Bwana Yesu Kristo apewe sifa!!!
Nimefunuliwa juu ya somo hili ili kukusaidia
mtu wa Mungu kwamba unapokuwa na hofu ya shetani ni kumdharau Mungu. Fahamu
kwamba kuna tofauti ya kubwa hofu ya Mungu nahofu ya shetani.
Hofu ya Mungu au kumcha Mungu (fear of the
Lord) ni hali ya kumheshimu na kumuogopa Mungu kwakuwa Mungu ni Mkuu mno kuliko
mwanadamu (Ayubu 33:12b“Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.”)
na ndiye aliyetuumba sisi na ndiye anayetupa uhai na riziki za kila siku. Hofu
ya shetani ni kumuogopa shetani kuliko Mungu na kumheshimu shetani kuliko Mungu
na jambo hili ni machukizo mbele za Mungu.
CHANZO CHA
HOFU NI KUKOSA IMANI
Hofu ya shetani (wasiwasi/woga) hutokana na
kushindwa kumuamini Mungu na kuona kuwa shetani anazo nguvu za kumshinda Mungu.
Yaani unaposhindwa kuona kuwa Mungu ni Mkuu na anweza kukuvusha na ukaanza
kumuona shetani ana nguvu na atakushinda basi hapo ufahamu kuwa umemuamini
shetani kuliko Mungu. . Yaani unaposhindwa kuona kuwa Mungu ni Mkuu na anweza
kukuvusha na ukaanza kumuona shetani ana nguvu na atakushinda basi hapo ufahamu
kuwa umemuamini shetani kuliko Mungu. Wakati wanafunzi wa Yesu wanataka kuzama
baharini wakamuita Yesu awasaidie, Yesu aliwaambia kuwa ni waoga (yaani wana
hofu) na chanzi cha hofu yao ni ukosefu wa imani kama tunavyosoma katika
maandiko matakatifu (Mark 4:40“Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna
imani bado?”Math 8:26“Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa
imani haba?Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.”)
HOFU NI ROHO
Hofu ni roho kamili (pepo) na inaweza kukuvaa
wakati wowote kama vile mtu anavyoweza kuvamiwa na pepo wa udhaifu,
uasherati/uzinzi, wizi, uongo, umasikini; roho hii ya hofu inatoka kwa shetani
na sio kwa Mungu sawasawa na Neno la Mungu kutoka 2Tim 1:7“Maana Mungu hakutupa
roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.” Kumbe Neno
la Mungu linasema kuwa roho ya woga (hofu) haitoki kwa Mungu bali kwa shetani.
Mtu wa Mungu fahamu jambo hili kwani ni
ufunuo; kabla hofu haijaingia ndani yako lazima litangulie tukio la kipepo (la
kichawi) litakalo kufanya uipokee roho ya hofu ndani yako
Sasa tutazame mifano kadha wa kadha kwenye
Biblia inayotuonesha namna roho ya hofu inavyofanya kazi.
Habari ya
Petro kuzama majini
Tunasoma habari za Petro kwamba aliweza
kutembea juu ya maji kwa kumuamini Yesu baada ya Yesu kumita petro, lakini ni
nini kilitokea hadi Petro akaanza kuzama katika yale maji?
Mathayo
14:28-30“28 Petro
akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. 29
Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili
kumwendea Yesu. 30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga
yowe, akisema, Bwana, niokoe.”
Biblia inasema kuwa “Lakini alipouona upepo, akaogopa”, kumbe upepo ndio tukio
lililotengenezwa kwaajili ya Petro ili kumtia hofu, na baada ya hofu ya ule
upepo (yaani pepo wa hofu) kumuingia Petro tunaona Petro anaanza kuzama majini
“akaanza kuzama, akapiga yowe,”. Tunaonakuwa
kilichomfanya Petro azame sio upepo bali ni ile hofu iliyoingizwa ndani yake na
ule upepo aliyouona.
Mtu wa Mungu kata kila hali inayopelekea
kuingiwa na hofu ndani yako kwani kinachokushinda wewe sio shetani bali ni ile
hofu yako kwa shetani ndio adui yako mkuu.
Habari za
Ayubu kupatwa na madhara ya hofu
Ukishaingiwa na hofu kama ni nilivyosema hapo
awali, hiyo hofu ndio adui wako mkubwa na ndio itakayokutesa kwani hofu ni roho
kutoka kuzimu. Ayubu aliikubali hofu nayo roho ikamvaa na kama vile alivyohofu
ndivyo ilivyo tokea Ayubu3:25“Maana jambo hilo nichalo hunipata, Nalo
linitialo hofu hunijilia.”
Nataka kukuambia kuwa hofu hutokea kuwa kitu
dhahiri kwakuwa vitu vyote huanzia rohoni na baadae kudhihirika katika mwili.
Kuna watu wanaugua magonjwa mbalimbali ya mwili lakini kumbe ni hofu ndio
chanzo cha matatizo yao, Ayubu alipata ugonjwa wa mifupa kwaajili ya roho ya
hofu iliyomuingia Ayubu 4:14“Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha
mifupa yangu yote.”
Kuna watu wameiruhusu roho ya hofu kuwatawala
katika eneo la biashara na biashara zikaanguka, wengine wameruhusu kwenye afya
na wameugua magonjwa ya ajabu na wamekosa tiba, wengine wameikubali hofu ya
kifo na mauti imewapata katika maeneo mbalimbali ya maisha yao.
HOFU/WOGA NI
DHAMBI
Kama ulishawahi kufahamu kuwa kuna dhambi
ambazo mtu akitenda hawezi kuurithi Ufalme wa Mungu, basi moja ya hizo dhambi
ni hofu au woga. Biblia imeweka bayana kuwa waoga (wenye hofu) wote
hawataurithi uzima wa milele Ufunuo 21:8“Bali waoga,
na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao
waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto
na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”
Unaweza kujiuliza kuwa inawezekanaje
woga/hofu ikakupeleka kuzimu? Jibu ni rahisi sana, ni kwasababu hofu ni roho
kutoka kwa shetani na ujasiri/nguvu ni Roho kutoka kwa Mungu, hivyo mwenye hofu
ameingiwa na roho kutoka kwa ibilisi kama yanenavyo maandiko 2Tim 1:7“Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya
moyo wa kiasi.”
MUNGU
ANACHUKIA HOFU KWAKUWA NI KUMDHARAU YEYE
Kwa wale wasomaji wa Biblia mtafahamu kuwa
katika agano la kale vitabu vitano vya Musa sehemu kubwa inazungumzia matendo
makuu ya Mungu aliyowatendea wana wa Israeli kwa kuwatoa katika utumwa waliokaa
kwa zaidi ya miaka mia nne, vilevile BWANA
aliwashindia dhidi ya adui waliokutana nao katika safari yao. Kwa ujumla
ni kwamba wana wa Israeli walitembea kwa ushindi mkuu katika safari yao.
Lakini walipoikaribia ile nchi ya ahadi,
wakawatuma wapelelezi na baadhi ya wale wapelelezi wakaleta habari mbaya ya ile
nchi ni ya majtu na kwamba hawawezi kuingia katika nchi ile kwani wale watu wa
nchi ile wana nguvu zaidi yao. Kama tunavyosoma katika kitabu cha Hesabu 13:31-33“31 Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda
tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. 32 Wakawaletea wana wa
Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita
kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote
tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. 33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili,
wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama
mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.”
Joshua na Kalebu wakakanusha habari zile
mbaya kwa imani na kusema kuwa wataingia katika nchi ya Kaanani kwa nguvu za
Mungu na watawashinda adui zao kwani BWANA yupo upande wao; Hata hivyo wana wa
Israeli wakachagua habari zenye hofu na kuacha habari za imani ya kushinda kama
walivyosema Joshua na Kalebu kiasi cha kutaka kuwaua Joshua na Kalebu kama
tunavyosoma katika Hesabu 14:6-10“6 Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana
wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; 7
wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati
yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. 8 Ikiwa Bwana anatufurahia,
atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa
na asali. 9 Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana
wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja
nasi; msiwaogope. 10 Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo
utukufu wa Bwana ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli
wote.”
Kwasababu
yawana wa Isareli kushindwa kumwamini Mungu hasira ya Mungu ikawaka juu
yao na wakapewa adhabu kubwa ya kutoingia katika nchi ya ahadi kama
ilivyoandikwa katika Hesabu 14:11, 22-24“11 Bwana akamwuliza Musa, Je! Watu hawa
watanidharau hata lini?Wasiniamini hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo
zote kati yao….. 22 kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na
ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu
mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu; 23 hakika yangu hawataiona hiyo
nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana
atakayeiona; 24 lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine
ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo
aliyoingia; na uzao wake wataimiliki.”
Mungu anasema “…..Je!Watu hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini hata lini?.....”
kumbe kudharau kunatokana na kushindwa kuamini, kwahiyo unaposhindwa kumuamini
Mungu tayari unakuwa umemdharau na hasira ya Mungu inawaka juu yako.
Lakini tuanaona Mungu anasema kuwa mtumishi wake Kalebu amekuwa na roho nyingine
ndani yake, maana yake ile roho ya hofu na woga iliwavaa Israeli haikumvaa
Kalebu na Yoshua
Samson Mollel 0767 664 338
No comments:
Post a Comment