Friday, February 26, 2016

SOMO: UKOMBOZI WA ARDHI /NGUVU INAYOTEMBEA NA MAJINA (Mwl Melechzedech Shalua na Rachel Peter)

SOMO: UKO MAHALI SAHIHI AMBAPO MUNGU AMEKUSUDIA?/UKOMBOZI WA ARDHI

(Somo limefundishwa na Mwl Melechzedeck Shalua – Huduma ya MANA Mwanza)

SEMINA YA NENO LA MUNGU YA SIKU TATU (TAR 05-07/02/2016) KATIKA UKUMBI WA KWIDEKO – NGUDU KWIMBA. IMEANDALIWA NA NURU FELLOWSHIP NA UZIMA WA MILELE INTERNATIONAL MINISTRIES KWA KUSHIRIKIANA NA HUDUMA YA MANA MKOA WA MWANZA.

SIKU YA PILI TAREHE 06/FEBRUARI/2016

3Yohana 1:2“Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.”

MAMBO YANAYOFANYA WATU WASIFANIKIWE KWA VIWANGO MUNGU ALIVYO WAKUSUDIA
                          
Kuna mambo mbalimbali katika maisha ambayo yanawafanya walio wengi wasiweze kufanikiwa kwa viwango ambavyo Mungu aliwakusudia wafanikiwe. Biblia inatoa mifano ya watumishi wa Mungu ambao asili yao, majina yao, mazingira yao, n.k yalikuwa kikwazo katika utumishi wao.

MFANO : MTUMISHI WA MUNGU MUSA

JINA
Kutoka 2:1-10“1 Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaondoka akaoa binti mmoja wa Lawi.
 2 Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu. 3 Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto. 4 Umbu lake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata. 5 Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kisafina katika majani, akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta. 6 Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania. 7 Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu? 8 Binti Farao akamwambia, Haya! Enenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto. 9 Binti Farao akamwambia, Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee, nami nitakupa mshahara wako. Yule mwanamke akamtwaa mtoto, akamnyonyesha. 10 Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe. Akamwita jina lake Musa, akasema, Ni kwa sababu nalimtoa majini.”
Jina la Musa halikutokana na majina ya kiebrania bali lilitokana na kutolewa kwenye maji na hii ikamafanya akatengeneza tabia ya jina hilo
Hivyo asili ya Musa amefungamanishwa na maji, yaani roho za majini (Tabia ya kuziba nafasi wazi/kuwakilisha)

Kutoka 3:1-14“1 Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu. 2 Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. 3 Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei. 4 Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa. 5 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu. 6 Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu. 7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; 8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. 9 Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa. 10 Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri. 11 Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe wana wa Israeli watoke Misri? 12 Akasema, Bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe; na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii; utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu. 13 Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n'nani? Niwaambie nini? 14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu.”

Ø  Uwepo wa Musa kwa wana wa Israel unawakilisha uwepo wa Mungu, maana yake ni kwamba uwepo wa Musa ulionesha uwepo wa Mungu wa Musa.

Kutoka 32:1-4“1 Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata. 2 Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee. 3 Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni. 4 Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.”

Ø  Kwa kuondoka kwa Musa kwenda mlimani kuomba, uwepo wa Mungu wa Musa uliondoka katikakati ya wana wa Israeli ndio maana wakatengeneza mungu mwingine.
Walizivunja pete za dhahabu za masikio yao ili kuondosha usikivu kwa Mungu wa Musa na kuweka kwa mungu mpya (ndama wa dhahabu)
Hivyo jina la Musa liilibeba uwakilishi wa yule (MUNGU) aliyemtuma. Katika utumishi unapaswa kutafakali jina lako linabeba ujumbe gani katika kulitimiza kusudi la Mungu.

TABIA

i.                     Tabia ya upole
Hesabu 12:3”Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.”
Mungu alimuona Musa kuwa mtu mpole kuliko watu wote wa wakati wake. Japo asili ya Musa haikuwa upole kutokana na msingi wa uzao wake wa Lawi ambao walikuwa wakali na wenye hasira.

ii.                 Tabia ya ukali
Kutoka 32:19, 26-28“19 Hata alipoyakaribia marago akaiona ile ndama, na ile michezo. Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima 26 ndipo Musa akasimama katika mlango wa marago, akasema, Mtu awaye yote aliye upande wa Bwana, na aje kwangu. Wana wa Lawi wote wakamkusanyikia 27 Akawaambia, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake. 28 Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa, wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu.”

iii.                 Tabia kutoka kuzaliwa na kulelewa kwa Musa
Kutoka 2:1-2“1 Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaondoka akaoa binti mmoja wa Lawi. 2 Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu.”

Ø  Ukoo wa Musa ulitokana na Lawi ambao Yakobo baba yao anasema walikuwa wakali na hasira

Mwanzo 49:1-7“1 Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. 2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu. 3 Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. 4 Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu. 5 Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri. 6 Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe; 7 Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.”

Ø  Asili ya ukoo wa Musa ni ukali na hasira
 (Mwanzo 34:7-27“7 Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno lisilojuzu kutendeka…………..25 Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina, wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua waume wote. 26 Wakawaua Hamori, na Shekemu mwanawe, kwa makali ya upanga, wakamtwaa Dina katika nyumba ya Shekemu, wakatoka. 27 Wana wa Yakobo wakawajilia hao waliouawa, wakauteka nyara mji kwa sababu wamemharibu umbu lao.”)

Ø  Hasira yao (Lawi) ilikuwa imefungwa kwenye laana
(Mwanzo 49:7“Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.”)na laana hiyo ilimfuatilia Musa katika utumishi wake (Kutoka 32:19-20), naye aliendelea kuua (Kutoka 32:25-29)

Ø  Hasira ilipoteza tumaini la utumishi wa Musa hadi Musa akatamani kufa
(Hesabu 11:8-15“9 Umande ulipoyaangukia marago wakati wa usiku, hiyo mana ilianguka pamoja nao. 10 Basi Musa akawasikia watu wakilia katika jamaa zao zote, kila mtu mlangoni pa hema yake; na hasira za Bwana zikawaka sana; Musa naye akakasirika. 11 Musa akamwambia Bwana, Mbona umenitenda uovu mimi mtumishi wako? Kwa nini sikupata neema machoni pako, hata ukanitwika mzigo wa watu hawa wote juu yangu? 12 Je! Ni mimi niliyewatungisha mimba watu hawa wote je! Ni mimi niliyewazaa, hata ikawa wewe kuniambia, Haya, wachukue kifuani mwako, mfano wa baba mwenye kulea achukuavyo mtoto anyonyaye, uende nao mpaka nchi uliyowaapia baba zao? 13 Nipate wapi nyama ya kuwapa watu hawa wote? Kwani wanililia, wakisema Tupe nyama, tupate kula. 14 Mimi siwezi kuwachukua watu hawa wote peke yangu, kwa kuwa ni mzigo mzito sana wa kunishinda. 15 Na kama ukinitenda hivi, nakuomba uniulie mbali, kwamba nimepata fadhili mbele ya macho yako; nami nisiyaone haya mashaka yangu.”)

Ø  Musa anakasirika na kukosea maelekezo ya Mungu na kupiga mwamba mara mbili, hasira hiyo inampelekea Musa kukosa kufika katika nchi ya ahadi
(Hesabu 20:2-12“2 Na hapo hapakuwa na maji kwa ule mkutano; wakajikusanya juu ya Musa na juu ya Haruni…………………….. 7 Bwana akasema na Musa, akinena, 8 Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao. ……………. 11 Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia. 12 Bwana akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa.”)




SIKU YA PILI – SEHEMU YA PILI
MAJINA – By MAMA KITULO (RACHEL PETER)

Ø  Ibrahim (Baba wa Mataifa)
Mwanzo 17:1-6 “1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. 2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana. 3 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema, 4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, 5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.”
Kuitwa Ibrahim Mungu alimaanaisha kuwa ndani ya jina hilo limebeba Baraka ya ubaba wa mataifa

Ø  Sara (Mama wa Mataifa)
Mwanzo 17:15-17“15 Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara. 16 Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake.”
Jina la Sara lina maana ya kuwa mama wa mataifa na kwake watatoka wafalme
Kurithi majina kuna madhara (Usirithi majina ovyo ovyo)

Nahumu 1:14“Tena Bwana ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asipandwe tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.”

Ø  Hivyo ni vyema kutowafuatilisha watoto majina ya miungu au majina yasiyojulikana madhabahu zake. Unapoomba Mungu akupe mtoto umuombe akupe na jina la mtoto huyo kama vile bikira Mariam alivyoambiwa na Malaika Gabrieli (Mathayo 1:23“Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.”)

1Samweli 25:3, 25“3 Na jina la mtu huyo aliitwa Nabali; na jina la mkewe aliitwa Abigaili, na huyo mwanamke alikuwa mwenye akili njema, mzuri wa uso; bali yule mwanamume alikuwa hana adabu, tena mwovu katika matendo yake; naye alikuwa wa mbari ya Kalebu. 25 Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.”

Ø  Nabali ilimaanisha upumbavu na ni kweli mtu huyu akawa ni mpumbavu sawa sawa na jina lake
Danieli 1:6-7“6 Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria. 7 Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danieli, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.”

Ø  Neno la Mungu linatuambia kwamba Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria walibadilishwa majina yao na kupewa majina sawa sawa utawala ule waliowachukua mateka
Mwanzo 1:41-45“41 Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. 42 Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake. 43 Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri. 44 Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri. 45 Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe Yusufu akaenda huko na huko katika nchi yote ya Misri.”

Ø  Yusufu anapewa jina kuendana na miungu ya Misri ili atawale Misri na wakamuoza binti wa kuhani, yaani Yusufu aliungamanishwa na na miungu ya Misri

Isaya 26:13-14“13 Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako. 14 Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.”
Kupitia jina unaweza kuendelea kumilikiwa na waliokufa, yaani unaelekezwa na kusukumwa (na nguvu ya kiroho) kuishi maisha ya mwenye jina japo alikwisha kufa





SIKU YA PILI – SEHEMU YA TATU
UKOMBOZI WA ARDHI – Mwl Melechzedech Shalua

Ø  Katika kitabu cha Mwanzo tunaona kuwa ardhi inalaaniwa kwaajili ya Adamu
Mwanzo 3:17-19“17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; 19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”

Ø  Ardhi inaposemeshwa kwa habari za mtu Fulani au kitu Fulani inaweza kutunza kumbukumbu za maisha yako
Yeremia 22:29-30“29 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana. 30 Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.”

Ø  Ardhi inaandika na kutoa taarifa juu yako
Yeremia 17:13”Ee Bwana, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha Bwana, kisima cha maji yaliyo hai.”

Ø  Ardhi inaweza kuolewa na miungu mingine
Isaya 62:4“Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula;kwa kuwa Bwana anakufurahia ,na nchi yako itaolewa.”

Ø  Unaweza kutumia njia panda kuongelesha watu wa eneo husika
Ezekiel 21:18-24“18 Neno la Bwana likanijia tena, kusema, 19 Tena, mwanadamu, ujiwekee njia mbili, upanga wa mfalme wa Babeli upate kuja; hizo mbili zitatoka katika nchi moja; ukaandike mahali, upaandike penye kichwa cha njia iendayo mjini. 20 Utaagiza njia, upanga upate kufikilia Raba wa wana wa Amoni, na kufikilia Yuda katika Yerusalemu, wenye maboma. 21 Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huko na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini. 22 Katika mkono wake wa kuume alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome. 23 Jambo hili litakuwa kwao kama uganga wa ubatili, mbele ya macho yao waliowaapia viapo lakini ataufanya uovu ukumbukwe, ili kwamba wakamatwe. 24 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa mmeufanya uovu wenu ukumbukwe, kwa maana makosa yenu yamefunuliwa, hata dhambi zenu zikaonekana kwa matendo yenu; kwa sababu mmekumbukwa, mtakamatwa kwa mkono.”


Kwa habari ya nyayo katika ardhi
Zaburi 56:5-6“5 Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya. 6 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa wameniotea nafsi yangu.”

-          Wachawi hutumia nyayo za watu kuwaloga
-          Mipango yote unayoipanga inaweza kuharibiwa na wachawi kupitia nyayo zako
-       Kwa mtu uliyeokoka unapaswa kuombea nyayo zako ili kila unapokanyaga unaaachilia moto wa Mungu

Ayubu 13:27“Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyaaua mapito yangu yote; Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu;”

-      Mikatale ni kitu kinachofunga, watu wanaweza kuzichukua nyayo zako na kuzifunga ili wewe usifanikiwe
-          Mapito yako yote wanayaua na mipango yako ya mafanikio inateketea kabisa
-          Wanaandika na kusemesha nyayo za miguu yako ili usifanikiwe
 Ayubu 33:11“Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza.”

-         Kupitia ardhi ambapo ndipo zinpokanyaga nyayo, shetani anafunga watu na mafanikio yao yote.

No comments: