1. UTANGULIZI
Math. 13:10-17
10Wakaja
wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano? 11Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri
za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa. 12Kwa
maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye
na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa. 13Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa
wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.14Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema,
Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. 15Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa
masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho
yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka,
nikawaponya. 16Lakini, heri macho yenu, kwa
kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. 17Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye
haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia
ninyi, wasiyasikie.
Sura ya 13 ya Mathayo ni mwanzo mpya wa mafundisho ya Bwana
Yesu – hasa akielezea yatakayotokea baada ya Yeye kurudi mbinguni kama
“Mfalme atakayetawala”.
Wasomaji wa Biblia wanajua kuwa Mathayo anaanza Injili yake kwa kuonyesha
1.
Kuwa Yesu NDIYE Mtoto wa kiume aliyetabiriwa atakayemiliki
katika Kiti cha Enzi cha Daudi – Sura 1
2.
Kuwa ushahidi wa ufalme wake ni Mamajusi toka Mashariki
waliokuja kumwona pamoja na tunu; na ubatizo aliobatizwa na Yohana pale Yordani
– Sura 2 &3
3.
Kuwa baada ya Ubatizo na Majaribu, Bwana Yesu alitoa Kanuni sa
Ufalme wake ujao – katika Hotuba ya Mlimani – Sura 5-7
·
Misingi ya kanuni hizi ni misingi ya kiroho na Kimaadili –
kanuni zinazosimamia Ufalme wa Mungu
·
Kanuni hizi ndizo zile zilizotabiriwa juu ya ufalme wake hapa
duniani ambazo Masihi-Mfalme angelizileta akitokea
·
Kanuni hizi zina kweli ambazo hata leo zinatumika na zitatumika
katika Utawala wake wa Miaka 1000
4.
Miujiza inayomdhihirisha kuwa ndiye Mfalme – Sura 8-10
Hadi hapo ilikuwa dhahiri kuwa Wayahudi walikuwa wamekataa
kabisa ushahidi wowote kuwa Yesu ndiye Masihi na Mfalme aliyetabiriwa
5.
Kukataliwa na kuahirishwa kwa Ufalme wake vikitabiriwa.Bwana anaonyesha hili kwa kuikemea miji
ile ambayo miujiza yake mingi ilifanyika, na miji ile haikutubu – yaani
Korazini, Bethsaida nan Kapernaumu – Sura 11 (Hasa 21-25).
6.
Kuwa Mafarisayo wanafikia kiwango cha juu sana kukana katakata
Umasihi na Ufalme wa Yesu na kuanza kudai kuwa Bwana Yesu anatoa pepo kwa
Belzebul – mkuu wa pepo – Sura 12 (Hasa mistari ya 14, 22-29)
Sura ya 13 inakabili swali la nini kitakachotokea wakati Mfalme
aliyekataliwa atakaporudi mbinguni, yaani wakati ufalme aliouahidi
utakapoahirishwa hadi ajapo mara ya pili.
Wazo la kuahirishwa kunaeleweka tu kibinaadamu – kama ilivyotokea kule Kadeshi-Banea – lakini sio kaka mpango wa milele wa Mungu, kwani mpango wa Mungu haubadiliki.
Wazo la kuahirishwa kunaeleweka tu kibinaadamu – kama ilivyotokea kule Kadeshi-Banea – lakini sio kaka mpango wa milele wa Mungu, kwani mpango wa Mungu haubadiliki.
Labda sasa tuone kwa kifupi sana kilichotokea pale
Kadeshi-Banea:
1.
Hesabu 12 (Huko Hazeroth – Mst 16)
|
–
Haruni na Miriam wanampinga Musa kwa sababu ya kuoa mwanamke Mkushi
–
Mungu anampiga Miriam kwa ukoma
|
2.
Hesabu 13 (Nyika ya Parani – Mst 3,26)
|
–
Musa anatuma wapelelezi kuipeleleza Kanaani
–
Wapelelezi wanarudi wka Musa (Mst 26)
–
Wapelelezi wanatoa taarifa mbaya ya kukatisha tamaa (Mst 28-33)
|
3.
Hesabu 14 (Kadeshi-Banea)
|
–
Uasi mkuu (Mst 1-10).
–
Mungu anaamua kuwaangamiza wote (Mst 11-12)
–
Musa anawaombea neema kwa Mungu (Mst 13-19)
–
Mungu anawasamehe (Mst 20-21)
– Mungu anaahirisha kwa wana wa Israeli kuingia Kaanani kwa kizazi
kile hadi kifie jangwani. Mungu anaamua kuwa kila siku
waliyopeleleza Kanaani italipiwa kwa mwaka (Mst 26-35). Yaani Miaka 40 baadae
ndio wataingia Kaanani
–
Wale walioleta taarifa mbaya wanapigwa kwa tauni na kufa palepale (Mst 36-37)
–
Watu wanatubu na kuasi hapohapo (Msh 39-45)
|
Jambo lililo la dharura kwa mwanadamu kwa Mungu liko katika
mpango wake kabisa. Kuna mambo ambayo katika mipaka ya muda tunaona ni dharura,
lakini kwa Mungu kila kitu kiko katika muda unaoitwa sasa. Mambo yaliyopita, na
mambo yajayo yako sasa kwa Mungu.
Mpango wa Mungu kwenye mtazamo wetu unapaswa wakati wote
uonekane KUHUSISHA YALE YOTE AMBAYO YAMESHATOKEA (The plan of God always
includes what actually happened). Ndani ya mpango huo, bado mwanadamu mhusika
anawajibika sana.
Hebu tuone mistari mingine kuelezea ukweli huu:
Math. 18: 7Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya
kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule
aliletaye jambo la kukosesha!
Math. 26:24Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa;
lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake
mtu yule kama asingalizaliwa.
Luka
24: 25Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya
kuamini yote waliyoyasema manabii!26Je! Haikumpasa
Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? 27Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza
katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
Isaya
53: 10 Lakini Bwana aliridhika kumchubua;
Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao
wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi
mwake; 11Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika.
Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki;
Naye atayachukua maovu yao.
Tukijua kanuni hii haitakuwa shida kuelewa maneno ya Petro
katika Matendo ya Mitume 3:13-21:
13Mungu wa
Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake
Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa
hukumu yake afunguliwe. 14Bali ninyi
mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe mwuaji; 15mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua
katika wafu; na sisi tu mashahidi wake. 16Na kwa imani
katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na
imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi
nyote. 17Basi sasa, ndugu, najua ya kuwa mliyatenda haya kwa
kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda. 18Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani
kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza
hivyo.19Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe,
zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; 20apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu
zamani; 21ambaye ilimpasa kupokewa
mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa
kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.
Yaani, kukataliwa kwa Yesu, kuuawa kwa Yesu, Kifo chake, Ufufuo
wake, nk – vyote vilikuwa bado muhimu sana katika mpango wa milele wa Mungu kwa
ajili ya wokovu wetu!
Kwa mantiki haya, Ufalme wa Mungu ambao ulikuwa utokee mara
ULIAHIRISHWA hadi wakati mwingine. Mwanadamu alipokataa, Ufalme ULIAHIRISHWA –
yaani Ufalme aliouleta Yesu duniani uliahirishwa!
Kwanza kabisa nadhani ni muhimu sana tuone kwa kifupi sana
tofauti Iliyoko kati ya Ufalme wa MBINGUNI na Ufalme wa MUNGU.
Ukisoma Biblia utaona yakini kuwa kuna Ufalme wa MBINGUNI na
Ufalme wa MUNGU, na sehemu nying imeelezwa kuwa ni kitu kilekile. Ukiwa makini
zaidi kidogo kulinganisha maandiko utaona tofauti kubwa ya Ufalme wa MBINGUNI
na Ufalme wa MUNGU.
Ufalme wa MBINGUNI unazungumzia na unahusu tabia ya ukiri
(professing character) ya Ufalme – nawo unawahusu wasioamini kwa ndani, jinsi
wanavyoonekana kwa nje kuwa ni waumini na wanaoamini halisi – ndani na nje.
Ufalme huu unazo “ngano” na “magugu”.
Ufalme wa MUNGU unawahusu tuwaumini wa kweli (kwa ndani na kwa
nje). Ndio Bwana alitufundisha kuwa tuombe: “Ufalme wako uje”.
Kuona tifauti za kimafundisho ya ufalme wa MBINGUNI na Ufalme wa
MUNGUvitatusaidia sana kuelewa histria ya mpango wa Mungu katika Biblia. Ni
uelewa tu haba unaosababisha tusione hasa nafasi na kipindi cha Kanisa na
Israeli, kwa mfano, kwa sababu hatuoni tofauti hizi za Ufalme.
Inaweza kukushangaza kugundua kuwa Biblia ni ujumbe kuhusu
mashindano juu ya UFALME – yaani Ufalme wa Mbinguni wenye Ufalme pale
Yerusalemu (duniani). Waweza mara kujiuliza: kwa nini Wayahudi walimkataa Bwana
Yesu kama Masihi na Mfalme? Ni kwa sababu (kwa sehemu kubwa) walitegemea Yeye
atakayekuja amiliki Israeli ili Israeli sasa waitawale dunia. Tunasoma hivi
katika Maandiko:
5Tazama siku
zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye
atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika
nchi. 6Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa
salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu. 7Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema Bwana,
ambapo hawatasema tena, Aishivyo Bwana, aliyewatoa wana wa Israeli katika nchi
ya Misri;8lakini, Aishivyo Bwana, aliyewapandisha na
kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi
zote nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe. – Yeremia 23
Na tena:
1Bwana ndiye
aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima
wake mtakatifu. 2Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni
furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme
mkuu. 3Mungu katika majumba yake Amejijulisha kuwa
ngome. 4Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walipita wote
pamoja. 5Waliona, mara wakashangaa;
Wakafadhaika na kukimbia. 6Papo hapo
tetemeko liliwashika, Utungu kama wa mwanamke azaaye. 7Kwa upepo wa mashariki Wavunja jahazi za
Tarshishi. 8Kama tulivyosikia, ndivyo
tulivyoona, Katika mji wa Bwana wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu ataufanya
imara hata milele. Zaburi 48
Ndio maana Bwana alipowapa mikate, walimfuata wote. Tunasoma
hivi katika Injili ya Yohana 6:
24Basi mkutano,
walipoona ya kuwa Yesu hayuko huko wala wanafunzi wake, waliingia mashuani
wenyewe, wakaenda Kapernaumu wakimtafuta Yesu. 25Hata walipomwona ng’ambo ya bahari, walimwambia,
Rabi, wewe umekuja lini hapa? 26Yesu akawajibu,
akasema, Amin, amin, nawaambieni, Ninyi mnanitafuta, si kwa sababu mliona
ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.27Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali
chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa
sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.
30Wakamwambia,
Unafanya ishara gani basi, ili tuione tukakuamini? Unatenda kazi gani? 31Baba zetu waliila mana jangwani kama vile
ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale. 32Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa
aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha
kweli kitokacho mbinguni. 33Kwa maana
chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu
uzima. 34Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula
hiki.35Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye
ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe. 36Lakini naliwaambia ya kwamba mmeniona wala
hamwamini. 37Wote anipao Baba watakuja
kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. 38Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili
niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. 39Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba
katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya
mwisho. 40Kwa kuwa mapenzi yake Baba
yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima
wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
41Basi Wayahudi
wakamnung’unikia, kwa sababu alisema, Mimi ni chakula kilichoshuka kutoka
mbinguni.42Wakasema, Je! Huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu,
ambaye twamjua babaye na mamaye? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?
Alipoingia Yerusalemu, wote walimfuata wakiimba “Hosana…” yaani
“Okoa sasa…” (Yohana 12:13 na Marko 11:9-10). Walijua kuwa sasa Mfalme wao wa
kuwaokoa dhidi ya dola gandamizi la Kirumi amekuja, na pia kwa mara ya kwanza
wataanza kuitawala dunia!
Mafarisayo walimuulizauliza: Ufalme wa Mungu utakuja lini? Na
Yesu aliwajibu juu ya Ufalme wa Mungu kuwa UPO NDANI YAO – wala hauji kwa
kuuchunguza chunguza! Tunasoma hivi:
20Na alipoulizwa
na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa
Mungu hauji kwa kuuchunguza; 21wala hawatasema,
Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
Luka 17
Ukweli huu wa kiroho kuhusu Ufalme haukueleweka kwa Israeli kama
vile leo usivyoeleweka sana wka Kanisa.
Bwana Yesu alipoulizwa na Pilato kuhusu UFALME WAKE Yesu, Bwana
alimjibu wazi kuwa kwa sasa Ufalme wake sio wa hapa duniani:
33Basi Pilato
akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme
wa Wayahudi? 34Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi
kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? 35Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na
wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?
36Yesu akajibu,
Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu,
watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini
ufalme wangu sio wa hapa. 37Basi Pilato
akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni
mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja
ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti
yangu.
38Pilato
akamwambia, Kweli ni nini? Naye akiisha kusema neno hilo akawatokea Wayahudi
tena, akawaambia, Mimi sioni hatia yo yote kwake.
Bwana Yesu alimwambia nini Pilato? Alimwambia kuwa Yeye ni
Mfalme ambaye bado Ufalme wake halisi haujaja. Sasa ni Ufalme wa Mbinguni
unaoonekana, na Ufalme wa Mungu upo ndani ya watu!
Hebu, kwa mfano, tazama alivyomjibu mtu mmoja siku moja (Luka
12):
13Mtu mmoja
katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu.14Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa
mwamuzi au mgawanyi juu yenu?
(Yohana
8): 15Ninyi mwahukumu kwa kufuata mambo ya mwili; mimi
simhukumu mtu. 16Nami nijapohukumu, hukumu yangu
ni kweli; kwa kuwa mimi si peke yangu, bali ni mimi na yeye aliyenipeleka.
Hata wakati mwingine walitaka kumfanya awe Mfalme, akakataa.
Tunasoma hivi (Yohana 6):
14Basi watu
wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye
ulimwenguni.15Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja
kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.
Iko siku Ufalme wake utakuja – yaani Ufalme wa mbinguni na falme
zote za duniani vitakuwa ni Ufalme mmoja, Ufalme wa Mungu – Ufalme wako uje!:
15Malaika wa
saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa
dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki
hata milele na milele. Ufunuo 11
10Nikasikia
sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu
wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu
zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Ufunuo 12
Siku moja inakuja – asubuhi ya milele, wakati Haki itakapomiliki
duniani kwa sababu Ufalme wa Mungu utakuwa unatawala maisha wa duniani huku.
Biblia inatufundisha hivi:
44Na katika
siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa
milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote
vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. Danieli 2
13Nikaona
katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja
na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu
naye. 14Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili
watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni
mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza
kuangamizwa. Danieli 7
Na tena:
13Nakuagiza
mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu,
aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, 14kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo
lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; 15ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye
aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa
mabwana; 16ambaye yeye peke yake
hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna
mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata
milele. Amina. 1Timotheo 6
Wanafunzi wa Yesu walijua yakini kuwa:
1.
Ufalme wa Mungu uko ndani yao.
2.
Ufalme wa Mbinguni haujaja kwa nguvu kati yao. Wakamuuliza Bwana
kuwa huo Ufalme wa Mbinguni utakuja lini? (Mdo 1:6-10). Labda walikuwa na maana
juu ya Ufalme wa Mbinguni ambao umekuwa ni wa Mungu kwa maungamo na kwa
madhihirisho.
Bwana akawaambia wazi kuwa hiyo sio kazi yao kuyajua hayo majira
wala nyakati ambazo Baba ameweka katika mamlaka yake mwenyewe! Bwana akawaambia
kuwa wakati wanasubiri majira ya Baba, wahubiri juu ya Ufalme wa Mungu ndani ya
mioyo ya wanadamu – yaani Haki ipatikanayo kwa Imani katika Yesu Kristo, ambaye
hapo baadae atakuja kuuleta Ufalme wa Mungu duniani – yaani Mbingu zitatawala
duniani.
Wakati fulani
Paulo alifundisha kuwa: “17Maana ufalme wa
Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho
Mtakatifu. 18Kwa kuwa yeye amtumikiaye
Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu.” Warumi
14
Baadhi ya viongozi wa dini ya Kiyahudu hawakupenda kabisa Bwana
Yesu atawale juu yao. Tangu mwanzo Shetani na mawakala na wafuasi wake
hawakutaka (na hawataki) dunia itawaliwe na Mbingu za Mungu! Ndio maana
walimkataa Yesu kuwa Mfalme wao – wakampenda Kaisari zaidi ya Yesu. Na kwa
kweli walimpenda mnyang’anyi na muuaji – Baraba, badala ya Yesu (Yohana
19:12-15 na Luka 23:2 Mathayo 27:15-23).
Bwana Yesu alitoa unabii kuhusu Israeli kumkataa kabisa kama
Mfalme wao na Masihi. Katika Luka 19:11-27 Bwana anatoa mfano huu kwa sababu
walikuw anakaribia Yerusalema, na kuwa Wayahud walidhani kuwa Ufalmewa Mungu
ungelwa Mungu ungelitoitokea mara (Mst 11). Mfano huu unasema:
12Basi akasema,
Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na
kurudi. 13Akaita watu kumi katika watumwa
wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata
nitakapokuja. 14Lakini watu wa
mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu
atutawale. 15Ikawa aliporudi, ameupata
ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida
aliyopata kila mtu kwa biashara yake. 16Akaja wa kwanza,
akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. 17Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa
mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. 18Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta
mafungu matano faida. 19Akamwambia huyu
naye, Wewe uwe juu ya miji mitano. 20Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu
lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.21Kwa maana
nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.22Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa
mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna
nisichopanda; 23basi, mbona hukuiweka fedha
yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake? 24Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo
fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi. 25Wakamwambia,
Bwana, anayo mafungu kumi. 26Nawaambia, Kila
aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho
nacho. 27Tena, wale adui zangu,
wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu. (msisitizo ni
wangu)
Bwana Yesu ndiye aliyekwenda / amekwenda hadi sasa – Mbinguni
“nchi ya mbali” kuupokea (Ufalme wa Mungu) na kurudi – ATARUDI.
Wenyeji wa mji wake walimchukia. Hawa hayumkiniki ni Wayahudi
waliomkataa! (Yohana 1:12)
Aliporudi aliugawa Ufalme kwa miji kwa wale waaminifu (Bwana
atakaporkwa miji kwa wale waaminifu (Bwana atakaporudi ataugawa Ufalme wake kwa
wale waliokuwa waaminiflme wake kwa wale waliokuwa waaminifu)
Adui zake – yaani wale ambao walimkataa aliwaadhibu: “Tena, wale
adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.” Bwana
atakaporudi pia atafanya hukumu kwa wale wote waliomkataa!
Bwana Yeu atakaporudi mara ya pili (kumbuka sikusema
“atakapokuja mara ya pili” kwa makusudi) kama Mfalme, Mkuu wa Vita na Simba wa
Yuda, tutagundua tofauti kuu sana na ile ya kwanza alipokuja kama Mwana Kondoo
wa Mungu, mpole na mnyenyekevu sana!
Alipokuja mara ya kwanza ALICHINJWA, akamnunulia Mungu, kwa Damu
yake, “watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,” akawafanya “kuwa ufalme
na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi” – Ufunuo 5:9-10
Mpendwa, Kumiliki juu ya nchi kunakuja kwa hakika sana,
tukiendelea kuwa waaminifu kwa Bwana aliyesafiri.
Bwana ali[okuja mara ya kwanza alituacha tujenge UFALME WA MUNGU
ndani ya mioyo ya watu na kujenga mazingira hayo kwa kujenga Ufalme wa Mbinguni
duniani – yaani Kanisa! Kila anayeupokea Ufalme huu anaokoka na uharibifu
ulioko duniani kwa sababu ya tamaa (2Petro 2:4), na kuwa sehemu ya huo Ufalme
ambao Biblia inauita UFALME WA KIKUHANI (1Petro 2:9).
Iko siku Bwana Yesu atakuja duniani kama Mfalme wa Ufalme wa
Mungu duniani.
Tukisoma Injili zote tunagundua kuwa Bwana alipokuwa duniani
alihubiri jumbe mbili kubwa tofauti
1.
Kwa Wayahudi walioahidiwa Ufalme wa kisiasa, alihubiri Ufalme wa
Mbinguni (Math 4:17). Ni Ufalme ambao hata Yohana aliuhubiri (Math 3:2)Mitume
nao waliambiwa wahubiri vivyo hivyo (Math10:7): Tubuni kwa maana Ufalme wa
Mbinguni umekaribia
2.
Kwa wanadamu wote kwa ujumla – Wayahudi na Mataifa – Bwana
alihubiri Ufalme wa Mungu kuwa unakuja. Tazama kwa mfano Marko 1:14-15: Tubuni
na kuiamini Injili!
Kama mara tano tu Mathayo anasema kuhusu Ufalme wa Mungu (Math
6:33, 12:28, 19:24, 21:31&43. Marko yeye anasema mara 15. Tunajua kuwa kuna
sehemu ambazo Ufalme wa Mungu umetajwa kama Ufalme wa Mbinguni na kinyume chake
– kama Mathayo 18:3 na Marko 10:14, Mathayo 13:24 na Marko 4:28, Mathayo 11:12
na Luka 16:16
Injiili zote nne (4) katika Biblia, zinamtazama Bwana Yesu kwa
sura mbalimbali, labda pia kwa sababu Mungu aliwaandaa waandishi wake kwa jinsi
mbalimbali pia.
Marko na Luka hawakuwa wanafunzi (Thenashara) wa Yesu. Wao
walisikia habari za Bwana Yesu kutoka kwa wale waliotembea naye, nao wakaandaa
kumbukumbu kadhaa simulizi kumhusu Yesu. Luka, kwa mfano, anasema (Luka 1):
1Kwa kuwa watu
wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa
katikati yetu, 2kama walivyotuhadithia wale
waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea
mwanzo, 3nimeona vema mimi nami, kwa kuwa
nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa
taratibu, Theofilo mtukufu, 4upate kujua
hakika ya mambo yale uliyofundishwa.
Yohana na Mathayo ndio waandishi pekee wa Injili ambao walikuwa
wanafunzi wa Yesu.
Yohana anamtafakari Yesu katika ukiroho zaidi. Namhudhurisha kwa
wasomaji wake kama Mchungaji Mwema, Njia, Kweli, Uzima, Mkate wa Uzima, Maji
yaliyo hai, Neno la Mungu, Nuru, na kadhalika. Injili yake imejaa ukweli kuwa
Yesu Ni Mwana wa Mungu, Mwokozi wa ulimwengu (Yohana 20:30-31).
Mathayo (au Lawi) aliitwa kuwa mwanafunzi wa Bwana Yesu akiwa
mtoza kodi. Walikutana na Bwana Yesu forodhani (Mathayo 9:9, Luka 5:29). Bwana
alipomwita, aliacha kazi yaek ya kutoza kodi akamfuata.Mathayo anamtazama Yesu
kama Mpango wa Mungu kwa Israeli uliotimizwa, na mpango wa Mungu kwa mataifa
pia.
Akiandika Injili anajenga hoja ya siri ya Mungu kwa dunia. Hoja
hii inaanza na kumfunua Yesu kuwa Yeye Ndiye Mfalme aliyeahidiwa kwa Israeli.
Hebu sasa kwa kifupi tuone anavyojenga hoja hii:
Mathayo
Sura1
|
Mathayo
anaelezea ukoo wa Yesu ili kuonyesha kuwa huyu mtoto Yesu NDIYE Mtoto wa
Kiume aliyetabiriwa, atakayemiliki katika Kiti cha Enzi cha Daudi (Isaya
7:17)
|
Mathayo
Sura2&3
|
Anaonyesha
Ushahidi wa Ufalme wake unaokuja – yaani:
a.
Mamajusi wa Mashari(Mst 11) – Linganisha na Ushuhuda wa Wakuu wa Makuhani na
Waandishi (Mathayo 2:4,5, na Mika 5:2)
b.
Ubatizo wake pale Yordani na amdhihirisho mbalimbali (Mathayo 3:16-17): “Naye
Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu
zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na
tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu,
ninayependezwa naye”
Matokeo
yake?
Herode
(M-edomu, kizazi cha Esau) akatamani kumuua – na Mungu akamuokoa.
|
Mathayo
Sura 5-7
|
Baada
ya ubatizo na Majaribu, Bwana Yesu anatoa sasa kanuni za Ufalme wake ujao –
katika “Hotuba ya Mlimani”
Hizi
ni kanuni ambazo zimejaa maadili na uadilifu katika Ufalme wa Mungu ujao.
|
Mathayo
Sura 8-10
|
Baada
pia ya Ubatizo, Bwana anafanya miujiza mingi inayomdhihirisha kuwa Yeye ndiye
Mfalme ajaye.
Kwa
mara ya kwanza watu wanafunguliwa dhidi ya mateso ya pepo na magonjwa. Katika
historia ya mwanadamu, kwa mara ya kwanza, pepo wanawatoka watu!
“Na
habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi,
walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na
wenye kupooza; akawaponya.” – Mathayo 4:24
1.
Wenye ukoma wakatakaswa
2.
Mtoto wa akida akaponywa
3.
Mama mkwe wa Petro akaponywa homa
4.
Bwsana akatuliza mawimbi ya bahari
5.
Mgerasi mwenye pepo akaponywa
6.
Wenye kupooza wakaponywa
7.
Binti wa miaka 12 akaponywa
8.
Mama aliyetokwa damu kwa miaka 12 apaponywa
9.
Vipofu wakapata kuona tena
10.
Viziwi na bubu wanafunguliwa
“Hata
kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake,
akawaponya wote waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno lililonenwa na
nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa
yetu.” Mathayo 8:16-17 (Mathayo 9:31ff)
“1Akawaita
wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na
kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. 7Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema,
Ufalme wa mbinguni umekaribia. 8Pozeni
wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni
bure.” – Mathayo 10
Matokeo
yake?
Tangu
wafadhaike alipozaliwa hadi ajifunue kwa Israeli, wakuu wa Israeli
walichochea watu kukataa ushahidi wowote kuwa Bwana Yesu NDIYO Masihi na
Mfalme aliyetabiriwa!
Ni
muhimu sana kujua kuwa katika sura ya 10 Bwa aliwatuma Mitume wake 12
wakahubiri kwa Israeli tu. Aliwaamuru:
*
Wasiingie kwa mataifa
*
Wasiingie kwa walio machotara wa mataifa na Waisraeli – yaani Wasamaria
*
Watafute tu Waisraeli waliopotea
*
Wakatangaze kuwa Ufalme wa Mbinguni umekaribia (Mstari 5-7)
|
Mathayo
Sura11
|
Bwana
Yesu anakataliwa rasmi kuwa Mfalme na Masihi kwa Israeli. Ni katika sura hii
tunasikia kwa mara ya kwanza makemeo ya miji ale ambayo Bwana alifanya
miujiza mingi – miji ya Korazini, Bethsaida na Kapernaumu (Mathayo 11:21-25)
|
Mathayo
Sura12
|
Sura
hii ni kama Mafarisayo wanafikia kiwango cha juu cha kukataa umasihi na
ufalme wa Bwana Yesu. Wanadai kuwa anatoa pepo kwa Belzebuli, mkuu wa pepo
(Math 12:24).
Mpango
wa Mungu ulikuwa wazi tu – yaani kuinua Israeli kama Taifa la Mfalme, ili
dunia ibarikiwe KUPITIA WAO.
*
Israeli wakakataa mpango huu
*
Israeli wakakataa Ufalme wa Mungu katikati yao.
|
Mathayo
Sura13
|
Sura
13 ya Mathayo inaanza na
*
Somo jipya kabisa
*
Mbinu mpya kabisa za kuelezea mambo ya mbinguni, na za kufundishia.
Kabla
ya hapo, Bwana Yesu alitumia vielelezo (illustrations). Kuanzia sura ya 13
Bwana anaanza kutumia mifano (parables). Wakati yaonyesha kuwa vielelezo
vilikuwa na nia ya kumdhihirisha Bwana katika Israeli, mifano inakuwa na nia
ya kuufunua ukweli kwa wake wanaoamini tu, na hata kwa hao ilimpasa Bwana
kuwaeleza maana zake. Mifano ilikuwa ni kama vitendawili vyenye viashiria vya
maana zake.
Toka
sura ya 13 na kuendelea, kila alipozungumza na wasioamini,Bwana alitumia
mifano.
|
Mpango wa Mungu hauwzi kutotimia kamwe. Kuna ushahidi kwenye
Biblia kuwa mpango wa Mungu waweza kuahirishwa hadi baadae.
Katika Agano la Kale Mungu aliwahi kuahirisha kusudi na mpango
wake kwa Israeli pale Kadeshi-Banea. Tunasoma haya katika Kumbukumbu 1 na
Hesabu 12-14.
Hesabu
Sura 12 (Hazerothi)
|
*
Miriamu na Haruni wanampinga Musa kwa sababu ameoa mwanamke Mkushi. Mungu
anampiga Miriamu kwa ukoma, na kuelesa jinsi anavyojifunua kwa wanadamu
|
Hesabu
Sura 13 (Mst 3,36 – Parani)
|
*
Musa anatuma wapelelezi kuipeleleza Kanaani
*
Wapelezi wanarudi kwa Musa (Mst 26) kutoa taarifa
*
Wapelelezi wanaleta taarifa mbaya kwa wana wa Israeli na luwakatisha tamaa
sana (Mst 28-33)
|
Hesabu
Sura 14
|
*
Sura hii inafunua uasi mkuu kwa Israeli (Mst 1-10)
*
Mungu anaamua kuwaangamiza wote (Mst 11-12)
*
Musa anawaombea neema kwa Mungu (Mst 13-19)
*
Mungu, kwa neema yake anawasamehe (Mst 20-21)
* Mungu anaahirisha mpango wa kuingia Kanaani kwa Israeli kwa
kizazi kile (Mst 22-23)
* Mungu anaamuru miaka 40 ya kutangatanga jangwani – yaani mwaka 1
kwa kila siku 1 ya upelelezi (Mst 26-35)
*
Watu wanatubu na kuasi hapohapo (Mst 39-45 cf Kumb.1:40-45)
|
Mpango wa Mungu lazima utekelezeke!
Ni muhimu sana kujua kuwa jambo lolote lililo dharura kwa
wanadamu liko katika mpango kamili wa Mungu. Ni muhimu sana kujua, kwa mfano,
kuwa Kutataliwa kwa Yesu, Kuuawa kwa Yesu, Kifo cha Yesu, Ufufuo wa Yesu, na
Utawala wake – vyote vilikuwa na ni muhimu sana katika mpango mzima wa wokovu
wetu (Mdo 3:13-26).
Sura ya 13 inayo mifano saba ya muhimu sana kujifunza kuhusu
Ufalme wa Mbinguni.
Mfano 1: Mfano wa “Mpanzi”:
3Akawaambia
mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda
kupanda. 4Hata alipokuwa akipanda, mbegu
nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; 5nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na
udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; 6na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina
mizizi zikanyauka. 7Nyingine
zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga; 8nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa,
moja mia, moja sitini, moja thelathini. 9Mwenye masikio na
asikie.
Mfano 2: Mfano wa “Ngano na Magugu”
24Akawatolea
mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu
njema katika konde lake; 25lakini watu
walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda
zake. 26Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa,
yakaonekana na magugu. 27Watumwa wa
mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema atika konde
lako? Limepata wapi basi magugu? 28Akawaambia, Adui
ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende
tukayakusanye? 29Akasema, La; msije mkakusanya
magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.30Viacheni vyote
vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao,
Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano
ikusanyeni ghalani mwangu.
Mfano 3: Mfano wa “Punje ya Haradali”
31Akawatolea
mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali,
aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; 32nayo
ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote,
ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.
Mfano 4: Mfano wa “Chachu Ndani ya pishi Tatu”
33Akawaambia
mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke,
akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia.
Mfano 5: Mfano wa “Hazina iliyositirika”
44Tena ufalme
wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu
alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote,
akalinunua shamba lile.
Mfano 6: Mfano wa “Lulu Nzuri, Moja ya Thamani Kubwa”
45Tena ufalme
wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; 46naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda
akauza alivyo navyo vyote, akainunua.
Mfano 7: Mfano wa “Juya Lililotupwa Baharini”
47Tena ufalme
wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila
namna;48hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi,
wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.
Ni Mathayo peke yake anayeelezea mifano yote saba. Mifano ya
“Mpanzi” na “Haradali” pia hupatikana katika Injili za Marko 4:1-9,13-20, 30-32
na Luka 8:5-15.
Mfano wa “Chachu” pia hupatikana katika Injili ya Luka 13:20-21
Wanafunzi wa Yesu walipomuuliza juu ya mifano – kwa nini ameamua
sasa kutumia mifano badala ya vielelezo, ndipo aliposema maneno yale makuu:
NINYI MMEJALIWA KUZIJUA SIRI ZA UFALME (Mathayo 13:11).
Kabla hatujapita kuzipeleleza Siri za mifano ya Bwana katika Mathayo
13 na pengine, hebu tujaribu kujibu swali hili:SIRI NI NINI?
Siri (mystery) katika Agano Jipya (AJ) ni Ukweli ambao haukuwa
dhahiri katika Agano la Kale (AK), bali umefunuliwa katika AJ kwa Watakatifu.
Tunasoma hivi katika Wakolosai 1:26: “siri ile iliyofichwa tangu
zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake”.
NA katika
Waefeso 3 tunasoma: “5Siri hiyo hawakujulishwa
wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na
manabii zamani hizi katika Roho”
Kulingana na maelezo hayo hapo juu, Siri inazo sifa kuu mbili:
1.
Ukweli ambao ulifichwa na haukuwa dhahiri katika Agano la Kale
2.
Ukweli uliofunuliwa katika Agano Jipya kwa Watakatifu.
Sio lazima Siri iwe jambo gumu kulielewa – hasha! Ni ukweli
unaoeleweka vyema kwa kufafafnuliwa.
Kwa mfano, Agano la Kale linasema wazi juu ya Ujio wa Kristo na
kutawala katika Kiti cha Enzi cha Daudi – huu ukweli sio wa kificho.
Katika Mathayo 13 na kwingineko tunasoma juu ya Ufalme wa Kiroho
anaotawala Yesu wakati Yeye yuko Mbinguni, yaani kabla ya Yeye kurudi mara ya
pili kutawala.
Hivyo Siri za Ufalme Ufalme zinahusiana na kipindi katikati ya
ujio wake wa kwanza na ule wa pili – na sio utawala wake wa miaka 1000 akirudi
mara ya pili. Bwana katika hekima yake ameamua kutufunulia sisi kwa Roho.
6Walakini iko
hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao
wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika
siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu
wetu; 8ambayo wenye kuitawala dunia hii
hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa
utukufu; 9lakini, kama ilivyoandikwa,
Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia
katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. 10Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho
huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 11Maana ni nani
katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani
yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. 12Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho
atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. 13Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa
hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya
rohoni kwa maneno ya rohoni. – 1Wakorintho 2
Bwana Yesu anawaambia wanafunzi wake kuwa wamejaliwa kuzijua
SIRI ZA UFALME WA MUNGU – yaani akili na ufahamu wao vimefahamu wao
vimefunguliwa ili wajue. Unajua inamgharimu Mungu kwa Roho wake kutufungua
tujue hata maandiko ndani ya Biblia. Tunawajua akina Kleopa waliokutana na
Bwana Yesu wasimjue hadi akili zao zilipozibuliwa!
25Akawaambia,
Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!26Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia
katika utukufu wake? 27Akaanza kutoka
Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye
mwenyewe. 28Wakakikaribia kile kijiji
walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele. 29Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa
kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao.30Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa
mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.31Yakafumbuliwa
macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. 32Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu
hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko? – Luka 24
Ziko siri nyingi za Ufalme wa Mungu, bali zile zilizofunuliwa
kwetu zinatokana na huyu Yesu. Tunasoma hivi katika Neno:
2ili
wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa
kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo; 3ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na
maarifa zimesitirika.- Wakolosai 2
Katika Mathayo 16:17 Bwana Yesu akizungumza kumhusu Simon mwana
wa Yona anasema: “…Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu
havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.” Au kwa lugha nyingine
anamwambia kuwa yeye amefunuliwa Siri – Kristo – yaani sio Kristo Mwana wa
Daudi tu, bali Mwana wa Mungu!: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai”.
Katika Mathayo 16 Bwana Yesu anataja Siri ya ajabu sana –
yaani:
1.
Uahirishwaji wa Ufalme kwa Israeli – na anampa Simoni (Labda
Mnaftali toka Bethsaida, sio M-Yuda toka Bethlehemu) majukumu makuu ya ukuu: “18Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba
huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19Nami nitakupa
wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa
limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa
mbinguni.”
2.
Usimikwaji wa Masihi kwa ungamo la Petro: Kristo (yaani Mpakwa
Mafuta, yaani Masihi) Mwana wa Mungu aliye hai
3.
Uanzishaji wa “Taifa jingine” (Mathayo 21:43), taasisi mpya
iitwayo Kanisa: “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu
nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda”.
·
Hii ni taasisi yenye ushindi
·
Hii ni taasisi inayojenga Ufalme wa Mbinguni na kuuleta Ufalme
wa Mungu – kwanza kwa Israeli na kwa mataifa yote.
Hebu sasa turudi nyuma kidogo kwenye maandiko tuuone unabii
kuhusu mpango mzima wa Mungu na jinsi ulivyo kupitia Yesu.
Kupitia Israeli, Mungu alitamani sana kuibariki dunia kwa ahadi
au maagano mawili makubwa Mungu aliyoweka na Ibrahimu.
AHADI / AGANO 1:
Ahadi / Agano la kubariki dunia kupitia Abramu (Kumbuka sikusema Ibrahimu, kwa
sababu alikuwa hajabadilishwa jina na alikuwa hajatahiriwa. Alikuwa badi sio
baba wa mataifa yote!) – Mwanzo 12:3
Ahadi au agano hili ni kwa sababu ya uteule wa Abramu
AHADI / AGANO 2:
Ahadi / Agano la kujibariki (kulingana na Union Version Bible) – Mwanzo 22:18
(kumbuka Mwanzo 26:4 – Isaka – ahadi kwa Israeli ya kumiliki nchi, na dunia
kubarikiwa!)
Ahadi au agano hili ni kwa sababu ya UZAO (sikusema Wazao bali
Uzao) wake – yaani uzao wa Ibrahimu. Katika Wagalatia 3 tunasoma: “Basi
ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba
ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo.”
Ndani ya Ibrahimu Mungu tayari alikuwa na Masihi, Mwokozi wa
dunia. Mungu katika hekima yake akamchagua Isaka – na sio wale watoto wengine
wa Ibrahimu. Ibrahimu alipata neema kuwa na watoto nane. Ismaeli – mtoto wa
Hajiri (aliyemzaa akiwa na umri wa miaka 86), Isaka – mtoto wa Sara (aliyemzaa
akiwa na miaka 99). Baada ya Sara kufa, Ibrahimu alimuoa mwanamke aitwaye
Ketura (Mwanzo 25:1-6) akamzalia watoto 6, yaani Zimrani, Yokshani, Medani,
Midiani, Ishbaki, na Sua.
Inawezekana pia kuwa Ibrahimu, kwa kuwa ni baba wa mataifa
mengi, alikuwa hivyo kupitia kwa watoto hawa – yaani Waisraeli, Waishmailia,
Waedomu kupitia kwa Esau (Mwanzo 25:12-18), Waamaleki kupitia kwa mjukuu wa
Usau (Mwanzo 36:1-40), Wakenazi kwa Esau huyuhuyu(Mwanzo 36:12-16). Wamidiani
kupitia kwa Midiani, mtoto wa Ibrahimu, na Waashuru kupitia kwa Yokshani
(Mwanzo 25:1-5).
Ndani ya Isaka Mungu akawa na Mwokozi wa dunia. Mungu
akamchagua Yakobo (baadae Israeli) na sio Esau.
Ndani ya Israeli Mungu alikuwa na mwokozi wa Dunia – yaani Yesu.
Mungu akamchagua Yuda. Katika Mwanzo 49:10 Biblia inaitaja “Fimbo ya Enzi”
ambayo “haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata
atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.” Mungu hakuwachagua
wengine 11!
Ndani ya Yuda, Mungu alimwona Daudi aliyefanywa kuwa mfalme wa
pili wa Israeli. Mungu akafanya naye Agano la milele la ufalme wake – Biblia
inaliita “Agano la Chumvi”
Hesabu 18:19 – “Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu,
wana wa Israeli wavisongezavyo kwa Bwana, nimekupa wewe na wanao na binti zako
pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za
Bwana kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe.”
Walawi 2:13 – “Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia
chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la
Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.”
2Nyakati 13:5 – “je! Haikuwapasa kujua ya kwamba Bwana, Mungu wa
Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa agano la
chumvi?”
Yesu alipodhihirishwa duniani, alijulikana kama ‘Mwana wa
Daudi’. Hatujui kuwa wazo hili la ‘Mwana wa Daudi’ lilijengwaje ndani ya watu
kwa sababu kila alipopita – Yudea, Samaria hata nje ya mipaka ya Uyahudi, watu
walishuhudia kuwa Yeye ndiye ‘Mwana wa Daudi’ waliyemtarajia. Naamini ni Roho
wa Mungu aliliweka ndani yao!
Haikuhitaji
watu kufundishwa kuwa Yesu ni nani! Wote walimjua kuwa Yeye ni Mwana wa Daudi!
Hadi mbali sana, mipakani mwa Tiro na Sidoni, kwa Wakananayo, Yesu alijulikana
hivyo hivyo – Mwana Daudi!Math.15:21-22: “Yesu akaondoka huko,
akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka
ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti
yangu amepagawa sana na pepo.”.
Kumbe ndiyo maana unabii kuhusu Agano Jipya kwa Israeli unasema
kuwa Israeli “hawatafundishana kila mtu na jirani yake, na kila mtu na ndugu
yake, akisema, Mjue Bwana, kwa maana wote watanijua, tangu mdogo wao hata
mkubwa wao…” (Waeb.8:11).
Huyu ndivyo alivyofunuliwa. Ndivyo alivyo hadi milele. Katika
Ufunuo wa Yohana alionekana hivyo, Mwana wa Daudi, Mfalme! Malaika alishuhudia
kuwa yeye Yesu anao “Ufunguo wa Daudi” Uf.3:6-8. Yeye ni “Simba aliye wa
Kabila la Yuda, Shina la Daudi”.
Katika Uf.5:4-6 tunasoma:
Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye
kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Na mmojawapo wa wale wazee
akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye
ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba. Nikaona
katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale
wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe
saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.
Huu ni
ushuhuda wa wale Wazee wa mbinguni. Yesu mwenyewe anashuhudia kuwa yeye ndiye
“Shina la Mzao wa Daudi” Uf.22:15-17.
Nia ya Msingi ya wokovu wa Mungu ilikuwa ni kuiokoa dunia
kupitia Israeli!
Yesu alipofunuliwa aliendelea kukiri kuwa huduma yake ni Israeli
– “Kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” Math. 10:5-7. Hata alipotakiwa na
wanafunzi wake afanye muujiza wa kumponya mtoto wa mama kule katika mipaka ya
Tiro na Sidoni, Yesu alisema wazi kuwa wito wake wa msingi sio mataifa – la! Ni
Israeli!
23Wala yeye
hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache
aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. 24Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo
waliopotea wa nyumba ya Israeli. 25Naye akaja
akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie. 26Akajibu,
akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. 27Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula
makombo yaangukayo mezani pa bwana zao. 28Ndipo Yesu
akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo.
Akapona binti yake tangu saa ile. Math.15
Mara nyingi Yesu alitahadharisha hatari ya Israeli kutojali
nafasi ya uteule wao waliyopewa. Tena aliweka bayana kuwa Mungu anaweza kabisa
kuahirisha hata kubadilisha uteule wao.
Kwa tahadhari hiyo, Bwana Yesu alitoa mfano katika Luka
14:16-24, mfano wa bwana mmoja aliyefanya karamu lakini walioalikwa walitoa
udhuru kwa nia moja.
16Akamwambia,
Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi, 17akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale
walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.8Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza
alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali
unisamehe. 19Mwingine akasema, Nimenunua
ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. 20Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo
siwezi kuja.21Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya
mambo hayo..
Walioalikwa walipoamua kwa sababu zao kutofika, nafasi ilitolewa
kwa wale waliokuwa hawakualikwa mwanzo.
Basi, yule
mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika
njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu,
na viwete. 22Mtumwa akasema, Bwana, hayo
uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi. 23Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani
na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. 24Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa,
hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.””.
Katika Math.22:2-14 tunasoma zaidi habari ya wale waliokuwa
wamealikwa mwanzo:
2Ufalme wa
mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi. 3Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja
arusini; nao wakakataa kuja. 4Akatuma tena watu
kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu
yangu; ng’ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari,
njoni arusini.
5Lakini
hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara
yake; 6nao waliosalia wakawakamata watumwa wake,
wakawatenda jeuri, na kuwaua. 7Basi yule mfalme
akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza
mji wao.
8Kisha
akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa
hawakustahili. 9Basi enendeni hata njia panda za
barabara, na wote mwaonao waiteni arusini. 10Watumwa wale
wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi
ikajaa wageni.
11Lakini
alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja
asiyevaa vazi la arusi.12Akamwambia,
Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa. 13Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na
miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga
meno. 14Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni
wachache.
Unaona? Neno linasema kuwa wale walioila ile karamu ni wale
waliotoka “katika njia kuu na vichochoro vya mji”. Ni wale walioshurutishwa
kuingia ndani ili nyumba ya Bwana ipate kujaa. Ndipo Yesu akasema: “Maana
nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana mmoja atakayeionja karamu
yangu” Luka 14:24. Maneno makuu sana, maneno ambayo wahubiri wengi hata leo
hawataki kuyasikiliza kabisa. Bwana akisema “katika wale walioalikwa, hapana
mmoja atakayeionja karamu yangu”, ana maana ileile!
Walioalikwa,
hatuna shaka, ni Israeli. Ndio waliofanyiwa sherehe, wakatoa udhuru kila mmoja.
Aina ya upinzani Yesu aliokutana nayo katika huduma ulikuwa mkubwa. Wakati
fulani alitamka `ole’ nyingi sana kati ya viongozi wa Israeli (Math.23) kisha akatoa unabii juu ya Yerusalemu (Yaani
Israeli!): “Kwa maana nawaambia, hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema,
Amebarikiwa ajaye kwa Jina la Bwana” Math. 23:39.
Nyumba ya Israeli, Yesu alitamka, itaachwa ukiwa, na kweli
imeachwa ukiwa! Math. 23:38
Wakati Yesu akiingia Yerusalemu mara ya mwisho kabla ya kuuawa
alisema maneno haya magumu kwa machozi:
Laiti ungalijua hata wewe, katika siku hii, yapasayo amani!
Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako
watakujengea boma, likuzunguke, watakuzingira na kukuhusuru pande zote,
watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako. Wasikuachie jiwe juu ya
jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako – Luka 19:41-44.
Labda ni hekima tukagusa kidogo juu ya Israeli kumkataa Bwana.
Katika Injili ya Yohana (Yoh. 1:11) tunasoma wazi kuwa Yesu
alipokuja kwake, walio wake hawakumpokea. Katika Yoh.5:43 Yesu anasema wazi
kuwa yeye amekuja kwa Jina la Bwana, na hawampokei! Ndiyo maana Yesu
alipokuwa anaingia Yerusalemu kama Mfalme aliulilia mji ule
mtakatifu (Luka 19:41-44) – kuwa laiti wangalijua juu ya siku ile
aliyoingia Yerusalemu, juu ya yapasayo amani. Ole wa Yerusalemu kwa sababu
hawakujua majira ya kujiliwa kwake!
Yeremia
ni nabii wa ajabu aliyeona Mungu akikumbuka hukumu ya Israeli kwa sababu ya
kumkataa Masihi wao. Katika (Yer.30:4-11) tunaona juu
ya mateso kwa Israeli.
Na haya ndio maneno alivyosema BWANA, katika habari za Israeli
na habari za Yuda. Maana BWANA asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko na hofu,
wala si ya Amani. Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanaume aona utungu wa uzazi;
mbona basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye
na utungu, na nyuso zote zimegeuka rangi? Ole! Maana siku ile ni kuu, hata
hakuna inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini
ataokolewa nayo.
Yesu hakuacha kutahadharisha Israeli juu ya jambo hili. Katika
Math. 21:33-43 Yesu ananukuliwa akitoa unabii wa ufalme kutolewa kwa Israeli na
kupewa mataifa mengine (`taifa lingine’ – Swahili Union Version).
33Sikilizeni
mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la
mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga
mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. 34Wakati wa
matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee
matunda yake.
35Wale wakulima
wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga
kwa mawe. 36Akawatuma tena watumwa wengine
wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile. 37Mwishowe
akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. 38Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana,
wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi
wake. 39Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu,
wakamwua.
40Basi
atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima?
41Wakamwambia,
Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima
wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.
42Yesu
akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo
limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu
machoni petu? 43Kwa sababu hiyo nawaambia,
Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa
matunda yake. kuzaa matunda yake.
Yesu alipotoa
tuhuma nyingi za waandishi wa sheria ya Musa na waamini wa dhehebu la
Wafarisayo katikaMath.23, anasema juu ya mji uliopendwa. “Ee Yerusalemu
Yerusalem…. angalieni nyumba yenu mmeachwa hali ya ukiwa. Kwa maana nawaambia
hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema ‘amebarikiwa ajaye kwa Jila la
Bwana’”. Math 23:37-39
Kalvari ikawa ndio mwisho wa nyumba ya Israeli mpaka
kipindi cha baadaye. Mpango wa Israeli ukaahirishwa!
Ni muhimu sana kukumbuka kuwa unabii kuhusu Israeli kumkana
Mwokozi ulitolewa na manabii wengi. Mmoja aliyetaja sana jambo hili ni Danieli.
Danieli 9 ni unabii unaohusu mpango wa Mungu kubariki mataifa kupitia Israeli
pamoja na matokeo yake.
Katika sehemu hii malaika anamwambia Danieli: “Muda wa majuma
sabini umeamuriwa juu ya watu wako na juu ya mji wako mtakatifu” – yaani watu
wa Danieli – Israeli, na mji mtakatifu – yaani Yerusalemu. Hii ni amri kwa watu
wa Israeli. Muda huu ni majuma 70 kiunabii au miaka mia nne na tisini
(490). Kanuni hii ya “sabato ya miaka” inatajwa katika Walawi 25:3-4.
24Majuma sabini
yameamriwa kwa ajili ya watu wako na kwa ajili ya mji wako mtakatifu ili
kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, kuleta
haki ya milele, kutia muhuri maono na unabii pia kumtia mafuta yeye aliye
mtakatifu sana. 25Ujue na kuelewa hili: Tangu
kutolewa kwa amri ya kuutengeneza na kujenga upya Yerusalemu mpaka kuja kwa
Mpakwa mafuta, aliye mtawala, kutakuweko majuma saba na majuma sitini na
mawili. Barabara zitajengwa tena pamoja na mahandaki, lakini katika wakati wa
taabu. 26Baada ya majuma sitini na mawili Mpakwa mafuta
atakatiliwa mbali wala hatabakia na kitu – Danieli 9
Katika muda huu, malaika anasema kuwa mambo yafuatayo yatatokea:
1.
Kukomesha makosa
2.
Kuishiliza dhambi
3.
Kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu
4.
Kuleta haki ya milele
5.
Kutia muhuri maono na unabii
6.
Kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu
Mtiririko wake ni mrahisi tu. Mwanzo wa miaka 490 tunasoma wazi
kuwa ni tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kujenga upya Yerusalemu – yaani
kipindi cha mfalme Artashasta kule Babeli. Twajua kuwa amri hii iliwekwa tarehe
1 mwezi wa Nisan mwaka 445KK, mfalme alipomruhusu Nehemia aende Yerusalemu
aujenge (Nehemia 2).
Miaka 483 (majuma saba na majuma sitini na mawili = majuma 69)
baadaye unabii ulitimia. Ni kweli, Masihi alikatiliwa mbali – kwa sababu unabii
ulisema kuwa “Masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu”. Kikalenda,
hili ni lile juma walilomwimbia Yesu “Hosana Mwana wa Daudi” – akiingia
Yerusalemu, na siku chache wakamuua (Luka 19:37 na kuendelea).
Majuma 69 ya Daniel yakakoma hapa, likabaki juma la 70, kwa
sababu “Muda wa Majuma sabini umeamuriwa juu ya (Israeli) na juu ya mji wa Yersalemu”
– Dan. 9:20-27.
Utaona wazi kuwa kati ya majuma 69 na 70 bado juma moja, na
kipindi kile cha juma moja kikaahirishwa. Hapo ndipo kipindi cha Kanisa
kikaingia katikati.
Baada ya “Kukomesha makosa” na “Kuishiliza dhambi” na “Kufanya
upatanisho kwa ajili ya uovu”, bado “Kuleta haki ya milele”, “Kutia muhuri
maono na unabii”, na “Kumtia mafuta yeye aliye Mtakatifu”.
Tunashangaa sana sasa na kuelewa kwa nini unabii wa Isaya katika
Isaya 61 unatimia Mstari 1-2a tu. Tunayaona haya kwa Yesu mwenyewe akisoma
gombo la chuo pale hekaluni siku ya kwanza ya huduma yake hekaluni hivi:
16Akaenda
Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama
ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 17Akapewa
chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, 18Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia
mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa
kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
20Akakifunga
chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi
wakamkazia macho. 21Akaanza
kuwaambia, ‘Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.’ – Luk 4:16-21
(linganisha na Isaya 61:1-2).
Pia tunaona kuwa unabii wa Yoeli (Yoeli 2) ukatimia mstari 28-29
tu. Tunajua kuwa bado 30-32.
Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu
wote Roho wangu. Watoto wenu, wanaume kwa wanawake, watautangaza ujumbe wangu;
vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto. Naam, hata
watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, nitawamiminia Roho wangu, siku zile, nao
watautangaza ujumbe wangu. Nitatenda miujiza juu angani, na ishara chini
duniani; kutakuwa na damu, moto na moshi mzito; jua litatiwa giza, na mwezi
utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya kutokea ile siku kuu na tukufu ya Bwana.
Hapo, yeyote atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa. Mdo 2:17-21
Yesu aliagiza: “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili”
(Math. 28:19, 20 na Marko 16:15-16). Hii ni baada ya kuwaagiza kuwa katika njia
ya mataifa wasiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria wasiingie; na kuwa
afadhali wafuatilie kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Math. 10:5, 6). Je,
utume wa Bwana umebadilika?
Mitume wakidhani kuwa Israeli wangelishituka wageuke, walianza
kuhubiri kwa nguvu Yerusalemu kwa Waisraeli.
Lakini Yesu aliwaambia kuwa sasa waanzie Yerusalemu –
Uyahudi wote, Samaria na hatimaye, mwisho wa nchi. Tunasoma:
6Basi
walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo
unapowarudishia Israeli ufalme? 7Akawaambia, Si
kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake
mwenyewe. 8Lakini mtapokea nguvu, akiisha
kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi (miisho
ya dunia). Mdo 1:6-8.
Mitume walidhani, kwa ushahidi wa mahubiri yao, kuwa maeneo yote
hayo – Yerusalemu, Uyahudi kote na Samaria na hata mwisho wa dunia – ni
kuwaleta Wayahudi katika Imani ili Yesu arejee haraka! Mara Petro akahubiri
siku ya kwanza Yerusalemu kwa Wayahudi (Waisraeli). Matunda yakawa ya kutisha,
wakaongoka watu zaidi ya 3,000 siku ile moja. Baada ya hapo tunasoma katika
kitabu cha Mdo 3:17-26 kuwa mkazo wa mahubiri ukawa kuwa watu watubu na
kurejea, ili Yesu Mfalme arejee haraka kama Mfalme wao!
Matokeo ya mwendelezo wa Injili ukawa mbaya sana! Wakafungwa
gerezani (Mdo 4:1-3) na mateso yakaanza rasmi. Stefano akauawa (Mdo 7-8:3) na
mitume wakatawanyika huko na huko.
Lakini jambo lingine la ajabu likatokea: mataifa na wachawi
wakaanza kuokoka (Mdo 8:4-40). Mara Sauli – Mbenjamini akaokoka (Mdo 9),
na akapewa naye ufunuo wa kuhubiri injili kuanzia kwa mataifa.
Wongofu wa Sauli ni muhimu sana kwa Kanisa. Yeye aliwekwa kuwa
“chombo kiteule (kwa Mungu) alichukue Jina (la Mungu) mbele ya mataifa, na
wafalme, na wana wa Israeli” – Mdo.9:15. Mjuzi wa torati huyu hakuamini kuwa
aanzie kwa mataifa, bali alianzia Dameski katika Masinagogi.
Matokeo yake yakawa mabaya sana. Wakataka kumuua hadi ndugu
wakamtorosha usiku baada ya kupata habari ya njama ile (Mdo 9:23-25). Biblia
inasema kuwa Sauli akakimbilia Yerusalemu kwa ndugu. Kule Yerusalemu,
akahojiana na Wayahudi wa Kiyunani na kuwafadhaisha sana kwa elimu yake kubwa.
Matokeo yake yakawa vilevile – mabaya. Wakajaribu kumuua. Ndugu wakaona vyema
wamrudishe Tarso – kwao – na Uyahudi kukatulia! Mdo 9:29-31
Hatimaye, Mungu alimwita rasmi, yeye na Barnaba (Mdo 13:1-3),
kwa wito mpya kabisa. Kwa neema ya Mungu wakawaacha Israeli rasmi na kugeukia
mpango mpya wa Mungu uitwao Kanisa.
“Hata hivyo, Paulo na Barnaba waliongea kwa uhodari zaidi,
wakasema, ‘Ilikuwa ni lazima Neno la Mungu liwafikieni ninyi kwanza; lakini kwa
kuwa mmelikataa na kujiona hamstahili uzima wa milele, basi, tunawaacheni na
kuwaendea watu wa mataifa mengine. Maana Bwana alituagiza hivi: `Nimekuteua
wewe uwe mwanga kwa mataifa, uwe njia ya wokovu kwa ulimwengu wote.’` Watu wa
mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi, wakausifu ujumbe wa Mungu;
na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uzima wa milele, wakawa waumini”. Mdo
13:46-48
Tunasoma hivi pia katika Mdo 18:1-11:
“ … Walipompinga na kuanza kumtukana, aliyakung`uta mavazi yake
mbele yao akisema, ‘Mkipotea ni shauri lenu wenyewe; mimi sina lawama yoyote
juu ya jambo hilo. Na tangu sasa nitawaendea watu na mataifa mengine’.
Basi, akatoka hapo akaenda kukaa nyumbani kwa mtu mmoja mcha Mungu aitwaye Tito
Yusto. Nyumba yake Tito ilikuwa karibu na lile sunagogi… Wakorintho wengi
waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na kubatizwa. …Basi, Paulo alikaa
huko akifundisha neno la Mungu kati yao kwa muda wa mwaka mmoja na nusu”.
Kwa kweli
waliwageukia mataifa ili mataifa na wana wa Israeli sasa
waingie katika mstakabali mpya wenye taasisi mpya iitwayo KANISA.
Biblia inasema wazi juu ya
kundi la Israeli pamoja na mataifa – yaani taasisi iitwayo Kanisa, ikaingia
kati ya Majuma 69 na lile la 70 la Israeli. Hii ni siri, Kanisa.
Siri hii walifunuliwa mitume na hasa Paulo. Hebu soma Neno
lisemavyo:
3ya kwamba kwa
kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno
machache.4Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu
katika siri yake Kristo. 5Siri hiyo
hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake
watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; 6ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi
mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika
Kristo Yesu kwa njia ya Injili; 7Injili hiyo
ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu
niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake. 8Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa
watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo
usiopimika; 9na kuwaangaza watu wote wajue
habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika
Mungu aliyeviumba vitu vyote; 10ili sasa, kwa
njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na
mamlaka katika ulimwengu wa roho; 11kwa kadiri ya
kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.12Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia
katika tumaini kwa njia ya kumwamini. Waef.3.1-12
Tunasoma
katika Warumi kuwa ni kweli ugumu umewapata Israeli “mpaka
utimilifu wa mataifa uwasili” (Swahili Union version)– na mpango wa
Israeli utaendelea, yaani “juma lao la 70” litaendelea.
Ninyi watu wa mataifa mengine, kwa asili ni kama tawi la mzeituni
mwitu, lakini mmeondolewa huko, mkapandikizwa katika mzeituni bustanini mahali
ambapo kwa asili si penu. Lakini, Wayahudi kwa asili ni kama mzeituni
bustanini, na itakuwa jambo rahisi zaidi kwao kupandikizwa tena katika mti
huohuo wao…Maana Mungu akisha wapa watu zawadi zake na kuwateua, hajuti kwamba
amefanya hivyo. Hapo awali ninyi mlikuwa mmemwasi Mungu, lakini sasa mmepata
huruma yake kutokana na kuasi kwao. Hali kadhalika, kutokana na huruma
mliyojaliwa ninyi, Wayahudi wanamwasi Mungu sasa ili nao pia wapokee sasa
huruma ya Mungu. Maana Mungu amewafunga watu wote katika uasi wao ili apate
kuwahurumia wote. Warumi11:24-32.
Katika War 9:25-33 tunasoma hivi:
“Maana ndivyo asemavyo katika kitabu cha Hosea: “Wale waliokuwa
`Si watu wangu` nitawaita: `Watu wangu!` Naye `Sikupendi` ataitwa: `Mpenzi
wangu’! Na pale walipoambiwa: `Ninyi si wangu` hapo wataitwa: `Watoto wa Mungu
hai`”. Naye nabii Isaya, kuhusu Israeli anapaaza sauti: “Hata kama watoto wa
Israeli ni wengi kama mchanga wa pwani, ni wachache tu watakaookolewa;
maana, Bwana ataitekeleza upesi hukumu yake kamili juu ya ulimwengu wote….”
Tena Paulo anaandika:
18Lakini
nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote,
Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. 19Lakini nasema,
Je! Waisraeli hawakufahamu? Kwanza Musa anena, Nitawatia wivu kwa watu ambao si
taifa, Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhibisha. 20Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema, Nalipatikana
nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia. 21Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa
naliwanyoshea mikono watu wasiotii na wakaidi. War 10:18-21
Katika War 11:8-12 anaongeza:
…Basi, nauliza: je, Wayahudi wamejikwaa hata wakaangamia kabisa?
Hata kidogo! Kutokana na kosa lao ukombozi umewajia watu wa mataifa mengine,
ili Wayahudi wapate kuwaonea wivu. Kosa la Wayahudi limesababisha baraka
nyingi kwa ulimwengu, na utovu wao kwa kiroho umeleta baraka nyingi kwa watu wa
mataifa mengine. Basi, ni dhahiri zaidi kwamba utimilifu wao utasababisha
baraka nyingi zaidi.
Tangu kipindi hiki cha Kanisa
kianze hadi kitakapofikia ukomo, watu wote huingia kwenye kundi liitwalo Kanisa
– Israeli kwa mataifa – kwa kumwamini Yesu! Nasema tena,wote – Wayahudi kwa Mataifa! Haya tunasoma katika
Waef.3:1-12, kama tulivyoona hapo juu. Watu wote, bila upendeleo huingizwa kwa
kumpokea Yesu moyoni!
Katika Wakolosai 1:13-29 tunasoma tena ukweli huu ukijirudia:
“Yeye alituokoa katika nguvu ya giza, akatuleta salama katika
ufalme wa Mwanae mpenzi, ambaye kwa njia yake tunakombolewa, yaani dhambi zetu
zinaondolewa…Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu
hapa duniani, nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya
Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani Kanisa. Nami nimefanywa kuwa
mtumishi wa Kanisa kufuatana na mpango wake Mungu ambao alinikabidhi kwa faida
yenu. Mpango wenyewe ni kuutangaza kwa ukamilifu ujumbe wake, ambao ni siri
aliyowaficha binadamu wote tangu milele, lakini sasa amewajulisha watu wake.
Mpango wa Mungu ni kuwajulisha watu wake siri hii kuu na tukufu ambayo ni kwa
ajili ya watu wote. Na, siri yenyewe ndiyo hii: Kristo yuko ndani yenu, na
jambo hilo lamaanisha kwamba ninyi mtaushiriki utukufu wa Mungu… Maneno mazito
sana!
Unajua, katika kitabu cha Ufunuo Neno linasema kuwa Yesu
anasimama mlangoni anabisha, na ni wajibu wa mtu kufungua mlango na
kumkaribisha Yeye. Tena katika Yohana tunapata ukweli kuwa wote waliomkaribisha
– yaani waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu – yaani wale
waliaminio Jina lake. (Soma Uf 3:20 naYoh.1:12).
Kanisa ni Mwili wa Kristo Mwenyewe. Katika Waef 1:22-23, 5:23
tunasoma:
Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake, akamkabidhi kwa
Kanisa akiwa mkuu wa vitu vyote. Kanisa ni mwili wa Kristo, na ukamilifu
wake yeye anayekamilisha vitu vyote kila mahali… Maana mume anayo mamlaka
juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya Kanisa; naye Kristo
mwenyewe hulikomboa Kanisa, mwili wake.
Kanisa nalo
linajengwa na Yesu mwenyewe.“Nami nakwambia: wewe ni Petro, na juu ya mwamba
huu nitalijenga Kanisa langu; wala kifo chenyewe hakitaweza kulishinda” – Math.16:18
Mungu alimsimamisha Paulo kama mjenzi mkuu wa Kanisa. Huu ndio
ushuhuda wake katika kuungana na Yesu:
“10Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama
mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu
yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.11Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka,
isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. 12Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu
au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu
itakuwa dhahiri. 13Maana siku ile
itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu
kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. 14Kazi ya mtu
aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.”. 1Wakor 3:10 – 14.
Watu wengine wote katika utumishi huliendeleza Kanisa kwa Karama
mbalimbali walizokirimiwa na Roho Mtakatifu! Tazama pia Waef 4:15-16,
1Wakor 12:23-27.
Tumeona kuwa kumekuwa na kuahirishwa kwa mstakabali wa Israeli
baada ya kumkataa Masihi, bali kwa kitambo kidogo. Hapo juu tumeona kuwa baada
ya “majuma 69”, Mungu alisitisha “juma 1” la sabini kwa kipindi kisichojulikana
– na kipindi hiki kinaitwa cha Kanisa. Na katika kipindi hiki ambacho tumekiona
kuwa kinaitwa kipindi cha Kanisa, tunajifunza kuwa kitaendelea hadi “utimilifu
wa mataifa uwasili”.
Mpendwa, sasa tunavyozungumza, Waisraeli na mataifa ni sawa
mbele za Mungu. Siku zinakuja Mungu atakapoanza kushughulikia Israeli kama
Israeli – yaani juma la sabini lililoahirishwa!
Kuna watu wanasumbua watu wa Mungu juu ya uteule wa Israeli ya
sasa. Hata wanapotaka kwenda kuhiji, sio kuona tu historia ya imani yao bali
wanadai kuwa ni ili kuvuna baraka kwa kulibariki ‘taifa la Mungu’. Huu ni
uzushu mkubwa! Baraka zetu hazitoki hapo. Tena Taifa la Mungu sasa ni Kanisa,
ambalo ndani yake lina Israeli na ‘mataifa’.
Kuna mambo makubwa mawili ambayo lazima kuyajua:
Baraka za mtu aliyempokea Yesu hazipo katika ‘kuwabariki
Israeli’. Hiki sio kipindi hicho! Kwa mtu aliyeokoka, AMEBARIKIWA KWA BARAKA
ZOTE, ndani ya Yesu. Hivi ndivyo Biblia inavyoshuhudia: “Ahimidiwe Mungu na
Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni,
katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo” – Waef.1:3
Katika Yesu Kristo, hakuna tofauti kati ya Myahudi au Myunani,
wote ni sawa kabisa mbele za Mungu. Biblia inasema hivi: “Kama yasemavyo
Maandiko, ‘Ye yote amwaminiye hatatahayarika’. Kwa maana hakuna tofauti kati ya
Myahudi na Myunani, Yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao.
Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokoka’’ – Warumi 10:11-13.
Katika 1Wakor 1:22-24 tunasoma: “Kwa sababu Wayahudi wanataka
ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; bali sisi tunamhubiri Kristo,
aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao
waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu”.
Tena Paulo anakaza katika Wagal 3: 26-29 kuwa
26Kwa kuwa
ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. 27Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa
Kristo. 28Hapana Myahudi wala Myunani.
Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote
mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.29Na kama ninyi ni
wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Katika 1Wakorintho 4:1-2 Paulo anasema kuwa watu watuhesabu kuwa
tu watumishi wa Kristo na mawakala wa siri za Mungu. Paulo pamoja na Mitume
wengine walifunuliwa siri kadhaa zinazohusiana na Ufalme wa Mungu.
Hebu sasa tuone siri kadhaa hasa zinazohusiana na Ufalme.
Katika
Wakolosai 2:1-2 Biblia inasema wazi kuwa Yesu ndiye Siri ya Mungu!
Siri zote za Munguzimefichwa ndani ya Yesu Kristo.
Paulo akiwaandikia Waefeso, anakwenda kwa undani kuhusu SIRI, na
kuwa Yesu NDIYE Siri ya Mungu kwa dunia.
Katika Waefeso 1:3-14 Neno linatuonyesha bila tashwishi kuwa
NDANI YA YESU tuna vitu vyote. Siri iko ndani ya Yesu Kristo. Tunasoma kuwa:
1.
Mungu AMEtubariki kwa
baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa roho, NDANI YAKE KRISTO (Mst 3)
2.
Mungu AMEtuchagua –
KATIKA YESU – kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili tuwe watakatifu, watu
wasio na hatia mbele zake katika pendo (Mst 4) – na sio katika Sheria na
Torati.
3.
Mungu ALITANGULIA kutuchagua
ili tufanywe wanawe kwa NJIA YA YESU KRISTO sawasawa na uradhi wa mapenzi yake
(Mst 5)
4.
KATIKA YESU tumepata neema (Mst 6)
5.
KATIKA YESU – kwa Damu yake – tunao ukombozi – yaani masamaha ya
dhambi sawasawa na wingi wa neema yake (Mst 7).
6.
KATIKA YESU Mungu amekusudia kutuzidishia hekima na ujuzi wa
kumjua Yeye (Mst 8) – kwa kuamua kutufunulia Siri ya Mapenzi yake – sawasawa na
uradhi wake alioukusudia katika Yesu (Mst 9)
Siri ya mapenzi yake ni kuleta madaraka ya wakati mtimilifu
(Wagal.4:4) ili kuvijumulisha vitu. vyot katika Yesu – vitu vyote duniani na
mbinguni (Tazama Wakol1:20) (Waef.1:10). Rejea pia 1Wakor.3:21-23 na
Wafil.2:9-10.
1.
Mungu ametufanya sisi kuwa urithi wa
Kristo na warithi pamoja na Kristo
(Rejea Waef.1:11, War.8:17, Waeb.1:1-4 ukilinganisha na Israeli katika
Kumb.4:20, 32:9 na Hosea 2:23)
2.
Mungu alituchagua hivyo tangu awali sawasawa na kusudi lake
Yeye, kwa shauri lake Yeye – ili tuwe sifa na utukufu wake (Mst 12)
3.
Mungu, kwa sababu hii, ametupa muhuri wa Roho wa Ahadi,
Mtakatifu, na Roho kama arabuni ya urithi wetu. Nia yake ni kuleta ukombozi wa
milki yake (yaani sisi – Kanisa) kuwa sifa ya utukufu wake (Mst 13).
Ndani ya Yesu kuna KANISA. Huu NDIO ufunuo mkuu sana wa Siri ya
Mungu.
Kama kuna sehemu Paulo ameandika kwa undani juu ya Ufunuo wa
Mungu ndani ya Yesu ni Waefeso 2,3 alipoandika kuhusu Ufunuo wa KANISA. Hebu
kwa neema ya Mungu tupitie kwa kifupi kuhusu funuo hizi.
Waefeso
2:1-3
|
Biblia
inasema ukweli wa ajabu sana kuwa sisi sote tulikuwa WAFU. Kuna kweli 7
kuhusu UFU katika Agano Jipya
1.
Kuna watu wanaoishi lakini ni wafu (dead living people). Math 8:22, 2Wakor
5:14, Uf.3:1: “Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao”
“Maana,
upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa
kwa ajili ya wote, basi walikufa wote”
“Nayajua
matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa”
2.
Watu waliokufa bali ni hai (Living dead people). War.6:2,7-14, 2Tim2:11:
“2Hasha! Sisi
tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?… 7 kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki
mbali na dhambi. 8Lakini tukiwa
tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye; 9tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu
hafi tena, wala mauti haimtawali tena. 10Maana kwa kule
kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake,
amwishia Mungu.
11Vivyo hivyo ninyi nanyi
jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo
Yesu. 12Basi, dhambi isitawale ndani
ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; 13wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha
za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya
kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. 14Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu
hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.”
“Ni
neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye
pia”
3.
Miili iliyokufa kwa sababu ya dhambi, yenye roho zilizo hai kwa sababu ya
haki. War.8:10: “Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya
dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.”
4.
Miili iliyokufa. Yohana 5:28-29, Yakobo 2:26: “28Msistaajabie
maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini
wataisikia sauti yake. 29Nao watatoka;
wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa
ufufuo wa hukumu.”
“Maana
kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo
imekufa”
5. Kazi
mfu. Waeb.6:1,9:14: “1Kwa sababu
hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili
tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na
uhai,…”, “14…basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba
kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa,
itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?”
6.
Imani mfu. Yakobo 2:17,20,26: “17Vivyo hivyo na
imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. 20Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu,
kwamba imani pasipo matendo haizai? 26Maana kama
vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.”
7.
Dhambi iliyokufa. War.7:8: “Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya
ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.”
|
Waefeso
2:4-7
|
Mungu
alituhuisha PAMOJA na Kristo – yaani tumeokolewa kwa neema:
·
Alitufufua pamoja na Kristo
·
Alituketisha pamoja na Kristo katika ulimwengu wa roho KATIKA Kristo (Mst 6)
·
Kuna jinsi atakavyoudhihirisha wingi wa neema yake upitao kiasi – katika siku
zijazo (Mst.7)
“Nasi
katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea
Kristo tumaini letu” – Waefeso 1:12
|
Waefeso
2:11-12
|
Zamani
tulikuwa (sisi wa Mataifa):
·
Wasiotahiriwa
·
Watu wasio na Kristo
·
Watu waliofarakana na jamii ya Israeli
·
Wasio na maagano na ahadi ya urithi
·
Wasio na tumaini
·
Watu wasiokuwa na Mungu
Lakini katika Kristo hali yetu IMEbadilika sasa
|
Waefeso
2:13-22
|
Biblia
inafungua ukurasa mpya kabisa – KATIKA YESU:
Tumeletwa
karibu na Mungu kwa damu ya Yesu (Mst 13)
Uadui
na tofauti za Israeli na Mataifa ZIMEKUFA – wawili (yaani Israeli na Mataifa)
waMEkuwa mmoja – yaani kuna amani sasa (Mst 14)
Matika
MWILI wa YESU – Waisraeli na Mataifa ni MMOJA! Uadui umefishwsa kwa Msalaba
wa Yesu (Mst 16-17)
Yesu
sasa NDIYE NJIA ya pekee ya kumkaribia Baba kwa Roho mmoja (Mst 19)
Sasa
Mataifa, kama walivyo Israeli, ni wenyeji pamoja na Watakatifu – watu wa
nyumbani kwake Mungu (Mst 19-22)
|
HII NDIYO SIRI Mungu aliyoifunua katika Kristo – Siri ya
Munbgu juu ya wanadamu wote! Katika Waefeso 3:1-13 Biblia inafafanua juu ya
Siri hii. Hebu tuone kidogo:
1.
Neno linasema kuwa kwa kweli Mungu ndiye aliyeamua kutujulisha
Siri yake Kristo (Mst 1-5)
2.
Siri hii ni: MATAIFA NA ISRAELI NI:
·
Warithi pamoja, wenye urithi mmoja (Mst 6)
·
Washiriki wa Mwili mmoja (Mst 6)
·
Washiriki pamoja wa Ahadi za Mungu (“Ahadi yake” iliyo) katika
Kristo (Mst 6)
·
Tamko la Ushiriki huu ni INJILI!
3.
Injili – ambayo Paulo alifanywa mhudumu wake (Mst 7) – ni hii:
·
Kuwahubiria Mataifa kuwa sasa mlango umefunguliwa (Mst 8)
·
Kuwaangazia watu wote – Mataifa na Israeli – wajua madaraka (au
mamlaka) ya Siri hii
·
Kuwafunulia wanadamu ukweli kuwa sasa Mungu amejifunua kwa
“taasisi” iitwayo KANISA (Mst 10-11)
·
Kuwaamsha watu wote wajue kuwa kwa Yesu
·
Tuna Ujasiri na uwezo wa
kukaribia kwa Mungu katika tumaini
·
Tuna Njia ya kumkaribia Mungu katika tumaini, Njia hiyo ni
KUMWAMINI YESU (Mst 12)
Ndio maana paulo anasema wazi kuwa sasa WATU WOTE (Mataifa na
Israeli) wanaweza kuwa washiriki wa Ufalme wa Mungu kwa NJIA MOJA TU, nayo ni
KUMWAMINI YESU.
Katika Wakolosai sura ya kwanza tunasoma wazi:
24Sasa
nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili
wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani,
kanisa lake; 25ambalo nimefanywa mhudumu wake,
sawasawa na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la
Mungu;26siri ile iliyofichwa tangu
zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu
wake; 27ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri
wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu 28ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila
mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu
mtimilifu katika Kristo. 29Nami
najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake
atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.
Kwamba Mungu hakuwatupa kabisa Israeli ni Siri nyingine ambayo
Munbu ameifunua kwetu. Labda bado tunakumbuka ile picha:
Biblia inasema wazi kuwa karama za Mungu hazina majuto, wala
mwito wake (Warumi 11:29).
Kipindi cha kanisa kilianza baada ya majuma 69 ya Danieli – kama
tulivyosema hapo juu. Hii ni baada ya Israeli kumkataa Mfalme asiwe Mfalme wao.
Mpango wa Mungu ukasitishwa kwa muda, na kuliahirisha JUMA LA 70 la Israeli.
Mungu katika hekima yake akatangaza “Taifa jingine” lenye kuzaa
matunda, yaani KANISA (Mathayo 21:33-43).
Lakini JUMA LA 70 litaanza SIKU ZA KANISA ZIKIKOMA – yaani
Kanisa litakaponyakuliwa.
Katika Warumi 11:25-32 Paulo anaweka ukweli huu bayana sana:
25Kwa maana,
ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba
kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa,
Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 27Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea
dhambi zao. 28Basi kwa habari ya Injili
wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa
wapenzi kwa ajili ya baba zetu. 29Kwa sababu
karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake. 30Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu,
lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao; 31kadhalika na hao
wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema. 32Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili
awarehemu wote.
Tmesoma nini?
1.
Mataifa wasiwe wajinga – bali waijue Siri ya Mungu pia kuhusu
Israeli
2.
Kuwa ugumu umewapata Israeli kwa muda tu – na sio milele
3.
Kipindi cha ugumu wa Israeli Mungu amewaruhusu Mataifa waingie –
na idadi yao Mungu ameiweka (“mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili”), Kumbuka
Luka 11:24 na War.11:7-12:
“24Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara
na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata
majira ya Mataifa yatakapotimia.”
“7Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa
akikitafuta hakukipata; lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine
walitiwa uzito. 8Kama ilivyoandikwa, Mungu
aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata
siku hii ya leo. 9Na Daudi asema,
Meza yao na iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao;
10Macho yao
yatiwe giza ili wasione, Ukawainamishe mgongo wao siku zote. 11Basi nasema, Je!Wamejikwaa hata waanguke
kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa lao wokovu umewafikilia Mataifa, ili wao wenyewe
watiwe wivu. 12Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa
ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana
utimilifu wao?”
4.
Israeli wote hatimaye wataokoka – yaani Mabaki! “27Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema,
Hesabu ya wana wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari,ni mabaki yao tu
watakaookolewa.28Kwa maana Bwana atalitekeleza
neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.” War.9
Kipindi hii cha Israeli nj kipindi kipya kabisa chenye kanuni
tofauti na zile za Kanisa. Ni Juma la 70 la Danieli 9.
Katika Juma hili – yaani miaka kama 7 hivi,
1.
Kanisa litakuwa halipo – limeondoka. Waaminifu wamenyakuliwa, na
taasisi iitwayo Kanisa imefungwa!
Unyakuo utakuwa umetokea. Hebu kwa kifupi sana niseme juu ya
Unyakuo:
1.
Utakuwa SIO KWA WATU WOTE, yaani sio kwa Wakristo wote! Utakuwa
kwa wanawali wenye busara (Math.25:1-13). Wale
wasiokuwa na busara Bwana atawaambi “siwajui” ni sio “sikuwajua”. Aliwajua kwa
kuwa waliokoka, bali kwa habari ya unyakuo, hawakujiweka tayari, hivyo HAWAJUI.
Linganisha na Math 7:21-23 na Luka 13:23-30 Bwana anaposema “Sikuwajua”
2.
Tunajua kwa hakika kuwa Bwana AMECHELEWA kuja (Math 25:1-13)
3.
Katika Unyakuo huu kutakuwa na matengano makuu! Watu wawili
watakuwa kitanda kimoja, au wakisaga nafaka, au wakiwa shambani, mmoja atwaliwa
mmoja aachwa.(Math.24:39-42 na Luka 17:34-37). Wakati wa unyakuo wa
Elia, kulikuwa na matengano makuu kati ya Elia na Elisha (2Wafalme 2:1-18)
4.
Watu wengi watabaki, na watajaribu kuwa na maelezo mengi juu ya
jambo lililotukia. Baada ya Unyakuo, miujiza mingi pia yawezekana itafanya
duniani, kwa sababu Roho wa Neema na Kuomba atakayemwagwa kwa Israeli atafanya
miujiza mara dufu kwa Kanisa – yaani upako mara mbili. Kumbuka kuwa Elisha
alikuwa na upako mara mbili ya Elia (Elia alifanya miujiza 8 iliyonukuliwa
katika Biblia wakati Elisha alifanya 16). Kumbuka pia Ufunuo 7 juu ya wahubiri
144,000 walio na upako – labda ni uke upako wa Zekaria 12:10
5.
Roho Mtakatifu atakuwa ameondoka na Kanisa
6.
Roho atakayeletwa duniani ni Roho wa Neema na Kuomba – kama
asemavyo Zekaria 12:10: “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji
wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma;
nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao
wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya
mzaliwa wake wa kwanza.”
7.
Roho wa Muhuri atakaa juu ya waisraeli 144,000 – kila kabila
watu 12,000. Nao wataitwa “Watumwa” wa Mungu (Ufunuo 7
8.
Kutakuwa na amani kwa Israeli kwa miaka 3kulingana na Danieli
9:27: “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa
nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama
chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa
juu yake mwenye kuharibu”
9.
Hekalu la Yerusalemu litajengwa ili kuanza ibada za daima na
kafara
10.
Kipindi cha miaka 3ya kwanza kitakuwa mateso kwa Wakristo
waliochwa, kwa kuwa hawana taasisi ya kuwasaidia, wala Roho Msaidizi. Lakini
inawezekana kutakuwa na Mvua za Mwisho – yaani uamsho mkuu sana dumiani (Hosea
6:3, Yoeli 2:23, na Zekaria 10:1)
11.
Baada ya miaka 3Israeli itaanza kipindi cha mateso. Kumbuka
unabii huu: “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma
moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na
mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu
iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu”. Watateswa kwa maana
watampinga mtawala ajiinuaye juu ya Mungu – yaani Mpinga Kristo na Nabii wa
Uongo. Kumbuka Nabii hizi: 2Wathe.2:1-4,Yer.30:1-15, Dan 9:12,
12:1, Amosi 5:18 na Zephania 1:14.
12.
Vita vitainuka kuimaliza Israeli. Tunasoma juu ya uvamizi toka
Kaskazini (Ezekieli 38:1-16)
Mungu atawapigania sana – Zekaria 14:1-5, 12
Labda hii ndio vita ya Harmagedoni ya Ufunuo 16:12-21, 19:11-21.
Katika 2Petro 3:1-15 tunasoma haya:
… 9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama
wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote
apotee, bali wote wafikilie toba. 10 Lakini
siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa
mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi
zilizomo ndani yake zitateketea. 11 Basi, kwa
kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia
gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, 12 mkitazamia
hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu
zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? 13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia
mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. 14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo
hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele
yake. 15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa
ni wokovu…
Tena Petro anasema: “Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia
mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu
mbele zake”. Kuna mambo matatu yanatajwa hapa katika eneo hili. Jambo la kwanza
ni wito wa kuishi maisha matakatifu, na la pili ni sisi kuitazamia siku ile
ije, na jambo la mwisho ni sisi kuihimiza siku ile.
Jambo la kwanza litakalokuhakikishia unyakuo si asili ya
utakatifu tu bali tabia ya utakatifu iliyo matokeo ya asili ya utakatifu. Asili
ya utakatifu ni YESU aliyeko moyoni mwako. Mungu alimfanya Yesu kwetu
kuwa haki, utakatifu na ukombozi – 1Wakor.1:30.
Ukimpokea Yesu moyoni unazaliwa kuwa na asili nyingine iitwayo
mwana wa Mungu au tabia ya uungu (Yoh. 1:12, 2Petro 3, 4). Asili yako inabadiliki.
Unazaliwa katika “boma” jingine – boma la Mungu mwenyewe; na unarithi asili hii
ya utakatifu kwa sababu aina ya roho unayepewa ni Roho wa Utakatifu – au Roho
Mtakatifu.
Mungu anataka nini baada ya hayo? Wewe na mimi tubadilike
tabia ili idhihirishe utakatifu tulioupata! Huu ni wito – utakatifu
kwa tabia. Biblia inasema wazi kuwa lazima tutafute kwa bidii utakatifu (Waeb.
12:14, War. 6:21-23, 2Wakor.7:1-2, Waef. 4:23-25).
Wapendwa,
Njia ya Mbinguni bado haijawa pana, wala mlango wa kuingilia juu haujaongezeka
hata kidogo (Math. 7:13,14). Matakwa ya Mungu ya utakatifu ni yale yale
aliyoyaweka kwa Danieli (dhidi ya dola lile ovu la Babeli), ni yaleyale
aliyowawekea mitume kipindi kile cha Warumi wabaya wale hadi kipindi cha leo
chenye elimu iliyozidi sana – 1Pet. 1:16-25! Bado viwango vya utakatifu (1Pet.
1:16-25) ambavyo Mungu anavyotaka tuviamini na kuvifikia ni vile vile vyake
mwenyewe: “Kama yeye aliyewaita alivyo Mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu
katika mwenendo wenu wote” mst.15.
Mungu tunayemtumikia
hata leo ni Mungu yule yule MTAKATIFU. Roho anayeliongoza Kanisa la Mungu leo
ni Roho yule yule wa Mwanawe ambaye Biblia inamwita Roho Mtakatifu. Bado vigezo
vya kuingia kule Mbinguni na mtindo wa hukumu havijabadilika! Kila mtu
atahukumiwa sawasawa na matendo yake! Uf.20:12,13 (Linganisha
na Dan. 12:2).
Utakatifu wa Yehova aliouona Isaya ni ule ule utakaotuangusha
mbele zake kama mtu mfu (Isa.6:1ff) – kwa sababu pamoja na unabii wake mkuu,
mbele za Yehova alisema: “Ole wangu” kwa sababu aligundua AMEPOTEA.
Mungu tunayemngojea ni Mungu Mtakatifu. Huyu ndiye aliyekutana
na Simoni mwana wa Yona kando ya Ziwa la Genesareti akampa muujiza wa samaki
wengi hata vyombo vikataka kuzama, akaanguka miguuni/magotini kwa Yesu
akasema: “ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana” –
Luka 5:1-11.
Huyu ndiye Mungu aliyekutana na Sauli pale njiani Dameski
akasema na Sauli. Ndiye aliyemwambia Sauli: “Ni vigumu kwako kuupiga
mateke mchokoo” – Mdo 26:14. Huyu ndiye Mungu aliyepambana na kiburi cha Herode:
“Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu, akaliwa na
chango, akataka na roho” Mdo 12:20:23. Kwa nini? Kwa sababu hatampa mwingine
utakatifu wake (Isa 48:10,11)!
Kila watu katika kizazi chao, Mungu alidai utakatifu kwao. Haijalishi
kuwa hali iko je, Mungu alidai Utakatifu kwa sababu aliandaa mawezesho. Mungu
hadai kitu kwetu asichotuwezesha kukifanya. Katika utumishi wetu, katika shida
zetu, katika mafanikio yetu, Mungu anadai Utakatifu. Hebu tuone mifano kidogo
kuelezea ukweli huu:
MUSA
Tunamjua
mtumishi huyu wa Bwana kwa jinsi anavyonenwa katika Biblia, kuwa alikuwa mpole
sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya nchi (Hes.12:3). Katika
Waebrania 3:5 tunasoma kuwa Musa alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya
Mungu kama mtumishi. Ndiye ambaye alikataa kabisa kwenda hudumani kwa sababu
aliona hawezi na Mungu akamtia nguvu. (Kut. 3:9-4:1-16).
Pamoja na Mungu “Kum’bembeleza”, bado alidai utakatifu kwake!
Katika Kut.4:22-26 tunamwona Mungu akipambana naye kwa sababu alidharau agano
la tohara. Tunamshukuru Mungu kuwa katikati ya hali hiyo, Sipora alikuwepo!
Akamtahiri mwanae (labda alikuwa Gerson) kwa dhiki nyingi ili kuutimiza
utakatifu! Ndiye Musa huyu huyu aliyechoshwa na uasi wa Israeli hata
akajikwaa kwa MANENO NA MAZOEA yake.
Utakumbuka Kut 17:1-7 kwenye bara la Sini kule Refidimu? Mungu
alimwamuru Musa alipige jabali ambalo Mungu AMESIMAMA JUU YAKE – maji yakatoka,
watu wakanywea lile jabali. Lakini katika Hes 20:1-13, miaka mingi
baadae, tunaona tena kule Kadeshi. Mungu alimwamuru Musa auambie Mwamba
utoe maji YAKE – Mwamba wenye maji ndani yake! Musa hakufanya hivyo kwa sababu
ya uzoefu wa kwanza pamoja na maudhi ya wana wa Israeli aliokuwa anawaongoza;
na likawa kosa kubwa sana mbele za Bwana. Bwana akamwambia yeye na Haruni kuwa
hawataingia Kanani “Bwana akajionyesha kuwa Mtakatifu kati yao” Hes. 20:13.
SAULI.
Mungu wetu aliyemchagua Sauli na kumkataa baadaye! – Sauli
mfalme wa kwanza wa Israeli.
Vita ya kwanza iliyomjaribu ni ile ya Wafilisti (1Sam.13:5-14).
Sauli hakuwa mvumilivu, kwa sababu alipaswa amsubiri Samweli kwa ajili ya kutoa
sadaka ya kuteketeza. Badala yake akawa na pupa na kuitoa sadaka ya kuteketezwa
– naye sio kuhani. Samweli akauita UPUMBAVU (Hebu soma Mst. 13-14)! Unabii
ukatoka juu ya Sauli hivi: “Bwana amejitafutia mtu ampendaye moyo wake….”.
Vita ya pili ni ile ya Waamaleki (1Sam.15). Sauli alipewa amri
kuwa aende akawaangamize Waamaleki kabisa: “Basi sasa enda ukawapige Amaleki,
na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni,
mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda
” (mst. 3). Biblia inasema kuwa Sauli hakufanya hivyo: “… Sauli na watu wake
wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng’ombe, na vinono, na
wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali
cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa ” (mst.
9). Sauli akawaogopa watu, akazirukia nyara (mst. 19) na kufanya uovu mbele za
Mungu. Unajua alilolifanya Mungu? Samweli akamwambia Sauli, “… je! Bwana
huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu sawasawa na kuitii sauti ya Bwana?
Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; kwa
kuwa umelikataa neno la Bwana, yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme ” (mst.
22,23) Mungu akauraruwa ufalme wake milele!
DAUDI
Daudi, kipenzi cha Mungu, hakukosa kupitia kwenye moto wa vipimo
vya utakatifu wa Mungu! Katika 2Sam.11 tunasoma dhambi ya Daudi na Bathseba
mkewe Uria. Toba yake haikuondoa ukweli kuwa aliwapa “adui za Bwana nafasi
kubwa ya kukufuru” 2Sam.12:14 – na mtoto aliyezaliwa Mungu alimuua!
Tunapochezea maisha ya utaua na utakatifu, tunawapa ‘adui za
Bwana nafasi kubwa ya kukufuru’, na Mungu anawaka hasira juu yetu. Mungu hawezi
kukaa nasi iwapo hatujali kuishi maisha ya utakatifu.
ANANIA NA SAFIRA
Anania na Safira – leo hii tunawaona sio watu wa kiroho.
Walikuwa ndugu, tena wapendwa walioongolewa na Bwana – lakini waliuchezea
utakatifu wa Mungu (Mdo 5:1-11). Hawakuweza kuhimili vishindo vya kumwambia
uongo Roho Mtakatifu. Tunapofanya dhambi, tunauchezea utakatifu wa Mungu.
Mungu huyu mtakatifu hivi ndiye tumwabuduye. Mungu aliyewafanya
watoto wa Anania na Safira kuwa yatima, na Kanisa likamwogopa Mungu.
Mpendwa kama
tulivyotangulia kusema, katika Waeb. 12:14 Neno liko wazi: tafuteni kwa bidii.
Narudia tena; utakatifu wetu chanzo chake ni Yesu aliyeko moyoni (1Wakor.1:30).
Katika Waeb.10:14 tunasoma pia kuwa “kwa toleo moja
amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa”. Tunapoingia katika kuokoka
tunampokea Yesu Moyoni. Roho zetu zinaokoka lakini wokovu wetu hauishii
hapa.
Wapendwa, Mungu anatamani tuwe watakatifu. Neno liko wazi kuwa
utakatifu kama ilivyo amani na watu wote hutafutwa kwa BIDII -Waeb. 12:14.
Paulo amefundisha katika 1Wathe. 4:3-8 kuwa mapenzi ya Mungu ni kutakaswa kwetu
– kwa sababu Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso! Katika 2Wakor.
7:1 Biblia inafundisha juu ya kujitakasa nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na
roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.
Mtume Petro katika Roho amefundisha kuwa HATUNA UDHURU katika
kuishi maisha ya utakatifu (2Pet. 1:3,4). Mungu ametupa sisi mawezesho yote ya
kuishi maisha ya UZIMA, yaani kuokoka, na utauwa – yaani usafi na utakatifu.
Tena Mtume anatufundisha kuwa tabia hii ya UTAKATIFU ni tabia ya uungu ambayo
TUNAWEZA KABISA KUWA WASHIRIKA WAKE – na mpango kamili wa Mungu ni kutuokoa
sisi na uharibifu ulioko duniani kwa sababu ya tamaa. Neno linasema: “Kwa kuwa
uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa
kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo
ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa
washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu
ya tamaa ” (2Petro 2:3,4).
Hebu tuone Neno lasemaje katika Isaya 35:8-10: “Na hapo patakuwa
na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita
juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga,
hawatapotea katika njia hiyo. Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali
hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika
njia hiyo. Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba;
na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha,
huzuni na kuugua zitakimbia”. Katika kifungu hiki tunasoma juu ya
Njia kuu na Njia iitwayo “Njia ya utakatifu”. Utakatifu sio kituo au hali
tunayofikia wakati tunapookoka, bali ni HATUA, NI NJIA. Tena si hivyo tu,
tunasoma kuwa ni jambo moja kukwea juu ya njia hii, ni jambo jingine kupita juu
ya njia hii. Njia hii ni kwa wale walioamua kusafiri – na Bwana ameahidi
kuwashika mkono, WAJAPOKUWA WAJINGA, hawatapotea.
TUNAANZAJE KUTEMBEA KATIKA NJIA
YA UTAKATIFU?
Katika kitabu cha Ezekieli 36:25-27 tunasoma: “Nami
nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu
wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho
mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami
nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha
katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda”. Hapa
tunapata utaratibu Mungu alionao kwa wale wanaotamani kwenda Mbinguni. Katika
mistari hii, Neno la Mungu liko wazi kabisa juu ya hatua za kuokoka na kuishi
maisha ya Utakatifu. Tunaelezwa wazi kuwa maisha yetu ya kiroho yanayo hatua
mbalimbali zenye mambo mawili tu – KUFANYIWA (mambo 5) na KUFANYA (jambo 1) –
hii ndiyo neema!
HATUA 1. Kuwa safi kwa kunyunyiziwa maji – KUFANYIWA
HATUA 2. Kutakaswa na uchafu na vinyago vyetu – KUFANYIWA
HATUA 3. Kupata moyo mpya: kutoa moyo wa Jiwe ndani yetu
na kupewa ule wa nyama – KUFANYIWA
HATUA 4. Kupata roho mpya : kutia roho ya Mungu
ndani yetu – KUFANYIWA
HATUA 5. Kutuendesha katika sheria za Mungu –
KUFANYIWA
HATUA 6. Kuzishika na kuzitenda Sheria za Mungu- KUFANYA
Yawezekana na ni hakika kuwa sisi sote tuliookoka tumeletwa
hadi HATUA 5. hapo juu – tunaye Roho wa Mungu, na Mungu anatuendesha
katika sheria zake. Swali ni hili, moyo wako na roho yako vimeongoza mwili wako
hadi UKAMTII BWANA? Je umeanza KUZISHIKA na KUZITENDA sheria za
Bwana?
Namna
nyingine ya kutazama Ezek. 36:25-27 ni kupondeka, kama inavyoelezwa na Bwana
mwenyewe katika Math.21:43-44: “Kwa sababu hiyo
nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye
kuzaa matunda yake. Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye
yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki”. Yawezekana umeliangukia jiwe
(Yesu) maishani – yaani uliamua kuokoka. Je, umepiga hatua kukubali jiwe
likuangukie – Yesu sasa atawale maamuzi yako? Paulo katika Wagal. 5:25
anasema: “Tukiishi kwa roho (tukiamua kuokoka), tuenende kwa roho
(tuvunjike na kumtii Mungu).”
Hii
inawezekana unapopiga hatua kuomba sasa ili mwili wako na nia/nafsi yako
pia viokoke. Hapo ndipo unapogundua kuwa udhaifu wako uko hapa na pale, na
unapaachia Msalabani (Waeb.12:1-4).
Paulo katika War. 6:11-14 anawafundisha Warumi kuwa “Short Cut”
ya utakatifu ni:
1.
Kujihesabu mfu kwa dhambi
2.
Kujihesabu hai kwa Mungu katika Kristo
3.
Kukataa kutii tamaa ya mwili – kusema “No” kwa dhambi
4.
Kutompa Shetani viungo vyako avitumie kutendea dhambi
5.
Kumpa Yesu viungo vyako avitumie kama “Silaha za haki”
Ukifanya mambo haya kuna matokeo ya ajabu sana: “… dhambi
haitawatawala ninyi”.
Utakatifu wetu unapimwa kwa matunda matatu ambayo tunapaswa
kuyadhihirisha:
1.
Tunda la Roho: 5:22
2.
Tunda la Nuru: 3:4
3.
Tunda la haki: Yakobo 3:18
Hatua hii
ndiyo Biblia inaiita KUWA NDANI YA YESU – 2Wakor. 5:17 (1Yoh.4:17). Yesu alisema
kuwa mtu wa jinsi hiyo HUZAA SANA (Yoh. 15:1-5). Ahadi ya Yoh.15:7 ni kwa watu walio ndani ya Yesu na sio
kinyume chake! Mtu aliye na Yesu ndani, bali yeye hakuyaendea masafa ya
Utakatifu, Biblia inamwita mtu wa “tabia ya mwilini” naye ni mtoto mchanga
katika Kristo – 1Wakor.3:1-3. Tabia ya mwilini ni tofauti na wa “tabia ya
asili” (1Wakor. 2:15). Mtu wa tabia ya asili ni mtu ambaye kabisa hajawahi
kuokoka. Mtu wa tabia ya mwilini ni mtu ambaye ameokoka, bali bado anaishi
maisha ambayo sio ya utakatifu.
Nikupe shauri – Tafuta kwa bidii utakatifu! Anza leo kuishi
maisha ya utakatifu. Hii ni hatua ya kuanzia, na wewe na mimi tuna safari ndefu
ya kuyaishi maisha ya utakatifu ambayo lazima tuyaanze. Kweli tutaomba neema ya
Mungu imwezeshe kila anayesoma maneno haya ili aweze kuanza. Mungu
anasubiri ukomavu wako – siku zimekwenda, anza.
Sijui kama
unajua kuwa ingawa Mungu atashughulikia magugu yaliyoota na ngano siku ya
hukumu (Math.13:24-30), lakini pia atashughulikia makapi yaliyotia
joto ngano (Math.3:12) na ni ngano tu iliyostahimili vishindo vya pepeto
itaingia ghalani! Watu wengi sana wanadhani ni rahisi sana kwenda mbinguni –
sio! Ni ngano tupu zitakazoingia ghalani.
Dunia hii na elimu zake tutaishinda tu kwa kuweka changamoto
kwake – MAISHA YA UTAKATIFU!
♫ HALELUYA GIZA LAISHA ♪
Haleluya siku i karibu, kumwona Mwokazi wetu
Kuachana na dunia hii, ya machozi kwenda Mbinguni.
Tutaipa dunia kwaheri, Mwokozi akitunyakua
Tukipaa juu Mawinguni, kumlaki Mwokozi wetu.
Sasa wangojani msafiri, kushuhudia ya Mwokozi
Kesha, funga, omba, shuhudia, leta Roho kwa Bwana Yesu.
Hivyo ndugu yangu jipe moyo, tumalize huduma yako,
Wajiandaaje kusimama mbele ya Kiti cha hukumu
٪ Aleluya giza kwisha, Yesu anarudi mawinguni
Natamani toka nchi hii, ya machozi kwenda Mbinguni.
♫ SIRI YA UTAKATIFU ♪
Ungejua siri ya Utakatifu, ya kukaa ndani ya Yesu.
Ungejua jinsi ya kumtumikia, na kupata baraka zake.
Ungejua giza lililo njiani, unaposafiri kwenda juu
Ungejua vita vya waendao juu, ungeomba nguvu kwa Yesu.
Ungejua Pendo na nguvu za Yesu, kwao wamtegemeao
Ungempa Yesu Moyo wako wote, na kuleta watu kwa Yesu
Sasa wangojani, wewe msafiri, tulia-tu ndani ya Yesu
Siku zinakwisha, Yesu anarudi, maliza safari vizuri
٪ Ungemwita Yesu akusaidie katika udhaifu wako!
Wahitaji nguvu za Roho wa Kweli kumaliza safari yako
Jambo la pili ni kuishi kama wasafiri. Siku kwa siku
lazima tutazamie kuondoka.
Siri ya
Sikukuu ya Vibanda kati ya Israeli ni hii: wao ni wasafiri! Ibrahimu na wanawe
waliishi katika mahema daima kwa sababu walijihesabu kuwa wao siku zote ni
wasafiri. “Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi
isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye
wa ahadi ile ile… Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali
wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na
wasafiri juu ya nchi. Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba
wanatafuta nchi yao wenyewe. Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka,
wangalipata nafasi ya kurejea. Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya
mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji
”Waeb.11:9, 13-16.
·
Asubuhi tazamia Unyakuo, mchana tazamia Unyakuo
·
Jioni tazamia Unyakuo.
·
Ukiwa kazini tazamia Unyakuo, ukilala tazamia Unyakuo.
·
Ukisafiri tazamia Unyakuo!
·
Ukiumwa tazamia Unyakuo,
TAZAMIA UNYAKUO!
Lakini watazamiao huhimiza pia siku hiyo. Je, tunawezaje
kuihimiza? Yesu alifundisha kuwa Habari Njema ya Ufalme itahubiriwa kila
mahali, ndipo mwisho utakapokuja – Math. 24:14. Tunavyowavuta wengine ufalmeni
ndiyo siri ya kuhimiza siku ije!
Ukijua siku iko karibu, unakuwa na haraka na wepesi wa kumaliza
kazi ya Bwana. Unajua, siku ya kutoa hesabu iko karibu sana. Unaihimiza.
Math. 25:24-30. na Danieli 12:1-3.
Bwana ametuita kuwa tuwaelezee wengine kuwa Yesu ni Bwana.
Lazima wengine waelezwe habari za Yesu Kristo.
Lazima tulie sana mbele za Mungu ili wengine wazaliwe. Watu
wengi ni mateka kwa shetani – hata watu wengi waliookoka ni mateka, hadi neema
iwazukie waweze kufunguliwa. Kanisa lazima lilie machozi.
No comments:
Post a Comment