Monday, March 21, 2016

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE (Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam) SOMO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO NA WALIO NA HAJA YA KUPONA.

SIKU YA TANO
Mistari ya kusimamia: Isaya 61:1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.” Yeremia 6:14 “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.”

UTANGULIZI
Maeneo manne lazima yapokee uponyaji huu ili uwe uponyaji kamilifu na si wajuu juu ni haya yafuatayo:-
ü  Moyo wenyewe
ü  Mwili wako
ü  Kile kilichosababisha moyo kuvunjika
ü  Chanzo cha chombo kilicho sababisha kujeruhi moyo

...Tunaendelea na kichwa kile cha MOYO ULIOVUNJIKA KUPITIA KWENYE NDOTO ULIOOTA NA MADHARA YAKE YANAYOWEZA KUTOKEA.

1.                 Baadhi ya ishara zitakazokuonyesha ya kuwa ndoto uliyoota unahitaji kuifuatilia
Kumbuka vyanzo ni vingi hivyo lazima kuwepo na ishara zikusaidie ipi ufutalie na kuishikilia

ISHARA HIZO NI KAMA:-

a.      Kuota ndoto hiyo hiyo zaidi ya mara moja
Mwanzo 41:1, 4-5, 7, 32 “1 Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto….. 4 Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. 5 Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. 7 Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu……. 32 Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.”
ü  Si lazima uote ndoto hiyo hiyo mara mbili kwa usiku mmoja, waweza ota ndoto hiyo siku nyingine na nyingine hiyo hiyo ama yenye maana hiyo hiyo
ü  Maana MUNGU usema mara moja tena mara mbili na kila asemalo ulithibitisha na ulitimiza. Ayb 33:14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.”

b.     Kukutia hofu
Daniel 4:5 “Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.”
ü  Angalia kama ndoto uliyoota imekutia hofu
ü  Hii ni ishara mojawapo ya kutohidharau ndoto hiyo.

c.      Kukufadhaisha au kufadhaisha moyo wako na kukupa maangaiko moyoni
Daniel 4:5 “Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.”
ü  Si tu kupata hofu bali itakuletea mafadhaiko moyoni mwako
Mwanzo 40:5-6 “5 Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. 6 Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika.”
ü  Ndoto hizi zilikuwa halisi na kuleta mafadhaiko hata nyuso zao zilikosa furaha.
ü  Kuna ndoto zinakuja kama taarifa tu na kuna nyingine ni vigumu kuzizuia kijuu juu tu kama ujapata msaada rohoni zitakusumbua tu.

d.     Cheki kama uliloota limetokea katika mwili wako wakati huu
ü  Mapambano katika ndoto ni mabaya sana na wengi uyaombea kwa maombi ya kawaida tu

e.      Kukunyima usingizi
Daniel 2:1 “Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha.”
f.        Kuwa na hamu ya kutaka kujua tafsiri yake
Mwanzo 40:7-8 “7 Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo? 8 Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie.”
ü  Walipoamka hawakuweza kutulia ndani yao walitaka kutafuta na kujua maana yake
Mwanzo 41:7-8 “7 Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu. 8 Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.”
ü  Usipuuze msukumo utakao kupata na usilizike mpaka upate na kujua maana sahihi

g.      Ndoto kutaka kuangaisha imani yako na utumishi wako kwa MUNGU
Yeremia 23:25-27 “25 Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, Nimeota ndoto; nimeota ndoto. 26 Je! Mambo hayo yatakuwa katika mioyo ya manabii wanaotabiri uongo hata lini, manabii hao wenye udanganyifu katika mioyo yao wenyewe? 27 Wanaodhania ya kuwa watawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao, wanazomhadithia kila mtu jirani yake, kama vile baba zao walivyolisahau jina langu, kwa ajili ya Baali.”
ü  Wapo watu wasemao ndoto lakini nia yao ni kuwaondoa watu kwa YESU. Kuwa nao makini
Kumb 13:1-3 “1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.”
ü  Shetani pia utumia sana ndoto kuvuruga imani za watu na utumishi wao
ü  Anatumia ndoto pia kwa kujitengenezea wafuasi na watumishi wake
Hesabu 12:5-6 “5 Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. 6 Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.”
ü  MUNGU utumia ndoto na maono kusema na watumishi wake halisi
ü  Na shetani utumia mlango huu huu pia
ü  Lazima ujue kuombea vizuri mlango huu wa ndoto, usipoomba shetani atakuvuruga kweli

h.     Moyo wako unakuwaje unapoikumbuka ndoto uliyoota huko nyuma?
Kama hali uliyoipata wakati umeota inakukuta vile vile ukikumbuka basi jua hiyo ni ishara MUNGU anakuambia bado kuna kitu hapo hakijatatuliwa

2.                 Andika ndoto unayoiona inahitaji kufuatiliwa hatakama ni fupi kiasi gani andika
Habakuki 2:2 “Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.”
ü  Andika tarehe, ulikuwa wapi, saa ngapi

3.                 Ikiwa umeota ndoto na ulipo amka umeisahau unafanyeje?
Dan 2:1-19
ü  Msihi ROHO MTAKATIFU akukumbushe maana yeye ndiye atukumbushae yote pia endelea kumsihi MUNGU na yeye atakuotesha tena na tena

4.                  Umeota ndoto tafsiri yake huijui ufanyeje?
ü  Omba MUNGU akupe ufahamu juu ya ndoto
Daniel 1:17 “Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.”
ü  Omba ufahamu ukae ndani yako ili ukiota ndoto nyingine unapata ufahamu hapo hapo
ü  Ufahamu unakaa ndani, ni wakudumu.
Mwombe MUNGU akupe tafsiri ya ndoto
ü  Tafsiri ni tofauti na ufahamu maana tafsiri ya ndoto moja ni tofauti na ndoto nyingine
ü  Tafsiri huja mara moja na MUNGU ndiye mfasiri pekee. Daniel 2:11, 26-28 na Mwanzo 40:8
Uwe na NENO la Biblia la kutosha ndani yako katika hekima yote
Ayubu 33:14-15 “14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;”
ü  Ndoto ni neno/ujumbe/maelekezo yanayoletwa katika picha
ü  Uja kama neno na kama ni neno basi lipo kwenye Biblia mahali
ü  Neno lina sauti Zab 103:20 “Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake.”
ü  Sauti uachilia kitu unachotakiwa kupokea na kupata
Rum 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.”
ü  Si tu kukuletea neno lazima usikie sauti iliyoko ndani ya neno kupata ufunuo, mwongozo, maelekezo, maarifa, hekima, ROHO ya uchaji na mengi mengi

Kolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.”
ü  Hekima hii hukusaidia mahali pa kusema nani wa kumshirikisha hiyo ndoto maana si kila mtu wa kumwambia.

MIFANO YA NDOTO NA TAFSIRI ZAKE KATIKA BIBLIA

Ukiota uko darasani
·         Unasoma
·         Umechelewa mtihani
·         na mengi yahusuyo darasani

Soma Daniel 1:1-…………

·         Mfalme aliandaa chuo na miaka ya kusoma ilikuwa 3
·         Darasa ni maandalizi ya hatua iliyoko mbele
·         Yawezekana umekwama ngazi hiyo uliyopo unahitaji kuvuka.
·         Muulize MUNGU umekwama eneo gani au wapi hujajiandaa kisawasawa ili uvuke.

Unaota mtu anakula

Zab 91:16 “Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.”
·         Amemaliza siku zake za kuishi ameshiba so ahitaji kuongeza miaka.

Isaya 29:8 “Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.”

·         Moja vita uliyonayo inatoka kwenye nafsi yako we unafikiri inatoka nje
·         Pili walioko nje wanatumia hali ya nafsi yako kukuletea vita ya kiroho

Luka 22:14-20 “14 Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye. 15 Akawaambia, Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; 16 kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu. 17 Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; 18 Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja. 19 Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.”

·         Cheki nani anakulisha
·         Kama unalishwa na watu usiowajua au waliokufa kuna mambo haya:
         i.            Kuna agano unahusika nalo lililopita kwa hao watu
       ii.            Kuna agano jipya wanataka kukuingiza
Vita hii ni mbaya sana usipopata msaada mapema uharibu hali yako na kuvuruga nyumba yako


1 comment:

Unknown said...

Bwana yesu asifiwe mtumishi ninatatizo la kuota ndoto nikiwa shule kwa namna tofauti na mazingira tofauti