Sunday, June 12, 2016

SEMINA YA MANA - MOROGORO Na Mwl. Chritopher Mwakasege (08-12/06/2016) SOMO:KUA KATIKA NEEMA ILI UNUFAIKE NA MSALABA (Imeandikwa na Samson&Joan MolleL, 0767 664 338 – www.uzimawamileleministries.blogspot.com)

SIKU YA NNE – SEMINA YA VIJANA (ASUBUHI - MCHANA)
Ezekiel 22:30-31 “30 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. 31 Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.”
SOMO: WITO KWA KIJANA ILI MUNGU AMTUMIE KATIKA KUOMBEA NCHI
1.     Unapoitwa kuombea nchi unaitwa na Mungu ili uingizwe katika kundi maalum sana kwa Mungu. Ni kwanini Mungu atafute mtu (Ezekiel 22:30-31) wakati anaona na kumjua kila mtu? Ni kwasababu jambo analotaka ulifanye ni zito sana na sio kila mtu anaouwezo wa kulibeba
·         Kundi lingine maalum ni pale Yesu aliposema amekuja kutafuta waliopotea (Ambao sasa ndio watu waliookoka) Mathayo 15:24 “Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.”
·         Kundi lingine maalum ni wale watakaomwabu Mungu katika roho na kweli, Yohana 4:23 “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.” Kuna tofauti kati ya kumsifu na kumuabudu Mungu, Kusifu ni kueleza matendo makuu ya Mungu na kuabudu ni kumwelezea Mungu ni nani kwako.
·         Kundi lingine maalum ni watenda kazi (Luka 10:2 “Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.”). Watumishi katika nyumba ya BWANA ni wengine lakini watenda kazi ni wachache, mtenda kazi siku zote anatafuta kufanya mapenzi ya Mungu.
Isaya 59:16a “Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi…………”. Kuna watu wengi sana wanaomba kwaajili ya mahitaji yao binafsi na shida zao, lakini ni wachache sana wanaoweza kuwa na mzigo kwaajili ya nchi
Kwasababu ya kukosa mtu wa kuiombea nchi, Mungu ameipiga nchi kwa ghadhabu yake
2.     Maombi ya kuombea nchi yanayomkaribisha Mungu awe mmoja wa wawekezaji muhimu kwaajili ya maendeleo na mafanikio ya nchi husika
Matendo 17:26-28 “26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; 27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.”
Katika hali ya kawaida viongozi wan chi wanapotaka wawekezaji waje ili nchi iweze kuwa na maendeleo makubwa; lazima nchi itaingia kwenye gharama kubwa za kuweka sera za kuwavuta/kuwavutia wawekezaji ikiwa ni pamoja na kufanya matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa.
Inapofika wakati wa kumkaribisha Mungu au miungu katika uwekezaji, sio rahisi sana ukasikia peupe wakisema kama nchi kuwa wanamkaribisha Mungu/miungu kuwekeza katika nchi isipokuwa kwa nchi chache sana ambazo zimeweza kufanya hivyo kama vile Japan na baadhi ya nchi kiarabu.
Katika baadhi ya nchi kama Tanzania, kumkaribisha Mungu/miungu kama muwekezaji vipo katika viwango vya mtu mmoja mmoja na wanamkaribisha Mungu/miungu katika biashara/kazi……. Nk.
Tunasoma katika Biblia kuwa mfalme Uzia alimkaribisha Mungu kuwa muwekezaji katika uongozi wake, katika mashamba na mifugo yake na Mungu alimfanikisha sana (2Nyakati 26:1-5 “1 Na watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia, naye alikuwa mwenye miaka kumi na sita, wakamfanya awe mfalme mahali pa Amazia babaye. 2 Huyo akajenga Elathi, akaurudisha kwa Yuda, baada ya kulala mfalme pamoja na babaze. 3 Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na miwili; na jina la mamaye aliitwa Yekolia wa Yerusalemu. 4 Akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Amazia babaye. 5 Akajitia nia amtafute Mungu katika siku za Zekaria, aliyekuwa na fahamu katika maono ya Mungu; na muda alipomtafuta Bwana, Mungu alimfanikisha.”)
Yeremia 29:7-11 “7 Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa Bwana; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani. 8 Maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Manabii walio kati yenu, na wabashiri wenu, wasiwadanganye ninyi, wala msisikilize ndoto zenu, mnazootesha. 9 Kwa maana kwa jina langu hutabiri maneno ya uongo kwenu; mimi sikuwatuma, asema Bwana. 10 Maana Bwana asema hivi, Babeli utakapotimiziwa miaka sabini, nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa. 11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”
Mungu aliwapeleka wana wa Israeli mateka huko Babeli, lakini anawaambia wamkaribishe awe muwekezaji katika mji waliochukuliwa mateka ndipo watakapofanikiwa.
Tukimfanya Mungu kuwa muwekezaji katika nchi na ikatoakea shida/janga, tukimlilia Mungu kwa habari ya tatizo letu iwe ni Ukame, mafuriko, tetemeko n.k. Mungu atatuambia kama ameleta yeye au ni shetani ameleta au ni uzembe wetu, yeye Mungu atatuambia na kutupa njia sahihi ya kutatua tatizo hilo kwakuwa nay eye amewekeza kwetu.

3.     Usikubali kikwazo chochote kikuzuie katika kuukubali wito
Unapofanya kazi ya Mungu, fanya kama vile hakuna mtu mwingine anayefanya ila ni wewe peke yako, uwe mwaminifu katika eneo ulilopewa. Usiruhusu kikwazo chochote kikuzuie
        i.            Umri usiwe kikwazo
2Nyakati 26:1-5 “1 Na watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia, naye alikuwa mwenye miaka kumi na sita, wakamfanya awe mfalme mahali pa Amazia babaye. 2 Huyo akajenga Elathi, akaurudisha kwa Yuda, baada ya kulala mfalme pamoja na babaze. 3 Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na miwili; na jina la mamaye aliitwa Yekolia wa Yerusalemu. 4 Akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Amazia babaye. 5 Akajitia nia amtafute Mungu katika siku za Zekaria, aliyekuwa na fahamu katika maono ya Mungu; na muda alipomtafuta Bwana, Mungu alimfanikisha.” Yeremia 1:6 “Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.”
Uzia alikuwa na miaka 16 alipoanza kutawala na Yeremia alijiona ni mdogo sana kuifanya kazi ya Mungu, lakini Mungu anapokuletea wito anafahamu yote hayo na anajua kwamba atakufanikisha.
     ii.            Nikikubali kuomba inamaanisha sitafanya kazi nyingine?
Angalia habari ya Uzia, alikuwa mfalme na alifanya majukumu ya kifalme (kiungozi) lakini pia alikuwa ni mkulima na mfugaji, 2Nyakati 26:10 “Akajenga minara tena nyikani, akachimba mabirika mengi, maana alikuwa na ng'ombe tele; katika Shefela pia, na katika nchi tambarare; tena alikuwa na wakulima na watunza mizabibu milimani, na katika mashamba ya neema; maana yeye alipenda ukulima.” pamoja na mambo yote hayo mfalme uzia aliweza kumuomba Mungu kwa bidii  . 2Nyakati 26:4-5 “4 Akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Amazia babaye. 5 Akajitia nia amtafute Mungu katika siku za Zekaria, aliyekuwa na fahamu katika maono ya Mungu; na muda alipomtafuta Bwana, Mungu alimfanikisha.”
Fahamu kwamba maombi ya kuombea nchi hayakutoi kwenye nafasi yako au kazi yako
Angali pia habari za nabii Danieli (soma kitabu cha Daniel), aliandaliwa kwa miaka 3 ili atumike kwa Nebukadreza. Kilichomsaidia Daniel na wenzake kupata kazi iliyokuwa na changamoto nyingi ni kwasababu walikuwa wanaomba, ukisoma sura ya pili Daniel ameanza kazi alidumu katika awamu nne za uongozi yaani awamu ya mfalme Nebukadreza, Belshaza, Dario na Koreshi. Lakini Daniel alifanikiwa katika vipindi vyote hivyo kwakuwa alidumu katika kuomba.


   iii.            Mimi sijui kuomba
Watu wengi wanapoitwa na Mungu huwa na visingizio vingi, Musa alijitahidi sana kujitetea kwa visingizio vingi lakini mwisho Mungu ndiye aliyemuwezesha kuutumia wito huo. Hata kama hujui kuomba, Mungu aliyekuita yeye atakupeleka “kindergatten” ya maombi mpaka utajua kuomba, Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.”.



SIKU YA NNE (11/06/2016)
Somo linaongozwa na Neno kutoka:- 2Petro 3:18 “Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.” 2Timoth 2:1 “Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.”
Kumbuka kuwa NEEMA ni jambo unalopewa bila ya kulifanyia kazi (Warumi 4:4-6 “4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. 5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki. 6 Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,” )
Inaendelea………………..Mungu anavyotumia Damu ya Yesu kukurudishia na kukupa haki zako ulizonyimwa/zilizopotea
   iv.            Damu inampa Mungu uhalali wa kukulinda na kukupigania dhidi ya adui
Kutoka 12:21-23, 12-13 “21 Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka. 22 Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. 23 Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. 12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. 13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.”
Paska sio jina la sikukuu, pasaka ni jina la sadaka ambayo BWANA aliwaagiza wana wa Israeli wajitwalie wana-kondoo na ndio sadaka hiyo ikaitwa pasaka, Mungu naye alimtoa pasaka (sadaka) yaani Kristo 1Wakorintho 5:7 “Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;”
·         Mungu alisema nitakapoiona hiyo damu nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; pigo halikuwapata Israeli, sio kwasababu wao ni Israeli ni kwasababu ya damu na imani walioiweka katika damu ile (Waebrania 11:8 “Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.”)
·         Damu haikuenda kiujumla jumla, iliekezwa kwa kila familia na pale ilipobidi familia ziliungana
·         Kuna jambo la muda, damu iliwekewa muda wa kuifanya kazi ile (Usiku hawakuruhusiwa kutoka nje) kwahiyo damu ilibana muda
·         Damu ilibeba eneo, eneo la nyumba za wana wa Israeli ndani kulikuwa ni salama, yaani kama wangetoka nje hawangekuwa salama
Damu ya Yesu ukiitumia kwa imani inafanya ofisi ya Kuhani Mkuu (Yesu) iingie kazini. Mahali popote ambapo unataka damu ilinde au ifanye kazi lazima ulitambulishe hilo eneo katika ulimwengu wa roho, kwa lugha nyingine ni kuweka wakfu.
LEO TUTAFANYA ZOEZI KWA VITENDO, TUTAMWAGA DAMU YA DAMU YA YESU HAPA UWANJANI, BWANA YESU AMENIRUHUSU KUFANYA HILO ZOEZI NA AMENIAHIDI KWAMBA YEYE MWENYE (KUHANI MKUU) ATAINGIA KAZINI.
Yeremia 22:29-30 “29 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana. 30 Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.”
Kuna watu ambao maisha yao yamefungwa katika ardhi, hii imetokana na ibada za miungu au laana nyingine. Inawezekana umefungwa kwenye ardhi ya nyumbani kwenu na hauwezi kupiga tena hatua kwenda mbele katika maisha yako. Leo tunamwaga damu ya Yesu inayonena mema ili kuondoa uhalali wa nguvu za giza zilizokufunga katika ardhi……………………..
MAOMBI YAMEFANYIKA KWA SEHEMU KUBWA SANA LEO, WATU WAMEFUNGULIWA, MAPEPO YALIYOKAA KATIKA ARDHI NA KUWAFUNGA WATU YANAKIMBIA OVYO OVYO UWANJANI NA WATU WANAZIDI KUFUNGULIWA…………….



***KARIBU TENA SIKU YA KESHO JUMAPILI AMBAYO NI MWISHO WA SEMINA***

1 comment:

Unknown said...
This comment has been removed by a blog administrator.