Imefundishwa na Mtumishi Isaac
Ridhiwan Omary (Semina ya MVUMO – Morogoro, 27th August 2016)
Imeandikwa na Samson Mollel – 0767 664 338
(www.uzimawamileleministries.blogspot.com)
Mwanzo
25:21-23
“21 Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya
mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua
mimba. 22 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi,
kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana. 23 Bwana akamwambia,Mataifa
mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni
mwako.Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo.”
Mwanzo
33:12-17
“12 Kisha Esau akamwambia, Twende zetu,
tusafiri, nami nitakutangulia. 13 Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto
ni wachanga, tena kondoo na ng'ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama
wakiharakishwa siku moja, watakufa wote. 14 Tafadhali bwana wangu na apite
mbele ya mtumwa wake; nami nitawaongoza polepole kwa kadiri ya mwendo wa
wanyama walio mbele yangu, na kwa kadiri ya mwendo wa watoto, hata nitakapofika
kwa bwana wangu huko Seiri. 15 Esau akasema, Nikuachie, basi, baadhi ya watu
walio pamoja nami. Akasema, Pana haja gani? Na nione kibali tu machoni pa bwana
wangu. 16 Basi Esau akarudi siku ile ile akishika njia yake mpaka Seiri. 17
Yakobo akaendelea mpaka Sukothi. Akajijengea nyumba, akawafanyia makundi yake
vibanda. Kwa hiyo jina la mahali pale pakaitwa Sukothi.”
Jana tumejifunza kwa habari ya mtu kama taifa
la Mungu aliye hai, na tukaona kuwa ukiwa taifa unakuwa na mipaka yako, watu
wako, lugha na usemi wako, mwongozo/katiba yako
Tulijifunza pia; kama taifa huruhusiwi kubeba
au kuruhusu mtu yoyote kuingia ndani ya mipaka yako bila kufuata taratibu, sheria
na kanuni zinzozostahili (yaani za ufalme wa Mungu). Ni lazima mtu anayetaka
kuingia katika taifa lako atomize vigezo vya kuingia katika taifa la Mungu,
yaani lazima mtu huyo atomize vigezo vyote vya kuingia kwenye mipaka ambayo
Mungu amekupa.
Sasa wewe ukifanya makosa ya kuruhusu mtu
yoyote akaingia ndani ya mipaka yako bila utaratibu, unavurugwa.
Jambo la kufahamu leo ni kwamba ukiwa kama
taifa takatifu la Mungu aliye hai, Mungu anataka ufanikiwe katika mambo yote.
Ndio maana Mungu atakupa mfumo wako wa maisha
wa kuzalisha mkate wako wa kila siku (hii ni pamoja na mavazi, kiwanja,
kujenga, magari …..)
Vilevile Mungu atakupa uwezo wa kuwasaidi
watu wa malango na wale walio nje ya malango yako
Katika mfereji huo wa kuzalisha lazima uwe
makini (wewe kama taifa lenye mipaka) ni nani unayetembea naye katika
uzalishaji wa makate wa kila siku; iwe ni kazi au biashara au kilimo lazima
ujikague upon a nani? Usiwabebe watu kutoka kwenye chungu cha kusaidia
ukawaweka kwenye mfereji wako wa kuzalisha kwani ukifanya hivyo hiyo shughuli
ya uzalishaji lazima itakufa tu!
Katika mfereji huo wa kuzalisha lazima
utembee na watu wa taifa lako na mipaka yako, mnaoelewana lugha na usemi na
ambao wanaelewa ni wapi unapoelekea
Fahamu yakuwa kuzaliwa tumbo moja (baba mmoja
na mama mmoja) sio kuwa taifa moja. Unaweza mkawa nit umbo moja lakini mataifa
tofauti na kabila tofauti, yaani hata lugha na usemi tofauti kama tunvayosoma
katika: Mwanzo 25:21-23 “21 Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke
wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua
mimba. 22 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi,
kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana. 23 Bwana akamwambia,Mataifa
mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni
mwako.Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo.”
Rebeka anaenda kuuliza mbele za BWANA kwa
habari ya mashindano ya watoto walio tumboni mwake. Mungu anamjibu jambo la
kushangaza sana “Bwana akamwambia,Mataifa
mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni
mwako.Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo.”
Jibu la kwanza ni kwamba ndani ya tumbo moja
kuna mataifa mawili (Maana yake katika
tumbo moja wantoka watu ambao wanayo mipaka tofauti na watu wake ni tofauti)
Jambo la pili ni kabila mbili za watu (maana katika tumbo moja hawafanani lugha
wala usemi wao sio mmoja)
Vilevile tunaona yakuwa kabila moja linapewa
kuwa hodari kutoka ndani ya tumbo moja, na pia linapewa kutawala kabila
lingine; lakini kumbuka watoto hawa wamezaliwa na mama mmoja na baba mmoja
lakini ni mataifa tofauti kabisa.
Hata baada ya kuzaliwa mfumo wa maisha ya
Esau ulikuwa tofauti kabisa na mfumo wa maisha ya Yakobo ndugu yake, Yakobo
alikuwa mkulima na Esau alikuwa mwindaji (Nasema Yakobo alikuwa mkulima kwakuwa
alikuwa anaweka akiba ya chakula, kwa kawaida mwindaji haweki akiba).
Baada ya miaka mingi Yakobo anakutana na
Essau kama tunavyosoma: Mwanzo 33:12-17
“12 Kisha Esau akamwambia, Twende zetu,
tusafiri, nami nitakutangulia. 13 Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto
ni wachanga, tena kondoo na ng'ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama
wakiharakishwa siku moja, watakufa wote. 14 Tafadhali bwana wangu na apite
mbele ya mtumwa wake; nami nitawaongoza polepole kwa kadiri ya mwendo wa
wanyama walio mbele yangu, na kwa kadiri ya mwendo wa watoto, hata nitakapofika
kwa bwana wangu huko Seiri. 15 Esau akasema, Nikuachie, basi, baadhi ya watu
walio pamoja nami. Akasema, Pana haja gani? Na nione kibali tu machoni pa bwana
wangu. 16 Basi Esau akarudi siku ile ile akishika njia yake mpaka Seiri. 17
Yakobo akaendelea mpaka Sukothi. Akajijengea nyumba, akawafanyia makundi yake
vibanda. Kwa hiyo jina la mahali pale pakaitwa Sukothi.”
Baada ya kukutana essau alitaka asafiri
pamoja na Yakobo lakini Yakobo kwa kujua kuwa wao ni mataifa tofauti katafuta
sababu na akakataa kusafiri pamoja na ndugu yake; Mwanzo 33:12, 14 “12 Kisha
Esau akamwambia, Twende zetu, tusafiri, nami nitakutangulia. …….. 14 Tafadhali
bwana wangu na apite mbele ya mtumwa wake; nami nitawaongoza polepole kwa
kadiri ya mwendo wa wanyama walio mbele yangu, na kwa kadiri ya mwendo wa
watoto, hata nitakapofika kwa bwana wangu huko Seiri.
Maisha ya mtu ni safari, usikubali kusafi na
mtu asiye wa taifa lako katika mfereji wako wa uzalishaji kwani mambo
yatakuharibikia, hata kama ndugu yako au ni rafiki yako au ni mlokole mwenzako
wote wanaweza kuwa sio taifa lako.
Laki Essau alitaka kumwachia baadhi ya watu;
lakini Yakobo alikataa pia kama tunavyosoma Mwanzo 33:15 “Esau akasema,
Nikuachie, basi, baadhi ya watu walio pamoja nami. Akasema, Pana haja gani? Na
nione kibali tu machoni pa bwana wangu.
Yakobo alijua kwamba kuna watu ukibaki nao
katika safari yako wanaweza kukuletea roho za kukukwamisha. Yaani ukiwapokea
watu wasio wa taifa lako katika mfereji wako wa uzalishaji utaishia kupata
hasara kila mwaka.
Fahamu hili: kwenye mkate wa kila siku
hauwaandai watu kwenda mbinguni bali unaandaa kipato chako cha kila siku
Kwenye mfumo wa kuzalisha Mungu anakuinulia
mtu/watu wa dini yoyote katika kuzalisha, hivyo isikupe tabu kufanya
kazi/biashara na watu wa dini/imani nyingine. Wewe nenda na watu wanaoelewa
lugha na usemi wako, ambao hawakuelewi waweke pembeni kwa jina la Yesu.
No comments:
Post a Comment