Monday, March 21, 2016

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE (Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam) SOMO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO NA WALIO NA HAJA YA KUPONA.

SIKU YA NANE

Mistari ya kusimamia: Isaya 61:1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.” Yeremia 6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.”

SOMO LA LEO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO KWASABABU YA KUCHOKA MOYONI KULE KUNAKOLETA KUKATA TAMAA.

1.     Nini maana ya kuchoka moyoni kunakoleta kukata tamaa?
Ø  Kukata tamaa ni maneno mawili. Kukata. Tamaa.
Ø  Tamaa maana yake ni hamu, kiu, msukumo, kiu  kutoka moyoni wa kutaka kupata unachotaka kukipata.
Ø  Kukata ni kuachanisha au kutenganisha kitu kunakoumiza kwa nia ya kuondoa muunganiko au mtiririko wa kitu.
Sasa kukata tamaa ni kitendo kinafanywa na mhusika wakati kukatishwa kinafanywa na mwingine.
Hivyo, Kukata tamaa maana yake Kuchoka moyoni kunakuja na maumivu kunakukuvunja nguvu kuendelea kufuatilia unachotaka kukifuatilia. Kunaondoa tarajio au tumaini. Matokeo ya kukata tamaa unakuona tu. Unaacha kufuatilia. Hapo ujue moyo umeumia. Utafutie msaada haraka.

2.     Moyo haukuumbwa ili uchoke. Kule kuchoka kunakokatisha tamaa
Isaya 40:28-31 “28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. 29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. 30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; 31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”
Mwanzo 1:26-27 “26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.”
Moyo haukuumbwa peke yake. Uliumbwa na uungu ndani yake. Kama Mungu hachoki kule kukata tamaa sio zao la moyo wa Mungu.  Kuokoka ni kuchukua sura ya Kristo. Ukiona umechoka moyo kuna shida. Usijifiche. Usijihesabie haki. Msalaba wa Yesu pekee unakupa dawa.

3.     Mifano ya kuchoka kwa moyo wa mtu kunakoleta kukata tamaa. Mifano kutoka kwenye Biblia.
Hatusomi somo hili kwakuwa tunazo notes! Ni kwasababu Mungu amelitoa kwa kusudi maalum kwa wakati huu, kama wewe haujavunjika moyo chukua somo hili kama chakula cha njiani kwani itakusaidia.

A.     Vita vya muda mrefu bila kupata ushindi uliotarajia.
1Samweli 31:3-4 “3 Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde. 4 Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.”

Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata, hata akafadhaika sana kwasababu ya wapiga upinde. Ndipo Sauli akamwambia yule mchukia silaha zake, futa upanga wako unichome nao, wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli ukautoa upanga wake akauangukia.
Moyo wake Sauli ndio uliomuua kutokana na mazingira. Mazingira yalimuua kabla ya upanga wake. Alifadhaika sana. Alipomwambia mbeba upinde wake amchome inaonyeshwa hakutaka kufa. Mazingira yalimuua.

1Wafalme 19:1-4
Mfalme Ahabu alimsimulia mkewe Yezebeli mambo yote aliyofanya Elia na jinsi alivyowaua manabii wa Baali kwa upanga. 2Yezebeli akatuma mjumbe kwa Elia amwambie: “Miungu waniulie mbali, nakuapia, ikiwa saa hizi kesho sitakuwa nimekufanya kama mmoja wa hao manabii.” 3Elia akakimbilia mjini Beer-sheba mkoani Yuda, alikomwacha mtumishi wake, 4naye akatembea mwendo wa siku nzima kuingia jangwani. Basi, akafika, akaketi chini ya mti mmoja, mretemu. Hapo, akaomba afe, akisema, “Imetosha! Siwezi tena. Ee Mwenyezi-Mungu, sasa utoe uhai wangu. Mimi si bora kuliko wazee wangu.”
Eliya anaomba kwa maneno magumu sana kwenye sala yake. Eliya yule yule tunayemuona kwenye sura iliyopita(18) akiwa na upako mwingi sana lkn anaumia moyo wake tena badala ya kusherekea ushindi. Vita kubwa kwa muhubiri sio jumamosi au jumapili bali jumatatu. Unapomuombea mtumishi mbele wakati wote

Zaburi 69:1-4 “1 Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. 2 Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha. 3 Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu. 4 Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.”
Unapokuwa kwenye maombi magumu na moyo wako unakata tamaa angalia ndoto zake sasa.
Mithali 24:10 “Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.”
Eliya alichoka kwakuwa hakuwa anakula chakula. Ndio yule malaika anamletea chakula. Wengi wanaishiwa nguvu sana kwakuwa wanajitahidi kutafuta mistari kwenye Biblia badala ya chakula. Kila kitu kinapaswa kuwa na uwiano. Malaika alimwambia kwanini anampa chakula. Kama wakristo wengi leo ambavyo wakila maneno ya Mungu jumapili wanalala mpaka jumapili tena. Wanalala kwenye mretemu

Ayubu 7:1-6 “1 Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa? 2 Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake; 3 Ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha. 4 Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke. 5 Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena. 6 Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.”
Wengi huwa tunawafikiria wanaotupiga vita. Lakini wewe lala ukimtumaini Bwana ingawa si rahisi kumtumaini wakati umevunjika moyo, jitahidi. Inapofika hapo ndipo tunapaswa kujilisha mapema Neno la Bwana wakati ukiwa salama halafu ukifika wakati wa shida unatumia tanki la akiba!

B.     Kuuchosha moyo kwa hasira na uchungu na kujikuta unalipa kisasi
Yeremia 6:11 “Lakini nimejaa ghadhabu ya Bwana; nimechoka kwa kujizuia; imwageni juu ya watoto walio njiani, na juu ya kusanyiko la vijana pia; maana hata mume atatwaliwa pamoja na mkewe, mzee pamoja na yeye aliyetimiza siku zake.”

Yeremia 15:6-7 “6 Umenikataa mimi, asema Bwana, umerudi nyuma; ndiyo maana nimenyosha mkono wangu juu yako, na kukuangamiza; nimechoka kwa kughairi. 7 Nami nimewapepea kwa kipepeo katika malango ya nchi nimewaondolea watoto wao, nimewaharibu watu wangu; hata hivyo hawakurudi na kuziacha njia zao.”

Yeremia amejawa na hasira ya Bwana. Anaogopa asiseme maana yatawapata mambo magumu sana. Ukiwa na cha Mungu unapaswa kuwa mwangalifu sana unachokiongea. Unaweza ukajikuta umekivaa kibwebwe umemvaa mtesi wako na kuokoka unaweka pembeni. Unahitaji hekima.
Hasira ni pepo. Usisubiri ishuke. Kemea litoke. Au ingia kwenye maombi hata kama ni kazini nenda chooni kaombe huko au kalie huko mbele za Bwana naye anachukua machozi yako na kukufariji.


C.      Kuuchosha moyo kwa kutafuta msaada kwa miungu mingine

Isaya 16:12 “Tena itakuwa, Moabu akionekana, na kujichosha kwa kulia juu ya mahali pa juu, na kuingia katika patakatifu pake aombe, hatapata kushinda.”

Isaya 47:12-15 “12 Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda. 13 Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata. 14 Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao. 15 Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatanga-tanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.”

Kuna watu wanatafuta msaada tangu ujana wao lakini wanatafuta kwa miungu mingine. Unauchosha moyo wako. Unakata tamaa ya maisha. Dawa ipo kwa Yesu tu. Hata ukienda kwa Yesu kama ni wa dini yoyote mfuate Yesu kama daktari basi. Ukishapona ndio utauliza dini!

D.     Kuchoka moyo kwa kuutafuta mlango
Mwanzo 19:11 “Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango.”
Kuna watu wamechoka mioyo kwakuwa wamechoka kuutafuta mlango. Nenda kwa Yesu maana ndiye mlango. (Yohana 10:1-9 “1 Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang'anyi……….. 9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.”)
Isaya 43:22 “Lakini hukuniita, Ee Yakobo, bali umechoka nami, Ee Israeli.”
Moyo uliovunjika unaondoa msukumo kabisa. Usione kama Mungu amekuangusha. Achana na marafiki wataabishaji. Wasikuondolee msukumo wa kumtafuta Mungu wako. Kama marafiki wa Ayubu.

Yesu kakupitisha kwenye mangapi miaka yote hii mpaka umkatie tamaa leo kwenye hilo tuu??!  Biblia inasema siku za mwisho kutakuwa kuna njaa ya neno la Mungu. Biblia zitakuwepo lkn maneno ya Mungu yakupayo tumaini ndio hayatakuwepo. Utazunguka kutafuta neno la Mungu hata ibada 4 asubuhi moja hutapata. Jilishe neno la Mungu sasa kuupa usalama moyo wako.

Ukichoka kushindana na dhambi unakuwa mtumwa wa dhambi. Una jisalimisha. Unahitaji kujisalimisha kwa Yesu. Vita ya jana sio ya leo. Mungu anakulisha chakula kipya kila siku. Wokovu sio dini mpya bali upya ndani yako. 

No comments: