Friday, August 12, 2016

KONGAMANO LA MAOMBI YA KITAIFA 2016 KUOMBEA NCHI YA TANZANIA MAHALI:CHUO KIKUU CHA DODOMA (2ND – 6TH August, 2016) Mwl. Chistopher & Diana Mwakasege Imeandikwa na Samson Mollel (www.uzimawamileleministries.com)

SIKU YA PILI.............................

KUOMBA MBINGU ZIWE WAZI KWAAJILI YA KUSIMAMISHA KUSUDI LA MUNGU KATIKA NCHI

Isaya 66:1 “Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?”

Isaya 48:12-13 “12 Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita; mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia. 13 Naam, mkono wangu umeuweka msingi wa dunia, na mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu; niziitapo husimama pamoja.”

Mbingu na nchi zina wito na Mungu anaziita husimama pamoja, na kati ya wito mmojawapo wa mbingu ni mbingu kuwa kiti cha enzi, kiti maana yake nafasi inayotumika kwaajili ya kutawala na kumiliki, kwahiyo kazi mojawapo ambayo Mungu aliamua mbingu zitumike ni kuwa kiti cha chake enzi, anapotaka kutawala dunia na vitu vyote vilivyopo chini ya mbingu anatumia mbingu kama kiti chake cha enzi. Pamoja na kuwa mbingu na nchi zina wito maalum kwa Mungu, Yakobo (Israel) ameitwa. Mungu anapomuita mtu anaita na Mbingu anaita na nchi kwa wakati mmoja, Mungu akiita nchi uwe na uhakika Mbingi zinaitika na akiita Mbingu nchi inaitika, kwahiyo ameweka mbingu na chi ili zifanye kazi kwa pamoja na kwa karibu ili kulitimiza kusudi la Mungu.

Mathayo 3:16-17 “16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; 17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.”

Marko 1:10-11 “10 Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake; 11 na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.”

Luka 3:21-22 “21 Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; 22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.”

Hawa waandishi wamendika jambo moja kwa utofauti na sio kimakosa, Roho Mtakatifu anataka tuone kuhusika kwa mbingu na maisha ya watu na maisha ya nchi. Luka 3:21-22, inazungumzia juu ya hali ya mbingu ilikuwa ngumu ilikuwa imefungwa ndio maana ametumia neno kupasuka, mbingu kumfunukia ni kwaajili yake binafsi ndio maana si kila aliyebatizwa mbingu zilimfunukia, mbingu kufunuka ni “for general purpose” kwa ujumla, maana yake zilifunuka kwaajili ya watu wengine ili kutumia kilichopo ndani yake.

Ayubu 38:33 “Je! Unazijua amri zilizoamuriwa mbingu? Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?”

Zaburi 19:1 “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.”

Zaburi 50:6 “Na mbingu zitatangaza haki yake, Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.”

Utagundua kwamba waandishi wa vitabu 3 vya injili (Mathayo, Marko na Luka) walipokuwa wanaandika habari za mbingu, Roho alishuka kiasi cha kwamba Yohana aliweza kumtambua jinsi alivyokuja na maneno yale aliyosema Baba hayakuwa kwaajili ya Yesu kwani hata kama asingesema Yesu alifahamu kuwa Baba anampenda, maneno yale yalisemwa kwaajili yetu, kuna kitu kilikuwa kinaachiliwa

Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.”
Kama tulivyojifunza kuwa mbingu ni kiti cha enzi, unaweza kuusoma mstari huu kwa jinsi hii “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya kiti cha enzi.” Kiti cha enzi ni nafasi ambayo Mungu anayo ya kutawala na kumiliki ambayo ameamua kuiweka katika mbingu ili kutawala mambo yote yaliyoko chini ya mbingu ili kutawala na kuyaratibu katika utaratibu na msingi ambao Mungu amekusudia

Matendo 17:26-28 “26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; 27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.”

Habakuki 2:1-4 “1 Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu. 2 Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. 3 Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. 4 Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.”

Kati ya vitu vilivyopo ndani ya mbingu ambavyo ni muhimu sana kuachiliwa kwaajili ya nchi na kikae sawasawa

Amri zilizoamriwa mbinguni, amri haizungumzii juu ya sheria inatokana na “ordinances” neno linalotokana na “order” yaani utaratibu; kwahiyo utaratibu wa mambo yaliyopo duniani upo kwenye mbingu, maana yake kile kilichopangiwa kwaajili yako wewe binafsi (by order) kwa utaratibu wa kimbingu kimefichwa katika mbingu. Mbingu zikifungwa juu yako huwezi kujua taratibu za Mungu kwenye maisha yako; mbingu zikifungwa juu ya nchi, nchi itakuwepo lakini haiwezi kwenda kwenye “order”, kama mbingu zimefungwa kwenye familia yako utaishi lakini sio kwa “order” au kwa hatua za Mungu, kama mbingu zimefungwa juu ya huduma yako uwe na uhakika utabahatisha, utaiga, utatafuta msaada kwa watu wengine lakini hutajua kutembea kwa ujasiri kwenye hatua za BWANA kwasababu mbingu zikifungwa, amri zilizoamriwa mbingu kwaajili vitu vilivyopo hapa hazitoki, hazionekani, hazifamiki, hazijulikani, zimefichwa kwenye mbingu. Na ndio maana ni muhimu sana hata watu waliookoka kuhakikisha kuwa Yesu ni Bwana, sio kwamba ni BWANA tu lakini ni mfalme, kwasababu ukishakubali namna hiyo unampa Mungu nafasi ya kuketi kwenye nafasi yake ya kuongoza hatua, Mungu kama amekuumba akakuleta Duniani ameshatayarisha kila hatua, suala la hatua alilokupangia kwaajili ya kufanikisha halina majadiliano; hii ni kwasababu Mungu ametupa kuchagua na majibu ya uchaguzi wetu ametupa pia kwamba kama ukichagua jambo Fulani matokeo yake ni haya na kama ukichagua jambo jingine matokeo yake ni haya, basi sasa hakuna haja ya kuchagua kwakuwa matokeo yote tayari unayo. Yaani ni sawasawa na asingekupa uchaguzi ulio mbaya na akakupa uchaguzi ulio mzuri na kakaupa na tiki. Kwa lugha nyingine hauna uchaguzi kwakuwa lile jambo sahihi tayari umepewa.

Biblia inasema “Mbingu zikamfunukia”; inamaanisha Mungu alikuwa anafungua order aliyokuwa amekusudia kwaajili ya Yesu, ndio maana Yesu ana miaka 33 lakini huoni vitu vingi vimerekodiwa, hivyo unavyoona ni baada ya mbingu kumfunukia Yesu kabla ya hapo mbingu zilikuwa zimefungwa na baada ya mbingu kumfunukia vikaandikwa maana vilikuwa kwenye order. Kabla mbingu hazijamfunukia hakujua amri zilizoamrikwa na kiti cha enzi kwaajili yake. Lakini kwasababu kuja kwa Yesu duniani kulikuwa kunafungua kurasa si kwasababu tu ya kuja kwa Yesu duniani lakini kwasababu ya watu wengine wanaotaka kuingia kwenye order kwahiyo mbingu zilifunuka “for general use”

Zaburi 16:1 “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.”
Utukufu kazi yake ni kutengeneza mazingira ya kiroho yanayoruhusu kufanya na kusimamia kusudi la Mungu katikati ya wanadamu kwa uhuru anaotaka “spiritual atmosphere”, ndio maana wale makuhani walipokuwa wanaimba kwa Mungu kuja ndani ya hekalu, walijua amekuja kwasababu utukufu ulibadilisha hali ya mazingira/hali ya uhusiano wako na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu pamoja na kwamba amekuja kwaajili ya kila mtu, utukufu wa BWANA ukifunguliwa utajua kabisa kuna upako wako binafsi na upako wa kijumla. Ndio maana haijalishi unasali kanisa gani jambo la Muhimu ni kuhakikisha mbingu zinzfunguka kwaajili yako na utamsikia Mungu akisema “Wewe ni mwangu mpendwa nimependezwa na wewe” na hakuna mtu anaweza akakunyang’anya hicho kwasabu mbingu zinaachilia haki, zinaachilia utukufu. Biblia inasema mbingu zinatangaza haki yako, huwezi kupoteza haki kwasababu Mungu ndiye mwenye kukuhesabia haki, usifikiri mazingira hayatakuwepo ya kutafuta namna ya kukunyang’anya haki yako, yatatokea mengi tu yatakusumbua lakini ukishajua kwamba mbingu zimekufunukia (sio kwamba zimefunuka tu kwa kila mtu) unajua kuna za kwako, wanaweza wakanyimwa wengine lakini wewe utapata kwasababu unajua.

Kutoka 12:2 “Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.”

Kwa miaka mia nne mbingu zilifungwa kwa wana wa Israeli, hapo ndipo mbingu zilipowafunukia wana Israeli. Unapoona watu wanaishi kama jana ni kwasababu wamepoteza saa zao, wamepoteza order ujue mbingu zimefungwa.

Mafanikio ya nchi ya Tanzania zipo kwenye mbingu zilizoamriwa kwaajili ya Tanzania, ni kazi yetu sisi kama waombaji kwenda mbele za Mungu kuomba mbingu zifunguke kwaajili ya nchi, na zikifunguka kwaajili ya nchi uwe na hakika mbingu zinawasiliana na ardhi iliyoko Tanzania na ghafla kunakuweko namabadiliko Fulani kwasababu haitaachilia tu amri, lazima ikutengenezee na mazingira ambayo itakuwa rahisi kwako kutekeleza zile amri ambazo umewekewa na Mungu.

Daniel 4:26 “Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala.”

Kazi yako, biashara, huduma, familia, kanisa litakuwa imara kwako hapo utakapojua yakuwa mbingu ndizo zinaweka order na pale utakapokubali kukaa chini ya kiti cha Mungu, ndio maana shetani akikuvuruga kwenye mbingu amekuvuruga mahali pabaya, akisababisha mbingu zikafungwa amekubania vitu vingi.

Uwe makini na mafundisho unayopokea/unayosikia kwakuwa imani huja kwa kusikia na inategemea unasikia nini. Kuna watu wengine wanazo mbingu 4 wengine 7, hao ni wale waliojaribu kushindana na kiti cha enzi cha Mungu na kila katika kila mbingu wanaweka pepo. Biblia inazungumza kuwa zipo mbingu tatu tu (2Wakorintho 12:1-51 Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana. 2 Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. 3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua); 4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene. 5 Kwa habari za mtu kama huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika habari ya udhaifu wangu.”)



No comments: