NINI MAANA
YA MALENGO?
Malengo
ni hatua Fulani katika maisha ya mtu ambayo hajaifikia na anatarajia kuifikia.
Jambo la msingi unalopaswa kulielewa; Ni muhimu kulifahamu lengo lako vizuri
ambalo unatakiwa kulifikia. Ni vizuri ulifafanue vizuri lengo lako ili
lieleweke kwani ufafanuzi mzuri wa lengo/malengo yako utakusaidia katika
kujiwekea mikakati mizuri ya utekelezaji.
Ni
vizuri kujua mahitaji ili kufikia malengo yako, hii itakusaidia ili ujue
unatakiwa kuomba nini na kwa kiasi gani.
Mtu
wa Mungu tuutazame mfano wa Hana katika Biblia na namna alivyo muomba Mungu (1Samweli 1:1-20)
1. Hana alijua
kuwa alikuwa na lengo kubwa (Kuomba mtoto kwa Mungu) hivyo alisukuma maombi
mwaka baada ya mwaka-1Samweli 1:3
(sio siku moja, sio mwezi mmoja, sio mwaka mmoja ni miaka ilipita). Uchokozi wa
Penina haukumkatisha tamaa bali ulikuwa ni mtaji (chachu) kwa Hana na akendelea
kushughulikia lengo lake.
Inawezekana wewe mtu wa Mungu unatafuta mume/mke lakini siku ya
kwanza ulipotukanwa au kudhalilishwa kwamba hautaolewa/hautaoa basi umekiri na
kukubali kabisa kwamba kwakuwa miaka imepita mingi basi siwezi kufanikiwa tena;
Hapana usikate tamaa angalia malengo yako (stay focused) kwani unapoongea
maneno ya kujifunga shetani anaenda nayo mbele za Mungu kukushitaki (Mithali 18:20-21 “20 Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya
midomo yake. 21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao
watakula matunda yake.”). Wana wa Mungu wengi wamejifunga wenyewe kutofikia
malengo yao
2. Fahamu
kwamba wapo watu ambao wataendelea kukupa moyo ili uridhike na hali mbaya ya
maisha uliyonayo na kuishia kuteseka bila kufikia malengo. Hana alijua kuwa
sadaka na maneno mazuri aliyopewa na Elikana (mume wake) ni kitanzi cha
kuendelea kukaa katika hali ngumu (1Samweli
1:4-8), yaani vilimfanya akubaliane na matatizo yake kuwa ni sehemu ya
maisha yake. Mtu wa Mungu amka na umgeukie BWANA ili uweze kutimiza malengo
yako ya miaka mingi katika mwaka huu 2017 kama alivyofanya Hana (1Samweli 1:9-10).
3. Jambo
lingine napenda kukukumbusha mtu wa Mungu kuhusu kuweka nadhiri, kuweka nadhiri
lazima upime gharama ya nadhiri yako. Wapo watu kutokana na uzito wa matatizo
yao wameweka nadhiri kwa Mungu, halafu malengo yao yanapotimia wanasahau
kuondoa nadhiri zao na kumsahau Mungu (Kumbukumbu
8:12-14 “12 Angalia, utakapokuwa
umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; 13 na makundi
yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako
itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka; 14 basi hapo moyo
wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri,
katika nyumba ya utumwa;”)
4. Jambo
jingine ambalo unahitaji kujua ili kufikia malengo yako nmna ya kukabiliana na
dharau ya kuhani (Mchungaji, Padre, Shemasi, Kasisi, Mwinjilisti, Katekista,
Nabii, Mtume n.k). Tunamuona kuhani Eli anamwita Hana kuwa ni mlevi (1Samweli 1:14), lakini Hana hakuumizwa
na dharau ya kuhani bali alizidi kuwa
mnyemnyekevu na kumtazama BWANA ili lengo lake litimie. Kuna watu wanatathimini
mazingira yako ya maombi na kukuambia mambo ya kukukatisha tamaa, usikate tama
songa mbele na malengo yako
5. Ni muhimu
kuomba mpaka ufikie malengo yako, fahamu kuwa unapoona dalili za kufikia
malengo sio uhakika ya kwamba malengo yametimia (Yaani kupata mimba sio kupata mtoto) unahitajika kuendelea kuomba
bila kukoma mpaka maleengo yako yatimie. Kumbuka unapoomba madhabahuni,
unapofanikiwa rudi madhabahuni kumshukuru Mungu.
ü Kwa
muombaji/mwanamaombi ni vyema kuweka malengo mapema kabla ya mwaka mpya
haujaingia na kama ulikuwa na malengo ya mwaka unaomalizikia fanya tathimini
kwanza kisha fanya maamuzi ya kuweka malengo mapya. Inawezekana mpaka sasa
ulikuwa haujaweka malengo kwa mwaka huu mpya 2017, bado unaweza kuweka malengo
yako na ukapanga mikakati ya utekelezaji.
ü Kumbuka kuwa
matatizo au changamoto ulizokabiliana nazo mwaka jana (2016) zifanye ziwe mtaji
wa kukuongezea umakini unapoweka malengo mapya mwaka huu mpya 2017. Kuna
waombaji/wanamaombi wengine changamoto walizokutana nazo katika
huduma/kazi/ndoa/biashara n.k. zimewavunja moyo kabisa na hawawezi kuendelea
tena na yale malengo ambayo hawajayafikia; mkumbuke Hana alivyoweza kugeuza
changamoto kuwa mtaji wake *(1Samweli
1:1-20)* Hana aliomba kwa bidii
kubwa pamoja na ukweli kwamba alitukanwa sana na kudharauliwa na kuchokozwa na
Rebeka.
ü Fahamu pia
kwamba ni hatari sana kubaki unafikiri au unawaza juu ya matatizo yaliyokupata
au yaliyopo katika kukamilisha malengo yako, jambo la kufanya ni kufikiri zaidi
juu ya kukabiliana na matatizo na kusonga mbele.
ü Ukweli ni
kwamba malengo yanafungwa ndani ya muda, ukiweka malengo pia upange na mikakati
na jinsi ya kuitekeleza hiyo mikakati ndani ya muda maalum; yaani kila lengo
lipe muda wa utekelezaji wake *(Muhubiri
3:1-8 _“1 Kwa kila jambo kuna majira
yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu………………………..”)_* Fahamu
majira na nyakati katika utekelezaji wa malengo yako; yaani kama wewe ni
mkulima lazima ulime na kupanda kwa kufuata kalenda ya kilimo kwa zao husika na
sio upande wakati wa palizi au uaplilie wakati wa kuvuna, fahamu mafanikio ya
malengo yako yamefungwa na muda. Kwasababu hiyo, Muda ni ufunguo muhimu sana wa
kukusaidia kufikia malengo yako; kwahiyo lazima ujifunze kufikiri ki-muda na kufanya
kazi kwa kufuata muda.
*MAMBO
MATANO MUHIMU KATIKA KUPANGA MALENGO*
A. Weka malengo
yako mapema kwa kufuata vipaumbele vya kwako kwa uongozi wa Roho Mtakatifu
B. Weka
mikakati ya kukusaidia kutekeleza lengo lako kwa uongozi wa Roho Mtakatifu
C. Fanya
tathimini ya utekelezaji wa malengo yako kila baada ya muda kwa uongozi wa Roho
Mtakatifu
D. Boresha
malengo yako kwa kadiri muda unavyokwenda kwa kuzingatia tathimini uifanyayo
mara kwa mara kwa uongozi wa Roho Mtakatifu
E. Jenga mazoea
ya kuyasoma na kufanya tafakari juu ya malengo yako mara kwa mara na
kuwashirikisha watu wanaoweza kukusaidia kwa uongozi wa Roho Mtakatifu
*MUHIMU:*
v Kumbuka kuwa
mtu aliye mwana wa Mungu hawezi kuweka malengo yeye binafsi kwasababu yeye (mtu
aliyeokoka) anao ubia (Ushirika) na Mungu kuanzia rohoni hadi mwilini, yaani
kwa kila kitu anachokifanya lazima amshirikishe Mungu. *(Yohana 14:23, 15:1-8, Wakolosai 1:29)*
v Fahamu
kwamba kuwa mwanamaombi haimaanishi kuwa haupaswi kutumia akili kwani unapokosa
akili unakuwa mpumbavu *(Mathayo 7:24)*
na hata kama utaomba kiasi gani pasipo kutumia akili na maarifa hauwezi kufikia
malengo (Hosea 4:6)
v Kila unachotaka
kufanya lazima umuulize Mungu kama ndilo kusudi lake ufanye jambo hilo au lah!
Kwani unapokuwa umeokoka sio wewe tena bali ni Yesu aishiye ndani yako. Hapo
ulipo mtu wa Mungu upo pamoja na Mungu *(Yohana 14:23)* hivyo kila
unachokifanya umshirikishe Mungu.
v Kwahiyo
jifunze kushirikiana na Roho Mtakatifu katika kila hatua za maisha yako,
ukifanya hivyo utakuwa katika mahali pazuri katika hatua za maisha yako *(Warumi 8:12-17)*. Ni muhimu kutambua
kuwa unaishi kwaajili ya kutimiza kusudi la Mungu na sio la kwako, ukijua hilo
utatafuta malengo ya Mungu zaidi kuliko malengo yako binafsi *(Waefeso 2:8-10, Yeremia 1:4-10)*.
Katika
miili yetu (Damu na nyama) tumebebeshwa sheria ya mwili inayotupele kinyume na
mapenzi ya Mung (yaani kuikataa sheria ya Mungu); kwasababu hiyo kuna watu
wanaotegemea kuongozwa na Roho Mtakatifu wakati wa Ibada, lakini katika mambo
mengine ya maisha hawapo na Roho Mtakatifu. Mungu anachosema ni kwamba
unapomkubali Yesu unaingia kwenye Mkataba na Mungu *(Yohana 14:23)*, Roho Mtakatifu anakuwa ndiye kiongozi wetu na
unapomshirikisha ROHO hautaweza kukwama.
Kumbuka
hata Yesu aliongozwa na ROHO kwenda jangwani, na kama ROHO alimuongoza kwenda
kujaribiwa vilevile ROHO alimuongoza kujibu/kushinda mitego ya shetani.
*_KWANINI
UNATAKIWA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUPANGA MALENGO YA MWAKA HUU MPYA
2017 NA SIO KUONGOZWA NA AKILI AU MAWAZO YAKO?_*
1.
*ILI
TUSITIMIZE TAMAA ZA MWILI*
*(Wagalatia
5:16, Warumi 8:7)*
Kwa
kawaida mwili huwa na “mvutano” na Roho wa Mungu. Roho wa Mungu atakuongoza
katika njia yake na mwili nao utakuongoza katika njia zake, hivyo nafsi yako
inategemea ni roho yupi kapewa kipaumbele. Kumbuka siku zote Roho Mtakatifu na
roho ya shetani, wote hutumia nafsi ya mwanadamu kupeleka kwenye mawazo ili
kuchujwa, na ufahamu kuwa nia ya mwili imebeba uadui juu ya Mungu. Unapoongozwa
na Roho Mtakatifu unaweza kuushinda ulimwengu na ukafanya mambo sawa sawa na
mapenzi ya Mungu. Bila kuongozwa na Mungu ile nia ya mwili itakutawala na
kukufanya ufuate mambo ya dunia na hautaweza kufanya mapenzi ya Mungu.
2.
*ILI TUPATE
KUYAELEWA MAFUMBO YA MUNGU*
Moja
ya sababu ya muhimu ya kuongozwa na roho mtakatifu katika kupanga malengo ya
mwaka huu mpya 2017, ni ili uweze kuayelewa mafumbo ya Mungu na kuatafakari
mambo ya rohoni katika roho. Roho wa Mungu ndiye mwenye ufahamu na kuyachunguza
na kuyafasiri mambo ya rohoni na kutusaidia kuelewa kilichopo (Makusudi ya
Mungu) kwenye ufalme wa Mungu kuhusu wewe na mipango yako ya kila siku
Roho
Mtakatifu akiisha kukufahamisha malengo unayopaswa kuweka, anakusaidia katika
kuyatekeleza ili yalete faida juu ya maisha yako. *(1Wakorintho 2:10)*
3.
*ILI TUPATE
KUYAJUA TULIYOKIRIMIWA NA MUNGU*
Jambo
lingine linalo jibu swali la kwanini unatakiwa kuongozwa na Roho Mtakatifu
katika kupanga malengo ya mwaka huu mpya 2017, ni ili upate kuyajua yale
uliyokirimiwa na Mungu na kuyapokea mambo ya roho wa Mungu kwa uaminifu (1Wakorintho 2:10-16).
Yapo
mambo ambayo ni lugha ya rohoni sana kiasi ambacho hata Mungu akisema na wewe
hauwezi kuelewa, ukikubali kuongozwa na Roho Mtakatifu; yeye ROHO atakupa
kuyajua yote ambayo Mungu amekukirimia katika maisha yako kwa ujumla.
Unapokubali
kuongozwa na Roho Mtakatifu ndipo unapopata msaada wa kujijua wewe mwenyewe,
maana atakusaidia kujua tabia yako, Baraka zako na uelekeo wako wa maisha ya
sasa nay a baadae. Nje ya Roho Mtakatifu ni vigumu kutambua hayo, ukiwa ndani
ya Roho Mtakatifu atakusaidia kufanya kazi pamoja nawe katika kila hatua *(Zaburi 32:8)*.
4.
*ILI
ATUSAIDIE KUOMBA YALE TUNAYOTAKIWA KUOMBA*
Sababu
nyingine ya kuongozwa na Roho Mtakatifu ni ili ROHO atusaidie kuomba yale
tunayotakiwa kuomba kwa wakati ule. Mtu wa Mungu usijijengee mfumo wa kuomba
kwa mazoea kwa kufuata ratiba ulizopanga wewe, lazima umruhusu ROHO akuongoze
kuomba kwa wakati unaostahili, ROHO akikuambia uombe usisubiri mpaka muda
uliopanga wewe ndio uombe; ukifanya hivi hautaweza kuyafikia malengo yako kwa
mwaka huu mpya.
Unapokataa muongozo wa Roho Mtakatifu basi
yeye (ROHO) anakuacha na wewe na unaanza kuwa dhaifu katika kutekeleza mikakati
ya kufanikisha malengo yako, udhaifu unatokana na kushindwa kumruhusu ROHO
aongoze maisha yako, Roho Mtakatifu anapoacha kuongoza maisha yako utaona hizi
ishara:-
v Sio rahisi
kuomba kwa muda mrefu na wakati mwingine unavutwa na mawazo mbalimbali
(Mfano:-Matatizo ya siku hiyo au changamoto unazokabiliana nazo katika maisha
yako).
v Kushindwa
kuomba jinsi itupasavyo. Unapomshirikisha Roho Mtakatifu anatusaidia kuomba
itupasavyo na anatuwezesha hata tunapochoka, pia anatufundisha namna ya kuomba
na anatuongoza yapi tuyaombee kwa wakati huu. Pia ROHO anatufunulia vita
iliyoko mbele yetu na kufundisha namna ya kuishinda. *(Warumi 8:26-27, 1Yohana 5:13-15)*
5.
*ILI
ATUONGOZE KATIKA KUFANYA MAAMUZI*
Hakuna
namna unayoweza kufanya maamuzi sahihi kama ndani yako hauna msaada wa Roho
Mtakatifu, bila Roho Mtakatifu utavutwa na tama za mwili, utavutwa na shetani
kisha utafanya maamuzi mabaya.
Kufanya
maamuzi ni sehemu ya maisha ya mwanadamu, yako maamuzi mengi sana ambayo
anatakiwa kuyafanya na hawezi kuyakwepa; maamuzi hayo yatafanyika kwa usahihi
tu kama utakuwa na Roho Mtakatifu ndani yako na kumruhusu akusaidie kufanya
maamuzi yako. *(2Wakorintho 3:17, Warumi
8:1-2, Kumbukumbu 16:18-20, 17:8-13)*
Unaweza
kumzuia Roho Mtakatifu asikuongoze, Roho Mtakatifu ni Mungu mwenye nguvu zote
na maarifa yote, Yeye pia (ROHO) anayo hiari ya kufanya kazi na mtu. Kumbuka
kuwa Roho Mtakatifu ni msaidizi kwetu (Yaani yupo mwenye majukumu {wewe} lakini
yeye ROHO anasaidia) *[Yohana 4:24,
14:18-23, 1Wakorintho 3:16-17, 6:19-20, 2Wakorintho 6:16]*
*MUHIMU:* Fahamu ya
kuwa unaweza ukamzimisha Roho Mtakatifu ndani yako *(1Wathesalonike 5:19)*; unamzimisha Roho Mtakatifu kwa kukataa
uongozi wake kwani yeye ROHO halazimishi kukuongoza ila anatamani mfanye
mashauriano kwa kila jambo *(Yohana
14:16)*
Samson Mollel 0767 664
338
_Uzima
wa Milele International Ministries (Yohana 17:3)_
*_www.uzimawamileleministries.blogspot.com_*