Sunday, May 7, 2017

MTAZAMO WANGU KWA JINSI YA KIROHO KWA HABARI YA AJALI YA WANAFUNZI WA SHULE YA LUCKY VINCENT - ARUSHA

Bwana Yesu Asifiwe Watu wa Mungu!!!

Watu wa Mungu nimepitia katika mitandao ya kijamii na kusoma mambo mengi na  mawazo na hisia za watu wengi kuhusu ajali iliyohusisha wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent na kuuwa watu 35 kati yao wanfunzi 32. Wapo watu wanoulaumu uongozi wa shule kwa kuwasafirisha wanafunzi umbali mrefu wakidai kuwa hapakuwa na sababu ya kufanya hivyo, wengine wanasema ni hali ya hewa na maneno mengi yamesemwa.

Mimi ninayo machache ya kusema kwa kuzingatia Neno hili Zaburi 90:10 “Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;…….”

1.      Kwanza tuombe toba kama waombaji kwani ninaamini ya kwamba kama kuna jambo lolote liwe baya au zuri kabla halijatokea Mungu huwafahamisha watumishi wake (Amosi 3:7 “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.”). Ninaamini kuwa yawezekana kabisa mmoja wetu alipokea taarifa hii na hakuifanyia kazi ipasavyo.

2.      Pili tuombe toba kama walinzi, Sisi waombaji ni walinzi katika maeneo tuliyopo (Isaya 62:6 “Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;”). Inawezekana kabisa kuna mahali walinzi (waombaji) walilala lindoni na kuruhu mwizi (shetani) kuingia kuvunja, kuchinja na kuharibu.

3.      Jambo la tatu ni swali la kwangu binafsi; Arusha umekuwa ni mji wa kusifika kwa maendeleo makubwa ya kiroho na kuwepo kwa watumishi wakubwa wa Mungu katika mji wa Arusha, Je! Kuna nini kimetokea kwa watumishi hawa wa Mungu au ni kosa gani wamelifanya hata BWANA asiseme nao juu ya jambo hili?

Kuna jambo la kiroho ambalo nimeliona na lipo dhahiri kwa jinsi ya kiroho kwani nilimuona wakala wa kuzimu katika mwili baada ya kuutimiza uharibifu huu na ninaomba tuangalie ajali hii kwa mtazamo wa harakati za kuzimu kuwaumiza watakatifu wa Mungu.
Kwa jinsi ya rohoni kwa upande wa giza “kuzimu” ajali hizi hutengenezwa ili kupeleka kafara huko kuzimu, na ili ajali itokee lazima kupatikane sababu ya kimwili itakayoleta hiyo ajali yaani lazima kutengenezwe mtego kama Neno la Mungu linavyosema katika Yeremia 5:26 “Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu.”

Sasa kumbe kuna watu wanotega mitego ili kunasa watu. Sababu ya kunasa watu ni kuchukua roho za hao watu kabla ya wakati wa Mungu kuwachukua haujafika kama tunavyosoma katika kitabu cha Ezekiel 13:18-19 “18 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe? 19 Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.”

NAMIMI KATIKA JINA LA YESU NINAIPELEKA OLE! KWAO WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI, SAWASAWA NA NENO LA MUNGU KUTOKA KATIKA KITABU CHA UFUNUO 18:6 “MLIPENI KAMA YEYE ALIVYOLIPA, MKAMLIPE MARA MBILI KWA KADIRI YA MATENDO YAKE. KATIKA KIKOMBE KILE ALICHOKICHANGANYISHA, MCHANGANYISHIENI MARADUFU.”

KATIKA JINA LA YESU NA KILA MWANA WA MUNGU ASEME AMEN!

***** Samson Mollel – www.uzimawamileleministries.blogspot.com *******