Bwana
Yesu Asifiwe Watu wa Mungu!!!
Watu
wa Mungu nimepitia katika mitandao ya kijamii na kusoma mambo mengi na mawazo na hisia za watu wengi kuhusu ajali
iliyohusisha wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent na kuuwa watu 35 kati yao
wanfunzi 32. Wapo watu wanoulaumu uongozi wa shule kwa kuwasafirisha wanafunzi
umbali mrefu wakidai kuwa hapakuwa na sababu ya kufanya hivyo, wengine wanasema
ni hali ya hewa na maneno mengi yamesemwa.
Mimi
ninayo machache ya kusema kwa kuzingatia Neno hili Zaburi 90:10 “Siku za miaka
yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;…….”
1. Kwanza
tuombe toba kama waombaji kwani ninaamini ya kwamba kama kuna jambo lolote liwe
baya au zuri kabla halijatokea Mungu huwafahamisha watumishi wake (Amosi 3:7 “Hakika
Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii
siri yake.”). Ninaamini kuwa yawezekana kabisa mmoja wetu alipokea taarifa hii
na hakuifanyia kazi ipasavyo.
2. Pili tuombe
toba kama walinzi, Sisi waombaji ni walinzi katika maeneo tuliyopo (Isaya 62:6
“Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala
usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;”). Inawezekana kabisa
kuna mahali walinzi (waombaji) walilala lindoni na kuruhu mwizi (shetani)
kuingia kuvunja, kuchinja na kuharibu.
3. Jambo la
tatu ni swali la kwangu binafsi; Arusha umekuwa ni mji wa kusifika kwa
maendeleo makubwa ya kiroho na kuwepo kwa watumishi wakubwa wa Mungu katika mji
wa Arusha, Je! Kuna nini kimetokea kwa watumishi hawa wa Mungu au ni kosa gani
wamelifanya hata BWANA asiseme nao juu ya jambo hili?
Kuna
jambo la kiroho ambalo nimeliona na lipo dhahiri kwa jinsi ya kiroho kwani
nilimuona wakala wa kuzimu katika mwili baada ya kuutimiza uharibifu huu na
ninaomba tuangalie ajali hii kwa mtazamo wa harakati za kuzimu kuwaumiza
watakatifu wa Mungu.
Kwa
jinsi ya rohoni kwa upande wa giza “kuzimu” ajali hizi hutengenezwa ili
kupeleka kafara huko kuzimu, na ili ajali itokee lazima kupatikane sababu ya
kimwili itakayoleta hiyo ajali yaani lazima kutengenezwe mtego kama Neno la
Mungu linavyosema katika Yeremia 5:26
“Maana katika watu wangu wameonekana watu
waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu.”
Sasa
kumbe kuna watu wanotega mitego ili kunasa watu. Sababu ya kunasa watu ni
kuchukua roho za hao watu kabla ya wakati wa Mungu kuwachukua haujafika kama
tunavyosoma katika kitabu cha Ezekiel 13:18-19
“18 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole
wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso
juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za
watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe? 19 Nanyi mmeninajisi kati ya
watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua
roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao
haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.”
NAMIMI
KATIKA JINA LA YESU NINAIPELEKA OLE! KWAO WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI, SAWASAWA
NA NENO LA MUNGU KUTOKA KATIKA KITABU CHA UFUNUO
18:6 “MLIPENI KAMA YEYE ALIVYOLIPA,
MKAMLIPE MARA MBILI KWA KADIRI YA MATENDO YAKE. KATIKA KIKOMBE KILE ALICHOKICHANGANYISHA,
MCHANGANYISHIENI MARADUFU.”
KATIKA
JINA LA YESU NA KILA MWANA WA MUNGU ASEME AMEN!
No comments:
Post a Comment