MWALIKO WA SADAKA TOKA KWA MUNGU
Utoaji wa sadaka
ni mwaliko binafsi utokao kwa Mungu ili ukutane nae. 2Wakorintho
9:6-7 “Lakini nasema neno hili apandae haba atavuna haba;
apandaye kwa ukarimu atavuna ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni
mwake, si kwa huzuni wala si kwa lazima, maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa
moyo wa ukunjufu,”
Kwa maana
kutoa ni moyo, Mungu akikutana na moyo wako anaangalia na Imani uliyo
nayo. Hajalishi umekuja na sadaka kiasi gani. Mtu mwenye Imani ana uhakika ya
kwamba ameona na hivyo basi utoaji wako wa sadaka usiegemee ni kwa jinsi gani
umeskia mahubiri bali yale maelekezo uyasikiayo toka kwa Mungu ndani ya moyo
wako.
Kum 12:10-14 “Lakini
mtakapovuka Yordani na kukaa katika nchi anayowarithisha BWANA, Mungu wenu,
akawapeni raha, akiwaokoa na adui zenu pande zote mkakaa salama; (11) wakati
huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe
jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za
kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono
yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA. (12) Nanyi
mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, ninyi na wana wenu, na binti zenu, na
watumishi wenu wanaume na wanawake, na Mlawi aliyemo mlangoni mwenu; kwa kuwa
hana sehemu wala urithi kwenu. (13) Ujihadhari usitoe sadaka zako za
kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; (14) bali katika mahali
atakapopachagua BWANA katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako
za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo,”
Kama maandiko
yanavyosema hapo juu utoaji wa sadaka ni Mwaliko toka kwa Mungu. Katika utoaji
wa sadaka unafuata maelekezo ya Mungu na hii ina maana unatoa kwa Imani. Hutoi
sadaka kama unavyotaka wewe bali maelekezo ya Mungu ndiyo
yakuongozayo. Huwezi toa sadaka kwa sababu watu wana shida, lakini msaada
unawza toa. Kama mstari wa 13 unakupa onyo kabisa kwamba ujihadhari usitoe
sadaka zako za kuteketezwa kila mahali upaonapo. Na mstari wa 14 unaonyesha
utoe sadaka mahali ambapo Mungu amekuelekeza.
Ntajuaje
kuwa hapa ndo bwana alipochagua?
Pale BWANA
alipoamua kulikalisha jina lake ndipo unapotakiwa kutoa sadaka zako. Kama
kitabu cha Mathayo
18:20 kinavyosema “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa
jina langu, name nipo papo hapo katikati yao”. Kama mahali ambapo jina lake halipo basi usitoe sadaka. Kwa
maana baadhi ya watu wanapenda kutoa sadaka sehemu ambazo wanaona wanapaswa
kutoa. Toa sadaka mahali ambapo uwepo wake umekaa. Mathayo 6:21 “ Kwa
kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako,”. Unapoenda
kutoa sadaka sio kwamba Mungu ana shida nayo bali anataka kukutana na moyo
wako. Kama ni Kanisani Mungu atakuonyesha kanisa gani. Na ikumbukwe kwamba
Imani huja kwa kuskia na sio kila asikiae ana imani. Muombe Bwana auhidhirishe
uwepo wake kwako.
Ni makosa kwa
kanisa kufikiri linaweza kutengezea heshima ya Mungu katika jamnii. Ni Mungu
pekee ndo anaweza kufanya hivyo. Elia alipoomba akasema na ijulikane leo ya
kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya kila kitu sawa sawa na neno lako.
Maneno haya maana
yake kuna nguvu za Mungu zinakuweko mahali halafu zinanyamaza, unatakiwa
uziactivate. Kule kunyamaza sio kwamba hazipo. Na
kuactivate/kuziamsha kwake ni kwa kutoa sadaka kwa kusema na
ijulikane leo kwa maana utakutana nae (MUNGU). Sema na Mungu ya kwamba unataka
Ijulikane leo unapotoa sadaka.
Mungu nataka
ijulikane leo unapotoa sadaka hii. Ukisoma biblia KUTOKA
25:1-23 kuhusiana na ujenzi wa hema jiulize Mungu alipokuwa anaagiza
hii sadaka alikuwa anataka nini? Sio kwamba Mungu alikuwa na shida nayo bali
hitaji lake ni kutafuta mahali pa kukaa kama mstari wa nane unavyoonyesha
wazi “Nao
wanifanyie patakatifu, ili nipate kukaa kati yao”. Kwa maana
hiyo hitaji la Mungu katika kutoa sadaka si sadaka bali anatafuta mahali pa
kukaa.
Kwa sababu
alikuwa haihitaji (angalia mstari wa 8). Tafuta sababu ya Mungu ya kukuambia
utoe sadaka. Hitaji la Mungu katika kutoa sadaka si sadaka bali anatafuta a
DWEILLING PLACE yaani mahali pa kukaa! KUTOKA 29:42,43 “itakuwa ni sadaka ya
kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania
mbele ya BWANA; hapo nitakapokutana nanyi, ili ninene na wewe hapo. Nami
nitakutana na wana wa Isreaeli hapo, na hiyo hema itafanywa takatifu na utukufu
wangu”
Utakatifu/Utakaso
is to be set apart for the purpose of God. Utukufu wa Mungu ni uwepo wa Mungu
uliofunuliwa. Kama unaamini Mungu anaponya lazima kuwe na manifestation kwenye
physical being. Hema ni presence ya Mungu. What sets a person apart is the
presence of God. Kwa mfano, Kama mhubiri hana anointing juu yake, akihubiri
sehemu yenye anointing huhubiri tofauti na watu kusema Yule
mhubiri mbona kwake hajawahi kuhubiri kama hivi? Ikumbukwe kwamba
sio yeye bali ni uwepo wa Mungu umemuwezesha kutoa mafundisho ya kipekee
tofauti na akiwa kanisani kwake, sio yeye ni Presence ya God imemuwezesha kutoa
mafundisho kama hayo.
"Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa,
jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa
amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. Ikawa siku zile akaugua, akafa;
hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. Na kwa kuwa mji wa Lida
ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko,
wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu. Petro
akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote
wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona
Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. Petro akawatoa nje wote,
akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka.
Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua,
akaketi. Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale
watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai" - Matendo
9:36-41
Na Mwl.
Christopher Mwakasege
No comments:
Post a Comment