Monday, March 21, 2016

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE (Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam) SOMO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO NA WALIO NA HAJA YA KUPONA.

SIKU YA SITA

Mistari ya kusimamia: Isaya 61:1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.” Yeremia 6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.”

UTANGULIZI
Mambo mawili ya msingi ya kukumbuka
·         Maana ya neno moyo (rejea somo la siku ya kwanza)
·         Moyo uliovunjika ni moyo wa namna gani (pia rejea somo la siku ya kwanza)
Kumbuka MUNGU husema na watu kwa njia ya ndoto pia tena si mara moja Ayb 33:14-18
Ukiona uoti kabisa si zile za kuota siku moja moja ujue kuna shida sehemu msihi MUNGU afungue mlango huu pia kwako

VIPENGELE MUHIMU VYA KUOMBEA IKIWA MOYO WAKO UMEJERUHIWA NA NDOTO

1.     Omba maelekezo kutoka kwa BWANA juu ya kufuatilia ndoto uliyoota

Daniel 4:19, 27-29 “19 Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako. 27 Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha. 28 Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza. 29 Baada ya miezi kumi na miwili, kuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. 30 Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?”
·         Si kila kilichopo kwenye ndoto lazima kitimie
·         Daniel alimwambia mfalme ndoto hii isikupate wewe wala tafsiri yake..alimpa ushauri na maelekezo ya kufanya lakini mfalme akufanya hivyo ndipo ndoto ile ikatikilizika kwake
·         Wewe unaweza kubadilisha/kuhahirisha matokeo ya ndoto maana mfalme alipewa nafasi ya kutengeneza miezi 12 lakini hakufanya hivyo

2.     Omba MUNGU akupe tafsiri ya ndoto
Daniel 1:17 “Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.”
·         Omba MUNGU akupe ufahamu wa ndoto
·         Omba tafsiri yake
·         Omba MUNGU akusaidie kusoma NENO la kutosha likusaidie kutafsiri ndoto hizo

3.     Omba Toba kwa kutokufuata maelekezo na maonyo yaliyokuja na ndoto na hukuyafuata
Ayubu 33:14-18 “14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; 16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, 17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; 18 Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.”

·         MUNGU husema nawe pia kupitia ndoto, mara nyingi anakupa taarifa, kukuonya, kukufundisha, kukuelekeza, kukupa maono mapya na n.k
·         Kutofuata maelekezo na maonyo yaliyoko kwenye ndoto kama ni adhabu itakugharimu sana mkumbuke Mfalme Nebukadreza alipewa adhabu kwa kutofuata maelekezo miaka 7 kondeni

Mathayo 1:18 “ Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.”
·         Yusuph alitokewa kwenye ndoto kutomkimbia mariam. Pia alipewa maelekezo kumtorosha mtoto maana Herode alitaka kumuua
·         Ukidharau maelekezo maumivu na madhara yake yatakutesa wewe na familia yako hata nchi nzima.
·         TOBA ni kumruhusu MUNGU kuingilia kati

4.     Omba ili king'olewe kilicho pandikizwa kwa njia ya ndoto
Daniel 4:4-5 “4 Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi. 5 Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.”
·         Baada ya ndoto hofu ilimwingia
·         Peleka kwa MUNGU ili aking'oe kile kilicholetwa na ndoto maana ukikiacha kitakutesa sana

5.     Weka ulinzi wa DAMU ya YESU kwenye mlango wa ndoto ili shetani asiutumie kukuvuruga
Ayubu 33:14-16 “14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; 16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
·         MUNGU hufungua masikio(mlango) wa mtu ule wa ndani
·         Swala si tu DAMU ya YESU bali ni Imani inayotumika kuombea DAMU ya YESU
·         Ndoto ni lango lazima lilindwe kwa DAMU ya YESU ambaye ni PASAKA wetu. Kut 12:21-23, 1Kor 5:7-

MALANGO YAPO YA AINA 2 YA KUSHUGHULIKIA
        I.            Nafsi ya yule mtu na roho yake
      II.            Lango la pili ni lango la muda

·         Angalia ndoto unazoziota ni muda gani kawaida
·         Mara nyingi mlango mkubwa sana wa ndoto ngumu ni saa 9-10 usiku

6.      Ombea mahali unapolala au Omba TOBA kwa kuto-kupaombea ipasavyo unapolala na kupata mashambulizi kwa njia ya ndoto
Mwanzo 28:10-22 “10 Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. 11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. 12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.”

7.     Omba uponyaji kamili wa moyo na eneo uliloumia
Yeremia 6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.”Isaya 61:1
·         Omba mpaka upone
·         Omba mpaka MUNGU amekuonyesha umevuka
NJIA 2 ZA KUJUA
·         Imani yako. Utajua mafadhaiko na maangaiko yameondoka
·         Umepona mpaka mwili umekuwa mwepesi

8.      Omba MUNGU akusaidie kuondoka ulipokwama
·         Ndani ya ndoto utaonyeshwa umekwama wapi

9.      Futa maneno uliyotamkiwa kwenye ndoto ambayo ni kinyume na mapenzi ya MUNGU

Dan 4:13-17 “13 Nikaona katika njozi za kichwa changu kitandani mwangu, na tazama, mlinzi, naye ni mtakatifu, alishuka kutoka mbinguni. 14 Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake.
 15 Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi; 16 moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake. 17 Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.”

·         Omba urejeshewe vile vilivyo haribika kwa sababu ya jeraha lililotokea kwenye ndoto


Dan 4:34-37 “34 Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; 35 na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? 36 Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi. 37 Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.”

1 comment:

Sammollel said...

Shalom! Nimepata hilo somo