Friday, April 17, 2020

MAOMBI NA DUA KWAAJILI YA NCHI YA TANZANIA (TOBA KWAAJILI YA UGONJWA WA KORONA – COVID-19) - Samson Mollel 0767/0713 - 664338






_Maombi haya yanatoka (Isaya 1:18, Zaburi 103:12, Isaya 43:25, 41:21, 43:26  na Daniel 9:4-19, Isaya 53:5)_

Baba katika jina la Yesu umesema katika Neno lako kwamba; Haya, njoni, tusemezane, dhambi zetu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Umesema pia BABA yangu kwamba; Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo ulivyoweka dhambi zetu mbali nasi. BABA umesema wewe, naam, wewe, ndiwe uyafutaye makosa yangu kwa ajili yako mwenyewe, wala hutazikumbuka dhambi zangu. Na BWANA umeniagiza kuwa nilete maneno yangu, nitoe hoja zangu zenye nguvu, umesema mfalme wa Yakobo kwamba nikukumbushe, na tuhojiane; nieleze mambo yangu, nipate kupewa haki yangu kutoka kwako.

Ninaungama kwako, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ushikaye maagano na rehema kwao wakupendao, na kuzishika amri zako; mimi na familia yangu na ukoo wangu na jamaa zangu na taifa langu tumefanya dhambi sana, tumefanya ukaidi mwingi, tumetenda maovu mno, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii/wachungaji/wainjlisti/mitume/walimu, ambao kwa jina lako walisema na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi. Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa familia yangu, na kwa ukoo wangu, nan chi yangu Tanzania tulio katika hofu kuu ya ugonjwa wa korona, kwa sababu ya makosa yetu tulikukosea na maovu ya baba zetu. Ee Bwana, kwetu sisi kuna haya ya uso, viongozi wa familia zetu, na viongozi wa jamii zetu na viongozi wa nchi yetu Tanzania, kwa sababu tumekutenda dhambi. Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii/wachungaji/wainjlisti/mitume/walimu. Naam, familia na ukoo wote wameihalifu sheria yako, kwa kugeuka upande, tusiisikilize sauti yako; basi kwa hiyo laana ya ugonjwa huu wa korona imemwagwa juu yetu, kwa sababu tumemtenda dhambi. Basi Bwana umeyaweka mabaya hayo, ukatuletea; maana Wewe Bwana, Mungu wetu ni mwenye haki katika kazi zako zote uzitendazo; na sisi hatukuitii sauti yako.

Na sasa, Ee Bwana Mungu wetu, uliyewatoa watu wako hawa katika nchi ya Misri kwa mkono hodari, ukajipatia sifa, kama ilivyo leo; tumefanya dhambi, tumetenda maovu. Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuisamehe nchi yangu Tanzania; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu na viongozi waliotutangulia, adhabu hii kali imeachiliwa juu yetu. Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi yangu mimi mtumishi wako, na dua zangu, ukaangazishe uso wako juu ya nchi yangu Tanzania ambayo tumekaa katika hali ya ukiwa ukiwa, kwa ajili ya adhabu yako Bwana. Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mimi mtoto wako ninayeitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi. Ee Bwana, usikie; Ee Bwana, usamehe; Ee Bwana, usikilize, ukatende, usikawie; kwa ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu mimi na familia yangu tunaitwa kwa jina lako kwakuwa tumempokea mwana wako Yesu Kristo na tumeoshwa kwa damu ya Yesu, Bwana kumbuka rehema.

Asante BABA kwani umemtuma Kristo Yesu ambaye alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona, tumepona ugonjwa huu wa kutisha katika jina la Yesu Kristo, AMEN!

*Samson Mollel 0767/0713-664 338*
*_Huduma ya Uzima wa Milele (Yohana 17:3)_*
*www.uzimawamileleministries.blogspot.com*
```© April 17, 2020```

Thursday, March 12, 2020

MAMBO AMBAYO UKIYAFANYA UNAUNGANISHWA NA MADHABAHU ZA MASHETANI (Samson Mollel 0767/0713 – 664 338)



Bwana Yesu apewe sifa kanisa la Yesu!

Napenda ufahamu kwamba yapo mambo mengi sana ambayo ukiyafanya (kwa kujua au kutojua) unaunganishwa na madhabahu za mashetani; inawezekana kwamba matatizo ya maisha yako huenda yameanza kutokana na kufanya au kufanyiwa moja ya mambo hayo katika maisha yako.

Mimi binafsi kutokana na huduma nilizozifanya na kwa kujifunza kutoka kwa watumishi wengine nimepata ufahamu wa mambo kadha wa kadha na baadhi ya hayo nimeyaandika katika somo hili. Nakusihi mtu wa Mungu kwamba pamoja na haya niliyoandika bado jambo muhimu na kubwa la kujiweka salama ni kumtegemea Yesu kwa uaminifu na kuishi maisha matakatifu yanayompendeza Mungu (Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;)

Nimeanza kwa kusisitiza habari ya utakatifu kwani kuna watu wanataka kumuona mungu na kuzipata Baraka zake lakini hawamtaki Mungu wala hawataki kuishi kwa kufuata sheria za Mungu na kuzishika amri zake; yaani watu hawa wanaishi maisha ya kidunia/kimwili halafu wanataka kuvuna Baraka za Mungu na kufunguliwa kutoka katika vifungo (Efeso 5:19-21)

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo ukiyafanya unaunganishwa na madhabahu za uharibifu/za mashetani na madhara yatatokea mahali Fulani katika maisha yako.


  •  Kutoa sadaka na matambiko
Kutoa sadaka na kufanya matambiko kwa miungu (mizimu) ni moja ya njia ambayo humuunganisha mtu na madhabahu za uharibifu kwa kujua au bila kujua. Kuna watu ambao huenda kwenye koo au familia zao na kuchinja wanyama mbalimbali ili kutoa damu ya wanyama hao kwa mababu na baada ya hapo mnyama aliyechinjwa huliwa kwa utaratibu maalum; kwa mfano nyama ya kidari atakula baba mkubwa, nyamba ya paja atakula mtoto wa kwanza wa kiume na nyama ya kichwa atakula mtoto wa kwanza wa kike. Unapokuwa umeshiriki kwa kujua au bila kujua katika matambiko kama hayo unaunganishwa na ile madhabahu ambayo sadaka ya matambiko imetolewa. Kwa jinsi hii watu wengi sana walioshiriki katika matambiko wana mahusuiano na zile madhabahu zilizotolewa matambiko.

1Wafalme 11:1-8 “1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. 3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. 4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. 5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. 6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. 7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. 8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.”

1Falme 21:25-26 “25 (Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa Bwana ambaye Yezebeli mkewe alimchochea. 26 Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.)”

1Falme 16:31-33 “31 Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia. 32 Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria. 33 Ahabu akaifanya Ashera; Ahabu akazidi kumghadhibisha Bwana, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.”

Mfalme Sulemani na mfalme Ahabu wote walio wanawake kutoka kwenye familia za waabudu miungu, na kama unavyofahamu kwamba hawakuiacha miungu yao bali walikuja nayo kwa Ahabu na kwa Sulemani na hivyo walifanya matambiko (ibada za miungu) ndani ya nyumba za waume zao (Ahabu na Sulemani)  na waume zao walishiriki (kwa kujua au bila kujua) na kilichofuata ni wafalme hawa (Ahabu na Sulemani) kuunganishwa na miungu na madhabahu za mashetani na wao kumuacha Jehova na hasira za Jehova zikawaka juu yao na familia zao.
Inawezekana hata wewe nyumbani kwako kuna matatizo ya kiroho na haujui ni kwanini unapatwa na matatizo hayo, kumbe ni mume/mke wako au mtumishi wako (House girl/House boy) amekuja na miungu ya kwako nyumbani kwako na umeunganishwa na madhabahu za mashetani.


MAOMBI:
Baba katika jina la Yesu Kristo, naomba toba kwa kuwa nimeshiriki kwa kujua na bila kujua na nikatoa sadaka na matambiko kwenye madhanahu za mashetani, ninaomba rehema Baba Yangu kwa jina la Yesu kwakuwa wakati mwingine nilitoa mali yangu nikijua masaidia watu kumbe walinuia mabaya ili wanitenganishe na wewe wakaenda kutoa mali na fedha zangu kwa mashetani, nirehemu Baba kwaajili yake Yesu Kristo. Katika jina la Yesu naamuru mahali popote sadaka yangu ilipo kwenye madhabahu za mashetani ibadilike kuwa moto wa Roho Mtakatifu na kuwateketeza makuhani wote wa kichawi kwa jina la Yesu Kristo, naiondoa sadaka yangu niliyoitoa kwa miungu kwa kujua au bila kujua kwa jina la Yesu! Amen!

  •  Kushiriki au kushirikishwa katika mambo ya kiganga
Unaposhiriki au unaposhirikishwa kwenye mambo ya kiganga kwa kujua au bila kujua unaunganishwa na madhabahu za mashetani na hasira ya Mungu inakuwa juu yako hata kama haukufanya kwa ufahamu wako. Inawezekana huo uganga ameshiriki baba/babu/dada/kaka yako na wewe bila kujua amekutaja kwenye hiyo madhabahu, basi unakuwa mshirika na mateso yanayoletwa na hiyo madhabahu yanakuwa juu yako pia.

Hali kama hii iliwahi kumtokea Gideoni pale ambapo baba yake mzazi (mzee Yoashi) alipokuwa kuhani wa madhabahu ya baali; Gideoni hakuwa akishiriki katika ile madhabahu lakini kwakuwa baba yake alishiriki basi na yeye Gideoni akabeba adhabu ya kuwa mshiriki

Waamuzi 6:11-15, 25-26 “11 Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani. 12 Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa. 13 Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye Bwana, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani. 14 Bwana akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma? 15 Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu……….. 25 Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo; 26 ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.”

Kwahiyo tunajifunza kwamba hali ile ya uduni wa Gideoni na umasikini wake na kabila lake ulitokana na madhabahu ya baali ambayo BWANA alimuamuru kuivunja na kujenga madhabahu ya BWANA. Inawezekana hata wewe umeunganishwa na madhabhu za mashetani lakini pasipo kufahamu.

Vilevile tunasoma habari ya mfalme wa Babeli aliwaunganisha wananchi wa nchi yake na madhabahu za mashetani kwa kufanya uganga na matambiko kama ilivyoandikwa katika Neno la Mungu.

Ezekieli 21:21-23 “21 Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huko na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini. 22 Katika mkono wake wa kuume alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome. 23 Jambo hili litakuwa kwao kama uganga wa ubatili, mbele ya macho yao waliowaapia viapo lakini ataufanya uovu ukumbukwe, ili kwamba wakamatwe.”

Tunaona hasira ya Mungu inaachiliwa juu ya wote ambao mfalme amewaapia viapo hata kama hawakushiriki hicho kiapo kwa uhiari/ufahamu wao. Hebu tafakari mtu wa Mungu; ikiwa kiongozi Fulani katika nchi ya Tanzania alifanya uganga na kututaja wa Tanzania, hivi tuko salama? Ikiwa mkuu wa ukoo au familia yenu alikutaja kwenye uganga, kweli uko salama. Inawezekana hata sasa umeunganishwa na madhabahu za mashetani kwa njia hiyo; omba maombi haya ujinasue:


MAOMBI:
Baba yangu katika jina la Yesu Kristo, ninaomba toba kwakuwa nimeshiriki katika ibada za kiganga kwa kujua au bila kujua, wakati mwingine ndugu na jamaa wametaja jina langu kwenye madhabahu za mashetani na mimi nikaunganishwa na roho za mashetani, ninaomba toba Kwa Damu ya Yesu na kwa Jina la Yesu Kristo. Ninajitoa sasa kwenye madhabahu za waganga zilizopo makaburini, baharini, misituni, njia panda, angani na kwenye nyumba za wachawi. Natoka kwenye hizo madhabahu kwa jina la Yesu Kristo. Nauwasha moto wa Roho Mtakatifu nawateketeza mashetani yote walionishikilia kwenye madhabahu kwa jina la Yesu! Naitoa nchi yangu Tanzania kwenye madhabahu za mashetani kwa damu ya Yesu! na kwa jina la Yesu! Amen!


  • Majina yenye uhusiano na madhabahu yanaweza kukuunganisha na madhabahu
Ili Yusufu aweze kuwa mtawala wa misri alipewa jina la kimisri ili apokelewe na miungu ya Misri, yaani jina lina nguvu ya kumuunganisha mtu na madhabhu na kumpa nguvu ya ile madhabahu.Yusufu asingetawala Misri pasipo kupatanishwa na madhabahu za wa-Misri na hilo lilifanyika kwa njia ya kupewa jina lenye nguvu ya madhabahu za miungu ya Misri (Kumbuka wa-Misri ni waabudu miungu na hawakumjua Mungu wa kweli)

Mwanzo 41:42-45 “42 Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake. 43 Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri. 44 Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri. 45 Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe Yusufu akaenda huko na huko katika nchi yote ya Misri.”

Wote waliomkubali Yesu na kulibeba jina la Yesu kwa imani ndani ya mioyo yao, wamepokea nafasi katika ulimwengu wa roho na kuunganishwa na madhabu ya Mungu Jehova

Yohana 1:12Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

Warumi 8:16-17 “16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.”

Wafilipi 2:8-10 “8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. 9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;”

Jina la Yesu ni jina la urithi ambalo amepewa na Baba yake (Mungu Baba), lakini alipolipokea hilo jina tu akapewa kiti cha enzi cha Mungu na mamlaka kubwa kuanzia mbinguni mpaka duniani na kwa jina hilo viumbe vyote vinaanguka na kusujudu.
Jina linaweza kukunganisha na madhabahu na ukapokea nguvu ya hiyo madhabahu, inategemea umeunganishwa na madhabahu gani.


MAOMBI:
Bwana Yesu ninaomba toba kwaajili ya majina niliyopewa yenye mahusiano na madhabahu za mashetani, naomba toba kwaajili yangu na watoto wangu, wazazi wangu, mabibi na mababu…… turehemu Bwana kwa jina la Yesu. Ninalidumbukiza na kulizamisha jina langu kwenye kisima cha damu ya Yesu kwa jina la yesu Kristo. Ninaamuru mapepo yaliyokamata jina langu na kulivuta kwenye uharibifu Achiaaaa kwa jina la Yesu Kristo!!! Achiaaaa jina langu kwa jina la Yesu Kristo!!! Achiaaaa kwa jina la Yesu Kristo!!! Amen!


  • Mavazi yenye mfumo wa madhabahu au nembo za madhabahu yanaweza kukuunganisha na madhabahu
Yapo mavazi yenye mfumo wa kimadhabahu na hata yametambulika katika jamii kama mavazi kwaajili ya watu fulani au kabila fulani au dini fulani. Kuna mavazi ukiyaona tu unaanza kuhisi kwamba huyu aliyevaa anaweza kuwa mganga wa kienyeji au mchawi. Mavazi ya namna hii yana nguvu za madhabahu na yanaweza kukuunganisha na madhabhu za giza.

Katika Biblia tunajifunza habari za nabii Eliya kwamba alikuwa na mavazi ambayo hayakufanana na watu wengine (2Falme 1:7-8 “7 Akawaambia, Je! Mtu yule aliyetokea, akaonana nanyi, akawaambia maneno hayo, alikuwa mtu wa namna gani? 8 Wakamwambia, Alikuwa amevaa vazi la manyoya, tena amejifunga shuka ya ngozi kiunoni mwake. Naye akasema, Ndiye yule Eliya Mtishbi.”)

Ulipofika wakati wa kunyakuliwa kwa Eliya tunaona Elisha anabaki na vazi la Eliya na ule upako uliokuwa kwa Eliya unakuja kwa Elisha mara dufu.

2Falme 2:11-15 “11 Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli. 12 Naye Elisha akaona, akalia, Baba yangu, baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake! Asimwone tena kabisa; akashika mavazi yake mwenyewe, akayararua vipande viwili. 13 Kisha akaliokota lile vazi la Eliya lililomwangukia, akarudi, akasimama katika ukingo wa Yordani. 14 Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi Bwana, Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka. 15 Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake.

Katika Biblia tunajifunza pia kwa habari ya mavazi tangu enzi za Musa na Haruni ambapo yalitengenezwa mavazi ambayo walipovaa Haruni na watoto wake walitakasika na kuweza kusogea mbele za Mungu kwaajili ya wana wa Israeli.

Kutoka 28:2,41 “2 Nawe utamfanyia Haruni ndugu yako mavazi matakatifu, kwa utukufu na kwa uzuri., 41 Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.”

Unachotakiwa hapa ni kuwa makini na mavazi unayovaa, sio ukiletewa nguo yoyote wewe unaivaa tuu, unaweza kuvaa nguo zilizotoka kwa mashetani ukaingizwa katika uharibifu wa madhabahu za mashetani.


MAOMBI:
Baba katika jina la Yesu Kristo, ninaomba toba na msamaha mahali popote nilipojiunganisha na mashetani kwa njia ya mavazi iwe ni rohoni au mwili, nirehemu baba yangu kwaajili ya mwana wako mpendwa Yesu Kristo. Kwa moto wa Roho Mtakatifu ninayateketeza mavazi yote ya kimadhabahu niliyovishwa nikiwa rohoni au mwilini, enyi mapepo mliokuja na mavazi hayo ninawateketeza kwa moto wa Roho Mtakatifu kwa jina la Yesu!!! Amen!


  • Kutumia ishara na alama za madhabahu za giza (Chale, Hirizi, alama na ishara zinaweza kuita roho za giza)
Kuna ishara ambazo zinazoonekana kwa jinsi ya mwilini lakini zina maana kubwa sana katika ulimwengu wa roho, ishara hizo zinapofanyika zinakuunganisha na madhabahu inayohusiana na ishara hiyo. Katika agano la kale kuna ishara kadhaa zilifanyika na zilikuwa na maana  kubwa katika ulimwengu wa roho.

Kutahiriwa katika agano la kale ilikuwa ni ishara ya agano la Mungu na wana wa Israeli, ilionekana kama tendo la kibindamu lakini ilikuwa ni ibada ya utakaso na mtu ambaye hakutahiriwa alitengwa na kuonekana kama mtu najisi (mchafu). Katika agano jipya tohara ni kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, kama haujampokea Yesu ni sawa na mtu asiyetahiriwa yaani upo nje ya agano (ni najisi/mchafu).

Mwanzo 17:10-11, 14 “10 Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. 11 Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi…..14 Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.”

Vilevile tunaona ishara ya damu ambayo kila aliyepaka damu kwenye miimo ya mlango wake yule muharibu hakuweza kuingia katika nyumba yake.

Kutoka 12:12-13 “12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. 13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.”

Ubatizo nalo ni tendo la ishara ambalo hufanyika kwa jinsi ya mwili lakini matokeo yake yapo rohoni na kuleta mabadiliko ya rohoni

Marko1:4 “Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.”

Zipo ishara nyingi ambazo zimewaunganisha wakristo na madhabhu za giza pasipo wao kujua na madhara yameanza kutokea katika maisha yao lakini hawajui chanzo. Kumbe chanzo ni yale mafuta/maji/chimvi uliyopaka kwa nabii wa uongo (vipo vitu kama hivyo  vyenye nguvu za Mungu). Wapo watu wamevaa nguo zenye ishara mbalimbali za mashetani na wanashambuliwa na nguvu za giza lakini hawakijui chanzo cha matatizo yao.


MAOMBI:
Katika Jina la Yesu Kristo, kila mahali penye ishara ya kishetani katika mwili wangu, nina mimina damu ya Yesu Kristo naondoa uhalali wa ishara na alama hiyo katika maisha yangu. Mahali ilipowekwa hilo alama na ishara napitisha Damu ya Yesu na Moto wa Roho Mtakatifu naziteketeza kabisa hizo alama na ishara kwa jina la Yesu. Naamuru mapepo yanayolinda hizo ishara za kishetani Toooka!!! Kwa Jina la Yesu Kristo!!!! Toooka!!! Kwa Jina la Yesu Kristo!!!! Toooka!!! Kwa Jina la Yesu Kristo!!!!


  • Vitu vilivyo vuviwa kwa makusudi ya madhabahu za giza na vifaa vilivyowahi kutumika kwenye madhabahu za giza (Pete, Shanga, Hereni, michezo ya kipepo)
Katika ulimwengu wa roho sahau sayansi ya viumbe hai na visivyo hai kwani rohoni vitu vyote vinatumika (watumishi) ama na Mungu Jehova au na shetani ambaye naye ni mungu wa dunia hii.

Zaburi 119:91 “Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo, Maana vitu vyote ni watumishi wako.”

Lakini pamoja na ukweli kwamba vitu vyote ni watumishi wa Mungu, Neno la Mungu linatupeleka mbali zaidi kwamba vitu hivyo vimetiishwa katika ubatili, yaani vinatumika nje ya mpango wa Mungu

Rumi 8:19-22 “19 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. 20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini; 21 kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. 22 Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa.”


MAOMBI:
Katika jina la Yesu naachilia damu ya Yesu kwenye kitu chochote nilichovaa au kuvalishwa na mashetani kupitia waganga au ndugu wa karibu, namimina damu ya Yesu naharibu nguvu ya giza kwa jina la Yesu. Naachilia moto wa Roho Mtakatifu uteketeze kila nguvu ya giza iliyopo kweye pete za kishetani, shanga, bangili, mikufu, manukato, viatu, nguo za ndani n.k. naachilia Motooo!!! kwa Jina la Yesu Kristo!!! Motooo!!! kwa Jina la Yesu Kristo!!! Motooo!!! kwa Jina la Yesu Kristo!!!


  • Kutumia vyakula/vinywaji vilivyonuiziwa kwa matumizi ya kimadhabahu na kufanyiwa ibada za tambiko linalikuunganisha na madhabahu.
Mtu wa Mungu sio kila unachokiona kinafanana na chakula basi unakula tu, vipo vya kula vya kiibada ambavyo ndani yake vimebeba roho za uharibifu kutoka kwa mashetani. Wana wa Israeli waliwahi kula chakula kilichonuiziwa na kufanyiwa ibada za miungu na wao wakaanza kuiabudu ile miungu kwakuwa kile chakula kilibeba nguvu ya uharibifu

Hesabu 25:1-3 “1 Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli.”

Ufunuo 2:14 “Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.”

Vilevile vipo vyakula kutoka kwenye madhabahu ya Jehova ambavyo ni vitakatifu na vimebeba nguvu ya Mungu wa kweli kama tunavyosoma katika

Kutoka 29:31-34 “31 Nawe twaa huyo kondoo mume aliyekuwa wa kuwekwa kwa kazi takatifu, na kuitokosa nyama yake katika mahali patakatifu. 32 Na Haruni na wanawe wataila ile nyama ya kondoo, na mikate iliyo katika kile kikapu, hapo mbele ya mlango wa hema ya kukutania. 33 Nao watakula vile vitu ambavyo upatanisho ulifanywa kwa hivyo, ili kuwaweka kwa kazi takatifu na kuwatakasa; lakini mgeni asivile, maana, ni vitu vitakatifu. 34 Na kwamba kitu cho chote cha ile nyama, iliyo kwa ajili ya kuweka kwa kazi takatifu, au cho chote cha hiyo mikate, kikisalia hata asubuhi, ndipo utavichoma kwa moto hivyo vilivyosalia; havitaliwa, maana, ni vitu vitakatifu.”

Luka 22:19-20 “19 Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.”

Yesu anatufundisha kwamba unaweza kubadili chakula chako kuwa mwili wake na kinywaji chako kuwa ni damu ya Yesu. Kila unapopewa chakula kumbuka kukitakasa na kukifanya kuwa mwili na damu ya Yesu ili kila unapokula ushikiri mwili na damu ya Yesu na uliimarishe agano la Jehova na wewe.


MAOMBI:
Bwana Yesu ninaomba toba kwa kushiriki katika chakula cha mashetani kwenye meza ya adui, naita damu ya Yesu Kristo ndani ya tumbo langu na mfumo mzima wa mwili wangu ambao umepokea vyakula ambavyo ni roho kutoka kwa mashetani; ninaamuru sasa kwa jina la Yesu, enyi vyakula mliongia ndani kichawi/kiganga iwe ni kwenye ndoto au kwa jinsi ya mwili, tokaaa!!! Kwa jina la Yesu!!! tokaaa!!! Kwa jina la Yesu!!! tokaaa!!! Kwa jina la Yesu!!!


  • Kuishi au kwenda kwenye maeneo yenye madhabahu za giza bila ya kuwa na kinga ya damu ya Yesu/nguvu za kutosha
Kuna wakati unaweza kuwa upo mahali lakini tayari mahali hapo panamilikiwa na miungu/mashetani, au inawezekana mahali hapo tayari papo chini ya adhabu ya Mungu kutokana na ibada za kishetani zilizofanyika hapo.

Walawi 18:24-25 “24 Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; 25 na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa.”

Ikiwa utaenda maeneo kama haya na wewe kiroho chako upo chini, ndipo pale kila unachokifanya hakiendi, biashara zinakufa, elimu, ndoa, afya vyote vinaharibika. Lakini tatizo ni kwamba umeunganishwa na madhabahu za mashetani bila kufahamu.

Wakati mwingine unaweza kuunganishwa na madhabhu ya Mungu Jehova kwakuwa ardhi uliyoikalia ilifanyiwa ibada za Mungu wa kweli. Yakobo alilala mahali ambapo babu yake Ibrahim alijenga madhabahu ya Jehova na akapaita Betheli.

Mwanzo 28:12-16 “12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. 13 Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. 14 Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. 15 Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia. 16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.”

Jambo la muhimu hapa ni kuanza kutafakari maisha yako ya kiroho, inawezekana mahali ulipokaa umekutana na madhabahu za mashetani na uwezo wako wa kivita ni mdogo ndio maana umekwama hata sasa katika afya, ndoa, elimu, ujenzi, biashara n.k


MAOMBI:
Kwa damu ya Yesu ninaomba toba kwaajili ya ardhi ya mahali ninapoishi/ninapofanyia shughuli zangu, naifuta kwa damu ya Yesu mikataba yote iliyotoa uhalali kwa mashetani kumiliki ardhi hii na kunitesa bila mimi kujua au kwa kujua, ninaikomboa ardhi hii na kuiamuru kuwa upande wangu sasa kwa jina la Yesu. Enyi mashetani mlioshika eneo hili na kulifanya madhabahu yenu, ninawaamuru tokaaaa!!! Kwa jina la Yesu……


  • Kwenda kwenye ngoma au sherehe za manuizio ya nguvu za giza
Zipo sherehe na ngoma ambazo zinaonekana kama za kawaida lakini ndani yake ipo nguvu ya madhabahu za mashetani. Wewe utaona tu kwamba tangu umeenda kwenye ile ngoma mpaka sasa hauwezi kuacha kwenda lakini kuna katabia kamekuingia na hata ukitaka kukiacha hauwezi kukiacha hako katabia. Ukiona hayo fahamu kwamba umeshiriki sherehe na ngoma za mashetani.

Wakati Fulani wana wa Israeli walishiriki kwenye sherehe ya sadaka za miungu ya wamoabu, na mara baada ya hapo wakamkosea Mungu kwakuwa haikuwa sherehe ya kawaida ilikuwa ni ya mashetani.

Hesabu 25:1-3 “1 Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli.”

Danieli 3:7 “Basi wakati huo, watu wa kabila zote walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.”


MAOMBI:
Kwa jina la Yesu Kristo najitoa kwenye sherehe za mashetani ambazo nimeshiriki au kushirikishwa, natoka kwenye hizo ibada za miungu kwa jina la Yesu Kristo! Amen!


  • Kuoa au kuolewa kuna kuunganisha na madhabahu
Inawezekana unadhani kuoa au kuolewa ni kitu cha kawaida kawaida tu. Kuna watu wameo/kuolewa lakini ili wakubaliwe katika familia ya mke/mume imewabidi kuingizwa katika mikataba fulani fulani. Jambo hili halikuanza leo, inawezekana umeshao/kuolewa kabisa na baada ya hapo mume/mke anakuletea utaratibu wa nyumbani kwao (Yaani anakuungamanisha na miungu ya kwako).

1Falme 11:1-9 “1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. 3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. 4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. 5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. …….7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. 8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu. 9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,”

Inawezekana wewe ili uoe/uolewe ulifanyiwa jambo la uharibifu, wengine walinyweshwa maziwa na bibi/babu wa huko ukweni, wengine walinyolewa nywele, wengine waliketishwa kwenye kigoda cha ukoo n.k; lakini sasa kuna uzito mkubwa kwenye maisha yako na unajua kabla ya ndoa haikuwa hivyo.

Biblia inatufundisha habari za Isaka alipomuoa Rebeka, akamchukua mpaka kwenye hema la mama yake (Sara) na baada hayo Rebeka akawa tasa.

Mwanzo 24:67 “Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake.”

Mwanzo 25:21 “Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.”



MAOMBI:
Bwana Yesu inawezekana katika kuoa au kuolewa kwangu nimeingizwa katika madhabahu za mashetani katika familia nyingine kwa kujua au bila kujua, ninaomba toba Bwana Yesu, naomba unirehemu na kuniokoa sasa. Kwa damu yako najitenga na kila madhabahu za mashetani lizoingia au kuingizwa. Naamuru mashetani walionifunga kwa ibada za miungu tokaaaa!!! kwa jina la Yesu!!!


  • Kutenda aina yoyote ya dhambi unaunganishwa na mashetani
Tafsiri rahisi ya dhambi ni uasi/kuhalifu maagizo/sheria za Mungu, unapokuwa nje ya maelekezo ya Mungu wewe unatenda dhambi sawa na neno la Mungu 1Yohana 3:4 “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.”

Kitu kikubwa kabisa na cha kwanza ambacho dhambi hufanya kwenye maisha ya mwanadamu ni kumtenganisha na Mungu na baada ya kumtenganisha na Mungu, shetani anapata nafasi ya kumtesa mwanadamu.

Dhambi inapokutenganisha na Mungu inasababisha hasira ya Mungu kuwaka juu yako na shetani anafurahia kwani ndio mwanya wake wa kuingiza uharibifu wake katika misha yako (Isaya 59:1-2 “1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; 2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”)

Kwakuwa dhambi ni uasi, unapotenda dhambi unakua umeamua kwa hiari yako kufunga mkataba/agano na mashetani kinyume na Mungu na unakuwa umemkubali shetani.

Waefeso 2:1-3 “1 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; 2 ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; 3 ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.”

MAOMBI:
Baba katika jina la Yesu ninaomba toba kwa mambo yote niliyoyatenda kinyume na mapenzi yako na nikaichukua sura ya uasi, ninaomba rehema na toba kwa damu ya Yesu. Katika jina jina la Yesu, enyi mapepo ya uasi ninawaamuru ondokeni katika maisha yangu kwa jina la Yesu



Thursday, February 20, 2020

SOMO: BALAA LA DHAMBI (Samson Mollel 0767/0713 – 664 338)


UTANGULIZI

Tafsiri rahisi ya dhambi ni uasi/kuhalifu maagizo/sheria za Mungu, unapokuwa nje ya maelekezo ya Mungu wewe unatenda dhambi sawa na neno la Mungu 1Yohana 3:4 “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.”
Neno la Mungu linaenda mbele zaidi kwamba kama unajua/unafahamu kutenda mambo mema na ukaacha kuyatenda hayo mema kwako hilo ni dhambi (kumbuka hapa haujakosea kwenye amri za Mungu); Yakobo 4:17 “Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.”

Dhambi ikimpata mtekelezaji wake (mtenda dhambi) basi inazaa mauti. Neno la Mungu linatufundisha kwamba uchungu wa mauti ni dhambi 1Kor 15:56 “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.”, katika tafsiri ya kiingereza “The sting of death is sin” yaani sumu inayoletelezea au inayopelekea mauti ni dhambi, ni sawa na kusema matokeo ya dhambi ni mauti. Mtu wa Mungu hata dhambi irembwe kiasi gani au iwe tamu na nzuri kiasi gani matokeo yake ni mauti kuanzia rohoni hadi mwilini. (Rumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”)

ASILI YA DHAMBI

        i.            Dhambi ni danganyifu
Waebrania 3:13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
Mtu wa Mungu napenda ufahamu kwamba kila dhambi unayoiona lazima ikujie kwa jinsi ya udanganyifu pasipo kuonesha matokea yake halisi au pasipo kujionesha yenyewe. Pale bustani ya Edeni Mwanamke alipotokewa na nyoka na kudanywa na baadae Adamu hawakuwa na taarifa sahihi ya tukio walilokuwa wanalifanya (uasi), shetani alifahamu lakini aliwandanya kwa maneno ya kuwavutia na kuwaonesha kwamba watapanda cheo na kufanana na Mungu kama tunavyosoma katika Mwanzo 3:4-5 “4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” shetani anawaeleza habari za kuwa sawa na Mungu lakini hawaambii kwamba watakufa, na baada ya kula tunda dhambi ikaingia duniani na hatimaye mauti ikatuvaa wakati huo.

     ii.            Dhambi inatoa furaha ya muda tu
Waebrania 11:25 “akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo;”
Jambo lingine la muhimu sana la kufahamu ni kwamba dhambi hutoa furaha au starehe ya muda mfupi na mateso ya milele hufuata baadae. Dhambi inatokana na mambo ya mwili na baada ya mwili kuipoteza roho kwa starehe za muda mfupi roho inapokea adhabu ya milele
Luka 16:19-23 “19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, ……….. 22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. 23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.”
Tajiri alipata raha ya muda mfupi tu akiwa duniani lakini mateso ya milele

   iii.            Dhambi ni uharibifu/inaangamiza
Mithali 11:3 “Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.” Yakobo 1:15 “Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.”
Matokeo ya mwisho ya dhambi ni mauti, pasipo kujali aina ya dhambi na namna ya udanganyifu wake lazima mwisho wa dhambi iwe ni uharibifu na maangamizo yaani mauti.

MAMBO AMBAYO DHAMBI INAWEZA KUYAFANYA

1.     Dhambi inakutenganisha na Mungu
Kitu kikubwa kabisa na cha kwanza ambacho dhambi hufanya kwenye maisha ya mwanadamu ni kumtenganisha na Mungu na baada ya kumtenganisha na Mungu, shetani anapata nafasi ya kumtesa mwanadamu.
Dhambi inapokutenganisha na Mungu inasababisha hasira ya Mungu kuwaka juu yako na shetani anafurahia kwani ndiomwanya wake wa kuingiza uharibifu wake katika misha yako
Isaya 59:1-2 “1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; 2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”

2.     Dhambi inaleta aibu
Mwanzo 3:10 “Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.”
Mithali 28:13 “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”
2Thesalonike 2:7 “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.”

3.     Dhambi huleta uharibifu
Mithali 11:3 “Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.”

4.     Dhambi huleta udhaifu (Magonjwa/kufungwa na ibilisi)
Mithali 14:30 “Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa.”
Yesu alimwambia Yule mgonjwa amesamehewa dhambi na akapona Mathayo 9:2-7 “2 Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. 3 Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. 4 Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu? 5 Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende? 6 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako. 7 Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake.”

Magonjwa mengi (au yote) ni laana
Kumb 28 :15-68 “15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata….. 21 Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki. 22 Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie….. 27 Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa…..35 Bwana atakupiga magoti na miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa……59 ndipo atakapofanya Bwana mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana. 60 Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe. 61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa.”

5.     Dhambi huondoa amani
2Nyakati 15:3-6 “3 Basi tangu siku nyingi Israeli wamekuwa hawana Mungu wa kweli, wala hawana kuhani afundishaye, wala hawana torati; 4 lakini walipomgeukia Bwana, Mungu wa Israeli, katika msiba wao, na kumtafuta, akaonekana kwao. 5 Hata na zamani zile hakukuwa na amani kwake atokaye, wala kwake aingiaye, ila fadhaa kubwa juu yao wote wakaao katika nchi. 6 Wakavunjika-vunjika, taifa juu ya taifa, na mji juu ya mji; kwani Mungu aliwafadhaisha kwa shida zote.”
Unapokosa amani unabaki na bumbuwazi la moyo na ufahamu Kumb 28:28 “Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;”
Amani hupatikana kwa kumlingana Mungu Ayubu 22: 21-23 “21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. 22 Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako. 23 Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa; Ukiuondoa udhalimu mbali na hema yako.”

DHAMBI ZENYE NGUVU ZINAZOANGAMIZA KANISA (WAKRISTO)
1.     ZINAA (UZINZI/UASHERATI)
Hakuna dhambi kwenye biblia iliyoleta maangamizo makuu kama zinaa (uzinzi na uasherati). Katika historia ya wana wa Israeli kama tunavyoisoma katika agano la kale hakuna mahali popote walifanya dhambi na dhambi hiyo ikasababisha mauaji makubwa kama dhambi ya uzinzi na uasherati wa kiroho na kimwili waliofanya wana wa Israeli na kumkasirisha Mungu kama tunavyosoma katika
1Kor 10:8 “Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.”
Hesabu 25:1-8 “1 Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli. 4 Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli. 5 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori. ……….. 9 Nao waliokufa kwa hilo pigo walikuwa watu elfu ishirini na nne hesabu yao.”

a.      Uzinzi/uasherati wa kiroho (ushirikina na uchawi)
Katika ulimwengu wa roho Mungu Jehova ni mume kwa wote wanaomwabudu na sisi tunao mwabudu ni kama wake kwake kama tunavyosoma katika maandiko
Yeremia 31:31-32 “31 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.”

Kwa maana hiyo Yesu ni mume kwa kanisa kama tunavyosma katika Neno la Mungu
Waefeso 5:23 “Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.”
Mathayo 25:1-2 “1 Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.”
Mtu yoyote anayefanya ibada za miungu mingine kama vile matambiko na kuwaendea waganga wa kienyeji na wasoma nyota na watu wa namna hiyo unakuwa umefanya zinaa kwa jinsi ya roho yaani umefanya uzinzi na uasherati na hasira ya Mungu inawaka juu yako kwa wivu mkubwa

b.     Uzinzi/uasherati wa kimwili
Katika amri kumi za Mungu tunaonywa kwamba uzinzi ni dhambi kama tunavyosoma katika kitabu cha Kutoka 20:14 “Usizini.” Vilevile tunasoma katika Waefeso 5:3 “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;”
Mungu anazidi kutuonya kwa habari ya uzinzi na uasherati katika kitabu cha Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,”
Kumbe hapa Mungu anaonya juu ya uzinzi/uasherati wa kimwili au uanaofanyika katika miili hii tuliyonayo ndio maana mtume Paulo anaita kuwa ni matendo ya mwili.
Mtu wa Mungu anataka ujue kuwa mwili wa mtu sio mali ya mtu mwenye huo mwili bali ni mali ya Mungu sawa na Neno la Mungu “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;”. Kuna hatari kubwa katika kutumia mwili uliopewa na Mungu kwaajili ya uzinzi na uasherati kwani jambo hilo linamkasirisha sana Mungu na kuna hatari kubwa mbele yako kwa kufanya uzinzi/uasherati

1Kor 6:16-20 “16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. 18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”
Sasa nataka ufahamu kwamba asili ya dhambi ni uharibifu, mtu yeyote anayefanya uasherati na uzinzi anauharibu mwili wake na Mungu hawezi kukubali ukaliharibu hekalu lake au ukalichafua hekalu lake lazima akuharibu na wewe sawasawa na Neno lake

1Kor 3:17 “16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.”
Mungu anataka alitumie hekalu lake yaani wewe kwaajili ya kuipeleka injili mbele lakini wewe umeenda kuliharibu hekalu lake kwa ulevi, uzinzi na uasherati, uwe na uhakika kwamba Mungu atakuharibu kwani Neno la Mungu ni kweli na hakika

2.     KUTOKUMUAMINI MUNGU (HOFU/WOGA)

Yohana 16:7-9“7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. 8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. 9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;”

Kama ulishawahi kufahamu kuwa kuna dhambi ambazo mtu akitenda hawezi kuurithi Ufalme wa Mungu, basi moja ya hizo dhambi ni hofu au woga. Biblia imeweka bayana kuwa waoga (wenye hofu) wote hawataurithi uzima wa milele Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”

Unaweza kujiuliza kuwa inawezekanaje woga/hofu ikakupeleka kuzimu? Jibu ni rahisi sana, ni kwasababu hofu ni roho kutoka kwa shetani na ujasiri/nguvu ni Roho kutoka kwa Mungu, hivyo mwenye hofu ameingiwa na roho kutoka kwa ibilisi kama yanenavyo maandiko 2Tim 1:7 “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.”

Kwa wale wasomaji wa Biblia mtafahamu kuwa katika agano la kale vitabu vitano vya Musa sehemu kubwa inazungumzia matendo makuu ya Mungu aliyowatendea wana wa Israeli kwa kuwatoa katika utumwa waliokaa kwa zaidi ya miaka mia nne, vilevile BWANA  aliwashindia dhidi ya adui waliokutana nao katika safari yao. Kwa ujumla ni kwamba wana wa Israeli walitembea kwa ushindi mkuu katika safari yao.

Lakini walipoikaribia ile nchi ya ahadi, wakawatuma wapelelezi na baadhi ya wale wapelelezi wakaleta habari mbaya ya ile nchi ni ya majtu na kwamba hawawezi kuingia katika nchi ile kwani wale watu wa nchi ile wana nguvu zaidi yao. Kama tunavyosoma katika kitabu cha Hesabu 13:31-33 “31 Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. 32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. 33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.”

Joshua na Kalebu wakakanusha habari zile mbaya kwa imani na kusema kuwa wataingia katika nchi ya Kaanani kwa nguvu za Mungu na watawashinda adui zao kwani BWANA yupo upande wao; Hata hivyo wana wa Israeli wakachagua habari zenye hofu na kuacha habari za imani ya kushinda kama walivyosema Joshua na Kalebu kiasi cha kutaka kuwaua Joshua na Kalebu kama tunavyosoma katika Hesabu 14:6-10 “6 Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; 7 wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. 8 Ikiwa Bwana anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. 9 Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope. 10 Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa Bwana ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote.”
Kwasababu  ya wana wa Isareli kushindwa kumwamini Mungu hasira ya Mungu ikawaka juu yao na wakapewa adhabu kubwa ya kutoingia katika nchi ya ahadi kama ilivyoandikwa katika 
Hesabu 14:11, 22-24 “11 Bwana akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao….. 22 kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu; 23 hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona; 24 lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na uzao wake wataimiliki.”

Mungu anasema “…..Je! Watu hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini hata lini?..... kumbe kudharau kunatokana na kushindwa kuamini, kwahiyo unaposhindwa kumuamini Mungu tayari unakuwa umemdharau na hasira ya Mungu inawaka juu yako.
Lakini tuanaona Mungu anasema kuwa  mtumishi wake Kalebu amekuwa na roho nyingine ndani yake, maana yake ile roho ya hofu na woga iliwavaa Israeli haikumvaa Kalebu na Yoshua


3.     TAMAA YA FEDHA/MALI
Neno la Mungu linatufundisha kwamba kupenda fedha na mali ni mzizi wa uovu wa kila namna; ukiwa unapenda fedha kuliko kumpenda Mungu, yaani wewe bora uache ibada lakini uende kwenye biashara au kazi yako, kama ukiona umeweka pesa mbele kuliko kumtumikia Mungu yaani ili kutoa huduma lazima upewe fedha basi ufahamu kwamba fedha na mali zimekuwa Mungu wako.

1Timotheo 6:10-11 “10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. 11 Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.”
Uchu wa fedha umepelekea watu wengi hata wakristo kumtenda Mungu dhambi kwani wengine wamewatoa watoto wao au ndugu zao kafara ili wapate fedha na mali. Eneo hili limeharibu utakatifu kwa sehemu kubwa kwani hata watumishi wa Mungu wamebadilishwa na kuwa kama waganga wa kienyeji kwaajili ya kupenda fedha kama ilivyokuwa kwa balamu aliyepokea ujira wa uganga (fedha na mali za kiganga) ili awalaani wana wa Israeli (Hesabu 22:7 “Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki.”)

Tamaa ya fedha na mali inaweza kukuingiza katika shida kubwa na hata ikakuharibu kabisa kama ilivyotokea kwa Gehazi yule mtumishi wa nabii Elisha amabye kwa kutamani fedha na mali aliingia katika matatizo makubwa ya maisha yake yote sawasawa na Neno la Mungu kwamba “Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.” (1Tim 6:9). Hebu tazama habari hii ya Gehazi na tamaa ya fedha na mali

2Falme 5:20-22 “20 Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama Bwana aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake. 21 Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani? 22 Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili. 23 Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele……… 26 Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi? 27 Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.”

Matokeo ya tamaa ya mali na fedha ni uharibifu kama ilivyokuwa kwa gehazi na kama ilivyokuwa kwa Baalamu yule nabii mchawi aliyekuja kuuwa kwa upanga (Yoshua 13:22).

KUABUDU MALI/FEDHA (Ibada ya miungu)
Mali inaweza kukuzuia usiupate uzima wa milele yaani usiirithi ile ahadi ya Mungu Jehova ya maisha ya milele, siku moja Yesu aliuliza “Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?” (Marko 8: 36). Kumbe hakuna faida ya kuwa na mali na fedha halafu ukaukosa uzima wa milele.
Kuna watu katika maisha yao yamegeuza mali/fedha kuwa ndio Mungu wao, kuna watu wamegeuza kazi na biashara zao kuwa ndio Mungu wao kitu kinakuwa ni Mungu wako pale unapokipa kipaumbele kuliko unavyompa Mungu kipaumbele; yaani jambo lolote lililokaa katika nafasi ya Mungu ndio ibada yako, hata kama ni mke/mume/mtoto ikumuweka mbele zaidi ya mungu huyo ndiye ibada yako.
Kulikuwa na mtu mmoja kwenye Biblia ambaye aliweka mali mbele kuliko kitu chochote na Yesu akampa kazi ya kufanya na akaishindwa ile kazi kwasababu ya mali zake (mali/fedha zikamzuia)

Marko 10:17-23 “17 Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? 18 Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu. 19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako. 20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu. 21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. 22 Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi. 23 Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!”
Mtu wa Mungu kumbuka kuwa na fedha na mali sio dhambi kwani katika Biblia tunasoma habari za watumishi wa Mungu ambao walikuwa na fedha na mali nyingi na bado walimtumikia Mungu kwa mali zao, baadhi ya mifano ya watu hao ni Ibrahimu baba wa imani na Mariamu Magdalena ambao walimpendeza Mungu na Mungu aliwabariki.

TUNAWEZA KUSHINDA TAMAA YA FEDHA/MALI
Mtu wa Mungu kumbuka jambo hili, Yesu alikuja duniani ili aishinde dhambi na katka ushindi wa Yesu nasisi tumeishinda dhambi. Yesu alipojaribiwa katika hali ya mwili kabisa alimshinda ibilisi pale ibilisi alipomtamanisha kwa fahari ya dunia hii ni pamoja na fedha na mali, lakini Yesu alimshinda na akakataa kumsujudia shetani ili apewe mali, vivyo hivyo nasisi leo tunaishinda tamaa ya mali inayoletwa na ibilisi kwa jina la Yesu na kwa nguvu ya Neno lake.
Luka 4:5-8 “5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. 8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.”

4.     DHAMBI YA UASI (NI SAWA NA DHAMBI YA UCHAWI)
Uasi ni roho kutoka kwa ibilisi mwenyewe, Neno la Mungu linaifananisha dhambi ya uasi kama ile ya uchawi (1Samweli 15:23 “Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi………..”), yaani muasi ni sawa na mchawi. Kwahiyo ukiona mtu anayo hiyo roho ya uasi katika maisha yake basi uchawi upo jirani naye sana au pengine anao pia uchawi.

a.      Uasi mbinguni
Hata kabla ulimwengu haujaumbwa roho hii ilionekana kwa mara ya kwanza ndani ya ibilisi akiwa ni malaika mbinguni.

Isaya 14:12-19 “12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. 15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.……………”

Shetani alifanya uasi mbinguni pale aliposema …..Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu….. alitaka kukaa kwenye kiti cha Mungu Jehova au kwa lugha nyingine alitaka kumpindua Mungu, lakini uasi huu ulisababisha vita kubwa mbinguni

Ufunuo 12:7-8 “7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.”

Vita hii ilisababisha madhara makubwa mbinguni kwani theluthi ya malaika mbingu walioasi pamoja na ibilisi walitupwa pamoja na ibilisi huku duniani (Ufunuo 12:4 “Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.”)

MUHIMU: Kabla ya mtu yoyote kuasi lazima shetani aingie ndani yake kwanza, kwa lugha nyingine shetani ndiye mhandisi (engineer) wa uasi wa aina zote. Tunasoma kwamba hata kabla yuda hajamsaliti (haja muasi) Yesu shetani aliingia ndani yake kwanza

Luka 22:2-4 “2 Na wakuu wa makuhani na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua; maana walikuwa wakiwaogopa watu. 3 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. 4 Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao.”


b.     Uasi duniani (Uasi wa Adamu)
Tangu shetani atupwe duniani roho ya uasi ikaingia duniani na ikaanza kutenda kazi kuanzia kwa mwanadamu wa kwanza yaani Adamu. Adamu alipomuasi Mungu, dhambi iliingia duniani.
Mwanzo 3:16-19 “16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. 17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; 19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”
Jambo baya ambalo hutokea katika kila dhambi ya uasi ni madhara ya uasi ambayo hayarekebishiki kabisa na hata yakirekebishika ni lazima Mungu aingilie kati YEYE mwenyewe.

c.      Uasi wa kora
Kora na familia yake pamoja na kundi lake la watu mia mbili na hamsini waliamka kinyume na Musa wakitaka kuchukua uongozi ambao Mungu alimpa Musa, roho hii ya uasi ilivyowaingia walijiona kwamba wao wako swan a Musa na Haruni na kwamba Mungu amewatuma na wao pia
Hesabu 16:1-49 “1 Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni; 2 nao, pamoja na watu kadha wa kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa; 3 nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, Bwana naye yu kati yao; n'nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa Bwana?.......... 28 Musa akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kwamba Bwana amenituma, ili nifanye kazi hizi zote; kwa kuwa mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. 29 Kama watu hawa wakifa kifo cha sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote; hapo basi Bwana hakunituma mimi. 30 Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana 31 Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; 32 nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. 33 Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni……..49 Basi waliokufa kwa tauni walikuwa kumi na nne elfu na mia saba, zaidi ya hao waliokufa katika jambo la Kora.”

Kama ni livyosema hapo mwanzo, kila uasi hupelekea madhara makubwa sana, Hasira ya Mungu ilipowaka ardhi ilipasuka na Koran pamoja na wenzake wakamezwa wote nan chi wakiwa hai, wale watu 250 waliteketezwa kwa moto na wote waliowakuwa upande wao walipigwa kwa tauni. Watu waliokufa kutokana na uasi huo ni zaidi ya 14,950 katika siku moja. Uasi ni dhambi inayoleta maangamizo makubwa sana katika maisha ya mwanadamu.

d.     Uasi wa Absalomu
2Samweli 15:1-6 “1 Ikawa baada ya hayo, Absalomu akajiwekea tayari gari na farasi, na watu hamsini wa kupiga mbio mbele yake. 2 Tena Absalomu huondoka asubuhi na mapema, na kusimama kando ya njia ya lango; kisha ikawa, mtu ye yote aliyekuwa na neno, lililokuwa halina budi kufika kwa mfalme ili kuhukumiwa, Absalomu humwita mtu huyo kwake, na kumwuliza, Wewe u mtu wa mji gani? Naye akasema, Mtumwa wako ni mtu wa kabila fulani ya Israeli. 3 Naye Absalomu humwambia, Tazama, maneno yako ni mema yenye haki; lakini hapana mtu aliyeagizwa na mfalme kukusikiliza. 4 Tena Absalomu husema, Laiti mimi ningewekwa kuwa mwamuzi katika nchi hii, ili kila mtu mwenye neno au daawa aje kwangu, nimpatie haki yake! 5 Tena ikawa hapo alipokaribia mtu ye yote kumsujudia, hunyosha mkono wake, na kumshika, na kumbusu. 6 Hivyo ndivyo Absalomu alivyowatendea Israeli wote, waliomwendea mfalme ili wapate hukumu; na hivyo Absalomu akawadanganya watu wa Israeli.”

Absalomu pamoja na kuwa alikuwa ni mtoto wa Daudi aliyependwa sana na baba yake aliona kusubiri mpaka apewe madaraka itachukua muda mrefu sana hivyo akaamua kumpindua baba yake madarakani. Roho ya uasi ikamwingia naye akamsaliti baba yake na kumfanyia uovu usio tamkika ili amuondoe madarakani na lengo lake ilikuwa ni kumuua kabisa baba yake mzazi. Lakini matokeo ya uasi yalimpata, Absalomu alikufa kwasababu ya ule uasi.

2Samweli 18:32-33 32 Naye mfalme akamwambia yule Mkushi, Yule kijana, Absalomu, je! Yu salama? Yule Mkushi akajibu, Adui za bwana wangu mfalme, na wote wainukao ili kukudhuru, na wawe kama alivyo yule kijana. 33 Naye mfalme akataabika sana, akapanda juu, akaingia kile chumba kilichokuwa juu ya lango, akalia; na katika kwenda kwake alisema hivi, Mwanangu Absalomu! Ee mwanangu! Mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!”

Mtu wa mungu Neno la Mungu linatuonya kwamba siku za mwisho kutakuwa na uasi mwingi katika ya wanadamu, kadiri unavyoona dhambi inaongeza kasi basi tambua kwamba ule mwisho uko karibu
2Timotheo 3:1-4 “1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. 2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, 3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, 4 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;”

MAOVU YAKISAMEHEWA MAGONJWA/UDHAIFU/LAANA VINAONDOKA
Pamoja na balaa linaloletwa na dhambi katika maisha ya mwanadamu Mungu kwa Neema yake alimtoa mwana wake Yesu Kristo ili kwa kufa kwake sisi tupokee uzima na uponyaji na tuwe mbali na kuonewa na nguvu za giza.

Yohana 3:16, Wakolosai 1:13 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;”
Zaburi 103:3 “Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,”

Isaya 33:24 “Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.”

Warumi 11:26-27 “26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.”


MAOVU, DHAMBI NA MAKOSA YAMETUWEKA MBALI NA MUNGU
Isaya 59:1-2 “1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; 2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”

TOBA INALETA UPONYAJI WA MAGONJWA YA MWILI NA VITU VINGINE PIA
2Nyakati 7:13-15 “13 Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; 14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. 15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.”

TUKIMPA YESU MAOVU, DHAMBI NA MAKOSA YETU TUNAPONA MAGONJWA YA MIILI YETU NA MATATIZO YA MAISHA YETU
Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.”

KUSAMEHEWA DHAMBINI KUTOLEWA KATIKA UTAWALA WA GIZA
Wakolosai 1:13-14 “13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; 14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;”

HABARI YA MGONJWA ALIYESAMEHEWA DHAMBI NA KUPONA UGONJWA
Mathayo 9:1-7 “1 Akapanda chomboni, akavuka, akafika mjini kwao. 2 Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. 3 Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. 4 Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu? 5 Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende? 6 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako. 7 Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake.”