Friday, August 12, 2016

KONGAMANO LA MAOMBI YA KITAIFA 2016 KUOMBEA NCHI YA TANZANIA MAHALI:CHUO KIKUU CHA DODOMA (2ND – 6TH August, 2016) Mwl. Chistopher & Diana Mwakasege Imeandikwa na Samson Mollel (www.uzimawamileleministries.com)

SIKU YA PILI

MAENEO YA KUOMBEA YALIYO NDANI YA MBINGU ILI YASITUMIKE KUVURUGA NCHI

        i.            Mbingu kama kiti cha enzi

Isaya 66:1 “Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?”

     ii.            Hekima zilizo katika mbingu

Zaburi 136:5 “5 Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.” Ukisoma kwa tasfsiri ya kiingereza inasema “To him that by wisdom made the heavens: for his mercy endureth for ever - KJV.” Neno fahamu zake linasimama badala ya hekima, kuna hekima zilizowekwa katika mbingu

   iii.            Mbingu kama mtoa Amri

Ayubu 38:33 “Je! Unazijua amri zilizoamuriwa mbingu? Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?”

   iv.            Mbingu kama Mahakama

Daniel 7:9-10 “9 Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. 10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.”
Zaburi 50:3-6 “3 Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote. 4 Ataziita mbingu zilizo juu, Na nchi pia awahukumu watu wake. 5 Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu. 6 Na mbingu zitatangaza haki yake, Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.”

      v.            Viapo katika mbingu

Mathayo 5:33-35 “33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; 34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; 35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.”
Hesabu 30:2 “Mtu atakapomwekea Bwana nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.”

   vi.            Wito wa mbingu

Zaburi 19:1 “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.”
Utukufu maana yake ni Mungu kujidhihirisha kwa namna ambayo inajulikana katika mwili yakwamba Mungu yuko upande wako (Yohana 1:14 “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.”). Utukufu wa Mungu unaweza kupungua (Rumi 3:23 “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;”)
Fahamu kwamba shetani anapoamua kuvuruga haki yako anavuruga kwenye Mbingu

MBINGU KAMA KITI CHA ENZI

Kuna tofauti kati ya Mbinguni na mbingu. Ukisoma Mwanzo 1:1,7-8 “1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 7 Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. 8 Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.”

Isaya 66:1 “Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?”

Dhambi ilipotokea shetani alichukua umiliki wa nafasi ya kiti cha enzi alichopewa mwanadamu, ndio maana Mungu alipomuangalia Adamu baada ya anguko pale Eden hakumuona kwenye nafasi yake (Mwanzo 3:9 “Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?”)

Daniel 4:24-26 “24 tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme; 25 ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng'ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote. 26 Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala.”

Anaposoma shetani hilo Neno “baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala.” Hahitaji kwenda mbinguni ili kufunga Baraka zako, anachohitajio ni kukamata mbingu na hapo anakuwa amekumaliza kabisa.

Isaya 33:22 “Kwa maana Bwana ndiye mwamuzi wetu; Bwana ndiye mfanya sheria wetu; Bwana ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.”

Mungu kuwa mwamuzi maana yake ni kuwa Mahakama, na Mungu kuwa Mfanya sheria maana yake ni kuwa Bunge la nchi na pia kuwa Mfalme wetu maana yake ni Mungu kuwa Raisi wan chi. Maana yake ni kwamba Mungu anataka mihimili ya nchi ili aweze kumiliki. Vilevile Mungu ndiye msimamizi wa uchaguzi katika nchi (Mithali 16:33 “Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za Bwana.”)

Kama nchi ukitaka kuimarisha/kuusimamisha uchumi ni mfumo wa ufalme/utawala. Ndio maana Neno la Mungu linasema katika Mathayo 6:31-33 “31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Kwahiyo sio kumtafuta Yesu peke yake bali tafuta haki ya ufalme iliyopotea katikakti ya wanadamu (Mfumo), na uchumi wako utakuwa sawa.

Mtu akikorofisha mfumo mlinzi kutoka mbinguni (Waombaji) anaweka pingu kwenye kiti kama ilivyokuwa kwa mfalme Nebukadreza.

No comments: