JITAMBUE YAKUWA WEWE NI TAIFA
TAKATIFU KWA MUNGU ALIYE HAI/MPATE YESU ILI UWE TAIFA TAKATIFU KWA MUNGU ALIYE
HAI
Imefundishwa na Mtumishi Isaac
Ridhiwan Omary (Semina ya MVUMO – Morogoro, 26th August 2016)
Imeandikwa na Samson Mollel – 0767 664 338 (www.uzimawamileleministries.blogspot.com)
Kumbukumbu
la torati 26:16-19 “16 Leo hivi akuamuru
Bwana, Mungu wako, kuzifanya amri hizi na hukumu; basi uzishike na kuzifanya
kwa moyo wako wote na roho yako yote. 17 Umemwungama Bwana leo, kuwa ndiye
Mungu wako, na kuwa yakupasa kutembea katika njia zake, na kushika amri zake na
maagizo yake, na hukumu zake, na kusikiza sauti yake; 18 naye Bwana amekuungama
hivi leo kuwa taifa iliyotengwa iwe yake yeye, kama alivyokuahidi, na kuwa
yakupasa kushika maagizo yake yote; 19 na kuwa atakutukuza juu ya mataifa yote
aliyoyafanya, kwa sifa, na jina, na heshima, nawe upate kuwa taifa takatifu kwa
Bwana, Mungu wako, kama alivyosema.”
Kumbukumbu
la torati 7:6 “Kwa maana wewe u taifa
takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake
hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.”
Somo
la leo lina vichwa viwili kama ifuatavyo
i.
Kama umeokoka – “JITAMBUE
YAKUWA WEWE NI TAIFA TAKATIFU KWA MUNGU ALIYE HAI”
ii.
Kama haujaokoka - “MPATE YESU ILI UWE TAIFA TAKATIFU KWA
MUNGU ALIYE HAI”
Ukizungumza
kuwa wewe ni Taifa kwa Mungu bila ya kujua thamani ya utaifa hauwezi kuelewa
vizuri.
Kama
leo ungepewa na Mungu nafasi ya kuchagua uzaliwe bara/nchi ipi, na ukaangalia
duniani kila nchi ilivyo ndipo uchague, kila mtu anayosababu ya msingi
angechagua nchi gani (Wengi katika mkutano wamechagua nchi za ulaya na
Marekani)
Nchi
za wenzetu (ulaya na Marekani) wanayotabia ya kuwajali sana watu wa taifa lao
mahali popote walipo. Kwamfano pakitokea vurugu yoyote ambayo hata haijafikia
kuwa ni vita katika nchi yoyte ambayo raia wa Marekani wapo, mara moja utasikia
Marekani inawarudisha raia wake; hivyo watawatumia ndege na wanajeshi wa
kuwarejesha kutoka mahali popote duniani walipo ili wasije wakadhurika na
machafuko.
Sasa
kama nchi za wanadamu wanaweza kufanya hivyo; si zaidi sana ukiwa taifa la
Mungu?
Wewe
haijalishi katika mwili umezaliwa wapi, kuzaliwa Tanzania ni kusudi la Mungu.
Mungu anakufanya wewe kuwa Taifa lake.
Unapotaka
kwenda kwenye taifa Fulani (mfano marekani), hauwezi kujiamulia tu kwenda bila
kufuata taratibu za kuingia katika taifa hilo. Hii ni kwasababu nchi ya
Marekani inayo mipaka yake na sheria zake na utaratibu wa namna ya kupokea
wageni.
Hivyo
basi unapotaka kwenda marekani lazima uwe na kusudio linalofahamika na
kukubalika na taifa la marekani ili uruhusiwe kuingia katika nchi yao.
Kuwa
taifa la Mungu ni zaidi ya kuwa mtumishi wa Mungu. Kuwa taifa maana yake
unakuwa na watu wako, unakuwa na mipaka yako, unakuwa na utaratibu na kanuni na
sheria za kufuata. Na kwasababu hiyo huwezi kuruhusu kila mtu kuingia katika
taifa lako bila ya kufuata taratibu na sheria za taifa lako.
Unapokuwa
taifa la Mungu unakuwa umekubali kufuata sheria na taratibu za taifa la Mungu
kama ilivyoandikwa kuwa umemkubali BWANA na sheria zake nayeye amekukubali ili
uzifuate hizo sheria/maagizo yake:
Kumbukumbu
la torati 26:17-18 “17 Umemwungama [UMEMKUBALI]
Bwana leo, kuwa ndiye Mungu wako, na kuwa yakupasa kutembea katika njia zake,
na kushika amri zake na maagizo yake, na hukumu zake, na kusikiza sauti yake;
18 naye Bwana amekuungama [AMEKUKUBALI ]hivi leo kuwa taifa iliyotengwa iwe
yake yeye, kama alivyokuahidi, na kuwa yakupasa kushika maagizo yake yote;”
Na
kwasababu hiyo; kwakuwa umekubali kufuata sheria na taratibu za Taifa la Mungu
naye Mungu amekukubali wewe, basi umekuwa Taifa la Mungu na unaishi kwa kufuata
sheria za Taifa la Mungu.
Kumbukumbu
la torati 7:6 “Kwa maana wewe u taifa
takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake
hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.”
Ukiwa
taifa mbele za BWANA wewe ni mmoja katika ya wengi “Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa Bwana” na wengi katika mmoja “amekuchagua kuwa watu wake hasa”
TANGU
UMERUHUSU WATU KUINGIA KATIKA MIPAKA YAKO UMEKWAMA
Basi
sasa kwakuwa umefahamu kuwa wewe ni Taifa kwa Mungu, huwezi kuruhu kila mtu
akaingia katika mipaka yako.
Tangu
umekaribisha watu fulani katika maisha yako mambo yako yamekwama, tangu
umeruhusu watu Fulani washauri kwenye ndoa yako ndoa imekwama, tangu uwaruhusu
watu fulani kwenye biashara, kazi, masomo, huduma vyote vimekwama.
Wewe
haukujua kwamba ni Taifa, na haupaswi kumruhusu mtu yoyote kuingia kwenye taifa
lako bila kufuata sheria ya ufalme wa Mungu hata kama mtu huyo ameokoka. Pale
ulipowaruhusu watu waingie wameingia na miungu yao na umepata matatizo katika
Taifa lako.
Kuna
watu umewakaribisha katika huduma yako kwasababu wameokoka kumbe wao sio wa
Taifa lako.
Kuna
watu umewashirikisha kwenye biashara, kazi, masomo, uchumi na mambo mengi ya
maisha yako kumbe sio wa Taifa lako na mambo yako yameharibika, wewe ulidhani
ni ndugu zako au watu wa karibu yako lakini wamekusababishia matatizo makubwa (Mathayo 10:36 “na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.”)
Fahamu
yakuwa watu wote wanaoingia ndani ya mipaka yako wanayo nafasi kubwa ya
kuathiri maamuzi yako.
Ukishakuwa
Taifa la Mungu mbingu ndio zinatawala, serikali ya Mungu ndio inatawala ndani
ya utaifa wa ki-Mungu
Hao
watu walioingia ndani ya mipaka usigomabne nao wewe kwakuwa kuna mkono wa BWANA
utawachomoa na kuwatoa nje ya mipaka yako kwa jina la YESU, mkono wa BWANA
unawatoa sasa nje ya ndoa yako, nje ya kazi yako, nje ya huduma yako, nje ya
ukoo na familia yako, nje ya miradi yako, nje ya kila mpaka waliongia
wanatolewa sasa kwa mkono wa BWANA kwa jina la YESU.
KWA MASOMO MENGINE
BOFYA HAPA: www.uzimawamileleministries.blogspot.com
No comments:
Post a Comment