kupitia ndoto, mara nyingi anakupa taarifa, kukuonya, kukufundisha, kukuelekeza, kukupa maono mapya na n.k
·         Kutofuata maelekezo na maonyo yaliyoko kwenye ndoto kama ni adhabu itakugharimu sana mkumbuke Mfalme Nebukadreza alipewa adhabu kwa kutofuata maelekezo miaka 7 kondeni

Mathayo 1:18 “ Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.”
·         Yusuph alitokewa kwenye ndoto kutomkimbia mariam. Pia alipewa maelekezo kumtorosha mtoto maana Herode alitaka kumuua
·         Ukidharau maelekezo maumivu na madhara yake yatakutesa wewe na familia yako hata nchi nzima.
·         TOBA ni kumruhusu MUNGU kuingilia kati

4.     Omba ili king'olewe kilicho pandikizwa kwa njia ya ndoto
Daniel 4:4-5 “4 Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi. 5 Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.”
·         Baada ya ndoto hofu ilimwingia
·         Peleka kwa MUNGU ili aking'oe kile kilicholetwa na ndoto maana ukikiacha kitakutesa sana

5.     Weka ulinzi wa DAMU ya YESU kwenye mlango wa ndoto ili shetani asiutumie kukuvuruga
Ayubu 33:14-16 “14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; 16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
·         MUNGU hufungua masikio(mlango) wa mtu ule wa ndani
·         Swala si tu DAMU ya YESU bali ni Imani inayotumika kuombea DAMU ya YESU
·         Ndoto ni lango lazima lilindwe kwa DAMU ya YESU ambaye ni PASAKA wetu. Kut 12:21-23, 1Kor 5:7-

MALANGO YAPO YA AINA 2 YA KUSHUGHULIKIA
        I.            Nafsi ya yule mtu na roho yake
      II.            Lango la pili ni lango la muda

·         Angalia ndoto unazoziota ni muda gani kawaida
·         Mara nyingi mlango mkubwa sana wa ndoto ngumu ni saa 9-10 usiku

6.      Ombea mahali unapolala au Omba TOBA kwa kuto-kupaombea ipasavyo unapolala na kupata mashambulizi kwa njia ya ndoto
Mwanzo 28:10-22 “10 Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. 11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. 12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.”

7.     Omba uponyaji kamili wa moyo na eneo uliloumia
Yeremia 6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.”Isaya 61:1
·         Omba mpaka upone
·         Omba mpaka MUNGU amekuonyesha umevuka
NJIA 2 ZA KUJUA
·         Imani yako. Utajua mafadhaiko na maangaiko yameondoka
·         Umepona mpaka mwili umekuwa mwepesi

8.      Omba MUNGU akusaidie kuondoka ulipokwama
·         Ndani ya ndoto utaonyeshwa umekwama wapi

9.      Futa maneno uliyotamkiwa kwenye ndoto ambayo ni kinyume na mapenzi ya MUNGU

Dan 4:13-17 “13 Nikaona katika njozi za kichwa changu kitandani mwangu, na tazama, mlinzi, naye ni mtakatifu, alishuka kutoka mbinguni. 14 Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake.
 15 Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi; 16 moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake. 17 Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.”

·         Omba urejeshewe vile vilivyo haribika kwa sababu ya jeraha lililotokea kwenye ndoto


Dan 4:34-37 “34 Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; 35 na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? 36 Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi. 37 Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.”