Friday, June 10, 2016

SEMINA YA MANA - MOROGORO Na Mwl. Chritopher Mwakasege (08-12/06/2016) SOMO: KUA KATIKA NEEMA ILI UNUFAIKE NA MSALABA

SEMINA YA MANA - MOROGORO Na Mwl. Chritopher Mwakasege (08-12/06/2016)
SOMO: KUA KATIKA NEEMA ILI UNUFAIKE NA MSALABA

Katika semina hii inayoendela hapa mjini Morogoro katika viwanja vya sule ya sekondari Morogoro, Mwalimu Christopher Mwakasege anafundisha somo “KUA KATIKA NEEMA ILI UNUFAIKE NA MSALABA” Semina hii unaweza kusikiliza live kupitia Top radio – Morogoro, Radio sauti ya Injili – Moshi (Inayosikika mikoa mbalimbali) na pia kwenye mtandao kwa njia ya sauti na video (www.mwakasege.org)

SIKU YA PILI (09/06/2016)
Somo linaongozwa na Neno kutoka:-
2Petro 3:18 “Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.”
2Timoth 2:1 “Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.”
Kumbuka kuwa NEEMA ni jambo unalopewa bila ya kulifanyia kazi (Warumi 4:4-6 “4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. 5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki. 6 Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,” )

UHUSIANO JUU YA NEEMA NA KUHESABIWA HAKI NA FAIDA ZAKE KWETU
Mambo muhimu ya kuangalia

1.     Neema tumeipokea toka kwa Yesu tunapompokea mioyoni mwetu
Yohana 1:14-17 “14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. 15 Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 16 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. 17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.”

2.     NEEMA hii kazi yake mojawapo ni kukupa kuhesabiwa haki
Tito 3:7 “ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.”
Warumi 3:24 “wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;”
Neema ndiyo inayotupa kuhesabiwa haki, kati ya kitu kimojawapo kilichobebwa na NEEMA tunapompokea Yesu ni kuhesabiwa haki bure! Hii ni kwasababu yupo aliyefanya kazi tayari kwa niaba yako (yaani Yesu), hivyo wewe ni jukumu lako kuamini na kupokea haki.

3.     Madhara ya dhambi katika kukunyima haki zako toka kwa Mungu
Neno haki ni la kimahakama, kwa tafsiri rahisi haki maana yake ni lililo lako kihalali kufuatana na sheria na hukumu za Mungu kama hakimu au kinachofanya hicho kitu kiwe chako ni kwasababu ya hukumu na sheria ziko upande wako.
Mungu alimuumbamtu na haki zake (haki za mtu). Sio kila mtu anaelewa madhara ya dhambi katika ilikuwa haki yake, au sio kila mtu anaelewa ni nini kilichopotea baada ya dhambi kuingia, na kama hujui kilichopotea (haujui haki yako) hauwezi kudai kwakua hauna cha kudai (kwasababu ya kutojua).

Baadhi ya haki mtu alizopoteza baada ya dhambi kuingia

i.                    Uzima wa Mungu ndani ya mtu
Mtu alipotenda dhambi, uzima wa Mungu ulipotea ndani yake (Mwanzo 2:16-17 “16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”. hii ni kwasababu mshahara wa dhambi ni mauti, yaani kutengwa na uzima wa Mungu (Rumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”)
Warumi 5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;”
Uasi ni kuenda kinyume cha utaratibu uliopo (1Yohana 3:4 “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.”)
Unapotenda dhambi unapoteza uzima wa Mungu, unapopoteza uzima wa Mungu unapoteza kile kilichopo ndani ya uzima. Uzima ulimpa mtu umilele alipopoteza uzima mauti ikatokea (Uzima wa milele ukaondoka)
Uzima unakuja na afya, baada ya kupoteza uzima magonjwa yakaingia
Uzima unakupa nafasi (position), ndio maana Mungu aliuliza Adam uko wapi? na sio umefanya nini? Neno uko wapi iliulizia nafasi (position) ya Adam kwakua nafasi aliyopewa ilipotea baada ya dhambi.
Ndio maana Yesu alikuja tuwe na uzima tena tuwe nao tele!

ii.                 Kukaa na Mungu
Mwanzo 3:24 “Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.”
Adam alipoteza haki yake ya uraia wa ufalme wa Mungu baada ya kuasi. Unapoamua kuokoka unarudishiwa uraia wa ufalme wa Mungu na unahamishwa kutoka katika nguvu za giza.

iii.               Haki ya kuangaliwa na Mungu
Habakuki 1:13 “Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;”
Mungu haangalii uovu, hii haimaanishi kwamba haoni, anaweza kuona lakini haangalii. Mwangalizi ni Yule anafuatilia kitu na kukilinda kisiharibike au kupotea (1Petro 2:25 “Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.”). Dhambi inapoingia inamaana unapoteza haki yako ya kuangaliwa na Mungu (Kutoka 2:23-25 “23 Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa. 24 Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. 25 Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia.”)
Unapokuwa ndani ya Yesu unapata “package” ikiwa ni pamoja na kuangaliwa na kulindwa na Mungu; yaani kuangaliwa ni haki yako.

iv.               Unapoteza haki ya kusikilizwa
Isaya 59:1-2 “1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; 2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”
Dhambi inaondoa haki ya kusikilizwa, sio kwamba Mungu hasikii ila hataki kukitekeleza kile unachokisema.

v.                  Unapoteza haki ya kuambatana na Mungu kule ambako wanaokuzunguka wanaona na wanajua Mungu yuko pamoja na wewe
Isaya 59:2lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia
Tumefarakana na Mungu katika vile vitu ambavyo vinahitaji kuelewana pamoja na Mungu, Mafarakano hayo yamezua uadui. Ili uende pamoja na mwenzako lazima mpatane kwanza ndipo mtee pamoja (Kutoka 33:12-18 “12 Musa akamwambia Bwana, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Walakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu. 13 Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. 14 Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. 15 Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. 16 Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi? 17 Bwana akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako. 18 Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako.”)

4.     Mungu anavyotumia Damu ya Yesu kukurudishia na kukupa haki zako ulizonyimwa
Warumi 4:25, 3:22-28 “25 ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki. 22 ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; 23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; 25 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa. 26 apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu. 27 Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani. 28 Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.”
Ukitaka kudai haki yako lazima uende mahali pa sheria na hukumu na pawepo na mtu anayejua sheria na hukumu ili uweze kupewa haki yako (hii ni kwa hapa duniani). Katika ufalme wa Mbinguni lazima uende kwa Yesu kwa njia ya Damu yake
Biblia inawazungumzia hao walioonewa na wenye haki lakini bado hawajui haki zao. Kwa njia ya Yesu Kristo hayo yote tuliyopoteza yanarudi na kuwa ni haki yako. Ukiweka imani yako kwenye Damu ya Yesu unauwezo wa kudai hak

Thursday, June 9, 2016

SEMINA YA MANA - MOROGORO Na Mwl. Chritopher Mwakasege (08-12/06/2016) SOMO:KUA KATIKA NEEMA ILI UNUFAIKE NA MSALABA (Imeandikwa na Samson&Joan MolleL, 0767 664 338 – www.uzimawamileleministries.blogspot.com)

Katika semina hii inayoendela hapa mjini Morogoro katika viwanja vya sule ya sekondari Morogoro, Mwalimu Christopher Mwakasege anafundisha somo “KUWA KATIKA NEEMA ILI UNUFAIKE NA MSALABA” Semina hii unaweza kusikiliza live kupitia Top radio – Morogoro, Radio sauti ya Injili – Moshi (Inayosikika mikoa mbalimbali) na pia kwenye mtandao www.kicheko.com na kwa njia ya sauti na video (www.mwakasege.org)

SIKU YA KWANZA:
2Petro 3:18 “Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.”
2Timoth 2:1 “Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.”

Tuanze kujifunza somo hili kwa kuangalia pointi zifuatazo kwa habari ya NEEMA.

11.   Maana ya neno NEEMA
Warumi 4:4-6 “4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. 5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki. 6 Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,”
Neema ni jambo unalolipata bila ya wewe kulifanyia kazi. Neema ni jambo unalolipokea kwa imani toka kwa Yule aliyekuhesabia haki ya kupokea jambo hilo.

22.Eneo lolote unalohitaji kukua ni lazima kwanza ukue(grow) katika Neema iliyoleta jambo hilo. Biblia isingesema kua kama hakuna kukua/kuongezeka katika Neema

MIFANO.

        i.            Neema iwaokoayo wanadamu
Tito 2:11-13 “11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;”
Kabla ya wokovu kuja kwako kinachotangulia kwanza ni NEEMA ndipo wokovu unafuatia, huwezi ukakua katika wokovu bila ya kukua katika neema iliyoleta wokovu wokovu huo

     ii.            Kuhesabiwa haki/kukubalika na Mungu kwa misingi yake
Tito 3:4-7 “4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; 5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 7 ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.”

   iii.            Kumtumikia Mungu
Wagalatia 1:13-16 “13 Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu. 14 Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. 15 Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, 16 alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;”
2Timotheo 1:9 “ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele,”
Wito unaletwa kwa NEEMA na sio kwa kadiri ya matendo yako, eneo lolote unalotaka kumtumikia Mungu lazima ujue NEEMA ilikuleta katika utumishi/huduma hiyo ili uweze kukua katika eneo hilo, hauwezi kukua katika huduma kama haujakua katika NEEMA iliyokuleta katika huduma hiyo.

   iv.            Kuomuomba Mungu
Waebrania 4:14-16 “14 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.”
Watu wengi sana wanapoenda kuomba hawangalii kiti kilichotoa NEEMA wanamwangalia mtu. Kuna tofauti kati ya kiti na mtu anayekaa katika kiti, yapo mambo ambayo mtu anaweza kukupa akiwa kwenye kiti lakini anapotoka kwenye kiti hicho hawezi kukupatia. Kukikaribia kiti kunategemea haki ya aliyekubalika kuingia na kupewa, Kiti kinautaratibu wa kutoa unachokihitaji na aliyekaa kwenye kiti anaweza kukupa utaratibu wa namna ya kukikaribia kiti cha NEEMA.

      v.            Mahusiano na watu wengine
Waebrania 12:14-15 “14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; 15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.”
Yaani usiishi chini ya kiwango “below standard” au usitumike chini ya kiwango cha NEEMA uliyoipokea au uliyoipewa au unayohitaji. Usipoifahamu hiyo NEEMA na wewe ukatumika/ukaishi chini ya kiwango cha NEEMA hauwezi kuhusiana na watu sawasawa na NEEMA uliyoipewa

   vi.            Kumwabudu Mungu
Waebrania 12:28-29 “28 Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho; 29 maana Mungu wetu ni moto ulao.”
Hauwezi kumwabudu Mungu nje ya NEEMA inayokupa kibali cha kumwabudu Mungu

 vii.            NEEMA ya kutawala
Warumi 5:20-21 “20 Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; 21 ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.”
Ni muhimu kuijua NEEMA iliyokupa nafasi ya kutawalaili uweze kuishi/kukaa katika nafasi hiyo

viii.            Mafanikio ya Mwili
2Korintho 9:8 “Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;”
NEEMA ikiachiliwa Mungu anawezesha kupata riziki ya kila siku. Kinachotoa NEEMA ni kiti, tunapokikaribia kiti kinatupa NEEMA, ndani ya NEEMA kuna vitu vyote tunavyohitaji.

3.     Kipindi cha NEEMA ni msimu kamili
Yohana 1:14-16 “14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. 15 Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 16 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.”
Katika Biblia kuna vipindi saba kuanzia kabla ya uumbaji………. Halafu uumbaji……. Kipindi cha sharia na sasa ni kipindi cha NEEMA, yaani huu ni msimu wa kuishi kwa NEEMA na sharia ikiwa imerahisishwa kwa kuandikwa mioyoni mwetu.

****** BWANA AKUBARIKI, KARIBU SIKU YA PILI TAR 09/06/2016*****