SIKU
YA KWANZA (07-03-2016)
UTANGULIZI:
Isaya
61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta
niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika
moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa
kwao.”
Luka
9:11 “Na makutano walipojua walimfuata;
akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale
wenye haja ya kuponywa.”
Lengo la semina ni kushughulika
na waliovunjika moyo na wale ambao wako tayari kupona. Hata kama haujavunjika
moyo, hebu chukua mafundisho haya kama chakula cha njiani kwani mafundisho haya
sijayatoa kwasababu ninazo notisi tu bali ni kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, Mungu
atawaponya wengi kwenye hii semina.
Maana ya neno moyo linavyotumika kwenye
Biblia:
ü Moyo ni kiungo kilichoko katika
mwili kinachotumika kusukuma damu
ü Moyo imetafsiriwa kama nafsi
ü Moyo imetafsiriwa kama roho
ü Moyo ni utu wa ndani wa mtu
(Nafsi +roho)
ü Moyo ni kiini cha uhai wa kitu
Moyo uliovunjika ni wa namna
gani? Ni moyo ulioharibika au kujeruhiwa baada ya kushindwa kubeba
ilichokibeba. Moyo uliumbwa kwa ajili ya kumbeba Mungu moyoni. Mambo ambayo
moyo hauwezi kuyabeba:
1.
Moyo hauwezi kubeba hasira au uchungu kwa zaidi ya masaa 12.
Efeso
4:26 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua
lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;”
2
Korinth 7:10 “Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu
hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya
mauti.”
2.
Moyo wa mwanadamu hautakiwi kubeba dhambi
Ezekiel
18:4 “Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile
roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile
itendayo dhambi itakufa.”
3.
Moyo haukuumbiwa kubeba au kupigana vita
1
samwel 31:3-4 “3 Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya
Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga
upinde. 4 Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako,
unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga.
Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli
akautwaa upanga wake, akauangukia.”
Vita ni vya Bwana na si vya mtu.
4.
Moyo haukuumbiwa kubeba lawama
Zab
69:19-20 “19 Wewe umejua kulaumiwa kwangu, Na
kuaibika na kufedheheka kwangu, Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote. 20
Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala
hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.”
5.
Moyo haukuumbiwa njia ndefu, au kuzimia au kuchoka
Hesabu
21:4-5 “4 Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia
ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu
ya ile njia. 5 Watu wakamnung'unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku
kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana
maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.”
·
Madhara ya moyo kuvunjika
yanaweza kuonekana kwa:
- moyo wa mtu mwenyewe
- marafiki wa mtu aliyevunjika
moyo
Mithali
28:24 “Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema,
Si kosa; Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu.”
·
Kiongozi akijeruhiwa ni hatari.
Matokeo yake yataonekana nje kwa
wale anaowaongoza
Nahumu
3:18-19 “18 Wachungaji wako wanalala usingizi, Ee
mfalme wa Ashuru; watu wako wenye heshima wamepumzika; watu wako wametawanyika
juu ya milima, wala hapana mtu wa kuwakusanya. 19 Jeraha yako haipunguziki;
jeraha yako ni nzito sana; wote wasikiao habari zako wapiga makofi juu yako;
kwa maana ni nani ambaye uovu wako haukupita juu yake daima?”
Kukataliwa kunaumiza moyo sana.
·
Nchi inaweza kujeruhiwa na Jeraha
inaweza kuwa kubwa
Yere
30:4,12 “4 Na haya ndiyo maneno aliyosema Bwana,
katika habari za Israeli, na katika habari za Yuda.…… 12 Maana Bwana asema
hivi, Maumivu yako hayaponyekani, na jeraha yako ni kubwa.”
Unaweza kupona jeraha juu juu tu.
Kwa hiyo ni vizuri kuhakikisha kujua hilo jeraha limeponyeka lote au la.
Yer
6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu
tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.”
Na pia ni vizuri kujua na
kushughulikia chanzo cha jeraha, na si tu mtu alitumiwa kuleta jeraha.
Haleluyah!
Haleluya!
Leo
tunaweka msingi, kuanzia kesho tutaanza kuangalia kwa undani zaidi.
Leo
nakutangazia ya kwamba Mungu anaponya majeraha na kwenye semina hii utapona.
1 comment:
Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni mara mbili ya pesa yangu kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada ilikuwa mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma
Kwaheri Gerd Ulrich
Post a Comment