UAMSHO
(Mwl.C.Mwakasege)
Je! Ni laana au ni baraka?
(Sehemu
ya Kwanza)
Hili swali linakuja kwako – tena kwa wakati wake hasa! Nilikuwa nafundisha
katika kanisa fulani hapa nchini – nilipouliza swali hili wengi wakajibu kwa
pamoja – ni baraka! Lakini wakati huo huo walikuwako wazee wa kanisa ambao
walikuwa wanauona uamsho ya kuwa ni laana!
Nilipokuwa
nahubiri kwenye kanisa moja huko Marekani ya kaskazini – Mchungaji na wakristo
wa kanisa hilo walinieleza juu ya uamsho uliotokea kanisani hapo miaka michache
ya nyuma – na baada ya kipindi si kirefu kanisa likagawanyika na wakristo
wengine wakahama, wengine wakarudi nyuma kiroho. Nilipowauliza chanzo cha
mgawanyiko huo ni nini – wakajibu bila hata kusita, wakasema “Ni Uamsho!”
Je! unakubalina na jibu hili ya kwamba
uamsho ukitokea katika kanisa huwa unagawa wakristo?
Sehemu
zingine vimetokea vikundi vya uamsho katika makanisa mbalimbali – mahali
pengine vimefurahiwa na mahali pengine vimechukiwa, hata kufika hatua hata ya
kuvipiga marufuku! Je! hii ni sawa?
Ni wakati
gani uamsho unakuwa ni laana na ni wakati gani uamsho – unakuwa ni baraka?
Katika mfululizo huu wa maswali na majibu tutajifunza na kujibu maswali
mbalimbali kuhusu Uamsho.
Ni maombi
yangu kwa Mungu ya kuwa mafundisho utakayoyapata katika majibu ya maswali
katika mfululizo huu yatakuimarisha zaidi katika maisha yako ya wokovu, na
katika kumtumikia Mungu.
Pia, ni
maombi yangu kwa Mungu, katika Jina la Yesu Kristo ya kuwa mafundisho haya juu
ya uamsho yatasaidia kutatua matatizo mengi yaliyopo katikati ya Wakristo –
hasa yanayotokana na uamsho.
Ndiyo maana
ni vizuri hata wewe uyasome majibu haya ukiwa katika hali ya maombi ili Mungu
afungue moyo wako na akili zako upate kuyaelewa na maandiko. Maswali
tutakayojibu ni haya yafuatayo:
SWALI LA KWANZA: Uamsho ni kitu gani?
Ni rahisi
sana kuchanganya maana za maneno na matukio yake, hasa tunapozungumza juu ya
Uamsho. Wengine wanachanganya maana ya uinjilisti na ile ya uamsho. Ni budi
ufahamu ya kuwa maneno haya Uinjilisti na Uamsho yana maana zinazotofautiana.
Neno
‘Uamsho’ limetafsiriwa toka kwenye neno la Kiingereza ‘revival’.
Na neno ‘revival’ linatokana na neno ‘revive’ ambalo lina
maana ya kuhuisha, kuchochea, kurudishia
nguvu, kufufua na kuamsha.
Kwa mfano Nabii Habakuki alipokuwa
anaomba alisema; “ Ee Bwana, FUFUA kazi yako katikati ya miaka …..”
(Habakuki 3:2). Na katika Biblia ya Kiingereza ya King James mstari huu
umeandikwa hivi; “O Lord, REVIVE thy work in the midst of the years …”
kwa maneno mengine Nabii Habakuki alikuwa anaomba juu ya uamsho
Uamsho unatokea wakati ambapo Mungu, kwa uweza wa Roho wake
Mtakatifu anaposhuka ndani ya mioyo au roho za watu wake ambao wamepoa, au
wamerudi nyuma kiroho, au wamekuwa vuguvugu au wamelala. Hawa watu mwanzo
walikuwa wameonja nguvu za Mungu, lakini
baada ya muda walirudi nyuma kiroho au wakapoa. Uinjilisti maana yake ni
kuitangaza habari njema – au kutangaza habari za Yesu Kristo. Uinjilisti
hutumika wakati wa kuwaleta watu wasiookoka katika ufalme wa Mungu. Uinjilisti
ni matokeo ya Uamsho katika Kanisa. Kanisa
lililopoa au kulala kiroho huwa halina mzigo wa Uinjilisti wala wa
kuleta mavuno ya roho za watu kwenye ufalme wa Mungu.
Kwa kusisitiza tu ni kwamba Uamsho ni matokeo ya
nguvu za Mungu kuwatembelea upya WATU WAKE.
Nguvu za Mungu zinapowatembelea watu ambao
hawajaokoka, na kuwafanya waokoke, hatuliiti tendo hili kuwa ni uamsho, bali ni
uinjilisti. Lakini nguvu hizi za Mungu zinapowatembelea watu waliokwisha
kuokoka tayari, na kuamsha upya kiu ya kumjua na kumtumikia Mungu, huwa
tunaliita tendo hili kuwa ni Uamsho.
Ndiyo maana ukienda katika madhehebu ambayo kuna
wakristo waliookoka na ambao hawajaokoka; wale waliookoka huwa mara nyingi
huitwa ‘Wakristo wa uamsho’. Ndiyo maana mara kwa mara unasikia maneno kama haya; mikutano ya uamsho, vijana wa uamsho, watu wa
uamsho, maombi ya uamsho, n.k.
Tunapozungumzia juu ya uamsho, ujue ya kuwa ni lazima
kuna kitu cha kuamsha. Kunakuwa na Uamsho, kwa kuwa kuna kitu cha kuamsha.
Kunakuwa na ufufuko, kwa kuwa kuna kitu cha kufufuka. Kunakuwa na kuhuisha, kwa
kuwa kuna kitu cha kuhuisha.
Kazi ya kuamsha roho za wakristo waliopoa, au
waliorudi nyuma kiroho, au waliolala kiroho, ni kazi ya Mungu mwenyewe, kwa
uwezo wa Roho wake Mtakatifu.
Mtu aliyekuwa ameokoka akirudi nyuma na kufa kiroho,
kazi ya kumfufua au kumwamsha upya si ya mwanadamu bali ya Roho Mtakatifu.
Ingawa ni kweli kwamba Mungu humshirikisha mtu
amtakaye katika kazi zake mbalimbali kama
tutakavyoona kadri tunavyoendelea; bado mwanzilishi na msimamishaji wa uamsho
ndani ya mtu ni Mungu mwenyewe.
Si vyema kumpa mwanadamu sifa ya kuleta uamsho mahali
fulani, badala ya kumpa Mungu ambaye amemtumia mtu huyo kama
chombo tu.
Fahamu “si kwa uwezo (wa mwanadamu), wala si kwa
nguvu (za mwanadamu), bali ni kwa ROHO YANGU, ASEMA BWANA WA
MAJESHI” (Zakaria 4:6)
SWALI LA PILI: Kwa
nini Mungu analeta Uamsho?
Ukisoma
katika Biblia utaona ya kuwa kuna sababu mbili kubwa ambazo zinamfanya Mungu
alete uamsho katikati ya watu wake.
Sababu
ya Kwanza ni UAMSHO WA KAZI YA BWANA. Nabii Habakuki aliomba hivi, “Ee
Bwana, FUFUA KAZI YAKO katikati ya miaka; katikati ya miaka tangaza habari
yake; katika ghadhabu kumbuka rehema” (Habakuki 3:2).
Sababu
ya Pili ni UAMSHO WA MIOYO YA WATU WA MUNGU. Mtunga Zaburi aliomba
hivi; “Je hutaki kurudi na KUTUHUISHA (Kutuamsha), watu wako WAKUFURAHIE?
(Zaburi 85:6). Na katika kitabu cha Nabii Isaya 57:15 imeandikwa hivi; “Maana
yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu;
asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na
yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu
na kuifufua mioyo yao
waliotubu”.
1.Uamsho wa
kazi ya Bwana
“Ee Bwana, FUFUA KAZI YAKO katikati ya miaka; katikati
ya miaka tangaza habari yake; katika
ghadhabu kumbuka rehema” (Habakuki 3:2)
Nilipoyasoma maombi haya ya Nabii Habakuki
nilijiuliza maswali kadhaa, na baadhi yake ni haya: Je! kazi ya Bwana maana
yake nini? Je! kazi ya Bwana nayo inahitaji kufufuliwa? Kitu gani kinaua kazi
ya Bwana hata ihitaji kufufuliwa?
Maswali haya yalinifanya nianze kukisoma kitabu cha Nabii
Habakuki kwa makini. Nilipokuwa nakisoma, niliyakuta mambo ambayo ningependa
kukushirikisha hapa.
Kitabu cha Habakuki kwa sehemu kubwa kinaeleza mazungumzo
kati ya Mungu na nabii wake Habakuki. Habakuki anaanza kwa manung’uniko na
malalamiko juu ya uharibifu wa haki, na kutokuonekana kwa kazi au uwepo wa
Mungu katikati yao .
“ Ee Bwana, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya UDHALIMU, ila hutaki KUOKOA.
Mbona wanionyesha uovu, na unitazamisha UKAIDI? Maana UHARIBIFU NA UDHALIMU u
mbele yangu; kuna UGOMVI, na MASHINDANO yatokea. Kwa sababu hiyo SHERIA
INALEGEA, wala HUKUMU HAIPATIKANI; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki,
kwa sababu hiyo hukumu ikipatikana imepotoka” (Habakuki 1:2-4).
Ni wazi kwamba katikati ya wana wa Israeli – uzao wa
Ibrahimu, kulitokea UDHALIMU, UKAIDI, UHARIBIFU, UGOMVI, MASHINDANO, UVUNJAJI
WA SHERIA, na HAKI KUTOKUWEPO. Habakuki
hakuona ya kwamba ni halali kwa mambo hayo kuwepo katikati ya watu wa Mungu, na
Mungu wao akae kimya.
Na Mungu alimjibu kuwa atalitumia kabila la Wakaldayo
kuwaadhibu wana wa Israeli (Habakuki 1:5 – 11)
Katika mahojiano yake na Mungu, Habakuki anakubali
kabisa ya kuwa wana wa Israeli wamekosa. Lakini anamwuliza Mungu ya kuwa kwa
nini Yeye, aliye mtakatifu, tena mwenye macho safi asiweze kuuona uovu huo (Habakuki 1:12 –
13), na kwamba amewachagua Wakaldayo wapagani, ili watwae kisasi juu ya taifa
teule.
Nabii Habakuki alitaka kujua kwa nini Mungu ameamua
kuwaadhibu wana wa Israeli kwa uovu wao kwa kuwatumia Wakaldayo walio waovu
zaidi kuliko wao. Tena, kwa nini amsaidie Mkaldayo aliye mjeuri asiye na haki,
ili apate ushindi? Kwa maneno mengine alitaka kufahamu kwa nini ujeuri, ugomvi
na dhuluma vitawale mataifa na si haki na amani?
Mungu alimpa Nabii wake Habakuki majibu mawili
muhimu; 1. Mwishoni haki itashinda;
2. “Mwenye haki ataishi kwa imani
yake” (Habakuki 2:4).
Baada ya mazungumzo hayo, ndipo Nabii Habakuki
alipoomba sala hii “ Ee Bwana, fufua kazi yako katikati ya miaka, katikati
ya miaka tangaza habari zake, katika ghadhabu kumbuka rehema” (Habakuki 3:2)
Kwa maneno mengine alikuwa anamwomba Mungu kuwa
badala ya kuadhibu akumbuke rehema ili awarehemu watu wake. Utendaji wa kazi
yake ufufuke au uamke kwa upya katikati ya watu wake. Palipo na ugomvi alete
amani. Palipo na dhuluma alete haki. Palipo na mashindano alete ushirikiano.
Palipo na ukaidi alete upole na unyenyekevu.
Je! huoni kuwa na sisi tunahitaji kuungana na Nabii Habakuki
kuomba juu ya uamsho wa kazi ya Mungu katika makanisa na vikundi vya watu wa
Mungu kama vya maombi vilivyopoa? Katikati ya
Wakristo kazi ya Mungu haionekani. Kumejaa dhuluma, ukaidi, ugomvi na
mashindano.
Wakati umefika wa wewe na mimi kumwomba Mungu kwa
juhudi ili kazi yake na matendo yake yaonekane tena katikati yetu. Palipo na
ugomvi atuletee amani ipitayo fahamu zote. Palipo na mashindano atuletee
ushirikiano katika Roho na kweli. Palipo na dhuluma atuletee haki na hukumu za
kweli zisizokuwa na upendeleo. Palipo na ukaidi atuletee upole na kunyenyekea.
Palipo na kuuchukia wokovu, alete kuupenda wokovu. Palipo na uchovu na uzito wa
kuifanya kazi ya Mungu, alete utayari na wepesi badala yake! Kama
ulikuwa hujaanza kuomba, basi anza sasa kwa ajili ya mahali unapotaka
mabadiliko yatokee kwa wakristo wote kwa ujumla. Pia umwombe Mungu kuwa “katika
ghadhabu akumbuke rehema”.
2. Uamsho wa mioyo ya watu
wa Mungu
“Je! hutaki kurudi na KUTUHUISHA, Watu wako AKUFURAHIE?" Zaburi 85:6)
“Je! hutaki kurudi na KUTUHUISHA, Watu wako AKUFURAHIE?" Zaburi 85:6)
Tafsiri nyingine ya maneno haya inasema hivi:
“Je hutatujalia tena maisha mapya ili watu wako wakufurahie?”
Na katika maneno ambayo Yesu Kristo aliwaambia
wanafunzi wake yanayozungumza juu ya FURAHA MIOYONI MWAO – alisema hivi;
“Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
FURAHINI NA KUSHANGILIA; kwa kuwa
thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa
maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu”
(Mathayo 5:11,12).
Ukiona mtu aliyeokoka anakosa amani na furaha wakati
anaposhutumiwa, anapoudhiwa, na anaposingiziwa uongo kwa sababu ya KUMWAMINI
YESU, ajue ya kuwa amepoa kiroho na anahitaji uamsho. Yesu alisema yanapotokea
hayo FURAHI na KUSHANGILIA.
Pia, Yesu Kristo alisema hivi:
“Amin,
amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi
mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa FURAHA. Mwanamke azaapo yuna
huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena
ile dhiki, kwa sababu ya FURAHA YA KUZALIWA MTU ULIMWENGUNI. Basi ninyi hivi
sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na MIOYO YENU ITAFURAHI, na FURAHA
YENU hakuna awaondoleaye. Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin,
nawaambia, mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa jina langu. Hata sasa
hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata furaha yenu iwe
timilifu "
(Yohana 16:20 – 24).
Furaha ya Bwana ndani ya mioyo yetu sisi tulio wakristo,
ndiyo nguvu ya kutuwezesha kuendelea katika wokovu bila manung’uniko. Ukiona
mtu anasema ameokoka na huku amekosa FURAHA YA BWANA ndani yake, basi ujue kuna
shida fulani katika maisha yake ya kiroho!
Katika kitabu cha matendo ya Mitume furaha inaonekana
wazi katikati ya wakristo hawa wa kwanza. Furaha inaonekana walipopokea nguvu
za Roho Mtakatifu (Matendo ya Mitume 13:52). Furaha inaonekana Bwana alipofanya
miujiza katikati yao
(Matendo ya Mitume 13:8). Furaha inaonekana katikati yao walipoona watu wengine wakiokoka na
kumfuata Yesu (Matendo ya Mitume 15:3). Na pia furaha inaonekana walipokuwa
wakiumega mkate (Matendo ya Mitume 2:46).
Na mtume Paulo katika nyaraka zake kwa waumini
anazungumzia furaha katika maeneo mawili muhimu. Kwanza ,
anazungumzia juu ya furaha aliyonayo anapowaona wale aliowaongoza kwa Yesu
wakiendelea katika imani ya wokovu (1Wathesalonike 2:19; Wafilipi 2:2). Pili,
anazungumzia furaha anayopata yeye na mkristo yoyote yule anapoteswa kwa ajili
ya Kristo, kwa kuwa si furaha ya kibinadamu, bali ni furaha iliyo tunda la Roho
ndani ya mtu (Wagalatia 5:22).
Ni wazi kabisa ya kuwa Mkristo asipoonekana ana FURAHA YA
BWANA, basi hata maisha yake ya kiroho yanakosa changamoto. Na wengine hufikia
hata kuacha wokovu.
Nakumbuka wakati fulani mtu mmoja alinifuata kwa ajili ya
ushauri na akasema hivi; “Mimi nimeokoka, lakini naona napata mawazo ya kutaka kuacha wokovu, na
niliona kabla ya kufikia uamuzi huo nije kwako unishauri”
Mara moja nilifahamu ya kuwa amekosa FURAHA katika njia hii
ya wokovu. Baada ya kuzungumza na kumweleza kitu cha kufanya kufuatana na
maandiko, nilimwambia asiache wokovu. Nikamuuliza “Ukimwacha Yesu utakwenda kwa
nani? Namshukuru Mungu ya kuwa huyo mtu alipokea ushauri niliompa na anaendelea
na wokovu.
SWALI LA TATU: Uamsho ukitokea mahali
kwa Uwezo wa Roho Mtakatifu, mambo gani yanatokea?
Uamsho unapotokea katikati ya watu wa Mungu, kuna
mambo mengi yanayotokea, lakini mambo makubwa yafuatayo hujitokeza:
1. Hofu ya Mungu
Palipo na uamsho pana hofu ya Mungu. Kuna wakati unafika
ambapo watu wa Mungu wanapoa na kutokujali sana mambo ya Mungu, na kutokupenda maombi ya
muda mrefu, na hata kufikia kutokwenda kanisani au kwenye vipindi vya masomo ya
biblia, kwa kujisingizia shughuli nyingi.
Ukiona mambo haya yanajitokeza au yamejitokeza, basi
ujue ya kuwa hofu ya Mungu haipo kati yao .
Na Mungu anapoamua kujidhihirisha upya katikati yao kwa uwezo wa Roho
wake Mtakatifu, kunatokea uamsho, na uwepo wa Mungu unakuwa wazi kwa kila mtu.
Na palipo na uwepo wa Mungu, pana hofu ya Mungu.
Hofu ya Mungu inapotokea
katikati ya watu wa Mungu inaleta mambo mpya. Ikiwa umekaa na watu waliookoka
utakuwa umeona ya kuwa, hofu ya Mungu isipokuwepo katikati yao , huwa wengi wao wanaenenda bila ushuhuda
na bila hekima, na matokeo yake ni kuleta makwazo na kuufanya udharauliwe.
Lakini hofu ya Mungu inaporudi katikati yao kwa sababu ya uamsho wa Roho Mtakatifu,
wanaanza upya kutembea katika ushuhuda na hekima. Je, unafahamu ni kwa nini?
Kwa kuwa imeandikwa; “Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, ……” (Zaburi
111:10).
Tafsiri nyingine ya hofu ya Mungu ni kumcha Bwana.
Mungu anapojidhihirisha upya katikati ya watu wake, kila mmoja wao anaona kama vile Mungu ameshuka kwa ajili yake tu na ameshuka
kumshughulikia yeye tu! Kwa hiyo utaona watu wakiwa wepesi kutubu dhambi zao na
kutengeneza maisha yao
ya kiroho.
Na kinachofuata ni watu hao kuanza kujishughulisha
upya na mambo ya Mungu. Utaona wanapenda utakatifu, utaona wanapenda maombi na
kumtumikia Mungu. Kunapotokea uamsho watu huona Mungu yuko karibu nao zaidi
kuliko alivyokuwa zamani.
Nakumbuka nilikuwa nahubiri mahali fulani hapa
nchini, na niliposema wale wanaotaka kutubu waje mbele, watu wengi walikuja na
kutubu kwa machozi, Roho wa Mungu alishuka kwa nguvu katika mkutano ule.
Na nilipowafuatilia hao waliotubu, nikaona ya kuwa
robo tatu yao
walikuwa ni watu waliokuwa wameokoka zamani lakini wakarudi nyuma na kuanguka
dhambini. Na neno lilipohubiriwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, wakachomwa mioyo yao , wakawa kama watu
walioamshwa toka usingizini, wakaamua kutubu na kumrudia Bwana.
Na matokeo yake ni vikundi vya maombi kuanza kwa
upya; ‘Fellowship’ na kanisa kupata nguvu mpya, na watu kushuhudia kwa ujasiri
na bila woga. Hii si kazi ya mtu, ni kazi ya Roho Mtakatifu aichunguzaye mioyo
ya watu na kuijua ilivyo.
2. Watu wengi wanaokoka
Watu wa Mungu wakipoa, hata watu wanaozaliwa upya
mara ya pili wanakuwa wachache. Watu wa Mungu wakiamka upya kiroho, watu wengi
wanaokoka. Ni wazi kwamba kunapotokea uamsho, mavuno ya roho za watu yanakuwa
mengi – kwa kuwa watu wanapata msukomo mpya wa kushuhudia.
Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa wanafunzi wa kwanza
wa Yesu Kristo.
Siku ya Pentekoste ilipotimia. Roho wa Uamsho aliwashukia
wale wanafunzi wa kwanza wa Kristo, ambao walikuwa wamejaa hofu na wasiwasi; na
baada ya kuwaamsha na kuwavika ujasiri walianza kumsifu Mungu kwa lugha
nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
Uamsho huu katikati ya wanafunzi wa Kristo, ulileta
mafadhaiko na mshangao kwa wale ambao hawakuwa wanafunzi wa Kristo. Imeandikwa:
“Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa ….
Wakashangaa wote ….” (Matendo ya Mitume 2:6,7).
Na wakati ule ule Petro ambaye alikuwa amewahi
kumkana Yesu Kristo mara tatu Roho Mtakatifu alimpa ujasiri wa kusimama na
kuhubiri kwa nguvu habari za Yesu Kristo.
Mtu aliyeamshwa na Roho Mtakatifu akisema maneno yake huwa
yamejaa moto ambao huwachoma wale ambao wanamsikiliza!
“Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo Yao, wakamwambia Petro na
Mitume wengine, Tutendeje ndugu zetu? Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kila
mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate
ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa
cha Roho Mtakatifu, Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu,
na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu
wamjie. Akawashu hudia Kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema,
jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Nao waliolipokea neno lake (walioamua
kuokoka) wakabatizwa na siku ile
wakaongezeka watu wapata elfu tatu”
(Matendo ya Mitume 2:37 – 41).
Kwa sababu ya uamsho wa Roho Mtakatifu katikati ya
watu wa Kristo, watu wengine ELFU TATU waliokoka kwa siku moja na kwa mahubiri
ya mtu mmoja, hii ni kazi ya Roho Mtakatifu!
Na hawa waliookoka si kwamba walitubu na kutawanyika
bali biblia inasema, “Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika
ushirika, na katika kuumega mkate na katika kusali. Kila mtu akaingiwa na hofu
…… Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa” (Matendo
ya Mitume 2:42 – 47).
3.
Uamsho unaleta Umoja
Watu wa Mungu wakipoa kiroho, matengano, magomvi na
mashindano hutokea katikati yao .
Watu wa Mungu wakipoa kiroho, huwa wanapambana wao kwa wao badala ya kupambana
na shetani.
Watu wa Mungu wakipoa kiroho hata baraka za Mungu
hazionekani katika makusanyiko yao ,
ndoa zao, na kazi zao. Wanakuwa ni watu wanaoishi kwa kujitahidi, na siyo kwa
nguvu za Roho Mtakatifu.
Imeandikwa hivi:
“Tukiishi
kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana
(Wagalatia 5:25 – 26)
“Tazama jinsi ilivyo vema, na kupendeza ndugu wakae pamoja, kwa UMOJA.………….. maana ndiko Bwana ALIPOAMURU BARAKA, Naam uzima hata milele” (Zaburi 133:1-3).
“Tazama jinsi ilivyo vema, na kupendeza ndugu wakae pamoja, kwa UMOJA.………….. maana ndiko Bwana ALIPOAMURU BARAKA, Naam uzima hata milele” (Zaburi 133:1-3).
Hii ni habari njema kusikia ya kwamba BWANA AMEAMURU
BARAKA ZAKE ZIENDE KWA WATU WANAOKAA PAMOJA NA KWA UMOJA!
Ni kweli kwamba vitu vingi vinaweza kutukusanya
pamoja, kama vile ndoa, harusi, misiba,
mikutano, ibada, ugomvi, mashauri; nakadhalika. Lakini kuwa pamoja haimaanishi
kuwa mnao umoja.
Narudia tena: Lakini kuwa pamoja haimaanishi kuwa mnao
umoja. Mnaweza kuwa pamoja katika ibada au harusi huku moyoni hampatani. Na
hivi ndivyo ilivyo kwa watu wengi wa Kristo, wanakaa au wanakutana pamoja
lakini hawana Umoja!
Umoja wa kweli hauletwi na taratibu za kibinadamu
hata kama ni nzuri sana .
Zinaweza kutufanya tuwe pamoja, lakini haziwezi kutufanya tuwe na umoja. Umoja
wa kweli huletwa na Roho Mtakatifu.
Ndiyo maana Roho Mtakatifu akijidhihirisha kwa upya
katikati ya watu wa Mungu huwa wanapatana na kuwa kitu kimoja bila kujali
tofauti ya madhehebu yao !
Mipaka ya mapokeo ya kidhehebu, ya kikabila, ya kiutajiri, ya kimaskini, huwa
inavunjika!
Ndiyo ilivyokuwa kwa wanafunzi
wa Kristo wa kwanza walipohuishwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
katika kitabu cha Mtendo ya Mitume 2:41 – 42 utaona jinsi
wenzetu walivyoishi kwa Umoja.
Imeandikwa: “Nao
waliolipokea Neno lake
wakabatizwa ; na siku ile
wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume,
na katika USHIRIKA, na katika kuumega mkate, na katika KUSALI ……. Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na
vitu vyote SHIRIKA wakiuza mali zao, na
vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama
kila mtu alivyokuwa na haja. Na siku zote kwa MOYO MMOJA walidumu katika hekalu, wakimega mkate NYUMBA KWA NYUMBA na
kushiriki chakula chao kwa FURAHA na kwa MOYO MWEUPE, wakimsifu Mungu, na
kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale
waliokuwa WAKIOKOLEWA”.
Kunapotokea uamsho, umoja wa kweli
hutokea. Kulipo na uamsho wa Roho Mtakatifu, ushirikiano wa kweli hutokea.
Kunapotokea uamsho, uchoyo unahama, ugomvi unahama, wivu unahama, uvivu
unahama, na ubinafsi unahama. Na tabia ya uamsho ni kuleta umoja wa kweli –
watu waliopoa kiroho wanaamka toka katika uchoyo, toka katika ugomvi, toka
katika ubinafsi na wivu, na badala yake wanaanza kushirikiana, kusaidiana,
kupendana na kusali pamoja katika Roho Mtakatifu.
Wakristo wenzentu wa mwanzo ndivyo ilivyotokea kwao Roho
Mtakatifu alipotawala maisha yao na uhusiano wao
– tunasoma hivi:
“Na jamii ya watu waliamini (waliookoka) walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alicho nacho nimali yake
mwenyewe; bali WALIKUWA NA VITU VYOTE SHIRIKA. Na mitume wakatoa ushuhuda wa
kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala hapakuwa
na mtu miongoni mwao mwenye MAHITAJI; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja
au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile walivyouza, wakaiweka
miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadri ya alivyohitaji” (Matendo ya Mitume 4:32 – 35)
“Na jamii ya watu waliamini (waliookoka) walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alicho nacho ni
Hata hivi leo maisha ya namna hii yanatokea na
ushirikiano wa namna hii unatokea ikiwa Roho Mtakatifu ataruhusiwa kuleta
uamsho kwa utaratibu wa Mungu wenye kuleta baraka na siyo utaratibu wa kibinadamu
au wa kishetani unaoleta laana.
(Mwezi ujao tutaendelea kujibu maswali mengine
juu ya Uamsho – usiache kututembelea katika ukurasa huu).
(Sehemu ya Pili)
Uamsho unapotokea
mahali kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kunatokea upinzani. Katika mfululizo wa
maswali na majibu mwezi uliopita, tuliona ya kuwa uamsho unapotokea mahali
kunatokea mambo yafuatayo:
1.
Hofu ya Mungu
2.
Watu wengi wanaokoka
3.
Umoja unaimarishwa.
Mwezi huu napenda tuangalie jambo la 4 la matokeo ya uamsho unapotokea mahali –
nalo ni upinzani. Upinzani unaotokea kwa sababu ya uamsho una sehemu tatu
kubwa:
1. Upinzani dhidi ya watumishi
wanaotumiwa na Mungu wakati wa uamsho.
2. Upinzani dhidi ya kazi ya Roho
Mtakatifu katikati ya watu.
3. Upinzani dhidi ya watu wanaokoka
kwa sababu ya uamsho.
Ni
vizuri tufahamu na tukumbushane ya kuwa uamsho wa Mungu unaletwa na Roho
Mtakatifu. Katika kambi ya watu wa Mungu kunapotokea uamsho - shetani naye huwa
anaamsha watu wa kambi yake ili waendeshe upinzani juu ya uamsho wa Mungu.
Kambi la watu wa Mungu likilala, si rahisi kuona upinzani wa mambo ya kiroho. Lakini kukitokea uamsho hata kama ni kwa mtu mmoja – ghafla anazungukwa na upinzani mkali – labda aaumue kujificha na kutojionyesha kwa watu kuwa amehuishwa na Roho Mtakatifu au ya kuwa ameokoka
Upinzani dhidi ya uamsho ni jambo la kawaida. Wala huhitaji kushituka. Lakini jambo lisilo la kawaida ni kwa watu waliookoka kuamua ‘kupoa’ na kurudi nyuma kiroho kwa sababu ya upinzani.
Kambi la watu wa Mungu likilala, si rahisi kuona upinzani wa mambo ya kiroho. Lakini kukitokea uamsho hata kama ni kwa mtu mmoja – ghafla anazungukwa na upinzani mkali – labda aaumue kujificha na kutojionyesha kwa watu kuwa amehuishwa na Roho Mtakatifu au ya kuwa ameokoka
Upinzani dhidi ya uamsho ni jambo la kawaida. Wala huhitaji kushituka. Lakini jambo lisilo la kawaida ni kwa watu waliookoka kuamua ‘kupoa’ na kurudi nyuma kiroho kwa sababu ya upinzani.
Pia ni
budi kufahamu ya kuwa shetani ndiye mpinzani wa uamsho usitokee au unapotokea
mahali. Shetani anaweza kupinga mwenyewe au kwa kuwatumia pepo wake au kwa
kuwatumia binadamu katika maeneo mbalimbali, kwa mfano:
MFANO: 1. Upinzani
dhidi ya watumishi wanaotumiwa na Mungu wakati wa uamsho.
Yesu Kristo
alisema maneno haya na wanafunzi wake: ‘’Heri ninyi watakapowashutumu na
kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo,kwa ajili yangu. Furahini, na
kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo
walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu’’ (Mathayo 5:11,12)
Wanafunzi
walipomuuliza dalili za siku za mwisho – kati ya mambo mengi aliyowaambia ya
kuwa yatatokea ni pamoja na mambo haya yafuatayo: ‘’Nanyi jihadharini
nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa,
nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kuwa ushuhuda kwao’’ (Marko
13:9)
Yesu
alijua upinzani mkali utatokea dhidi ya watumishi wake, na aliwaeleza mapema.
Kwa hiyo tunapoona upinzani unatokea dhidi ya watumishi wa Kristo tusishangae,
yaliandikwa ya kuwa yatatokea.
Kwenye Waebrania 11:36-38 inatueleza
baadhi ya mambo yaliyowapata watumishi wa Mungu katika utumishi wao –
imeandikwa hivi; ‘’wengine walijaribiwa kwa dhihaka na
mapigo, naam kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani; walipigwa kwa mawe, walikatwa
kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga kwa misumeno, walijaribiwa,
walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa
wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa
nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika
mapango na katika mashimo ya nchi’’.
Ukisoma kitabu cha Matendo ya Mitume utaona upinzani na mateso yaliyowapata
Stefano, Paulo, Yakobo, Petro na watumishi wengine wa Mungu. hata leo hivi
upinzani huu upo. Lakini tunapata neno la faraja katika I Petro 4:14 tukiambiwa
hivi: ‘’mkilaumiwa kwa ajili ya njia ya Kristo ni heri yenu; kwa
kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia’’.
MFANO 2: Upinzani dhidi ya kazi ya Roho
Mtakatifu katikati ya watu.
Kati ya mambo yanayotokea Roho Mtakatifu anapokuwa kazini katika uamsho ni uponyaji wa miili ya watu. Lakini kazi hii ya Roho Mtakatifu huwa mara nyingi inapingwa na kupata upinzani mzito ili isiendelee. Jambo lililo wazi tunaposoma kwenye Biblia ni kwamba upinzani dhidi ya uponyaji unatokea zaidi katikati ya watu wa dini – hasa wanapoona ya kuwa uponyaji umeingilia taratibu za dini au ibada zao au ukiwa tofauti na mafundisho wanayofundisha.
Kati ya mambo yanayotokea Roho Mtakatifu anapokuwa kazini katika uamsho ni uponyaji wa miili ya watu. Lakini kazi hii ya Roho Mtakatifu huwa mara nyingi inapingwa na kupata upinzani mzito ili isiendelee. Jambo lililo wazi tunaposoma kwenye Biblia ni kwamba upinzani dhidi ya uponyaji unatokea zaidi katikati ya watu wa dini – hasa wanapoona ya kuwa uponyaji umeingilia taratibu za dini au ibada zao au ukiwa tofauti na mafundisho wanayofundisha.
Ukisoma Marko 3:1,2 utaona habari za
Yesu zinasema hivi:
"Akaingia
tena katika sinagogi; na palikuwapo huko mtu mwenye mkono uliopooza; wakamvizia
ili kuona kama atamponya siku ya sabato;
wapate kumshitaki’’.
Hawa Mafarisayo na Maherodi walikuwa watu wa ajabu - wakati wengine wanatamani
kumwona Yesu akiponya ili Mungu atukuzwe na mgonjwa apone - wao walijali zaidi
utaratibu wao wa Sabato. Wakamvizia Yesu ili wamshitaki, ikiwa atamponya yule
aliyekuwa na mkono uliopooza. Yesu aliyajua mawazo yao na baada ya mahojiano nao – akamponya
yule mgonjwa naye akapona! Lakini angalia upinzani ulioinuka.
"Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu
yake pamoja na Maherodi jinsi ya kumwangamiza’’.
(Marko 3:6). Kosa ambalo waliona Yesu alifanya sio katika kumponya mgonjwa bali
kumponya mgonjwa siku ya Sabato ambapo dini yao ilikuwa inakataza.
Ukisoma tena kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 3 na 4 utaona upinzani
uliotokea wakati Mungu alipomponya yule mtu aliyezaliwa kilema – kwa kumtumia
Petro. Baada ya kuwafunga Petro na Yohana gerezani na halafu kuwahoji – mwisho
kuhani Mkuu akishauriana na wenzake wakaamua kuipinga kazi hiyo isienee;
"Lakini neno hili lisije likaenea katika
watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili. Wakawaita,
wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu’’
(Matendo ya Mitume 4:17,18).
Baada ya kuambiwa hivi, Petro na Yohana hawakutishika wala kuyumba, bali
wakajibu wakawaambia hivi; ‘’kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza
ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena
mambo tuliyoyaona na kuyasikia’’ (Matendo ya Mitume 4:19,20)
Je, umewahi kuona, kusikia au kukutana na upinzani wa jinsi hii unaolelekezwa
katika kazi anayoifanya Roho wa uamsho katikati ya watu?
MFANO 3: Upinzani dhidi ya watu
wanaookoka kwa sababu ya Uamsho
Tuliona mwezi uliopita tulipokuwa tunaanza kujibu maswali juu ya uamsho ya kuwa
mojawapo ya matokeo ya uamsho mahali ni watu wengi kuokoka!
Lakini sehemu nyingi watu wanapookoka
wanapata upinzani mkubwa au kutoka kwa ndugu zao au kutoka kwa rafiki zao, au
kutoka kwa watu wanaosali nao, au kutoka kwa watu aliokuwa akisali nao kabla ya
kuokoka; au kutoka kwa viongozi wa serikali, au kutoka kwa viongozi wa kazini
kwake.
Kosa lake wanaloliona ni kwa sababu
ameokoka-hilo tu. Je! kuokoka ni dhambi? Hebu soma habari hizi:“Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza
kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea
Kuhani Mkuu, akataka ampe barua za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi,
ili akiona watu wa Njia hii (wale waliookoka), waume kwa wake awafunge na
kuwaleta Yerusalemu’’(Matendo 9:1,2).
Hawa watu walikuwa wanauawa, wanateswa
na kufungwa kwa sababu wameokoka – hilo tu! Kwa sababu wameokoka! Hata hivi leo
kuna waliookoka ambao wamezungukwa na upinzani kwa sababu tu wameokoka! Je!
kuokoka ni dhambi? Je! kuokoka ni kosa?
Lakini Yesu alijua ……..
Pamoja
na kwamba upinzani wa namna hii ulikuwepo na upo hata sasa – Yesu Kristo alijua
ya kuwa utakuwepo na kwamba tutakumbana nao katika maisha haya.
Katika
mwezi ujao nitakufundisha kile ambacho Biblia inasema tufanye tunapokumbana na
upinzani kama tulivyoona katika mwezi huu.
Yesu alijua ya kuwa tutakutana na upinzani katika dunia hii kwa hiyo -usiogope!
UPINZANI
UNAPOTOKEA KUPINGA UAMSHO NA WOKOVU,
BIBLIA INAKUSHAURI UFANYE NINI?
BIBLIA INAKUSHAURI UFANYE NINI?
Katika majibu ya maswali yaliyopita tuliona ya kuwa
Uamsho wa kweli ni kazi ya Roho Mtakatifu katikati ya Kanisa. Pia, tuliona yale
yanayotokea Uamsho unapokuwepo mahali. Kitu kimoja-wapo kilicho dhahiri ni
kwamba palipo na uamsho pana upinzani pia.
Mara nyingi upinzani unaotokea unakuwa katika
maeneo ya kupinga uamsho, kupinga wokovu, kupinga mafundisho ya kweli, kupinga
miujiza ya kweli ya Mungu inayotokea na pia, kuwapinga watumishi wa Mungu
wanaotumiwa na Mungu katika uamsho.
Katika jibu la swali la mwezi huu ningependa
nikuwekee mistari mbalimbali kutoka katika Biblia inayotushauri tuwe tunafanya
nini unapotokea upinzani dhidi ya uamsho.
Ni vizuri kujua ya kuwa si kila mtu anakubaliana na
mambo ya uamsho, pia si kila dhehebu la kikrsto linakubaliana na uamsho wa Roho
Mtakatifu. Kwa hiyo ni vizuri ujiandae na ujue cha kufanya unapokutana na
upinzani.
Unaposongwa na upinzani Biblia inakushauri ufanye
yafuatayo:
1.
FURAHI WALA USIKASIRIKE!
(Mathayo 5:11,12; I Petro 4:12-16):
"Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi, na kuwanenea kila neno baya kwa
uongo, kwa ajili (ya Yesu) yangu. Furahini na kushangilia; kwa kuwa thawabu
yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla
yenu’’.
‘’Wapenzi,
msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama
moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama
mnavyoshiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake
mfurahi kwa shangwe. Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa
kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. Maana mtu wa kwenu asiteswe kama
mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama
mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. Lakini ikiwa kwa sababu ni
Mkristo (au ikiwa kwa sababu ameokoka) asione haya, bali amtukuze Mungu katika
jina hilo ”.
2.
BARIKI
WALA USILAANI! (Warumi 12:14; Luka 6:28, I kor 4:12,13)
"Wabariki
wanaowaudhi, barikini, wala msilaani pia, wabarikieni wale ambao wawalaani
ninyi’’.
Mtume Paulo akiwaandikia Wakorintho jinsi wao walivyofanya anasema;
“tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twastahimili; tukisingiziwa twasihi’’.
Na wewe fanya kama Mtume Paulo ukitukanwa kwa
sababu ya kuokoka bariki, ukiudhiwa kwa sababu ya wokovu stahimili au vumilia,
ukisingiziwa uongo, jifunze kujibu kwa hekima!
3. TENDA WEMA
USILIPIZE KISASI! (Warumi 12:17,18; Waebrania 12:14,15; Warumi
12:19-21; Luka 6:27
"Msilipe mtu
ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni
pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana
mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya
Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi
wakatiwa unajisi kwa hilo’’.
‘’Wapenzi, msijilipize kisasi,
bali ipisheni ghadhabu ya Mungu(mwachie Mungu jambo hilo linalokuletea hasira);
maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi, mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini,
adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo,
utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya
kwa wema’’.
‘’lakini nawaambia ninyi
mnaosikia wependeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi.’’
4. WAOMBEE
WANAOWAUDHI! Luka 6:28b;
Mathayo 5:43-45, Mathayo 26:41)
‘’Waombeeni
wale ambao wawaonea ninyi’’. ‘’Mmesikia kwamba menenwa, umpende jirani yako, na
umchukie adui yako, lakini mimi (Yesu) awaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni
wanaowaudhi; ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye
huwaangazia jua lake
waovu na wema,
huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki’’.
“ Kesheni,
mwombe, msije mkaingia majaribu; roho ii radhi, lakini mwili ni dhaifu’’.
5. USIKATISHWE
TAMAA ENDELEA KUFANYA ANALOKUAMBIA MUNGU KATIKA UTII NA HEKIMA! (Warumi
16:17-19)
‘’Ndugu zangu,
nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha
mafundisho mliyojifunza (ya kweli); mkajiepushe nao. Kwa sababu walio hivyo
hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya
kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu. Maana utii wenu umewafikilia
watu wote… lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga
katika mambo mabaya. Naye Mungu wa amani atamseta shetani chini ya miguu yenu
upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi’’.
6. WASHIRIKISHE
WATEULE WENZAKO WAKUOMBEE KATIKA UPINZANI UNAOKUZUNGUKA! (Warumi 15:30-32).
Ndivyo Mtume Paulo alivyofanya alipowaandikia wateule wenzake aliposema;
‘’Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa
Roho jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu;
kwamba niokolewe na wale wasioamini katika Uyahudi, na tena huduma yangu niliyo
nayo huko Yerusalemu ikubalike kwa watakatifu; nipate kufika kwenu kwa furaha
kama apendavyo Mungu, nikapate kupumzika pamoja nanyi’’.
Yamkini Mungu atajibu maombi ya wateule hao wakiomba kwa imani na kwa bidii juu
yako. Kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 12 kinatueleza jinsi ambavyo Mtume
Petro alipokumbwa na upinzani hata akafungwa-lakini (Kanisa) wenzake
waliokoka waliomba kwa juhudi kwa ajili yake na Mungu akamfungua toka gerezani.
7.
JIEPUSHE
NA MABISHANO!
(Tito
3:9; Wakolosai 4:5)
Mara nyingi upinzani wa wokovu na mambo ya uamsho unapotokea-kunatokea pia
maswali na mabishano yasiyokuwa na msingi wala maana yoyote. Wengi bila kujua
wamejikuta wameingia katika majibizano na mabishano juu ya wokovu na neno la
Mungu. Biblia inasema hivi:
‘’Lakini maswali ya upuuzi ujiepushe nayo, na
nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria (Neno la Mungu). Kwa kuwa hayana
faida, tena hayana maana’’ enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu
yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu
kila mtu’’.
8.
USIKATE
TAMAA, VUMILIA MPAKA MWISHO! (I Petro 3:13-17; Mathayo 24:13)
‘’Naye ni nani
atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema? Lakini mjapoteswa kwa sababu ya
haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo
Bwana mioyoni mwenu. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za
tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu’’.
Nanyi mwe na
dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale
wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo. Maana ni afadhali kuteswa kwa
kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya’’.
‘’lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka’’.
9.
USIONE
HAYA- SONGA MBELE KATIKA WOKOVU (Waebrania 12:1-3; I Petro
4:15,16)
‘’Basi na sisi
pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke
kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa
saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, mwenye
kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa
mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume
wa kiti cha enzi cha Mungu’’. ‘’Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au
mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu
ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. Lakini ikiwa kwa sababu ni mkristo
(au ameokoka) asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo ’’.
10. USIJIULIZE
– ULIZE UTAKACHOJIBU!
(Marko 13:9, 11)
‘’Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa;; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili (ya Yesu), kuwa ushuhuda kwao …. Na watakapowachukuwa ninyi, na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakavyosema, lakini lolote mtakalopewa saa ile, lesemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu’’.
11.
MUWE
NA KIASI NA KUKESHA!
(I
Petro 5:8-9; Yakobo 1:2-4; Yakobo 4:7; I Petro 5:10)
‘’Mwe na kiasi
na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama
simba angurumaye, huzunguka – zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni
huyo, mkiwa thabiti katika imani…’’ ‘’Ndugu zangu, hesabuni yakuwa ni furaha
tupu, mkiangikia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa
imani yenu huleta saburi (uvumilivu). Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate
kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno’’. ‘’Basi mtiini Mungu.
Mpingeni shetani, naye atawakimbia’’.
“ Na Mungu wa
neema yote aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo,
mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na
kuwathibitisha, na kuwatia nguvu’’
BIBLIA INAWASHAURI NINI VIONGOZI WA
KANISA
WALIOKO MAHALI PALIPO NA UAMSHO?
WALIOKO MAHALI PALIPO NA UAMSHO?
Tuliona katika mfululizo wa kujibu maswali miezi iliyopita ya kuwa uamsho
unapotokea mahali fulani mambo yafuatayo hutokea:
1.
Hofu ya Mungu
2.
Watu wengi wanaokoka
3.
Umoja unaimarishwa
4.
Upinzani
Viongozi wa Kanisa waliopo katika maeneo yaliyo na uamsho wana mtihani mkubwa
wakati huo. Biblia ina mambo mengi ya kuwashauri yanayoweza kuwasaidia katika
kuongoza makundi ya kondoo wa Mungu ambao wako chini yao . Biblia inashauri viongozi wa Kanisa
uamsho unapotokea, mambo yafuatayo:
1.
WASIMZIMISHE ROHO BALI WAPIME MAMBO YOTE!
(1Thesalonike 5:19 – 22; 1 Timotheo 4:1; 1Yohana 4:1)
Kuna
hatari ya kiongozi kukubaliana na kila kitu kinachosemwa na kinachotokea
katikati ya uamsho. Pia, si vizuri kwa kiongozi kukataa na kupinga kila kitu
kinachotokea katikati ya uamsho. Ndiyo maana Biblia inawashauri hivi viongozi:
“Msimzimishe Roho; msitweze (msizuie) Unabii; jaribuni (pimeni) mambo yote;
lishikeni lililo jema; jitengeni na ubaya wa kila namna”.
Kila
wakati unaposikia au kuona jambo likitokea katikati ya uamsho jiulize ikiwa
liko sawa na neno la Mungu katika Biblia; Imeandikwa hivi; “wapenzi
msiiamini kila roho, bali zijaribuni (zipimeni) hizo roho, kwamba zimetokana na
Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.” Pia “Roho
anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani,
wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”
Uwe mwangalifu – Biblia haisemi mambo ambayo hayawezi kutokea – ndiyo maana
inasema “zijaribuni hizo roho”
2. MAMBO YOTE
YAFANYIKE KWA UTARATIBU! (1Wakorintho 14:39,40,33)
Uamsho si chanzo cha machafuko makanisani, bali ni makusudi ya Mungu kuwa
uamsho ulete umoja zaidi kati ya watu wa Mungu.
“Kwa
ajili ya hayo, ndugu, takeni sana
kuhutubu, wala msizuie kunena kwa lugha. Lakini mambo yote na yatendeke kwa
uzuri na kwa utaratibu. Kwa maana Mungu si Mungu wa machufuko, bali wa amani,
vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya
watakatifu.”
3. WASIKILIZE
KILE ROHO MTAKATIFU ANACHOSEMA! (Waebrania 2:1 – 4; Ufunuo 2:29; Warumi 10:17)
“Kwahiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije
tukayakosa kwa maana, ikiwa lile Neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na
kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki, sisi je! tutapataje kupona, tusipojali
wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu
na wale waliosikia?” (Waebrania 2:1)
“ Mungu naye akishuhudia
pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya
Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.”
Kwa hiyo “ Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia
makanisa”. (Ufunuo wa Yohana 2:29)
Hii ina maana ya kuwa kiongozi
inampasa kuwa mtu wa maombi sana ,
na mwenye kulisoma neno la Mungu, na kulijua, na kulitumia katika hekima yote,
kwa sababu ‘kusikia huja kwa Neno la Kristo’.
(Warumi 10:17)
4.
WASIWE
WATAZAMAJI TU, WALA WATAWALA TU KATIKA MAMBO YA UAMSHO, BALI
WAWE WASHIRIKI NA VIONGOZI! (1Wakorintho 11:1; 1Timotheo 4:12b, 15, 16; Matendo
ya Mitume 20:28 – 31)
Ndiyo maana Mtume Paulo aliwaambia
Wakristo waliokuwa Korintho hivi; “ Mnifuate mimi kama
mimi ninavyomfuata Kristo”
Mtume Paulo alipomwandikia Timotheo
alisema mambo haya ambayo yanaweza kukusaidia hata wewe katika nafasi uliyonayo
ya uongozi
“Uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. Uyatafakari hayo; ukae katika hayo, ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote, jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.”
“Uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. Uyatafakari hayo; ukae katika hayo, ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote, jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.”
Mtume Paulo alipokuwa anawaaga wazee
wa kanisa pale Efeso alisema maneno yanayoweza kuwa msaada mkubwa katika nafasi
yako ya uongozi, aliposema
“Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha Kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.“Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi”.
“Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha Kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.“Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi”.
5. MAMBO YOTE
YATENDEKE KWA KUSUDI LA KUJENGA! (1Wakorintho 14:26)
Si mpango wa Mungu ya kwamba Roho
Mtakatifu anapoleta uamsho mahali – Kanisa limeguke na kuharibika, la hasha! Bali kusudi kubwa la uamsho ni kuliimarisha na kulijenga
kanisa.
Ndiyo sababu kiongozi katikati ya
uamsho ni muhimu sana
ayashike na kuyafuata maneno haya: “Basi, ndugu, imekuaje? Mkutanapo pamoja,
kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo
yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga”.
6. WAJIFUNZE
KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WENGINE WA KANISA! (Matendo ya Mitume 15:1 – 35)
Biblia inatuambia wazi ya kuwa Paulo na Barnaba walikutana na Wayahudi
waliookoka wakifundisha wakisema; “Msipotahiriwa kama desturi ya Musa
hamwezi kuokoka.”
Katika mashindano na mahojiano
yaliyotokea ilibidi “Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande
Yerusalemu kwa Mitume na wazee kwa habari ya swali hilo ”
Ukiendelea kuisoma habari hii utaona
jinsi tatizo hili lilivyotatuliwa. Ni muhimu hata sasa viongozi wa Kanisa
kushauriana na viongozi wenzao kwa kadri Roho Mtakatifu atakavyowaongoza
wanapokutana na mambo yanayowasumbua katika maombi ya uamsho.
Lakini ni vizuri kufahamu ya kuwa
ushauri mzuri ni ule unaosimama katika Neno la Kristo, na siyo katika mapokeo
ya dini kama Wayahudi walivyokuwa wanafundisha kama
tunavyosoma katika Kitabu cha matendo ya Mitume 15:1,2.
7. WAWE WAOMBAJI!
(Mathayo 26:40b, 41; Matendo ya Mitume 29:28 – 31)
Yesu anasema hivi:
“Je!
hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni
dhaifu”.
Paulo anasema hivi: “Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote
nalo ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate
kulilisha kanisa lake
Mungu alilolinunua kwa
damu yake mwenyewe. Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu
wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe
watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao. Kwa hiyo, KESHENI mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu usiku na
mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi”
8.
WAWE WA MASIMAMO! (Wagalatia 2:11 – 14)
Petro alikuwa mwanafunzi wa Yesu kati
ya wale wanafunzi wa kwanza, tena alikuwa kiongozi wa kiroho katika Kanisa lile
la kwanza.
Lakini ukisoma Wagalatia 2:11 – 14
utaona ya kuwa kuna wakati alionyesha hali ya kutokuwa na msimamo hasa mahali
pale ambapo Wayahudi waliookoka walipokutana na wale waliookoka wasio Wayahudi.
Mtume Paulo anaandika anasema; “Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana
naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu ….”.
Ni vizuri viongozi popote palipo na
Uamsho, wawe na msimamo unaokwenda sawa na Injili ya Kristo na Neno lake.
Wasiwe na misimamo yenye lengo la kuwafurahisha wanadamu – isipokuwa wawe na
misimamo ya kumfurahisha Mungu kwa kusimamia Neno la Mungu bila kuchanganya na
mapokeo ya dini.
(By
mwl C. Mwakasege)
No comments:
Post a Comment