SIKU
YA PILI (07-03-2016)
Mistari ya kusimamia: Isaya 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta
niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika
moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa
kwao.” Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao
habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.”
SWALI
LA MSINGI LA KUJIULIZA NA MAJIBU YAKE:
*** IKIWA UMEUMIA MOYONI AU MOYO WAKO UMEVUNJIKA NA HUWEZI KUOMBA
UFANYE NINI?
UTANGULIZI:
Dhara
mojawapo kubwa la kuvunjika ni mtu kushindwa kuomba
Zab
77:1-4 “1 Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam,
nimpazie Mungu, naye atanisikia. 2 Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana; Mkono
wangu ulinyoshwa usiku, haukulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika. 3
Nilipotaka kumkumbuka Mungu nalifadhaika; Nilipotaka kutafakari roho yangu
ilizimia. 4 Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Naliona mashaka
nisiweze kunena.”
·
Haijalishi
mazingira uliyonayo yanakuruhusu kuomba namna gani, kama moyo umevunjika
kumbuka mtu hawezi kuomba.
·
Daudi
alikuwa anajua kabisa akiomba MUNGU anamsikia lakini nafsi yake ilikataa
kufarijiwa!
·
Mstari wa 4
anasema hata MUNGU alishika kope zake, maana yake MUNGU alimsaidia kutolala ili
aombe lakini roho yake ilizimia, nafsi yake ilifadhaika.
Dhara hili ni kubwa sana kwa watu
wengi japo wengi hawajajua limetokana na kuvunjika kwa moyo.
Dhara hili uwapata watu wowote
wale wenye mwili wa nyama, si watu fulani fulani ni watu wote na kushindwa
kujua namna ya kuvuka hapa ni ngumu kuendelea.
Biblia inasema linda sana moyo
wako kuliko vyote ulindavyo maana huko ndiko zitokazo chemchem ya uzima.
Ukiweza hili itakusaidia kuvuka hata kwa yale uliyotarajia kuja yasipokuja
utakuwa salama!
Jifunze kwa Daudi, soma Zaburi
zake utagundua na utajifunza jinsi alivyovuka kwenye eneo hili la kulinda moyo
wake na mahusiano yake na MUNGU yakazidi kustawi!
MAMBO
YA KUFANYA SASA UKIWA KATIKA MAZINGIRA HAYO YA KUVUNJIKA MOYO
1.
Usilalamike
bali isemeshe nafsi yako tumaini ulilonalo kwa MUNGU
Zab 77:2 “Siku ya taabu yangu
nalimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa usiku, haukulegea; Nafsi yangu
ilikataa kufarijika.”
Mgomvi wake mkubwa alikuwa nafsi
yake
Zab
42:3-6 “3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu
mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako. 4
Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu, Jinsi nilivyokuwa
nikienda na mkutano, Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu, Kwa sauti ya furaha na
kusifu, mkutano wa sikukuu. 5 Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika
ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso
wangu, Na Mungu wangu. 6 Nafsi yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo
nitakukumbuka, Toka nchi ya Yordani, na Mahermoni, na toka kilima cha Mizari.”
§ Udhaifu wake ulikuwa ni
kulalamika
§ Ukiona unalalamika kwenye nyanja
yoyote ile jua Umeumia au hujapona bado.
§ Malalamiko uzaa manung'uniko na
mwisho wa manung'uniko ni dhambi.
§ Jifunze kuibebesha nafsi yako
maandiko, tumaini ulilonalo kwa KRISTO YESU Kivipi?? Kwa njia ya mawazo maana
ROHO MTAKATIFU yu ndani yako anapoachilia mistari ndani yako tafakari hiyo!
§ Acha kutafakari na kuwaza
matatizo ndani yako
§ Dawa ya nafsi kugeuzwa upya kwa
NENO la BWANA
§ Kama huna NENO la kutosha ndani
yako si rahisi kumsikia MUNGU na si rahisi kupona.
§ Pia ukiona mtu anakulalamikia
ujue AMEACHA KUKUOMBEA.
§ Anayekuombea ANAKUSHAURI.
§ Kulalamika kunaongeza tatizo la
KUAMBUKIZANA!
▶MAOMBI: Toba juu ya kulalamika na
kuponywa kwa mioyo iliyovunjika na kujeruhiwa!
No comments:
Post a Comment