Monday, June 13, 2016

SEMINA YA MANA - MOROGORO Na Mwl. Chritopher Mwakasege (08-12/06/2016) SOMO:KUA KATIKA NEEMA ILI UNUFAIKE NA MSALABA (Imeandikwa na Samson&Joan Mollel, 0767 664 338 – www.uzimawamileleministries.blogspot.com)

SIKU YA TANO (12/06/2016)

Somo linaongozwa na Neno kutoka:- 2Petro 3:18 “Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.” 2Timoth 2:1 “Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.”
Kumbuka kuwa NEEMA ni jambo unalopewa bila ya kulifanyia kazi (Warumi 4:4-6 “4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. 5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki. 6 Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,” )

JINSI NEEMA NA DAMU YA YESU INAVYOWEZA KUKUPA HAKI ULIYOPOTEZA KWASABABU YA HISTORIA YA KITU ULICHOFANYA AU KILICHOFANYWA NA MTU ANAYEHUSIKA NA WEWE.

Yeremia 22:29-30 “29 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana. 30 Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.”

Kuna tofauti kati ya taifa na nchi, ukisema taifa unaongelea watu na ukisema nchi unaongelea ardhi (land/earth).

Hebu tuangalie habari ya watoto ambao wamejitahidi sana kusonga mbele lakini hata wafanye vipi hawatoki, yaani hawawezi kuvuka kile kiwango cha wazazi wao, wakijitahidi sana wanaishia palepale wazazi wao walipoishia.

Hesabu 30:2-6 “2 Mtu atakapomwekea Bwana nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake. 3 Tena mtu mke atakapomwekea Bwana nadhiri, na kufunga nafsi yake kwa kifungo, naye aketi katika nyumba ya babaye, katika ujana wake; 4 babaye naye akasikia nadhiri yake, na kile kifungo chake alichofungia nafsi yake, na babaye akamnyamazia; ndipo nadhiri zake zote zitathibitika, na kila kifungo alichofungia nafsi yake kitathibitika. 5 Lakini kama huyo babaye akimkataza siku hiyo aliyosikia; nadhiri zake ziwazo zote, wala vifungo vyake alivyoifungia nafsi yake havitathibitika; na Bwana atamsamehe, kwa kuwa babaye alimkataza. 6 Tena kama amekwisha kuolewa na mume, wakati huo wa nadhiri zake, au wa neno hilo alilolitamka kwa midomo yake pasipo kufikiri, alilojifungia;”

Inawezekana mtu alinena bila kufikiri maneno yale yakampa Mungu nafasi au yakampa shetani nafasi katika maisha yake. Yawezekana hayo yalinenwa na wazazi wake, au mababu zake na yakampa shetani nafasi katika familia yao na hali hiyo inaendela kuwatesa familia.

Waebrania 7:5, 9-10 “5 Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu. 9 Tena yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya Ibrahimu, hata Lawi apokeaye sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi; 10 kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.”

Kutokana na andiko hili; wastani wa kizazi kibiblia ni miaka 100, kutoka Ibrahim mpaka Lawi ni vizazi vine (Ibrahimu – Isaka – Yakobo – Lawi), kwahiyo sadaka aliyoitoa Ibrahimu hata kabla Isaka hajazaliwa ilitolewa mpaka na Lawi. Kama mababu zako walitoa sadaka au walifanya agano na miungu maana yake hata wewe umefanya hilo agano.

Ezekieli 21:21-23 “21 Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huko na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini. 22 Katika mkono wake wa kuume alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome. 23 Jambo hili litakuwa kwao kama uganga wa ubatili, mbele ya macho yao waliowaapia viapo lakini ataufanya uovu ukumbukwe, ili kwamba wakamatwe.”

Mfalme wa Babeli alienda kufanya uganga kwenye njia panda na sadaka aliyoitoa katika uganga huo ni maini. Sasa fikiria kwamba uganga na sadaka hiyo ulifanywa na babu yako na wewe hujui chochote na BWANA anasema ataufanya uovu ukumbukwe katika familia hiyo. Baadae kwasababu wewe hukujua habari ya kutoa sadaka walizotoa babu zako na ndugu zako unaanza kushangaa magonjwa yanaanza, kama walikuwa wakitoa sadaka za miguu ya wanyama familia inasuimbuliwa na tatizo la miguu, kama ni maini kunakuwa na tatizo la maini n.k.

Agano ni mapatano yanayomfunga mtu kwenye mahusiano (Mwanzo 17:1-2, 7, 9, 20-21 “1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. 2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana…7 Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako…….9 Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako……20 Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu. 21 Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.”)

Katika uzao wa Ibrahimu, Ishamaeli mtoto wa kijakazi alipewa Baraka nje ya agano la Mungu na Isaka alipewa Baraka ndani ya agano na Mungu, sasa kwakuwa Agano ni mapatano yanayomfunga mtu kwenye mahusiano, Isaka (Taifa la Israeli) akivunja agano lazima apate shida kwakuwa anayo mahusiano na Mungu na Mungu hawezi kukubali kirahisi rahisi mahusiano yavunjike. Lakini Ishmaeli hata akienda tofauti na maelekezo ya Mungu ataendelea kufanikiwa tu kwakuwa yuko nje ya agano.

Hii ndio maana, kama kuna mahali wazazi waliingia katika agano wakapata mali halafu watoto wakavunja agano lililowapa wazazi mali hiyo, hiyo mali inapotea yote na hata kama ni kampuni inaanguka yote.

Rumi 5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;”

Kutoka 20:5 “Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,”

Uovu ni udhaifu unaotokea unapomkataa Mungu na akaondoa uwekezaji wake katika maisha yako.

Daniel baada ya kukisoma kitabu cha Yeremia alikubali kwamba amefanya dhambi yeye na taifa lote (kimsingi yeye hakuishiriki moja kwa moja ila aliikubali kuwa nayeye ameifanya kwakuwa ilifanywa na wazee/baba wake).

Daniel 9:4-9 “4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake; 5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; 6 wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi. 7 Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa. 8 Ee Bwana, kwetu sisi kuna haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda dhambi. 9 Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi;”

Baada ya kukiri kumtenda Mungudhambi kwakuwa walifanya uasi, Danieli alimuomba Mungu awasamehe

Danieli 9:16-19 “16 Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka. 17 Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana. 18 Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi.”

Haijalishi umezaliwa jangwani/ Misri/ Babeli au umejikuta kwenye shida gani ya kifamilia iliyosababishwa na makosa/dhambi/maovu, unaweza kwenda mbele za Mungu na kuziungama dhambi zote na damu ya Yesu Kristo ikapita na kufuta yote na ukawa mtu huru.

Hata kama umefanya kazi ya Mungu chini ya kiwango unakuwa umekosa mbele za Mungu hivyo inakupasa kuomba toba kwa damu ya Yesu (Warumi 3:23-26 “23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; 25 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa. 26 apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu.”)

Waebrania 9:14-15 “14 basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? 15 Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.”

Damu ya Yesu inapoachiliwa inapita na kufungua mafaili yako yote mpaka pale bustani ya Eden na kuanza kukagua mambo yote yaliyofanyika yanayoleta shida, wakati damu ikifungua mafaili yako kwa kipindi hicho Yesu Kristo (KUHANI MKUU) anasimama kama mdhamini wakati kesi yako ikiendelea wewe unakuwa uko huru nje ya kifungo na damu inakuwakilisha (yaani damu ya Yesu inasimama kama wakili mahali pako ikenena mema juu yako).

Kuna watu wanaota ndoto kuwa wanakula chakula, kula chakula kwenye ndoto ni ishara ya agano la ukumbusho; yaani wafu wanakukumbusha kuwa walifanya agano na mizimu na wewe upo katika agano hilo. Agano ni urithi, hivyo lazima afe mtu ili agano lirithishwe kwenda kwa mtu mwingine aliye hai.

MAOMBI YA KUVUNJA MAAGANO KWAAJILI YA WATU WANAOOTA WANAKULA KWENYE NDOTO…………………….. MAOMBI YANAENDELEA………..

MAELEFU ELFU YA WATU WAMEMPOKEA YESU……. HALELUYAAA….


*****MWISHO WA SEMINA*****

No comments: