Monday, March 21, 2016

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE (Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam) SOMO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO NA WALIO NA HAJA YA KUPONA.

SIKU YA TATU  (08-03-2016)

MSINGI: Isaya 61:1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Maandiko haya yalitimizwa na Yesu
Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.”
Yeremiah 6:14  "Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani Amani, wala hapana amani."

ü  Mungu hataki upone juu juu tu
ü  Kuna vitu moyo wa mwanadamu haikuumbiwa kubeba.
ü  kwa mfano moyo ilipoumbwa kulikuwa hakuna dhambi. Kwa hiyo moyo haina uwezo (capacity) wa kubeba dhambi au uchungu.
ü  Moyo ikibebeshwa hivi vitu madhara yake ni moyo kuvunjika.
ü  Kwa hiyo usijibebeshe mizigo. Mpe Yesu.

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”

"Moyo" una tafsiri mbalimbali kwa Biblia;
ü  Nafsi ya mtu
ü  Kiungo cha kusukuma damu
ü  Utu wa ndani (Nafsi + Roho / in English the Inner man)
ü  Roho ya mtu
ü  Kiini cha uhai wa kitu, k.m., ndoa, nchi, taifa, etc

MAGONJWA YA MWILI YANAYOSABABISHWA NA MOYO ULIYOJERUHIWA
Yeremiah 51:52 “Kwa sababu hiyo siku zinakuja, asema Bwana, nitakapozihukumu sanamu zake; na katika nchi yake yote waliojeruhiwa wataugua.”
- Majeraha ya moyo yanasababisha magonjwa.

1.      Ubovu wa Mifupa
Zaburi 6:2-4 “2 Bwana, unifadhili, maana ninanyauka; Bwana, uniponye, mifupa yangu imefadhaika. 3 Na nafsi yangu imefadhaika sana; Na Wewe, Bwana, hata lini? 4 Bwana urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.”
Mithali 17:22, , , “Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.”
Mithali 3:5-8 “5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. 7 Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu. 8 Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.”
Mithali 14:30 “Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa.”
Wafilipi 4:6-7 “6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”
§  Si kila kitu unachokutana nacho akili inaweza kubeba.
§  Hukupewa akili uitegemee; ulipewa akili uitumie.

2.      Vidonda vya Tumbo
Mithali 26:20-22, 28 “20 Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma. 21 Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, Na kama kuni juu ya moto; Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui. 22 Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo. Nayo hushukia pande za ndani za tumbo. 28 Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.”
Ayub 34:6 “Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo; Jeraha yangu haiponyeki, nijapokuwa sina makosa.”
§  unaweza jeruhiwa kwa kusingiziwa

3.     Macho kuharibika
Zaburi 6:6-7 “6 Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza kitanda changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu. 7 Jicho langu limeharibika kwa masumbufu, Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.”

4.     Kuishiwa nguvu mwilini
Zaburi 38:5-10 “5 Jeraha zangu zinanuka, zimeoza, Kwa sababu ya upumbavu wangu. 6 Nimepindika na kuinama sana, Mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika. 7 Maana viuno vyangu vimejaa homa, Wala hamna uzima katika mwili wangu. 8 Nimedhoofika na kuchubuka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu. 9 Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako, Kuugua kwangu hakukusitirika kwako. 10 Moyo wangu unapwita-pwita, Nguvu zangu zimeniacha; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.”

5.     Ngozi ya Uso
Mithali 15:13 “Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka.”
Mithali 14:10,13 “10 Moyo huujua uchungu wa nafsi yake, Wala mgeni haishiriki furaha yake. 13 Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.
§  Wengi wanajaribu kutibu tatizo la ndani kwa nje.
§  Furaha ndani ya mwili wako inaachia vitu (hormones) vinavyofanya ngozi yako kuwa laini.
§  Hivi ni vitu Mungu alitengeneza ili kulainisha ngozi zetu.
§  Mafuta (creams, oils) ni nyongeza ya kutusaidia
§  Dhambi ilipoingia ilituharibia - inabidi tutafute msaada wa mafuta
§  Ndiyo maana ukitembea na Mungu - siku zote umri wako utakuwa mbele kuliko mwili wako (always looking younger).
§  Hakuna ubaya wa kuwa mzee - uzee lazima uje - lakini kuna hatari ya kuchakaa mapema.
§  Kufanya kazi nyingi hakuzeeshi - kanakufanya uwe imara

6.     Mapepo
Ephesians 4:26-27 “26 Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; 27 wala msimpe Ibilisi nafasi.”
Mapepo yanaweza kukuingia kama moyo wako haujapona.
§  Ukikaa na uchungu kwa muda mrefu, mapepo yanaweza tumia huo uchungu kama lango.
§  Haijalishi umekosewa namna gani. Ni hatari kurusu uchungu na hasira zikae ndani yako kwa masaa zaidi ya kumi na mawili.

§  Si kila ugonjwa chanzo chake ni majeraha au shida ya moyo. Lakini kuna magonjwa hayawezi kupona mpaka moyo upone.
§  Usiponye dalili (symptoms); Ponya ugonjwa


No comments: