Tuesday, October 16, 2018

LANGO LA MUDA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO KWAAJILI YA MAANDALIZI NA TOBA - Samson Mollel 0767 664 338




UTANGULIZI

Kuna wakati katika maisha ya mwanadamu Mungu anaruhusu mabaya yawapate watu kama tunavyosoma katika 2Wafalme 21:12“kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalia, naleta mabaya juu ya Yerusalemu na juu ya Yuda, hata kila mtu asikiaye, masikio yake yatawasha yote mawili.”

Lakini inawezekanaje Mungu anaruhusu mabaya wakati YEYE anawapenda wanadamu na hapendi kuwahuzunisha kama ilivyoandikwa katika Zaburi 145:8“Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,” vilevile Mungu anasema katika Maombolezo 3:31-33“31 Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. 32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. 33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.Wala kuwahuzunisha.”

Kabla Mungu hajaachilia jambo baya au zuri litokee katika maisha ya mwanadamu, Mungu anakawaida ya kutanguliza taarifa ili kutoa muda (Lango la Muda) wa maandalizi kabla ya jambo lolote halijatokea na kuleta madhara katika ulimwengu wa mwili.


KUHUSU MUDA  NA MAANA YAKE

Muda (sekunde/dakika/saa/siku/wiki/mwezi/mwaka/nyakati/majira) ni kitu cha kiroho kinachotoa nafasi ya maamuzi katika jambo Fulani liwe zuri au baya.


Muda unaweza kuibiwa na kufichwa hivyo unahitajika kukombolewa sawa na Neno la Mungu kutoka Waefeso 5:15-17 “15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. 17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.”

Mstari wa 17 unasema Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.” Kumbe kwa kutokufahamu yaliyo mapenzi ya Jehova katika maisha yako yanaletelezea kuwa mjinga!!! Ukiyafahamu mapenzi ya Mungu kwako (Yeremia 11:29) utajua kwamba kila jambo linalotokea Jehova amepanga mema kwako.


Muda ni lango linaweza kuruhusu ushindi au kushindwa/ kuanguka au kusimama/ kufa au kupona/ kuanguka au kusimama. Kila jambo linalotokea linakuwa na lango lake la muda wa kutokea kwake sawa na Neno la Mungu kutoka Muhubiri 3:1-2 “1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa;”


MIFANO YA LANGO LA MUDA LILIVYOTUMIKA KATIKA BIBLIA

1.       Wakati wa Yona (Lango la muda wa toba)

Yona 3:1-4 “1 Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema, 2 Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. 3 Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. 4 Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.”

Watu wa mji wa Ninawi walitenda maovu na Mungu alikusudia kuuangamiza mji wa Ninawi, lakini kabla ya kuuangamiza akawafungulia lango la muda kwa siku 40 ili warejee na kutubu Yona 3:4 “Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.

Mfalme wa Ninawi akafahamu namna ya kulitumia lango la muda vizuri kama tunavyosoma katika Yona 3:6-10 “6 Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. 7 Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; 8 bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. 9 Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe? 10 Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.


2.      Wakati wa Nuhu (Lango la muda wa toba)

Wakati wa Nuhu watu walimuasi sana Mungu na Mungu alikasirika sana na kuamua kuwafutilia mbali wanadamu wote isipokuwa Nuhu.

Mwanzo 6:1-7 “1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. …………………………… 5 Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. …………………. 7 Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.”

Mungu akamuambia Nuhu atengeneze safina, Muda (lango la muda) Nuhu alipoanza kuitengeneza safina mpaka ilipokamilika ilikuwa ni miaka mingi sana lakini watu wa wakati ule hawakuweza kulitumia vyema lango hilo.

Baada ya safina kukamilika Mungu alimuagiza Nuhu kuingia ndani ya safina yeye na familia yake na wanyama aliowachagua, na akampa muda wa siku saba (Lango la muda) kuingia kabla ya mvua kunyesha. Lakini watu wa wakati ule walishindwa kulitumia lango la muda kwaajili ya kufanya toba na kurejea kwa Mungu wakaangamia.

Mwanzo 7:1-4 “1 Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. ……….………………... 4 Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.”


3.      Wakati wa Lutu (Lango la muda wa toba)

Wakati wa Lutu katika miji ile ya Sodoma na Gomora Mungu aliamua kuiteketeza kwa moto, lakini kabla ya kufanya hivyo Mungu alimuambia Ibrahamu mpango wake huo na Ibrahimu akajaribu kwa sehemu kuomba Mungu aufute lakini aliishia njiani katika maombi yake na hatimaye miji ile ikateketezwa kwa moto kama tunavyosoma katika

Mwanzo 18:23-33 “23 Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? 24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? …………………32 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. 33 Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake.”


4.      Ndoto za Yusufu (Lango la muda wa maandalizi)

Yusufu alianza kuona maono ya maisha yake ya baadae miaka mingi sana kabla ya kuyafikia maono yenyewe

Mwanzo 37:5-11 “5 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; 6 akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. 7 Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. 8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. 9 Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia. 10 Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi? 11 Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili.”

Hapo Yusufu alikuwa na umri wa miaka 17 kama tunavyosoma katika Mwanzo 37:2 “Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya.”

Miaka 13 baadae (lango la muda) Yusufu alikuwa ni waziri mkuu wa nchi ya Misri na ndugu zake walikuja na kumsujudia kama alivyoota.

Mwanzo 41:41-44,46 “41 Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. 42 Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake. 43 Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri. 44 Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri. 46 Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akapita katika nchi yote ya Misri.”


5.      Ndoto za Farao (Lango la muda wa maandalizi)

Mwanzo 41:1-36 “1 Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto…..…………… 26 Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja. 27 Na wale ng'ombe saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba; na yale masuke saba matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yatakuwa miaka saba ya njaa. 28 Ndivyo nilivyomwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu. 29 Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri. 30 Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi. 31 Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana. 32 Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi. 33 Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. …………….. 35 Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. 36 Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa.”


6.      Ndoto za wafanyakazi wa Farao (Lango la muda wa toba na maandalizi)

Mwanzo 40:5-18 “5 Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. 6 Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika. ………………..12 Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu. 13 Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake. ………………… 16 Mkuu wa waokaji alipoona ya kwamba hiyo tafsiri ni ya mema, akamwambia Yusufu, Mimi kadhalika nilikuwa katika ndoto yangu, na tazama, ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu ya kichwa changu. 17 Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu. 18 Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu.”

Katika ndoto hizi mbili za siku moja zenye maana tofauti, tunaona mnyweshaji akipewa siku tatu za maandali ya kurudi kwenye kazi yake ya zamani na mwokaji akipewa siku tatu za kutubu lakini bila ya kujua hakutubu na wala hatuoni akimwambia Yusufu amuombee kwa Mungu wake ili aepukane na tatizo lililopo mbele yake.


7.      Ndoto ya mfalme Nebukadreza (Lango la muda wa toba)

Daniel 4:1-37 “……..24 tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme; 25 ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng'ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote. 26 Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala. 27 Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha. 28 Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza. 29 Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. 30 Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu? 31 Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako”

Mfalme Nebukadreza aliota ndoto na tafsiri yake ni kama ilivyotolewa na nabii Daniel. Katika tafsiri hiyo mfalme anaombwa na nabii Daniel kwamba aache uovu ili neema ya Mungu impate na akasamehewe kama tunavyosoma katika Danieli 4:27Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha”lakini anaghairi na kuendelea na uovu.

Lakini Mungu akampa muda wa kufanya toba wa miezi 12 lakini bado hakufanya toba na mabaya yakampata

MAOMBI YA KUOMBEA LANGO LA MUDA ULILOPEWA KUJIANDAA AU KUOMBA TOBA.

ü  Omba toba na msamaha kwa Yesu kwa matumizi mabaya ya lango la muda (Zaburi 145:8 “Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,” vilevile Mungu anasema katika Maombolezo 3:31-33 “31 Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. 32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. 33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.Wala kuwahuzunisha.”)

ü  Achilia damu ya Yesu kwenye lango la muda wa toba ambalo haukulitumia inavyostahili na madhara yakatokea


ü  Achilia damu ya Yesu kwenye lango la muda wa maandalizi ambalo haukulitumia inavyostahili na ukapata jambo la kukushtukiza kwa kutokujiandaa kwako

ü  Achilia damu ya Yesu kufuta madhara yaliyotokana na kutokutumia lango la muda inavyostahili


ü  Kwa jina la Yesu amuru mapepo yaliyoshikilia lango lako la muda kuchilia sasa (Komboa wakati kwa jina la Yesu)