UTANGULIZI
Kuna wakati katika
maisha ya mwanadamu Mungu anaruhusu mabaya yawapate watu kama tunavyosoma
katika 2Wafalme 21:12“kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wa Israeli,
asema hivi, Angalia, naleta mabaya juu ya Yerusalemu na juu ya Yuda, hata kila
mtu asikiaye, masikio yake yatawasha yote mawili.”
Lakini inawezekanaje
Mungu anaruhusu mabaya wakati YEYE anawapenda wanadamu na hapendi kuwahuzunisha
kama ilivyoandikwa katika Zaburi 145:8“Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si
mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,” vilevile Mungu anasema katika Maombolezo 3:31-33“31 Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. 32 Maana ajapomhuzunisha
atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. 33 Maana moyo wake hapendi
kuwatesa wanadamu.Wala kuwahuzunisha.”
Kabla Mungu hajaachilia
jambo baya au zuri litokee katika maisha ya mwanadamu, Mungu anakawaida ya
kutanguliza taarifa ili kutoa muda (Lango la Muda) wa maandalizi kabla ya jambo
lolote halijatokea na kuleta madhara katika ulimwengu wa mwili.
KUHUSU MUDA NA MAANA YAKE
Muda
(sekunde/dakika/saa/siku/wiki/mwezi/mwaka/nyakati/majira) ni kitu cha kiroho
kinachotoa nafasi ya maamuzi katika jambo Fulani liwe zuri au baya.
Muda unaweza kuibiwa na
kufichwa hivyo unahitajika kukombolewa sawa na Neno la Mungu kutoka Waefeso 5:15-17 “15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na
hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi
ni za uovu. 17 Kwa sababu hiyo msiwe
wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.”
Mstari wa 17 unasema “Kwa
sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.” Kumbe
kwa kutokufahamu yaliyo mapenzi ya Jehova katika maisha yako yanaletelezea kuwa
mjinga!!! Ukiyafahamu mapenzi ya Mungu kwako (Yeremia 11:29) utajua kwamba kila
jambo linalotokea Jehova amepanga mema kwako.
Muda ni lango linaweza
kuruhusu ushindi au kushindwa/ kuanguka au kusimama/ kufa au kupona/ kuanguka
au kusimama. Kila jambo linalotokea linakuwa na lango lake la muda wa kutokea
kwake sawa na Neno la Mungu kutoka Muhubiri
3:1-2 “1 Kwa kila jambo kuna majira
yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 2 Wakati wa kuzaliwa, na
wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa;”
MIFANO YA LANGO LA MUDA LILIVYOTUMIKA
KATIKA BIBLIA
1.
Wakati wa Yona (Lango
la muda wa toba)
Yona 3:1-4 “1
Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema, 2 Ondoka, uende Ninawi, mji
ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. 3 Basi Yona akaondoka, akaenda
Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake
mwendo wa siku tatu. 4 Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza
sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.”
Watu wa mji wa
Ninawi walitenda maovu na Mungu alikusudia kuuangamiza mji wa Ninawi, lakini
kabla ya kuuangamiza akawafungulia lango la muda kwa siku 40 ili warejee na
kutubu Yona 3:4 “Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake,
akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi
utaangamizwa.”
Mfalme wa Ninawi
akafahamu namna ya kulitumia lango la muda vizuri kama tunavyosoma katika Yona 3:6-10 “6 Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake
cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.
7 Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme
na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya
ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; 8 bali na
wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa
nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio
mikononi mwake. 9 Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha
hasira yake kali, ili msiangamizwe? 10 Mungu akaona matendo yao, ya kuwa
wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu
akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.”
2.
Wakati
wa Nuhu (Lango la muda wa toba)
Wakati wa Nuhu watu
walimuasi sana Mungu na Mungu alikasirika sana na kuamua kuwafutilia mbali
wanadamu wote isipokuwa Nuhu.
Mwanzo
6:1-7 “1 Ikawa
wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2
wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia
wake wo wote waliowachagua. …………………………… 5 Bwana akaona ya kuwa maovu ya
mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni
baya tu sikuzote. …………………. 7 Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu
niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa
angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.”
Mungu akamuambia Nuhu
atengeneze safina, Muda (lango la muda) Nuhu alipoanza kuitengeneza safina
mpaka ilipokamilika ilikuwa ni miaka mingi sana lakini watu wa wakati ule
hawakuweza kulitumia vyema lango hilo.
Baada ya safina
kukamilika Mungu alimuagiza Nuhu kuingia ndani ya safina yeye na familia yake
na wanyama aliowachagua, na akampa muda wa siku saba (Lango la muda) kuingia
kabla ya mvua kunyesha. Lakini watu wa wakati ule walishindwa kulitumia lango
la muda kwaajili ya kufanya toba na kurejea kwa Mungu wakaangamia.
Mwanzo
7:1-4 “1 Bwana
akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana
nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. ……….………………... 4 Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea
dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai
nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.”
3.
Wakati
wa Lutu (Lango la muda wa toba)
Wakati wa Lutu katika
miji ile ya Sodoma na Gomora Mungu aliamua kuiteketeza kwa moto, lakini kabla
ya kufanya hivyo Mungu alimuambia Ibrahamu mpango wake huo na Ibrahimu
akajaribu kwa sehemu kuomba Mungu aufute lakini aliishia njiani katika maombi
yake na hatimaye miji ile ikateketezwa kwa moto kama tunavyosoma katika
Mwanzo
18:23-33 “23 Ibrahimu
akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? 24 Huenda
wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili
ya hao hamsini wenye haki waliomo? …………………32 Akasema, Bwana asiwe na hasira,
nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu
kwa ajili ya hao kumi. 33 Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu,
akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake.”
4.
Ndoto
za Yusufu (Lango la muda wa maandalizi)
Yusufu alianza kuona
maono ya maisha yake ya baadae miaka mingi sana kabla ya kuyafikia maono
yenyewe
Mwanzo
37:5-11 “5 Yusufu
akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; 6 akawaambia,
Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. 7 Tazama, sisi tulikuwa tukifunga
miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda
yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. 8 Ndugu zake wakamwambia, Je!
Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa
ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. 9 Akaota tena ndoto nyingine,
akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama,
jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia. 10 Akawaambia baba yake na
ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je!
Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi? 11 Ndugu zake
wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili.”
Hapo Yusufu alikuwa na
umri wa miaka 17 kama tunavyosoma katika Mwanzo
37:2 “Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo.
Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na
saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana
pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea
baba yao habari zao mbaya.”
Miaka
13 baadae (lango la muda) Yusufu alikuwa ni waziri mkuu wa nchi ya Misri na
ndugu zake walikuja na kumsujudia kama alivyoota.
Mwanzo 41:41-44,46
“41 Farao akamwambia Yusufu, Tazama,
nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. 42 Farao akavua pete yake ya muhuri
mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na
kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake. 43 Akampandisha katika gari lake la
pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo
akamweka juu ya nchi yote ya Misri. 44 Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao,
na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri. 46
Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme
wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akapita katika nchi yote ya
Misri.”
5. Ndoto za Farao (Lango la muda wa
maandalizi)
Mwanzo 41:1-36
“1 Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima,
Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto…..…………… 26 Wale ng'ombe
saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja.
27 Na wale ng'ombe saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba;
na yale masuke saba matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yatakuwa miaka
saba ya njaa. 28 Ndivyo nilivyomwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha
Farao atakayoyafanya hivi karibu. 29 Tazama, miaka saba ya shibe inakuja,
katika nchi yote ya Misri. 30 Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na
shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi. 31
Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye,
maana itakuwa nzito sana. 32 Na ndoto ya
Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu
amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi. 33 Basi, Farao na ajitafutie
mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. …………….. 35 Na wakusanye
chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa
Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. 36 Na hicho chakula kitakuwa akiba
ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri,
nchi isiharibike kwa njaa.”
6. Ndoto za wafanyakazi wa Farao (Lango
la muda wa toba na maandalizi)
Mwanzo 40:5-18
“5 Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu
ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na
mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. 6 Yusufu akawajia asubuhi,
akawaona wamefadhaika. ………………..12 Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii.
Matawi matatu ni siku tatu. 13 Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako,
atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama
desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake. ………………… 16 Mkuu wa waokaji
alipoona ya kwamba hiyo tafsiri ni ya mema, akamwambia Yusufu, Mimi kadhalika
nilikuwa katika ndoto yangu, na tazama, ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu
ya kichwa changu. 17 Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula
kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu. 18
Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu.”
Katika
ndoto hizi mbili za siku moja zenye maana tofauti, tunaona mnyweshaji akipewa
siku tatu za maandali ya kurudi kwenye kazi yake ya zamani na mwokaji akipewa
siku tatu za kutubu lakini bila ya kujua hakutubu na wala hatuoni akimwambia
Yusufu amuombee kwa Mungu wake ili aepukane na tatizo lililopo mbele yake.
7. Ndoto ya mfalme Nebukadreza (Lango
la muda wa toba)
Daniel
4:1-37 “……..24 tafsiri yake ni hii, Ee
mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme; 25 ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na
makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula
majani kama ng'ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba
zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki
katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote. 26 Na kwa kuwa
waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako,
baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala. 27 Kwa sababu hiyo, Ee
mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda
haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa
siku zako za kukaa raha. 28 Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza. 29 Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa
akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. 30 Mfalme akanena,
akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme,
kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu? 31 Hata neno lile
lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee
mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako”
Mfalme
Nebukadreza aliota ndoto na tafsiri yake ni kama ilivyotolewa na nabii Daniel.
Katika tafsiri hiyo mfalme anaombwa na nabii Daniel kwamba aache uovu ili neema
ya Mungu impate na akasamehewe kama tunavyosoma katika Danieli 4:27 “Kwa sababu
hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa
kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata
kuzidishiwa siku zako za kukaa raha”lakini anaghairi na kuendelea na
uovu.
Lakini
Mungu akampa muda wa kufanya toba wa miezi 12 lakini bado hakufanya toba na
mabaya yakampata
MAOMBI YA KUOMBEA LANGO LA MUDA ULILOPEWA KUJIANDAA AU KUOMBA TOBA.
ü Omba
toba na msamaha kwa Yesu kwa matumizi mabaya ya lango la muda (Zaburi 145:8 “Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni
mwingi wa rehema,” vilevile Mungu anasema katika Maombolezo 3:31-33 “31 Kwa
kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. 32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa
kadiri ya wingi wa huruma zake. 33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa
wanadamu.Wala kuwahuzunisha.”)
ü Achilia
damu ya Yesu kwenye lango la muda wa toba ambalo haukulitumia inavyostahili na
madhara yakatokea
ü Achilia
damu ya Yesu kwenye lango la muda wa maandalizi ambalo haukulitumia
inavyostahili na ukapata jambo la kukushtukiza kwa kutokujiandaa kwako
ü Achilia
damu ya Yesu kufuta madhara yaliyotokana na kutokutumia lango la muda
inavyostahili
ü Kwa
jina la Yesu amuru mapepo yaliyoshikilia lango lako la muda kuchilia sasa
(Komboa wakati kwa jina la Yesu)
No comments:
Post a Comment