Thursday, June 9, 2016

SEMINA YA MANA - MOROGORO Na Mwl. Chritopher Mwakasege (08-12/06/2016) SOMO:KUA KATIKA NEEMA ILI UNUFAIKE NA MSALABA (Imeandikwa na Samson&Joan MolleL, 0767 664 338 – www.uzimawamileleministries.blogspot.com)

Katika semina hii inayoendela hapa mjini Morogoro katika viwanja vya sule ya sekondari Morogoro, Mwalimu Christopher Mwakasege anafundisha somo “KUWA KATIKA NEEMA ILI UNUFAIKE NA MSALABA” Semina hii unaweza kusikiliza live kupitia Top radio – Morogoro, Radio sauti ya Injili – Moshi (Inayosikika mikoa mbalimbali) na pia kwenye mtandao www.kicheko.com na kwa njia ya sauti na video (www.mwakasege.org)

SIKU YA KWANZA:
2Petro 3:18 “Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.”
2Timoth 2:1 “Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.”

Tuanze kujifunza somo hili kwa kuangalia pointi zifuatazo kwa habari ya NEEMA.

11.   Maana ya neno NEEMA
Warumi 4:4-6 “4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. 5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki. 6 Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,”
Neema ni jambo unalolipata bila ya wewe kulifanyia kazi. Neema ni jambo unalolipokea kwa imani toka kwa Yule aliyekuhesabia haki ya kupokea jambo hilo.

22.Eneo lolote unalohitaji kukua ni lazima kwanza ukue(grow) katika Neema iliyoleta jambo hilo. Biblia isingesema kua kama hakuna kukua/kuongezeka katika Neema

MIFANO.

        i.            Neema iwaokoayo wanadamu
Tito 2:11-13 “11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;”
Kabla ya wokovu kuja kwako kinachotangulia kwanza ni NEEMA ndipo wokovu unafuatia, huwezi ukakua katika wokovu bila ya kukua katika neema iliyoleta wokovu wokovu huo

     ii.            Kuhesabiwa haki/kukubalika na Mungu kwa misingi yake
Tito 3:4-7 “4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; 5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 7 ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.”

   iii.            Kumtumikia Mungu
Wagalatia 1:13-16 “13 Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu. 14 Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. 15 Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, 16 alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;”
2Timotheo 1:9 “ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele,”
Wito unaletwa kwa NEEMA na sio kwa kadiri ya matendo yako, eneo lolote unalotaka kumtumikia Mungu lazima ujue NEEMA ilikuleta katika utumishi/huduma hiyo ili uweze kukua katika eneo hilo, hauwezi kukua katika huduma kama haujakua katika NEEMA iliyokuleta katika huduma hiyo.

   iv.            Kuomuomba Mungu
Waebrania 4:14-16 “14 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.”
Watu wengi sana wanapoenda kuomba hawangalii kiti kilichotoa NEEMA wanamwangalia mtu. Kuna tofauti kati ya kiti na mtu anayekaa katika kiti, yapo mambo ambayo mtu anaweza kukupa akiwa kwenye kiti lakini anapotoka kwenye kiti hicho hawezi kukupatia. Kukikaribia kiti kunategemea haki ya aliyekubalika kuingia na kupewa, Kiti kinautaratibu wa kutoa unachokihitaji na aliyekaa kwenye kiti anaweza kukupa utaratibu wa namna ya kukikaribia kiti cha NEEMA.

      v.            Mahusiano na watu wengine
Waebrania 12:14-15 “14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; 15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.”
Yaani usiishi chini ya kiwango “below standard” au usitumike chini ya kiwango cha NEEMA uliyoipokea au uliyoipewa au unayohitaji. Usipoifahamu hiyo NEEMA na wewe ukatumika/ukaishi chini ya kiwango cha NEEMA hauwezi kuhusiana na watu sawasawa na NEEMA uliyoipewa

   vi.            Kumwabudu Mungu
Waebrania 12:28-29 “28 Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho; 29 maana Mungu wetu ni moto ulao.”
Hauwezi kumwabudu Mungu nje ya NEEMA inayokupa kibali cha kumwabudu Mungu

 vii.            NEEMA ya kutawala
Warumi 5:20-21 “20 Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; 21 ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.”
Ni muhimu kuijua NEEMA iliyokupa nafasi ya kutawalaili uweze kuishi/kukaa katika nafasi hiyo

viii.            Mafanikio ya Mwili
2Korintho 9:8 “Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;”
NEEMA ikiachiliwa Mungu anawezesha kupata riziki ya kila siku. Kinachotoa NEEMA ni kiti, tunapokikaribia kiti kinatupa NEEMA, ndani ya NEEMA kuna vitu vyote tunavyohitaji.

3.     Kipindi cha NEEMA ni msimu kamili
Yohana 1:14-16 “14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. 15 Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 16 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.”
Katika Biblia kuna vipindi saba kuanzia kabla ya uumbaji………. Halafu uumbaji……. Kipindi cha sharia na sasa ni kipindi cha NEEMA, yaani huu ni msimu wa kuishi kwa NEEMA na sharia ikiwa imerahisishwa kwa kuandikwa mioyoni mwetu.

****** BWANA AKUBARIKI, KARIBU SIKU YA PILI TAR 09/06/2016*****


No comments: