_Maombi
haya yanatoka (Isaya 1:18, Zaburi 103:12, Isaya 43:25, 41:21, 43:26 na Daniel 9:4-19, Isaya 53:5)_
Baba katika jina la Yesu umesema katika Neno lako
kwamba; Haya, njoni, tusemezane, dhambi zetu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa
nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Umesema pia BABA yangu kwamba; Kama mashariki ilivyo
mbali na magharibi, Ndivyo ulivyoweka dhambi zetu mbali nasi. BABA umesema wewe,
naam, wewe, ndiwe uyafutaye makosa yangu kwa ajili yako mwenyewe, wala hutazikumbuka
dhambi zangu. Na BWANA umeniagiza kuwa nilete maneno yangu, nitoe hoja zangu
zenye nguvu, umesema mfalme wa Yakobo kwamba nikukumbushe, na tuhojiane; nieleze
mambo yangu, nipate kupewa haki yangu kutoka kwako.
Ninaungama kwako, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye
kutisha, ushikaye maagano na rehema kwao wakupendao, na kuzishika amri zako; mimi
na familia yangu na ukoo wangu na jamaa zangu na taifa langu tumefanya dhambi
sana, tumefanya ukaidi mwingi, tumetenda maovu mno, tumeasi, naam, hata kwa
kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; wala hatukuwasikiliza watumishi wako,
manabii/wachungaji/wainjlisti/mitume/walimu, ambao kwa jina lako walisema na
wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi. Ee Bwana, haki ina wewe, lakini
kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa familia yangu, na kwa ukoo
wangu, nan chi yangu Tanzania tulio katika hofu kuu ya ugonjwa wa korona, kwa
sababu ya makosa yetu tulikukosea na maovu ya baba zetu. Ee Bwana, kwetu sisi
kuna haya ya uso, viongozi wa familia zetu, na viongozi wa jamii zetu na viongozi
wa nchi yetu Tanzania, kwa sababu tumekutenda dhambi. Rehema na msamaha ni kwa
Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu,
kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi
wake, manabii/wachungaji/wainjlisti/mitume/walimu. Naam, familia na ukoo wote
wameihalifu sheria yako, kwa kugeuka upande, tusiisikilize sauti yako; basi kwa
hiyo laana ya ugonjwa huu wa korona imemwagwa juu yetu, kwa sababu tumemtenda
dhambi. Basi Bwana umeyaweka mabaya hayo, ukatuletea; maana Wewe Bwana, Mungu
wetu ni mwenye haki katika kazi zako zote uzitendazo; na sisi hatukuitii sauti
yako.
Na sasa, Ee Bwana Mungu wetu, uliyewatoa watu
wako hawa katika nchi ya Misri kwa mkono hodari, ukajipatia sifa, kama ilivyo
leo; tumefanya dhambi, tumetenda maovu. Ee Bwana sawasawa na haki yako yote,
nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuisamehe nchi yangu
Tanzania; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu na viongozi
waliotutangulia, adhabu hii kali imeachiliwa juu yetu. Basi sasa, Ee Mungu
wetu, yasikilize maombi yangu mimi mtumishi wako, na dua zangu, ukaangazishe
uso wako juu ya nchi yangu Tanzania ambayo tumekaa katika hali ya ukiwa ukiwa,
kwa ajili ya adhabu yako Bwana. Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie;
fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mimi mtoto wako ninayeitwa kwa jina
lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu
ya rehema zako nyingi. Ee Bwana, usikie; Ee Bwana, usamehe; Ee Bwana,
usikilize, ukatende, usikawie; kwa ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu mimi
na familia yangu tunaitwa kwa jina lako kwakuwa tumempokea mwana wako Yesu
Kristo na tumeoshwa kwa damu ya Yesu, Bwana kumbuka rehema.
Asante BABA kwani umemtuma Kristo Yesu ambaye alijeruhiwa
kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu
yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona, tumepona ugonjwa huu wa kutisha katika
jina la Yesu Kristo, AMEN!
*Samson Mollel 0767/0713-664
338*
```©
April 17, 2020```