SIKU
YA SITA
Mistari ya kusimamia: Isaya 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta
niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika
moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa
kwao.” Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari
za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.” Yeremia 6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani,
Amani, wala hapana amani.”
UTANGULIZI
Mambo mawili ya msingi ya
kukumbuka
·
Maana ya
neno moyo (rejea somo la siku ya kwanza)
·
Moyo
uliovunjika ni moyo wa namna gani (pia rejea somo la siku ya kwanza)
Kumbuka MUNGU husema na watu kwa
njia ya ndoto pia tena si mara moja Ayb 33:14-18
Ukiona uoti kabisa si zile za
kuota siku moja moja ujue kuna shida sehemu msihi MUNGU afungue mlango huu pia
kwako
VIPENGELE
MUHIMU VYA KUOMBEA IKIWA MOYO WAKO UMEJERUHIWA NA NDOTO
1.
Omba maelekezo kutoka kwa BWANA
juu ya kufuatilia ndoto uliyoota
Daniel
4:19, 27-29 “19 Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake
Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu
akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza
akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri
yake iwapate adui zako. 27 Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate
kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa
kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha. 28
Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza. 29 Baada ya miezi kumi na miwili, kuwa
akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. 30 Mfalme akanena, akasema,
Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo
wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?”
·
Si kila
kilichopo kwenye ndoto lazima kitimie
·
Daniel alimwambia
mfalme ndoto hii isikupate wewe wala tafsiri yake..alimpa ushauri na maelekezo
ya kufanya lakini mfalme akufanya hivyo ndipo ndoto ile ikatikilizika kwake
·
Wewe unaweza
kubadilisha/kuhahirisha matokeo ya ndoto maana mfalme alipewa nafasi ya
kutengeneza miezi 12 lakini hakufanya hivyo
2.
Omba MUNGU akupe tafsiri ya ndoto
Daniel
1:17 “Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu
aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na
ufahamu katika maono yote, na ndoto.”
·
Omba MUNGU
akupe ufahamu wa ndoto
·
Omba tafsiri
yake
·
Omba MUNGU
akusaidie kusoma NENO la kutosha likusaidie kutafsiri ndoto hizo
3.
Omba Toba kwa kutokufuata
maelekezo na maonyo yaliyokuja na ndoto na hukuyafuata
Ayubu
33:14-18 “14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam,
hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya
usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; 16 Ndipo
huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, 17 Ili amwondoe
mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; 18 Yeye huizuia nafsi yake
isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.”
·
MUNGU husema
nawe pia kupitia ndoto, mara nyingi anakupa taarifa, kukuonya, kukufundisha,
kukuelekeza, kukupa maono mapya na n.k
·
Kutofuata
maelekezo na maonyo yaliyoko kwenye ndoto kama ni adhabu itakugharimu sana
mkumbuke Mfalme Nebukadreza alipewa adhabu kwa kutofuata maelekezo miaka 7
kondeni
Mathayo
1:18 “ Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi.
Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana,
alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.”
·
Yusuph
alitokewa kwenye ndoto kutomkimbia mariam. Pia alipewa maelekezo kumtorosha
mtoto maana Herode alitaka kumuua
·
Ukidharau
maelekezo maumivu na madhara yake yatakutesa wewe na familia yako hata nchi
nzima.
·
TOBA ni
kumruhusu MUNGU kuingilia kati
4.
Omba ili king'olewe kilicho
pandikizwa kwa njia ya ndoto
Daniel
4:4-5 “4 Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe
katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi. 5 Nikaota ndoto
iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa
changu, zikanifadhaisha.”
·
Baada ya
ndoto hofu ilimwingia
·
Peleka kwa
MUNGU ili aking'oe kile kilicholetwa na ndoto maana ukikiacha kitakutesa sana
5.
Weka ulinzi wa DAMU ya YESU kwenye
mlango wa ndoto ili shetani asiutumie kukuvuruga
Ayubu
33:14-16 “14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam,
hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya
usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; 16 Ndipo
huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,”
·
MUNGU hufungua
masikio(mlango) wa mtu ule wa ndani
·
Swala si tu
DAMU ya YESU bali ni Imani inayotumika kuombea DAMU ya YESU
·
Ndoto ni
lango lazima lilindwe kwa DAMU ya YESU ambaye ni PASAKA wetu. Kut 12:21-23,
1Kor 5:7-
MALANGO
YAPO YA AINA 2 YA KUSHUGHULIKIA
I.
Nafsi ya
yule mtu na roho yake
II.
Lango la
pili ni lango la muda
·
Angalia
ndoto unazoziota ni muda gani kawaida
·
Mara nyingi
mlango mkubwa sana wa ndoto ngumu ni saa 9-10 usiku
6.
Ombea mahali
unapolala au Omba TOBA kwa kuto-kupaombea ipasavyo unapolala na kupata
mashambulizi kwa njia ya ndoto
Mwanzo
28:10-22 “10 Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda
Harani. 11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa
limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake,
akalala usingizi pale pale. 12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu
ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu
wanapanda, na kushuka juu yake.”
7.
Omba uponyaji kamili wa moyo na
eneo uliloumia
Yeremia
6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu
tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.”Isaya 61:1
·
Omba mpaka
upone
·
Omba mpaka
MUNGU amekuonyesha umevuka
NJIA
2 ZA KUJUA
·
Imani yako.
Utajua mafadhaiko na maangaiko yameondoka
·
Umepona
mpaka mwili umekuwa mwepesi
8.
Omba MUNGU
akusaidie kuondoka ulipokwama
·
Ndani ya
ndoto utaonyeshwa umekwama wapi
9.
Futa maneno
uliyotamkiwa kwenye ndoto ambayo ni kinyume na mapenzi ya MUNGU
Dan
4:13-17 “13 Nikaona katika njozi za kichwa changu
kitandani mwangu, na tazama, mlinzi, naye ni mtakatifu, alishuka kutoka
mbinguni. 14 Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi
yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na
waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake.
15 Walakini kiacheni kisiki cha shina lake
katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya
kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na
wanyama katika majani ya nchi; 16 moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu,
na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake. 17 Hukumu hii imekuja
kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai
wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa
amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.”
·
Omba
urejeshewe vile vilivyo haribika kwa sababu ya jeraha lililotokea kwenye ndoto
Dan
4:34-37 “34 Hata mwisho wa siku hizo, mimi,
Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia;
nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa
maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata
kizazi; 35 na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye
hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa
duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini
wewe? 36 Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu
wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na
madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu,
nikaongezewa enzi kupita kiasi. 37 Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa
mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia
zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.”
1 comment:
Shalom! Nimepata hilo somo
Post a Comment