Friday, February 26, 2016

UKO MAHALI SAHIHI AMBAPO MUNGU AMEKUSUDIA? (Mwl Melechzedech Shalua)

SOMO: UKO MAHALI SAHIHI AMBAPO MUNGU AMEKUSUDIA?/UKOMBOZI WA ARDHI

(Somo limefundishwa na Mwl Melechzedeck Shalua – Huduma ya MANA Mwanza)

SEMINA YA NENO LA MUNGU YA SIKU TATU (TAR 05-07/02/2016) KATIKA UKUMBI WA KWIDEKO – NGUDU KWIMBA. IMEANDALIWA NA NURU FELLOWSHIP NA UZIMA WA MILELE INTERNATIONAL MINISTRIES KWA KUSHIRIKIANA NA HUDUMA YA MANA MKOA WA MWANZA.

SIKU YA KWANZA TAREHE 05/FEBRUARI/2016

UKO MAHALI SAHIHI AMBAKO MUNGU AMEKUKUSUDIA KUWA ?

3Yohana 1:2“Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.”

Isaya 1:18-20“18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. 19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; 20 bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.”

Zab 16:3“Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.”
Umeokoka ndiyo,  unamtumikia Mungu, na unasoma Neno la Mungu na mafanikio yote yaliyoandikwa ndani ya biblia. Swali; Je, Kwanini hauli mema ya nchi?

Ø Kwakweli kila aliyeamua kumfuata Yesu anaamini kuwa ndani ya Yesu kuna mafanikio ya kiroho na kimwili na huu ni ukweli. Ingawa sijui kama tunafaidi Baraka ambazo Mungu ameziweka kwaajili yetu, maana pamoja na ahadi nyingi za Baraka hatujawa sehemu ya mafanikio hayo.

Luka 11:5-13“5 Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu, 6 kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake; 7 na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe? 8 Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake. 9 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. 10 Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. 11 Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka? 12 Au akimwomba yai, atampa nge? 13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”

Ø  Kuna wakati hatutapewa mahitaji yetu kwasababu ya urafiki wetu na Yesu, bali kwa vile usivyoacha kuomba. Kuomba na kutafuta ni vitu viwili tofauti, Kutafuta ni kujua kanuni, taratibu na sheria za Mungu unazopaswa kufuata ili ukutane na Mungu, Bisheni maana yake ni “Zungumza na Mungu mara kwa mara”

Rumi 8:12-17 “12 Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, 13 kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. 14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. 15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. 16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.”

Ø  Wakati mwingine unaingia kuomba na unaona kabisa Mungu hajajibu maombi yako na kama kajibu ni kwa kiwango kidogo, Kwanini hajajibu? Tatizo ni kwangu au kwa Mungu?

Rum 7:14-25 “14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. 15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. 16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. 17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu 18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. 19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. 20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 21 Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. 22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, 23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. 24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? 25 Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.”

Ø  Ndani ya mtu mmoja kuna sheria mbili zinatawala, Mwili umefungiwa sheria ambayo inatuzuia kumtafuta Mungu, sheria ya mwili imeweka kizuizi ambacho hakuna unavyoweza kutenda sawa sawa na mapenzi ya Mungu. Kuna mikataba/maagano yaliyofungwa katika maisha yako yanayokuzuia kutenda sawa na mapenzi ya Mungu. Tazama maisha ya ndugu zako yanafanana na yako (wewe uliye okoka) na wengine ni wapagani wanakuzidi.

Zaburi 11:1-3“1 Bwana ndiye niliyemkimbilia. Mbona mnaiambia nafsi yangu, Kimbia kama ndege mlimani kwenu? 2 Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo. 3 Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?”

Ø  Msingi wa maisha yako umejengwaje? (Vizuri au Vibaya)
Yeremia 1:4-9“4 Neno la Bwana lilinijia, kusema, 5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. 6 Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto. 7 Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. 8 Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana. 9 Ndipo Bwana akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;”

Uchafu wa kwanza ambao ungemzuia Yeremia kutumika ulikuwa tumboni, Msingi wa Yeremia ungeweza kuharibika tangu tumboni. Kuna misingi ambayo ingemzuia Yeremia maombi yake yasijibiwe ambayo imetokea tangu tumboni.

Zaburi 51:1-5“1 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. 2 Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. 3 Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. 4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu. 5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.”

Daudi anaamua kuomba toba baada ya kuona kuna mlango unaomzuia asikutane na Mungu kwa viwango vya tofauti na mlango huo ni wa misingi ya kuzaliwa kwake (Zaburi 51:5 “Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.”). Daudi aliamua kushughulikia uovu baada ya kujua kuwa kuna misingi ya uzinzi inagharimu maisha yake ya kiutumishi, alishughulikia uovu ili aweze kula mema ya nchi, yaani kufikia kiwango cha juu cha mafanikio

No comments: