SIKU
YA NNE
Mistari ya kusimamia: Isaya 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta
niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika
moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa
kwao.” Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao
habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.”
UTANGULIZI:
Maombi juu ya kufunguliwa
magonjwa yaliyosababishwa na majeraha ya moyo kujeruhiwa na kuvunjika
Wengi wamefunguliwa hakika sema
Hallelujah!!
Yer
6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu
tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.” MUNGU asingependa kukuponya
mwenye haja ya kuponywa nusunusu/kijuujuu bali anataka mtu aponywe kabisa
MOYO
ULIOVUNJIKA KUPITIA KWENYE NDOTO ULIYOOTA NA MADHARA YAKE YANAYOWEZA KUTOKEA
1.
Ndoto ni mlango wa kiroho ndani
ya mtu
Ayubu
33:14-18 “14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam,
hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya
usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; 16 Ndipo
huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, 17 Ili amwondoe
mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; 18 Yeye huizuia nafsi yake
isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.”
ü Ufungua masikio ya ndani ili
MUNGU anaposema kupitia ndoto upate kusikia
ü Ukuwezesha kugundua kuwa MUNGU
anasema nawe kwa kuthibitisha pale unapo pokea mafundisho yasiyo ya kweli ama
yale ya kweli
ü MUNGU anaweza kukusemesha juu ya
somo na mafundisho kupitia ndoto
ü Utuma ndoto katika nafsi ya mtu
ü Utumia mlango huu kusema na mtu.
2.
Si kila ndoto inatoka kwa MUNGU
Kuna vyanzo 4 vya ndoto
1.
Kutoka kwa MUNGU mwenyewe
Matendo
2:17 “Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu,
nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na
vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.”
ROHO MTAKATIFU uweza kuachilia
ndoto za MUNGU ndani ya mtu
2.
Kutoka kwa shetani
Kumb
13:1-4 “1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji
wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu
aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3
wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa
Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu,
kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu
wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni
na kushikamana naye.”
ü Usihishie tu kufurahi kwamba
ulichotabiriwa ama alichosema nabii fulani kimetimia ama kimetokea
ü La msingi angalia na fuatilia
baada ya kutokea hilo jambo je? hali yako ya kiroho imeongezeka? Iko pale pale?
ama imeshuka?
ü Kama unafundishwa ama unatabiliwa
kitu ama umeota na ukaona kimetimia lakini kimeua mahusiano yako na YESU kuwa
mwangalifu sana
ü Wakati mwingine hata kuomba kwako
kunashuka baada ya kutabiliwa kuwa makini sana maana za namna hyo hazitoki kwa
MUNGU.
3.
Uja kwa sababu ya shughuli nyingi
Muhubiri
5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli
nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.”
4.
Uja kwa sababu ya hali ya kiroho ya mahali
ulipolala
Mwanzo
28:10-17 “10 Yakobo akatoka Beer-sheba,
kwenda Harani. 11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua
lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa
chake, akalala usingizi pale pale. 12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa
juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu
wanapanda, na kushuka juu yake. 13 Na tazama, Bwana amesimama juu yake,
akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi
hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. 14 Na uzao wako utakuwa kama mavumbi
ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na
kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.
15 Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta
tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo
niliyokuambia. 16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana
yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. 17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha
kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.”
ü Waweza lala mahali ambapo pana
upako na wengi hawajui kuomba ktk maeneo hayo hata kuyaweka wakfu
ü Maana BWANA ujifunua ktk ndoto
ukilala maeneo hayo sababu ni madhabahu yake.
Ndoto
zote za uhakika zina tafsiri zake kwa hiyo usizipuuze
Daniel 2:45 “45 Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi
ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo,
na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo
yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.”
Ndoto
ilikuwa ni hakika na tafsiri yake ilikuwa thabiti
Mwz
41:1-7, 32 “1 Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima,
Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. 2 Na tazama, ng'ombe
saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. 3 Na
tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya,
wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto. 4 Kisha
hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi
Farao akaamka. 5 Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba
yalimea katika bua moja, makubwa, mema. 6 Na tazama, masuke saba membamba,
yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. 7 Kisha hayo masuke
membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka,
kumbe! Ni ndoto tu. 32 Na ndoto ya Farao kwa vile
ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu
atalitimiza upesi.”
Ayubu
33:14, 18 “14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam,
hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 18 Yeye huizuia nafsi yake
isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.”
ü MUNGU usema mara ya kwanza kama hujaelewa
ama umepuuza usema tena na tena kwa ndoto
ü Yeye ujaribu kukujibu maombi ulio
nayo shida ya mtu ni kutoelewa maana ya ndoto hizo
Ndoto
inaweza kutumika Kama mlango wa kujeruhi na kuvunja moyo wako na hali hiyo
inaweza kujitokeza kwenye maisha ya nje
MIFANO:-
I.
Kupitisha adhabu au ya MUNGU au
ya miungu
Daniel
4:4-33 “4 Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe
katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi. 5 Nikaota ndoto
iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa
changu, zikanifadhaisha……….10 Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa
hivi; naliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa
sana. 11 Mti ule ukakua, ukawa na nguvu, urefu wake ulifika mpaka mbinguni, na
kuonekana kwake mpaka mwisho wa dunia. 12 Majani yake yalikuwa mazuri, na
matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha watu wote; wanyama wa
kondeni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi
yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake. 13 Nikaona katika njozi za
kichwa changu kitandani mwangu, na tazama, mlinzi, naye ni mtakatifu, alishuka
kutoka mbinguni. 14 Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni
matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake,
wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake. 15 Walakini
kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba,
katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na
sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi; 16 moyo wake
ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba
zikapite juu yake. 17 Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa
neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala
katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye
mnyonge. 18 Mimi, Nebukadreza, nimeiona ndoto hii; na wewe, Ee Belteshaza,
eleza tafsiri yake, kwa maana wenye hekima wote wa ufalme wangu hawawezi
kunijulisha tafsiri yake; bali wewe waweza, maana roho ya miungu watakatifu
inakaa ndani yako. 19 Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa
kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza,
ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana
wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako. …….
31 Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka
mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme
huu umeondoka kwako. 32 Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako
yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng'ombe, na
nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki
katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote. 33 Saa iyo hiyo
jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu,
akala majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni,
hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha
za ndege.”
ü Adhabu aliyoipata Nebukadreza ni
kukaa na wanyama na kula majani kondeni kwa miaka 7
ü Aliona hayatimii alidharau na
kuona ni ndoto tu kwanza ameota miezi 12 iliyopita na hakuona kilichotokea
II.
Ndoto inaweza kufungua mlango wa
roho nyingine kuingia na kuharibu maisha yako
Ayubu
4:12-16 “12 Basi, nililetewa neno kwa
siri, Sikio langu likasikia manong'ono yake. 13 Katika mawazo yaliyotoka katika
maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu. 14 Hofu iliniangukia
na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote. 15 Ndipo pepo ilipita mbele ya
uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama. 16 Hiyo pepo ilisimama kimya,
nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa
kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,”
ü Hali aliyokuwa nayo ktk ndoto
ilifungua mlango na roho ya hofu ikamwingia mpaka kumtetemesha mifupa
Daniel 4:4-5 “4 Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe
katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi. 5 Nikaota ndoto
iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa
changu, zikanifadhaisha.”
ü Alikuwa hana hofu mpaka alipoota.
Ndoto ilifungua mlango roho ya hofu ikaingia ndani yake.
No comments:
Post a Comment